Tuesday, March 3, 2020

KIFO CHA KISU, USALITI NA LAANA




Kisu ni kifaa bapa kirefu kinacho tumika kukatia, ambacho aghalabu hutengenezwa kwa chuma, na kina makali upande mmoja. Lakini vilevile kisu kinaweza kukufanya wewe ufanye maovu makubwa sana duniani, tena  maovu yenye laana mbaya sana ,.Hapa Kijana Nelson alijikuta kwenye mhatatizo makubwa sana na miangaiko mikubwa ya dunia sababu ya KISU! Yaani Nelson alikuwa anatokea kwenye familia ya tabu sana kule kijijini kwao. Na kwao Nelson walizaliwa mapacha yeye na mwenzake aitwae steven. Hhata hivyo Nelson na mwenzake Steven, walikuwa wanampenda sana mama yao mzazi! maana ndiye alie kuwa tegemezi lao. kwa sababu baba yao mzazi alifariki wakiwa wadogo sana hivyo walimtegemea mama yao kwa kila kitu, kuliko mtu yoyote yule.
Nelson anasema, "sitasahau, kule kijijini kwetu walikuwa hawapendi  wachawi, na ikitokea ukajulikana kwamba wewe ni mchawi yaani unapigwa na wanakijiji mpaka wana kuua, Sasa Siku moja saa tisa usiku kule kijijini, kuna bundi alikuwa juu ya nyumba ya mwenyekiti wa kijiji kisha akaanza kupiga kelele kwa mda mrefu sana! Na mara nyingi  waliamini kwamba bundi ni mchawi au ndege anae tumwa na wachawi kwenda kuua! Mwenyekiti alivyo sikia bundi analia kwa mda mrefu, akatoka nje pole pole ili amuue yule bundi! Kweli alichukua fimbo nzuri na ndefu kisha akampiga nayo yule bundi! Bundi na mwenyewe alivyo pigwa akaanza kukimbia! mwenyekiti pia akaendelea kumkimbiza ili amuue, ila yule bundi , alikimbia kwa uchovu sana maana tayari alikuwa amepigwa fimbo.
Alafu siku hiyo pia mama yangu mzazi alikuwa hajalala kabisa, bali alikuwa analia sana siku hiyo maana alikuwa amemkumbuka sana marehemu mume wake ,! Kwa sababu baba kipindi ajafa, ndiye aliekuwa tegemezi lake sana. Na mwenyekiti nae hakuchoka kumfukuza yule bundi,  sasa na kibaya zaidi yule bundi alikuwa anakimbia kuja nyumbani kwetu na yule bundi alipo fika mlangoni  kwetu tu akapotea ghafla. Mwenyekiti akashagaa! Mama akatoka nje akasema, tatizo nini? mwenyekiti akasema "kumbe na wewe mama ni mchawi eh? lazima na wewe ufe, naomba umlete bundi aiwezekani apotelee hapa, ndipo akaanza kupiga mayowe ili mama auwawe! Mama akasema , mimi sio mchawi. Mwenyekiti aliendelea kupiga kelele, akisema "wanakijiji wenzangu , nimeshika mchawi njoo tumuue" mama alilia sana pale nje akisema, "mimi sio mchawi unanionea mwenyekiti wangu usiwaite wanakijiji nitakufa baba"  Ila hakusikilizwa kabisa ,! kipindi icho mimi na pacha mwenzangu tukiwa tumelala hatusikii chochote kile, maana ilikuwa ni usiku sana. Kumbe Watu wame jaa pale nyumbani wakitaka kumuua mama! wakauliza swali "mwenyekiti unauwakika kwamba huyu mama ni mchawi? Maana tumeishi nae miaka mingi sana ujue, na hatujawai kumuona kama anajiusisha na mambo ya kishirikina hata kidogo" mwenyekiti akawambia kuhusu bundi alivyo potelea pale mlangoni ghafla! Watu wote wakaamini kuwa mama yetu ni mchawi! Dah hawakuwa na huruma kabisa hata kidogo ,, ndipo wakaanza kumpiga mama pale nje tena kipigo kibaya sana cha kusikitisha moyo ,. Mimi nilishtuka usingizini nikashangaa kukuta watu wengi nje ya nyumba kibaya zaidi walikuwa wanampiga mama yetu mzazi ila Wanakijiji wakatukamhata mimi na pacha wangu kisha wakaturudisha ndani na kutufingia kwa nje ili tusione kinacho endelea.
Mama alipigwa sana ,, alipigwa sehemu za hhatari mpaka sehemu zake nyeti zakaanza kutokwa damu na macho yake yalianza kutokwa damu sana vilevile masikioni mwake pia, wanakijiji hawakulizika wakasema "hawa wachawi hawa, wanatutesa sana sisi, wanatuulia watoto wetu, maarubino, wanasababishia mhatatizo mengi hapa kijijini, hatupati mvua wala mavuno mazuri, tumuue afe kabisa huyu mama". Mama alikuwa analia akisema "mnanionea , mimi sio mchawi mwenyekiti ananisingizia mimi msiniue" mama aliongea vile huku damu zikimtoka mdomoni! Tuliumia sana tulipo msikia mama mzazi akilia, akipigwa kama mwizi. Nilijaribu kubomoa mlango nikamsaidie mama lakini sikuweza kabisa.
Sasa basi, wanakijiji walivyo mpiga mama vibaya ndipo wakamvua nguo zake zote mpaka nguo ya ndani , kila mtu akamtazama mama jinsi maumbile yake nyeti yalivyo kuwa,kisha wakambeba mpaka pembezoni mwa mto mkubwa sana kule kijijini, wakamfunga mama jiwe zito sana mgongoni kisha wakamzamisha mtoni. Mama mzazi alizama, alikufa! Sisi tukiwa tumefungiwa ndani.
Baada ya mama yetu mzazi kupoteza maisha! Mimi na pacha wangu hatukufunguliwa mlango kabisa, kila mtu aliondoka na kutuacha tukiwa tumefungiwa ndani. Na kipindi tupo mule ndani, Pacha mwenzangu akaongea kikabila kwamba "nyo idaun'gi yong" akimaanisha kwamba akitoka nje lazima mwenyekiti hatamkoma kwanini ka sababisha mama yetu afe! Hivyo basi Siku ya kwanza ikaisha bila mtu yoyote kutufungulia, siku ya pili pia hakuna alie fungua mlango Dooh, njaa kari sana ikatupiga mule ndani na hatukuwa na chakula chochote kile!
Ndipo tukaanza kupiga kelele dirishani ili watu watuonee huruma tuweze kufunguliwa mlango tutoke ndani. Ila hata wapita njia waliogopa kutufungilia wakisema kwamba ", msiende hapo kufungua, mama yao alikuwa mchawi mtalogwa bure, maana mtoto wa nyoka ni nyoka tu" baada ya siku nne kupita tukiwa ndani bila msaada wowote, tulisikia njaa sana maana tulikuwa hatuli, tulichafuka sana maana tulikuwa hatuogi, chumba kilitoa harufu maana tulijisaidia humo humo ndani kipindi tumebanwa! Ndipo nikamwambia pacha mwenzangu kwamba "steven ndugu yangu, tukizubaa tutafia humu ndani, bora tutumie njia ya ziada tutoke" Steven akajibu "sasa kaka tutatokaje ndani, tazama dilisha lilivyo na nondo ngumu, cheki mlango tumefungiwa kwa nje tutatoka vipi sasa" Nikamjibu kwamba "steven leta kisu nikuonyeshe" Ndipo Niliamua kupanda mpaka juu ya paa, kisha nikachana bati  kwa kile kisu na tukawa tumetoka nje mimi pamoja na ndugu yangu.
Tulishangaa kuona damu zimekauka pale nje za marehemu mama yetu. tuilia kama watoto wadogo sana pale nje ila hatukuwa na msaada wowote ule. Tulienda mtoni walipo mtupa mama labda tungephata mwili wake ili tumzike. lakini hatukuuona mwili kabisa,
Steven alipatwa na uchungu sana akasema "lazima nilipize, lazima mwenyekiti na yeye pia afe kama mama" Nilimzuia nikasema steven kumbuka tumebaki yatima hivyo sitaki nikupoteze pia ndugu yangu tumuachie mungu maana mama yetu amesingiziwa na ameuwawa bila makosa" Kumbe steven hakusikia ushauri, akamfhata mwenyekiti na akamwambia "wewe babu umesababisha mama yetu afe, lazima na wewe ufe" na hapo ndipo mdogo wangu alifanya kosa kubwa sana kuongea vile.
Pacha mwenzangu alifanya kosa kubwa sana kumtishia amani yule mwenyekiti,alafu kipindi anamtishia amani mwenyekiti, kwamba "kwanini umesababisha mama yetu afe lazima na wewe ufe" kiukweli mwenyekiti alipatwa na mshituko mkubwa sana aliogopa na alishtuka zaidi siku hiyo sababu mwenyekiti alikuwa na ugonjwa wa presha pia, hivyo  presha ya mwenyekiti ilipanda sana! Na ilipo fika saa tisa na dakika 40 usiku alizidiwa zaidi, kipindi wanhataka kumuwaisha mwenyekiti hospitali dooh alikufa palepale nyumbani kwake ,.Watu aliumia sana, wakasema "hama kweli tumeamini ile familia  niya kichawi sana looh, yaani mama yao alishikwa na bundi juzi tu hapa, sasa huyu mtoto wake anaitwa steven amemtishia amani mwenyekiti kwamba hatakufa, na kweli amekufa leoleo, ila lazima na yeye afe." Wanakijiji walikasilika sana kuona mwenyekiti wao mpendwa amefariki, na wote waliamini kuwa amelogwa na familia yetu kumbe steven hakumloga bali ni mshtuko ulisababisha. Mdogo wangu alipo sikia mwenyekiti amekufa alikimbia bila hata kuniaga mimi, sikujua steven ameenda wapi, nikawaza sana maana nilikuwa nimezoeana sana na ndugu yangu, hivyo niliona dunia yote chungu kwangu.
Sitosahau hili, yaani Nilisikitika sana, niliumia zaidi, na nililia kama mtoto mdogo pia, pale Wanakijiji walipokuja nyumbani wakiwa wamebeba visu, mapanga na fimbo mida ya usiku wakiwa wanataka kumuua steven. Lakini bahati nzuri siku hiyo steven alikuwa ameisha toroka nilikuwa peke yangu pale nyumbani. Walipo kuja wakanikamata mimi wakataka kunipiga, wakisema kwamba,"Steven yuko wapi, mtoto mchawi alie shindikana hapa kijijini! Ametuulia kiongozi wetu, mzee wawatu" Nikasema ", mimi sijui steven alipo, hata mimi nilipo rudi nyumbani sikumkuta" Nilipigwa kofi zito sikioni, nikapigwa teke chungu, kisha kaka mmoja akanidunga na bisibisi begani kwangu, akasema "usipo twambia mchawi mwenzako alipo, tutakuua wewe" Nilipiga mayowe nikisema sifahamu, sielewi, mimi nilimkataza asiseme vile kwa mwenyekiti ila hakunisikia kabisa" nilishikwa kama mwizi, nikafungiwa ndani kwetu, kisha wakachoma nyumba yetu moto kwa nje ili na mimi niungulie humohumo ndani, nilianza kupiga kelele nikiomba msaada, "uuuwiii, uuwiii nihurumie , sijamuua mimi nisaidie ndugu zangu napenda kuishi pia" Nililia sana maana nilijua siku yangu ya kufa tayari imefika. Ila cha kushangaza akuna hata mmoja alie pata moyo wa huruma kunitoa mule ndani, maana walijua familia yetu ndiyo iliyo usika katika wauaji ya mwenyekiti, hivyo hata huruma hawakua nayo kwetu. Bati la nyumba liliwaka moto sana, nyumba nzima ikaanza kupata joto kali! Mimi nikiwa ndani, nilianza kutokwa jasho uku nikianza kusikia joto kali sana linaanza kunichoma kwa mbali.Niliogopa nikaanza kijimwagia maji yaliyo kuwemo kwenye ndoo ili nipunguze joto. Nyumba nzima ikachemka joto, nikigusa ukuta naungua! Sakafu ikaanza kuchemka pia niliungua miguu sana maana nilikuwa sijavaa hata viatu.
Ikanibidi nipande juu ya meza. Ila pale kwenye meza kulikuwa na joto zito. Mwili wangu ulianza kubadilika nikaanza kusikia maumivu makali. Kibaya zaidi moto ulizidi kutanda nje ukiendelea kuingia ndani. Uvumilivu ulinishida sana maana sehemu zangu nyeti zilipata maumivu mazito nisiyo weza hata kuyasema. Kilicho kuja kunikosesha nguvu ni pale moshi ulipo jaa ndani, nikashindwa kupumua na nikapoteza fahamu, Hata macho nikashindwa kufumbua kwa sababu ya joto kali ndani. Wakati nimeanguka sina nguvu yoyote, nilisikia kwa mbali sauti kama ya kishetani ikisema "mwanangu mwanangu, ni mimi marehemu mama yako, nakuhurumia mwanangu, lakini hauto kufa nipo kukusaidia wewe, Maana haujafanya kosa lolote wanakuonea hawa binadamu wasio kuwa na roho ya huruma"
Baada ya hapo, nilishangaa sana mlango unabomolewa na kaka yake marehemu mama yangu! Kisha akanitoa nikiwa hoi, akanipeleka hospitali ili nipate matibabu nisiweze kufa. Niliongezewa maji na kushonwa vidonda, nilikaa hospitali mda mrefu sana na matibabu yalikuwa ya gharama pia. Nilijiuliza maswali mengi sana kichwani "hivi kwanini sauti ya mama ilinitokea, alafu mda huohuo, kaka yake mama anakuja kunisaidia dooh sikuphata jibu kabisa"Na vidonda vyangu vilikuwa vibichi mno yaani vilikuwa vinatoa maji maji tu yaani mpaka harufu. Daktari wa ile hospital alimuita mjomba wangu na kumwambia kwamba, "Kijana wako amephata nafuu! ingawa bado ana vidonda mwilini, lakini dawa tulizo mpa nina imani kuwa hatapona vizuri na atendelea na shughuli zake zingine.Hivyo tunakuomba umchukue na umpeleke nyumbani ili akapumzike" kwa upande wangu nilifurahi sana! maana nilikuwa nimechoka ku dungwa sindano mwilini wangu kila siku. Tulipo fika nyumbani kwa mjomba tulimkuta mke wake ambae nilikuwa namuita shangazi. Kibaya zaidi tulipo fika tu mjomba wangu akawa amesafiri kwenda mkoani kufatilia biashara zake, hivyo akawa ameniacha mimi pamoja na mke wake. Mimi ilionyesha upendo sana kwa shangazi na mjomba wangu maana ndiyo wazazi niliyo kuwa nimewabakiza na ndiyo nilio kuwa nawategemea, sababu pacha mwenzangu alitoroka, mama na baba yangu wote walikuwa wameisha fariki, na kibaya zaidi nyumba yetu ilikuwa imechomwa moto. Shangazi yangu alikuwa hana mtoto yoyote maana alikuwa awezi kuzaa yaani hana uzazi! Hivyo walikuwa wanaishi wawili tu ndani.
Wakati nipo sebreni nimekaa nasikia njaa, nilimuoa shangazi anapika chakula nilifurahi maana nilijua nitakula na kushiba vizuri! Ila alipo maliza kuivisha, nilisikitika sana maana alipakua chakula chote  kisha akala peke yake, Uvumilivu ulinishida nikaamua kuongea, "shangazi yangu nina hisi njaa sana, naomba unipakulie chakula" Shangazi akajibu kwa kunisonya "michuuu, mjinga nini wewe, yaani mume wangu ametumia pesa nyingi sana kukutibu, pesa ambayo angeninunulia vyombo vya ndani kaialibia kwako, alafu unakuja kwangu unhataka kupikiwa na upakuliwe kwani umenioa, alafu unanikela unavyo ishi humu ndani unanibana kwanza" Nililia kisha nikajibu, "shangazi yangu sio kwamba siwezi kupika, ninaweza shangazi, lakini ninaumwa ebu nitazame nilivyo jaa vidonda sasa napikaje?"
Shangazi akasema "mshenzi kweli, kawafufue wazazi wako waje wakupikie mimi sijawai kuzaa wala uchungu wa kuzaa siujui, na hapa utatoka tu, yaani unanikela na hiyo midonda yako, ebu angalia unavyo nichafulia vitambaa vyangu kwenye kochi, na leo usiku utalala chini maana vidonda vyako hivyo utanichafulia mashuka na damu damu" Nililia sana siku hiyo, nililia zaidi kisha nikasema, "shangazi nisamee kama nina kuhudhi kukaa kwako, ila nisaidie, maana sina sehemu yoyote ya kuishi, wazazi wangu wote wameisha tangulia mbele za haki! Na kaka yangu pia ameisha kimbia! Nyumba yetu imechomwa moto na wanakijiji hivyo nyie ndiyo wazazi wangu." Shangazi alipatwa na huruma kidogo kwa yale maneno mazito niliyo mwambia ndipo akaniambia, "ebu fungua kabati jikoni uchukue mkate ule" Nilitembea kwa shida, maana hata miguu yangu chini ilikuwa na vidonda ila nilijikaza kidogo kidogo tu, kabla sijafika kwenye kabati niliangua chini, lakini shangazi hakuwa na huruma hhata kidogo ya kuninyanyua, nilikuwa naumia sana nikitembea ndipo nikaamua kutambaa kama mtoto mdogo, ili niupunguze uchungu, mungu saidia! nikafika kwenye kabati, sasa wakati nimenyanyua mkono wangu juu ili nichukue mkate nile nikawa nimejitonesha kidonda cha kwapani maana kilikiwa kimeanza kukauka sasa nilivyo nyanyua mkono nilikuwa kama nakichana kidonda! nyama zikaachana, Wee! nilisikia maumivu sana ndipo nikaachia sahani ya mkate, Sahani ilianguka chini na kupasuka hapohapo maana ilikuwa ya udongo.
Shangazi akasema "mpuuuuzi kweli wewe, yaani unanipasulia vyombo. Sijui mume wangu kaleta lidude gani ili" Nilkasema "shangazi nisamee nilijitonesha kidonda ndo maana nimepasua" shangazi akafhata fimbo nje."Sikuamini macho yangu, shangazi alinichapa mwili mzima! Akisema "na utarudi kwenu, yaani mimi unaharibu vyomba vyangu, kanunue sahani yangu mjinga wewe, na mkate wangu sikupi leo" shangazi alinichapa sana na  nisinge weza hata kukimbia maana vidonda vyangu vya mguuni vilikuwa vinaniuma sana ,. Nilikuwa navuja damu tu maana alinitonesha mwili mzima hivyo vidonda vikawa vibichi upya, alafu ubaya wa shangazi alikuwa akikasilika ananichapa mwili mzima hata kichwani. Nilishinda njaa bila kula, huku nikisikia maumivu makali. Mjomba wangu alikuwa hayupo na alihisi nina ishi vizuri na mke wake. Kipindi shangazi ananifyonza ovyo ovyo, akiniangalia kwa jicho baya sikuwa na jinsi, maana nilikuwa na washwa sana mwilini, sababu ile fimbo yake ilikuwa na miba miba hivyo ilinichoma sana ile miba kwenye vidonda. Wakati nipo nalia njaa. Shangazi pia akaenda jikoni, sasa wakati anapanga vyombo vyake akapasua sahani yake pia kama mimi, Shangazi alipo pasua sahani yake inayo fanana na yangu niliyo pasua, aliona haibu sana, akasema "wewe Nelson unanitia mawazo sana mpaka napasua vyombo vyangu mwenyewe, sasa kwa mwendo huu si tuta maliza vyombo vyote, yaani we humu kwangu lazima utatoka tu" nilishangaa tukio kama lile kisha nikajiuliza moyoni, kwamba "yaani mimi nilipo pasua sahani amesema ninunue sahani yake, mungu saidia na yeye kapasua sahani kama hii hii tena leo leo basi na yeye akanunue" niliendelea kuishi kwa tabu  na shangazi yangu, lakini sikuwa na jinsi nilivumilia sana mpaka nikapona na nikawa safi, nikaphata nguvu kama zamani.
Siku moja usiku, kipindi tumeenda kulala, mimi nilibanwa na haja ndogo.Hivyo nikaamka polepole kwenda chooni ili niweze kukojoa.Sasa kipindi nafungua mlango nilishangaa sana kusikia maneno ya ajabu mno shangazi akiya ongea katika simu, kwamba.
"Hallow baby, nisamee mpenzi wangu, najua sahivi tunashindwa kukutana kufanya mapenzi, maana huyu Nelson anaweza kunisema kwa mme wangu na kumbuka mme wangu anawivu sana hivyo kama akigundua anaweza kutudhuru"

Baada ya mda mchache shangazi akajibu ile simu kwamba "sawa mpenzi nishauri tunamtoaje hapa huyu kijana ili tiendelee kujivinjari na mapenzi yetu maana mme wangu ameisha safiri kikazi uje nipate raha" yule hawara yake mama akampa mbinu nzuri ya kufanya ili mimi nifukuzwe pale nyumbani, kusudi wao waendelee kuzini! mjomba akisafiri kikazi. Na mara nyingi shangazi alikuwa hapendi nikae kwake maana alihisi nambana starehe zake za ngono. Nilisikitika sana tena zaidi ya sana maana shangazi yangu na hawara yale walikaa chini na kuandika barua eti kwamba mimi namtaka shangazi yangu kimapenzi, maana barua ilikuwa inasema hivi. "Shangazi, ni mimi Nelson, nhatambua fika kuwa wewe ni mke wa mjomba, lakini shangazi nisamee kama nitakuwa nimekukwaza, shangazi yangu naomba tufanye mapenzi, maana tunakaa humu ndani wawili tu, na mjomba awezi kujua, Alafu  ulikikubali nitakupa penzi tamu sana kuzidi mjomba maana tayari mjomba ameisha zeeka naamini hakupi ladha nzuri za mapenzi, utaburudika shangazi" Mama na hawara yake waliandika hiyo barua kisha wakaitunza ili mjomba akija aisome kisha ajue ni mimi ili nifukuzwe.
Shangazi aliichukua ile barua na kui hifadhi sehemu salama ili mjomba akija ampe aisome, ili kusudi apatwe na hasila na mimi nifukuzwe pale nyumbani kama mwizi.
Sasa siku moja saa 11 jioni shangazi alinifhata na kusema "mjomba wako anarudi leo, na leo leo ndiyo itakuwa mara yako ya mwisho kukaa kwangu, kama ni chakula kula cha kutosha ushibe kabisaaa maana leo ulali nyumbani kwangu na nimekuchoka sana wewe unanibana sana, yaani sifurahii maisha tangu nikujue" Shangazi aliongea vile kuwa nitafukuzwa kwa kujiamini maana alijua ile barua mme wake akiisoma atoweza kunisamee, hata paniki na kunifukuza nyumbani mda huohuo. Nikamwambia shangazi kwamba, "Shangazi tafadhari naomba nisamee, najua wewe ndiye mama mwenye nyumba, unaweza fanya lolote mimi nitoke hapa, Mimi nikifukuzwa hapa nita ishi kwa tabu sana, naomba nisamee shangazi, maana kama kazi zako zote nafanya nguo zako zote nakufuria hata nguo zako za ndani pia ukinipa nakufulia, kila kazi hata kukupikia, sasa nifanye nini ili uone thamani yangu"
Shangazi hakuwa na huruma kabisa, akasema, "usinililie bhana, we mwanaume kama shoga vile, tangu lini mwanaume analia ovyo" Baada ya mda kidogo mjomba akawa amewasili kutoka kazini akiwa amechoka sana "kabla hata hajaingia bafuni kuoga mke wake akaanza kulia kama mtoto, Mjomba akauliza, ", mke wangu mbona unalia, au ndiyo kuni missi" Shangazi akajibu uku akiwa analia "hapana mme wangu ni mtoto wako ananifanyia mambo ya ajabu sana, yaani ananitongoza akisema nimpe penzi, eti namtamanisha sana tunapo kuwa wawili mimi na yeye" Mjomba jasho likamjaa, alimiminika jasho sana mjomba wangu ,, akaniuliza "Nelson mwanangu ujue nakutegemea sana, na vilevile nakuamini mnoo, hivi leo hii unhataka kula mama yako, yaani wewe shangazi yako humu heshimu doooh, pepo gani hiii" Kipindi nipo nalia nhataka kuongea ili nijitetee maana sikuamini yale maneno shangazi aliyo yhatamka nilihisi kama ni ndoto ama muvii. Shangazi palepale akasema "mme wangu ngoja nikuletee ujumbe mfupi aliyo niandikia" Alipo ufhata akampa mme wake ujumbe  kisha mjomba akausoma. Mjomba akasema, "mwanangu unanivua nguo, ukisema, mimi simlizishi mke wangu? Toka kwangu ibilisi mkubwa wewe”
mjomba wangu alipo nifukuza kwake, nilisikitika sana, nalianza kulia, nikaomba msamaa kwamba "mjomba wangu, mimi sijamtongoza mke wako, shangazi ananisingizia tu" Mjomba akajibu "yaani ni bora ungemtongoza ningekuelewa, kuliko kunitukana kwamba mimi simlizishi shangazi yako, mtoto wangu umenivua nguo kabisa, ondoka sikutaki hapa nyumbani, kama wewe ni msaidizi wa wake za watu kajaribu nyumba zingine sio  kwangu" Nikajibu kwamba "mjomba mimi siwezi kusema hivyo nasingiziwa tu, kumbuka umenisaidia sana mpaka nimepona, sasa mjomba hivi ujasili wa kumtongoza shangazi yangu nimeutoa wapi ,, siwezi fanya hivi, huu ni ujanja ujanja tu nafanyiwa na shangazi” shangazi alipo muona  mjomba kama anhataka kunisamee, akaanza kulia kama mtoto huku akisema, "mme wangu tena huyu mtoto kuna siku alinifhata usiku chumbani akisema, shangazi mjomba yupo mbali sana naomba nilale na wewe tupeane jot, mimi nilikuwa mpole sikusema ili nisiwagombanishe nyie ndugu ila kwa sasa tabia zake zimenishinda kabisa , mi sitaki bhana aondoke tu" Mjomba akasema "hivi wewe mwanangu yaani msaada wote ninao kupa unhataka kulala na mke wangu,  kumbuka mimi mke wangu namuamini na amelelewa katika malezi bora, awezi kukubali kutoka nje ya ndoa, na mke wangu sio muongo awezi kukusingizia kabisa nimeishi nae kwenye ndoa ni miaka saba sahivi, sijaona tatizo lake, inakuwaje wewe ulete mhatatizo kwenye familia yangu" Nilisema, "mjomba hapana shangazi hanipendi, anaona nambana kukaa hapa maana anashindwa kufanya maovu yake akiwa free" Mjomba alinipiga kofi shavuni kisha akasema, "kwangu utaondoka tu, na utatoka kama ulivyo kuja, na usisahau ulikuja bila kitu hivyo hata nguo nilizo kununulia utaziacha"
Nilifukuzwa nyumbani nikiwa sina pesa yoyote mfukoni! Nilifukuzwa kama mwizi pale nyumbani, nilikaa nje ya nyumba pale nawaza nitaenda kula wapi au kulala wapi, nilikaa pale nje ya nyumba nikizani labda naweza kusameewa, mjomba alipo toka ndani na kunikuta pale, akasema, " hivi hutaki kuondoka, bora uondoke ukhatafute maisha yako, maana tayari umenihudhi, nimeisha kuogopa maana unaweza kumbaka mke wangu wewe" Sikuwa na namna yoyote ya kufanya,ndipo nikaamua kumuacha mjomba na mke wake tu.
Niliondoka kwa mjomba wangu nikiwa na mawazo sana, nilifika sehemu moja hivi kulikuwa na kivuli nika kaa chini, kisha nikajifikilia kwamba "nimetoka kwa mjomba wangu na sifa mbaya sana, alafu kibaya zaidi kosa lenyewe sijafanya mimi, na kinacho niuma ni kwamba mjomba ana amini fika kwamba kweli nilimtongoza mke wake, je jifanye nini ili mjomba a amini kuwa mimi sijafanya hiyo dhambi"Niliwaza kwamba, nirudi kwa mjomba wangu niombe msamaa nikiwa nalia! labda anaweza kunisamehe, nikaona ilo wazo bado dogo.

Nikawaza tena kwamba, "au nirudi kwa mjomba nikubali tu kuwa nimefanya kosa kweli alafu niombe adhabu nifanye"niliwaza sana sikuphata jibu, maana niliogopa kwamba, kama kweli sikufanya kosa alafu nimesingiziwa na kufukuzwa, je nikirudi mara ya pili si nitauliwa kabisa" Ilifika hatua nikaphata njaa sana, na kibaya sasa sikuwa hata na shillingi mfukoni. Nilikaa chini nikawaza sana  nifanye nini ili nipate kuweka kitu chochote mdomoni.Ndipo nikaphata wazo la kwenda kwa rafiki wakaribu sana na mjomba wake, Mr Zephania huenda angenisaidia, nilipo fika kwa Zephania, nilikalibishwa ndani!
Zephania akaniuliza maswali, "Nelson naona leo umeamua kuja kwangu bila hata taarifa? Na mbona unapiga miayo hivyo haujala?" Nilijitahid kujikaza nikashindwa, ndipo chozi likaaanza kunitoka. Zephania akauliza "kwanini unalia hivi, wewe kijana mkubwa?" Mke wa zephania akasema "mme wangu ukiona mwanaume analia hivyo, ujue kuna jambo zito sana ambalo lime msibu, ebu muulize vizuri mtoto" Zephania akasema tena "Nelson tatizo nini, nyamaza basi ili nijue jinsi ya kukusaidia" Nilijitahid kuongea lakini sauti ilikhataa kutoka nikashindwa kuongea maana  nilibanwa na uchungu moyoni na simanzi kubwa sana, nikaendelea kulia.
Mke wa zephania akaniletea maji ya kunywa. Nilipo maliza kunywa maji, ndipo nikasema ukweli kwa zephania, Nikamwambia hivi. "Mjomba amenifukuza kwake" Zephania na mkewe waka kaa kimya kidogo, Kisha zephania akaguna "mhhh" Zephania akasema, "mjomba wako alivyo mtu mpole, msikivu, akufukuze wewe mtoto wa marehemu dada yake, basi utakuwa umemfanyia kitu kibaya sana nyumbani" Niliamua kumwambia ukweli Zephania, maana ndiye nilie muamini kuwa anaweza kunitetea kwa mjomba ili nirudi kwake.
Nikasema"mjomba wangu amenifukuza kwake, amesema nisikanyage tena nyumbani, na mjomba anasema eti kwamba mimi nimemtumia mke wake barua ya kwamba, namtaka mkewe kimapenzi na kwenye ujumbe wa barua nimemtukana mjomba wangu kuwa hana nguvu za kiume za kutosha"
Nini? Akauliza zephania.
Nikajibu "ndiyo hivyo tu nilivyo kwambia"
Zephania akauliza "hivi kweli unaweza kuphata ujasili wa kufanya hivyo?" nikasema "hapana siwezi hata kuthubutu kufanya huo ujinga, ila ni shangazi tu hanipendi, na hanitaki mimi pale nyumbani, najitahidi sana kufanya kazi zake zote, namfulia, nadeki, napika mimi, vyombo naosha kila kazi nafanya mimi lakini hanipendi.  Mke wa zephania akasema kwamba, "mme wangu mimi ni mwanamke naelewa tabia zetu, huyu kijana hana kosa lolote, shangazi yake hatakuwa hapendi kukaa na ndugu wa mme wake, hivyo nenda kajalibu kumuombea msamaa, na akimkhataa basi mrudishe Nelson tutakaa nae sisi, hatatusaidia kazi za hapa nyumbani"
Nikasema "hapana mimi naogopa kurudi nyumbani, maana mjomba anaweza hata kuni ua labda niandike barua ya kuomba msamaa anipelekee" Zephania akasema, "wazo zuri sana, ebu andika" Niliandika barua nikajielezea vizuri maisha niliyo ishi na shangazi, mpaka anafika hatua ya kufukuzwa. Zephania akachukua ile barua na kwenda nayo nyumbani ili aniombee msamaa kwa mjomba. Kipindi Zephania anaingia ndania kabla hata ajakaa. Mjomba akasema, "rafiki yangu hivi nilikwambia yaliyo nikuta hapa nyumbani, dooh yaani uwezi amini, yule mtoto wa marehemu dada yangu si alimtongosha shangazi yake aisee tena kwa ushenzi akanitukana hata mimi eti simlizishi mke wangu wa ndoa" Zephania akamuuliza, una uwakika? Mke wa mjomba akadakia "nikweli shemeji, yule mtoto mtundu sana alinitaka kimapenzi" Hata barua ninayo ngoja nilete! Alipo leta barua yake, zephania akaisoma, dooh alisikitika kwa ule ujumbe. Zephania alipo pewa barua yangu ya kumtongoza shangazi, akafananisha mwandiko na ile barua niliyo andika mbele ya macho yake ya kuomba msamaa. Zephania alishangaa kuona miandiko ni tofauti akasema "shemeji humpendi Nelson, na hii barua sio yeye ameandika" Zephania aliendelea kumwambia shangazi kwamba,
"hii tabia yako ni mbaya shemeji, yaani kumbe wewe hupendi kukaa na ndugu wa mumeo sio? Na ni bora sasa useme ukweli kuwa humpendi mtu, kuliko kutunga uongo ili mwenzako aonekane mbaya na afukuzwe kama mnyama" Hicho kitu kilimkwaza sana Zephania, hakukaa kimya, akaamua kumwambia na mjomba wangu kwamba,
"Rafiki yangu tumeishi wote miaka mingi, ila sikujua kama una maamuzi ya kitoto yaani wewe unamsikiliza sana mke wako, yaani hata vitu vya uongo wewe una amini tu, sasa mtoto wa dada yako unamfukuza hivyo kumbe sio mkosaji, umefanya kosa kubwa sana rafiki yangu, najua kuwa unampenda mke wako lakini asikupelekeshe kiasi hicho mpaka ndugu zako unawaona wabaya , uo ni ujinga"
Mjomba wangu alishangaa sana, akasema "Zephania rafiki yangu mimi haya mambo naona kama siyaelewi kabisa, hivi Zephania unajua nime ishi na mke wangu miaka mingi sana kwenye ndoa, na ajawai kunidanganya hata siku moja, na kizuri zaidi mke wangu amelelewa katika malezi bora hivyo hana ujinga wowote ule, sasa nisimuamini vipi" Rafiki, huyo Nelson mimi simtaki kwangu kaishi nae wewe matusi aliyo nitukana yananitosha, na wewe kama unhataka mke wako atongozwe kaishi na huyo mtoto utaniambia tu"
Zephania akasema, "hivi wewe rafiki yangu unaongea mambo gani hayo ya ajabu sana,  mtazame mke wako yaani nafsi yake inamsuta, alafu wewe unajifanya kumtetea, tazama hapa hii miandiko haifanani kabisa na wala haiendani hata kidogo, huyu mtoto mnamsingizia, na kama msipo mrudisha nyumbani hapa napeleka hii kesi kituo cha polisi waisimamie wao, maana huu ni unyanyasaji, yule ni mtoto wenu na ni mwema inabidi mu mtunze sio kumnyanyasa, na mimi hizi barua mbili ndizo zitakuwa ushahidi wangu mahakamani" Kipindi shangazi ameinama chini anaogopa kesi isifike polisi, Mjomba akashangaa kuona mke wake kama ameishiwa nguvu yaani amenywea mnoo. Mjomba akamuuliza swali kwamba "mke wangu hivi ni kweli umemsingizia mtoto wangu ili nimfukuze hapa nyumbani" Shangazi akajibu akilia "nisamee mme wangu, ni shetani tu kanipitia sita rudia kosa mme wangu, na ni kweli Nelson hajaandika hiyo barua, nisamee"
Mjomba akasema "nini"
Zephania akadakia "unaona" Palepale mjomba akazimia
Mjomba alipo zimia Zephania aliogopa, maana mjomba kipindi anaanguka alianguka kichwa kikagonga vibaya pale chini mpaka damu zikaanza kumtoka, ndipo zephania akampigia simu mke wake, ili mimi na mkewe twende kwa mjomba wangu kumsaidia. Tulipo fika tukamtoa nje ili apunge upepo, na sisi pia tuliendelea kumpepea ili apate fahamu haraka lakini tuliogopa maana damu ziliendelea kumtoka. Zephania akasema "itabidi tumpeleke hospitali, maana hizi damu sio za kawaida kwa jinsi zinavyo mtoka" Kipindi wanambeba mjomba ili wampeleke hospital, pale pale akaphata fahamu! Shangazi akaanza kulia akisema, "mme wangu sitarudia nisamee, ni ujinga tu na uchoyo umenifanya nifanye vile, lakini hamna jingine mme wangu" Mjomba akajibu, "mke wangu kwenye ile barua ni bora ungesema maneno yote lakini lile neno la kwamba sikulizishi, linauma sana aisee, unaonyesha wazi kwamba, mimi sikulizishi, na sio hivyo tu labda ni kweli una wanaume wako wanao kupa furaha zaidi yangu, maana wewe ni mtu mzima iweje ufikilie vitu kama hivyo, labda unafanya kweli" Shangazi akasema "mme wangu nakupenda sana siwezi kusaliti ndoa" Mjomba akajibu, "sasa kwanini unamsingizia mtoto wa dada yangu kuwa anakutaka kimapenzi, yaani mpaka namfukuza kama mwizi," mjomba aliongea maneno yale huku machozi yakiwa yanamtoka. Zephania na mke wake walimshangaa sana shangazi wakamuona ni mtu wa ajabu sana. Shangazi akasema, "zephania shemeji yangu, naomba uniombee msamaa kwa mme wangu, kama alimfukuza Nelson anaweza kunifukuza hata mimi" Zephania akajibu " shemeji usijali nitaongea nae lakini punguza roho mbaya, roho ya kishetani hiyo kabisa sio nzuri", Zephania akasema "rafiki yangu msamee tu mke wako, naamini kwa ili lililo mkuta leo awezi kurudia tena ujinga" Mjomba kwa hasila akamkaba zephania! kisha akamwambia, "hivi unazani mimi ni mjinga sindio, hivi hata kama ni wewe kwa barua hii na tabia hii unaweza kumsamee mke wako ki rahisi" Mke wa zephania akasema "shemeji muachie mume wangu usimkabe" Mjomba alipo muachia zephania, akamwambia mke wake kwamba "kosa ulilo fanya mimi siwezi kukusamee kilaisi tu, chukua nguo zako nenda kwa wazazi wako nakuja uko"
Shangazi hakua na njisi, alifungasha nguo zake na akaenda kwa wazazi wake kukaa huko mpaka siku mjomba hatakayo enda kuzungumza na wazazi wake. Mjomba alipo nitazama mimi alilia sana ,, akanikumbatia kisha akasema, "nisamee mwanangu, najua nimefanya kosa kubwa sana kukufukuza kwangu, kumbe umesingiziwa na mke wangu, mimi sikujua nisamee ," Tulisameana wote, ndipo zephania na mkewe wakarudi nyumbani kwao. Mjomba alipatwa na wasiwasi labda anaweza kuangaika kipindi mke wake hayupo, lakini alishangaa sana! Maana nilikuwa naamka mapema nafanya kazi zote za ndani, namfulia nguo zake zote, nyumba inakuwa safi mda wote, kisha namuandalia chai asubui, anakunywa na kwenda kwenye shughuri zake.
Siku moja mjomba akasema, "mwanangu hivi unajua tangu mke wangu aondoke, mimi naishi kwa raha zaidi, yaani kumbe nilikuwa nateseka bila kujua, maana  kazi zote unafanya yaani nakupenda sana kijana wangu sijui kwanini nilitaka kukufukuza" Mimi nikasema asante mjomba wangu. Mjomba akasema "mimi sioni kama kuna umuhimu wa kumfhata mke wangu, maana sahivi naona tunaishi vizuri tu bora akae kwao tu" Nikamwambia mjomba, msamee shangazi maana hata yeye ni binadamu lazima akosee, Mjomba akajibu "hatakutesa huyu" Kumbe shangazi alivyo kuwa kwao, ni kama alikuwa amepewa uhuru wa kufanya ngono kwa furaha zaidi na yule hawara yake, na kibaya zaidi shanganzi alipo fika kwao hakusema kama amefukuzwa! Alisema kwamba ameenda kuwasalimia wazazi wake.
Sasa siku moja jumapili shangazi aliaga kwamba anaenda kanisani kusali, kumbe alikuwa anaenda kuonana na hawara yake ili waende GUEST kufurahia maisha yao.  Ila kuna baadhi ya wanakijiji walimuona shangazi akitoka kufanya mambo machafu kwenye nyumba za wageni! Wakaenda kwa wazazi wa shangazi, kumwambia kuwa, "jirani, mtoto wenu yule, si ameisha olewa, sasa mbona tabia anazo fanya sio nzuri kabisaa, yaani anatembea na vijana wahuni wakati ni mke wa mtu aisee" Mama yake shangazi hakuamini alikhataa akasema, "mwanangu yupo kanisani anasali acheni kumsingizia" Shangazi alipo rudi nyumbani akamkuta mama yake amenuna sana. Na siku hiyo hiyo ndiyo mjomba aliamua kwenda kwa wazazi wa mke wake kumshitaki makosa yake yote aliyo mfanyia nyumbani.                   
Sasa kipindi mjomba amefika kwao mke wake, alikaribishwa ndani, wazazi wa shangazi walifurahi sana kumuona mjomba pale walijisikia vizuri sana! Mama mkewe wa mjomba, akaenda kumuita shangazi ali aje amuone mme wake sebreni, Shangazi alitetemeka mno kwa aibu, maana alidanganya kwao kuwa ame ruhusiwa na mme wake kuja kusalimia wazazi na hakusema ukweli kama waligombana kule nyumbani. kipindi mjomba anaendelea kusalimiana na wazazi wa shangazi, baba mkwe wa mjomba akasema, "kijana wangu wewe ni mtu mzuri sana, maana una mruhusu mke wako aje kututembelea wazazi wake, na unampa mda mwingi, mpaka hata sisi wazazi tuna furahi, wanaume wengine wakisha hoa bhana, ndiyo basi tena, kumuona binti yako inakuwa kwa tabu sana, na kama akija anakaa siku moja au mbili kisha anaondoka" Mjomba akashituka kidogo kisha akauliza "nini" Baba mkwe akashangaa ule mshituko akauliza nini, nini? Mbona sielewi mwanangu. Mjomba akasimama, wazazi wote wa shangazi wakaa kimya, shangazi pembeni alikuwa analia akimu konyeza mjomba asimuumbue makosa yake kwao. Baba mkwe akauliza, "binti yangu mbona sielewi, yaani wewe unalia, wakati nilizani umefurahi kumuona mmeo" Mama mkwe akadakia ", kuna nini au kuna mtu amefariki mnaogopa kutwambia" mjomba alimzalau sana mke wake akamwambia kwa sauti kubwa tu "yaani mke wangu nime kuruhusu uje nyumbani uwambie wazazi wako makosa uliyo fanya ili wakulekebishe kusudi usirudie makosa, kumbe ndiyo bado unawadanganya eti kwamba  nimekuruhusu uje kusalimia tu, kweli hapa sina mke nimepotea njia, hivi mbona hukua hivi umejifunzia wapi tabia hizi?" Baba mkwe akasema "kwani binti yetu alifanya kosa? Maana sisi amesema umemruhusu aje kutusalimia, na baada ya mda utakuja kumfhata" Mjomba akasema "mngemlea vizuri mtoto wenu asinge weza kukaa chini na kutunga barua ya kutongozwa, alafu ana msingizia mtoto wa dada yangu kuwa ndiye anamtaka kimapenzi" Wazazi waliona aibu, binti yao ana wa aibisha, mama mkwe akakumbuka kuwa kuna watu walikuja kumshtaki mtoto wao kuwa anaingia nyumba za wageni na wahuni. Hivyo akaamini kuwa kweli binti yake ni mkosaji.Wazazi walimuombea binti yao msamaa, hivyo mjomba akarudi nyumbani na mke wake, tukaanza maisha upya.
Mimi, mjomba wangu pamoja na shangazi, tuliishi maisha mazuri ya kupendana na ya kuheshiamiana sana, nilifurahi sana kuona shangazi akicheka pamoja na mimi hivyo nikawa na furaha pia. Ila cha kushangaza siku moja saa sita mchana mjomba akiwa hayupo, na mimi nikiwa chumbani kwangu. Mama Anna  rafiki mkubwa sana wa shangazi alikuja nyumbani.Mimi nilikuwa nimepumzika ila nilisikia kicheko sebreni,  yaani yule mama alicheka kwa nguvu akimwambia shangazi kwamba "hahahaha pole sana shoga yangu kwa yaliyo kukuta bibie, maana nasikia mmeo alikufukuza ukarudi kwenu" Shangazi akamjibu "dah asante rafiki, yaani nilifukuzwa kabisa kidogo tu nipoteze ndoa yangu" Mama Anna akajibu "dah niliyasikia mwenzio kwamba ulikamatwa na barua shoga"
Shangazi akasema "ndiyo yule hawara yangu si alinishauri nifanye vile, yaani niliumbuka sana ," Mama anna akasema "ehh kwahiyo unhataka kusema m'meisha achana na yule hawara yako, maana mimi hawara yangu bado ninaye,na huu mwaka wa tano! lakini mme wangu hajajua, na unamfahamu mme wangu alivyo mjanja" Shangazi akajibu "hapana hawara yangu sijamuacha, lakini naogopa kuonana nae, uwa nasubilia mme wangu akiondoka kwenda kazini ndiyo nampigia simu ili nimsalimie tu" Mama Anna akamjibu "dooh pole shosti lakini usiwe mjinga pangilia mda wako wa kuonana nae, bila mtu yoyote kujua, maisha mafupi sahivi huyo mzee wako sizani kama anakufikisha popote kwenye yale mambo yetu bibie"Nilimsikia shangazi akicheka kisha akajibu, "Mama Anna sio kwamba sipendi lakini, yule kijana ninae ishi nae hapa, mtoto wa marehemu wifi yangu, ni m'beya sana, anaweza kunisema kwa mme wangu, na sasa hivi nikifanya kosa, nadhani  ndoa yangu itakuwa imevunjika" Mama Anna akamwambia shangazi kwamba "sogea ni kwambie kitu"
Ndipo mama Anna akamwambia hicho kitu sikioni, mimi bahati mbaya sikumsikia kabisa, Kumbe alimwambia kwamba, kuna dawa akiniwekea mimi kwenye chakula nikila tu hicho chakula, sitaweza kuongea wala kusikia kwa mda wa mwaka mzima. Shangazi alivyo ambiwa kile kitu moyo wake ulikhataa akasema hawezi kunifanyia vile. Lakini mama Anna akamwambia "usiwe mjinga wewe hiyo sio sumu unamfanya aache umbea tu. Ndipo shangazi yangu akakubali ushauri wa mama anna.
Mama anna alimpa shangazi ile dawa, ili shangazi aniwekee iyo dawa kwenye chakula nikila tu, nisiweze kuongea wala kusikia chochote kwa mda wa mwaka mzima, Sitasahau ,,  siku moja nimeamka asubui, nikaenda kwenye chumba cha shangazi kumuomba nguo zake zote ili nimfulie nilipo fika nikagonga mlango wake, akafungua. Akaniuliza kwa uoga "mwanangu kwema" nikamjibi "salama shaganzi yangu, nimekuja kukuuliza kama unanguo chafu nikakufulie" Akajibu "asante sana mwanangu nguo chafu ninazo, ngoja nikutolee ili ufue" Shangazi alitoa nguo zote chafu siku hiyo, nikaziweka kwenye beseni kisha nikaenda nje kuzifua. Sasa kabla ya kufua, nilikuwa na tabia ya kukagua mifuko ya nguo, ili kama kuna hela au hata nyembe au sindano niweze kuzitoa ili zisinichome au hela zisilowane.Sasa wakati nakagua mifuko ya nguo za shangazi, nikakuta ile dawa ya kunitegea mimi ili nisiongee wala kusikia kwa mda wa mwaka mzima, kwenye gauni lake alilo kuwa analipenda sana, Na ile dawa ilikuwa imefungwa kwenye mfuko mdogo mweusi, Nilishtuka kuitazama lakini nikafungua hivyo hivyo tu, nilikuta dawa ya unga yenye langi nyeusi.
Moyo wangu ukasita nikajiuliza swali, "mhh inakuwaje shangazi anatembea na dawa kama hizi" Nikamfhata chumbani kwake na  kumwambia kwamba, "shangazi nimekuta hii dawa kwenye nguo zako" shangazi alishtuka sana kisha akasema " ohh asante kwa kuniletea, hii ni dawa yangu ya chunusi,na ni ya miti shamba naipenda sana" Yaani kumbe nilifanya kosa kubwa sana kumpelekea ile dawa, maana nilikuwa kama najiua mwenyewe. Ndipo shangazi akaitengeneza ile dawa kama alivyo elekezwa, sasa kipindi tuna kula chakula cha usiku mimi, mjomba pamoja na yeye, Shangazi alikuwa ameisha niwekea dawa kwenye chakula changu, Nilikula chakula bila wasiwasi nikijua kipo salama, kumbe nilikuwa naangamia.
Sasa kipindi naendelea kula kumbe dawa inaendelea kufanya kazi mwilini, baada ya mda kidogo mjomba akasema "Nelson mwanangu kesho jiandae kuna kazi nimekutafutia twende ukaanze kujifunza" Ila mjomba akaona kimya simjibu, akarudia kuongea tena, akaona kimya.Akazani kwamba nafanya makusudi, Kumbe mimi dawa imeisha ni haribu sisikii chochote. Mjomba akasema, unakibuli sikuizi ehh?
Mjomba wangu alihisi kwamba nina kiburi, eti kwamba nafanya makusudi kuto kumjibu maswali yake, kumbe mimi nilikuwa sisikii chochote, Ndipo mjomba akamuuliza mke wake,"vipi tena huyu mtoto yaani tuna mdekeza sana mpaka ameanza kutu dharau kiasi hichi, yaani ananikalia hata mimi kimya namna hii" Shangazi akamjibu "mme wangu bora wewe, mimi nikimtuma hhataki, nikimwambia afue nguo hhataki, kupika siku hizi hhataki, na mimi naogopa kukwambia maana utanifukuza kwako, utasema sipendi ndugu zako mme wangu, ila nashukuru mungu unajionea mwenyewe dharau zake ni bora umtafutie sehemu nyingine akae, mimi nibaki peke yangu tu maana sioni faida yake" Shangazi aliongea vile maana alitamani sana kubaki nyumbani mwenyewe, ili hawara yake awe anaingia kwa ulaisi mule ndani kipindi mjomba hayupo. Mjomba hakuamini kama kweli simjibu maana alishangaaa kwanini nisiongee.Ndipo mjomba akavua mkanda wake wa ngozi kisha akaanza kunichapa bila huruma, akisema, "yaani unakuwa mjinga hivi, mpaka unakhataa kunijibu mimi mjomba wako, ngoja nikutandike niku nyooshe tabia yako. "Mjomba alinipiga sana lakini alishangaa! akasema " mke wangu mbona mtoto namchapa, analia lakini sauti haimtoki, alafu cha kushangaza machozi yanamtoka sana lakini  hatoi sauti, labda anaumwa"

Shangazi akasema "wewe mme wangu Nelson humjui, akiwa na hasila anakaa kimya kama bubu "Mjomba akajibu "lakini kweli hichi ni kiburi, maana tangu tunazaliwa kwetu hakuna mtu yoyote mwenye ugonjwa wa kutokusikia na kukaa kimya hivi naionea kwa huyu" Mimi kila nilipo jaribu kuongea nilihisi mdomo wangu ni mzito sana, na nilihisi kama napasuka mdomo pale nitakapo jilazimisha kutoa sauti na niliphata maumivu nisiyo weza hata kuya elezea ,. Ilipo fika asubui mjomba akawa ameacha elfu 50 kisha akasema "mke wangu mpeleke huyo mtoto hospitari, maana amechemka mwili wake sana, labda anaumwa kweli"
Shangazi akajibu "sawa mme wangu" Ndipo mjomba akaenda kazini. Baada ya mda mchache mama Anna akawa amekuja nyumbani, akamwambia shangazi, "nilikwambia shosti hile dawa kiboko, ebu muone Nelson wako alivyo kuwa kama zezeta, Ebu Shoga mpigie hawara yako simu , aje haraka ili mfanye raha zenu tena mbele ya huyu mpuuzi wako Nelson, Mama Anna alipo mwambia shangazi kwamba amuite hawara yake wafanye mapenzi mbele ya macho yangu, shangazi akaogopa akasema,"shosti naona aibu kufanya ilo tendo mbele ya mtoto". Mama Anna akamjibu "weeh acha ushamba bwana, unaogopa nini, kwani Nelson ni mtoto, ebu jaribu kumvulia nguo uone shughuli yake, tena nipe simu yako nimpige hawara yako aje kama wewe unaogopa"
Kweli mama Anna akampigia simu yule hawara kisha akamwambia "shemu njoo kwa mpenzi wako, tupo wenyewe, bwege yake (mume wake) ameisha enda kazini" Baada ya mda mchache, hawara yake shangazi akawa amefika, Nilisikitika sana pale shangazi alipo mkumbatia na kuanza kumlegezea macho yule kijana, huku akisema "niliku miss sana mpenzi wangu" mda huo mama Anna akiwa ana cheka kwa furaha teletele. Hawara yake shangazi aliogopa sana, kisha akasema, "bebi hivi humu ogopi Nelson, si hatatusema kwa mme wako au sahivi ameisha acha umbeya" Shangazi akajibu "hapana baby, yaani hapo alipo asikii wala aongei! kwahiyo kuwa huru hawezi sema chochote" Ndipo shangazi na yule hawara yake wakaanza kuonganisha midomo yao huku wakipapasana mili yao! mbele ya macho yangu,  dah sema kweli niliumia sana mpaka machozi yakani toka. Mama Anna akasema "unalia nini m'beya wewe na mwaka huu utakoma".
Sasa Kipindi shangazi na yule mwanaume wake wame angushana kwenye sofa, mimi nilishikwa na aibu, nikhataka kutoka nje, dooh nilishangaa kuona mama Anna ananivuta mkono wangu, akafunga mlango akisema, "Nelson tafadhali usiondoke, maana wameisha nitia hamu na mimi naomba tulifanye tendo pia, wewe sio mtoto Nelson, tufanye kidogo" Maneno ya mama Anna nilikuwa siya sikii lakini jinsi alivyo kuwa ananipapasa mikono huku akilembua macho yake, nikajua anhataka kunibaka, Nilitikisa kichwa nikimaanisha  sitaki kufanya lile tendo, ila alianza kujishusha akionyesha ni jinsi gani yupo tayari tuvuane nguo za ndani, niliogopa mno nikahisi labda ana maradhi na anhataka kunipatia na mimi, Nilivyo angalia kwenye sofa nikashangaa kuona shangazi yangu , amejisahau kama mimi ni mtoto wake, maana alikuwa tayari ameisha achia maziwa yake wazi wazi. Huku na mama anna akiitaji pia. Shangazi alipo jisahau na kuanza kuachia maziwa yake wazi wazi, kiukweli ilinisikitisha sana mpaka nilitamani kutoka nje, lakini ubaya ni kwamba Mama Anna tayari alikuwa ameisha funga mlango kwa funguo, na kibaya zaidi akaweka funguo kwenye sidiria yake, hivyo nikaogopa kumshika maziwa yake ili nitoe funguo nikimbie.
Kipindi shangazi anaendelea kufanya ile dhambi ya kuzini, mimi ikanibidi nifumbe macho maana niliona aibu kabisa. Nilishukuru mungu maana baada ya dakika kadhaa, yule hawara aliona anacho fanya mbele yangu sio kizuri, ndipo akamnyanyua shangazi na kumpeleka chumbani kwa mjomba wangu. Nilijiuliza maswali mengi kichwani kwamba, "hivi huyu shangazi hata kama anachepuka, ndiyo afanyie upumbavu wake kwenye chumba cha mme wake" sikuphata jibu. Sasa kipindi nimebaki sebreni mimi pamoja na mama Anna, nikashangaa kuona bado anhataka mimi na yeye tukutane kimwili, niliogopa nikamwambia kwa ishara kwamba "Mama anna mimi nina umwa sina nguvu za kufanya hivyo vitu" lakini alikuwa haelewi ninacho mwambia, ndipo nikamshikisha mkono wake shingoni mwangu, ili asikie nilivyo chemka joto mwilini, na ilikuwa ni sababu ya zile dawa zao walizo nitegea nisiongee wala kusikia. Mama anna alikuwa sio muelewa kabisa, na kilicho kuwa kina muharibu zaidi yule mama ni pombe alizo kuwa anatumia, Nilishangaa kuona ana nilizamisha kufanya nae, Mama Anna akani sukuma kwenye sofa kisha akanipandia juu yangu, na wakati huo mimi sina hamu wala siitaji kufanya ule ujinga, aka anza kushika sehemu zangu nyeti akihisi hatanisisimua lakini Mungu alinilinda, sikukubali hata kidogo, akaanza kusema hatanipa pesa nikubali kufanya nae! lakini nikakhataa huku niki hitaji atoke juu yangu, ila mama wawatu akan'gan'gania hhataki kutoka.Sasa kipindi yule mama anhataka kunivua shati langu ili nibaki kifua wazi, mara ghafla geti kubwa la nje lika gongwa, dooh kumbe ni mjomba alikuwa amefika, ndipo mama Anna akaniachia kwa uoga, na mda huo mke wa mjomba na yule hawara yake wapo  chumbani kwa mjomba wanazini bila kujua kama mjomba amefika.Ndipo mama anna akanipa ufunguo nikamfungulie mjomba, yeye akakimbia chumbani kumwambia shangazi avae nguo haraka ili yule hawara asije kukutwa ugoni. Kipindi mama anna amekimbia chumbani kuwazuia shangazi na hawara yake wasiendelee kufanya lile tendo, na mimi pia nilikuwa nawai kwenda kumfungulia mjomba wangu mlango ili aweze kuingia ndani, Mama Anna akamuita na kumwambia shangazi kwamba,
"shosti, shosti (rafiki) tafadhali acheni msiendelee kufanya, mme wako amekuja tokeni chumbani haraka, maana huyo hawara wako leo hata fumwa ugoni" Lakini cha kushangaza mama anna hakujibiwa! maana shangazi na hawara yake walikuwa wamenogewa sana chumbani, kwa burudani walizo kuwa wana peana. Mda huo mimi nimeisha mfumgulia mjomba mlango, na alikuwa ana karibia kuingia ndani, bila kujua kama mke wake ameingiza mwanaume mwingine chumbani, tena kibaya zaidi kwenye kitanda chake, wakitumia mashuka yaleyale anayo tumia mjomba! Mama anna alivyo chungulia dirishani akaona mjomba anakaribia kufika  sebreni! dooh aliogopa sana, ndipo akaanza kugonga mlango kwa nguvu sana ili amnusuru rafiki yake, kusudi mme wake asigundue kama mke wake ni msaliti. Shangazi na mpenzi wake walishituka baada ya kusikia mlango unagongwa, ndipo wakaamka haraka haraka, kisha waka vaa nguo haraka, maana mlango ulikuwa unagongwa sana! hivyo wakahisi kuna kitu cha hhatari kwa nje. Sasa kipindi mjomba anafungua mlango wa kuingia sebreni, na ndicho kipindi shangazi na hawara yake walikuwa wameisha vaa na kutoka haraka chumbani, na kusimama sebreni ili mjomba asigundue.Mjomba alipo ingia sebreni akashangaa kumuona yule mwanaume, aka wasalimia wote ndani, kisha akamwambia mke wake kwamba "mke wangu naona leo tumephata wageni, lakini huyu wa kiume simjui" Shangazi akajibu kwa uoga na uchovu "mme wangu huyu kaka ni tumbo moja na mama anna" Mjomba akasema, " mke wangu mbona unaonekana umechoka sana, ebu tazama nywere zako zimevurugika sana, na  umetokwa jasho sana, wewe na huyu kaka yake mama anna, mlikuwa mnafanya kazi gani?" Shangazi akasema "hapana mme wangu leo kuna joto sana" Mjomba akasema "mbona awa wengine wapo sawa iweje wewe na huyu kijana ndiyo mnaonekana kuchoka kiasi hicho" Mjomba akamuuliza hawara yake shangazi, "kaka mbona hujafunga zipu yako" Kumbe alivyo vaa nguo haraka alisahau zipu, Mjomba akamwambia mke wake kwamba "mke wangu njoo chumbani tuongee kidogo"
Mjomba alipo muingiza chumbani mke wake akamuuliza kwamba, "mke wangu tafadhali, naomba unieleze ukweli, huyo kijana umemtoa wapi?" Shangazi akajibu "Mme wangu huyo kaka, ni ndugu yake mama Anna, alafu ni mshataharabu sana huyo kaka, usimuhisi vibaya mme wangu". Mjomba moyo wake ulikhataa kabisa kukubaliana na mke wake, na aliongea maneno hayo huku akiwa haja tazama kitandani kulivyo vurugika ovyo. Dooh! Alivyo tazama kitanda akakuta kimevurugika mashuka yako ovyo ovyo!
Akamuuliza mke wake kwamba "mke wangu inakuwaje leo mashuka yako ovyo hivyo, wakati kila siku nikija hapa mda wowote ule, nakuta umetandika kitanda vizuri na mashuka yamekunjwa vizuri. Au leo umelala sana, ila huwezi kulala mpaka sahivi maana nimekukuta na wageni mme simama sebreni". Mjomba alikasilika kisha akasema "basi sawa, kama kutandika kitanda hutaki, ngoja nitandike mwenyewe, maana sipendi uchafu humu ndani"Wakati mjomba anhatandika kitanda, bahati mbaya mkono wake wa kulia, ukagusa maji maji ya sehemu nyeti za yule hawara yake mama, maana zilidondoka kwenye mashuka wakati wanazini. Mjomba alishituka sana alipo shika uchafu wa hawara yake shangazi, akamuuliza mke wake kwamba "hizi nini kitandani kwangu, mke wangu" Shangazi alikuwa amegundua kuwa ni uchafu wa hawara yake, akakaa kimya  kwanza ili kusikilizia, Mjomba akasema "ina maana unaniletea wanaume chumbani kwangu sio?" Shangazi alivyo mjanja, akapiga chafya hapohapo, kisha akasema "hapana mme wangu najihisi kama nina mafua, ndiyo maana napiga chafya sana, sasa kipindi nimelala nazani mafua yali dondoka kwenye mashuka sababu ya chafya" Mjomba akashusha pumzi yake chini, maana alikuwa ameisha kasilika sana. Baada ya hapo shangazi akatoa mashuka haraka, kisha akhatandika kitanda chake vizuri kwa mashuka masafi. Mama anna pamoja na hawara yake shangazi yangu, waliondoka bila mjomba kujua mchezo wao mchafu walio ufanya. Sasa kipindi mama Anna anafika kwake akashangaa kukuta mme wake analia kama mtoto. Akamuuliza "baba Anna tatizo nini mbona unalia? au tumefiwa" Baba Anna akamjibu kwa uchungu sana, "mke wangu nime kukosea nini mimi, kwanini umeleta virusi vya ukimwi ndani, mke wangu sisi niwa athirika sasa hivi!" Mama Anna akasema, "Nini?" Mama Anna alisikitika sana maana alikuwa anaogopa sana ukimwi, aliinama chini uku machozi yakiwa yana mtoka ,. Baba Anna akasema "mke wangu tangia nimeku oa sijawai kutoka nje ya ndoa, na kabla ya ndoa tulipa virusi tuka kuta wote tupo sawa, na kama unavyo juwa mimi na kuwa bize sana na kazi siku chungi kila mda, ukimwi umeutoa wapi?" Mama Anna akasema "mme wangu mimi sijui, hata mimi nashangaa maana sijawai kutoka nje ya ndoa" Baba Anna akajibu "hapana siwezi kukuelewa na siwezi kukubali kuishi kwa matumaini, ebu nieleze mwanaume gani ulie tembea nae, hata kipindi mwanangu Anna ana karibia kuzaliwa tulipima wote virusi, tulikuwa sawa, umeutoa wapi ukimwi mke wangu, naomba unieleze ukweli ili nikusamee, maana nimepima hospitali kama tatu na zote nimepewa majibu yale yale kuwa nime athirika!"
Baba Anna aliendelea kumwambia mke wake "usipo nieleza ukweli, kachukue kila kilicho chako utoke kwangu"
Mama anna,"usifike uko mme wangu, nikirudi kwetu baba yangu ni mkali sana ana weza kuniua"
Baba anna,"haya sawa nieleze ukweli"
Ndipo mama Anna akaamua kusema ukweli ili anusuru ndoa yake,
Akamwambia kuwa "mme wangu naomba unisamee ni kweli shetani alinipitia, nikatoka nje ya ndoa"
Baba anna,"eti nini, kwanini sasa?"
Mama Anna,"mme wangu sio mimi ila ni huyo kijana alikuwa ana nitongoza kila mda, akinijaza uongo uongo mpaka nikashawishika"
Baba Anna,"sio wewe ni nani?"
Mama anna akajibu kuwa "nilijikuta nafanya hivyo sababu, mda mwingine nilipo itaji faraja ya ndoa, wewe ulikuwa umechoka sababu ya kuwa bize na kazi, hivyo nikajikuta naingia majaribuni"Baba Anna alishika kichwa chake jasho likamtoka, akalia kama mtoto, Kisha akamuuliza mke wake "huyo mwanaume ni wawapi?"Mama Anna akajibu kwa uoga sana "ni yule mpangaji wetu, yule dereva wa magari" Baba anna akasema "mke wangu umaraya ume uanza lini ,, yaani unatembea na vijana wadogo namna hii"
Mama anna akapiga magoti akisema "sitarudia mme wangu" Baba anna akasema "mjinga nini, sasa hata usipo rudia ndiyo ukimwi utapona,Ndipo baba Anna akatoka nje ya nyumba akiwa na hasira,akamuacha mkewe akiwa analia. Na mama anna akapiga simu kwa shangazi ili amuelezee,Mama alipo mpigia shangazi simu akamwambia, "shosti yangu nimekutwa na mhatatizo nyumbani kwangu, sijui nifanyeje"
Shangazi akamjibu "mhatatizo gani shoga yangu" Ndipo mama Anna akamuelezea jinsi alivyo ambiwa na mmewe. Dooh shangazi yangu alishtuka pia, kisha akamwambia, "shosti kesho njoo nyumbani, nazani mme wangu hatakuwa kazini ili twende hosptali, na mimi nikapime pia maana nimeisha ogopa pia" Mama Anna akamjibu "sawa nakuja twende wote na mimi nikapime pia niakikishe labda sina" Kweli walitumia pesa ambayo mjomba alimuachia shangazi ili mimi nipimwe maana nilikuwa sisiki wala kuongea, sasa wao wakatumia hiyo hela kwenda kupima ukimwi. Walivyo pima, bahati mbaya Mama Anna alikuwa ame athirika kweli, lakini shangazi yangu alikuwa salama. Mama anna alisikitika sana akampigia hawara yake simu hapo hapo akamuomba waachane. Mama Anna akasema "shosti naumia sana roho maana mtoto wangu bado ni mdogo, na sisi wazazi wake ni waathirika! je tutamlea mtoto kweli , mpaka akue na amalize masomo yake, au sisi ni watu wafu tutakufa mda wowote tu" Shangazi alimtia moyo rafiki yake ili asifikilie sana. Mama Anna akasema "yule kijana Nelson ana nyota nzuri sana ,, kumbe na yeye angekubali kufanya mapenzi na mimi angephata maambukizi pia"Walivyo ondoka kutoka hospitali, mama anna alipo rudi kwake akakuta mme wake amemtolea mabegi yake yote nje akamwambia "naomba utoke kwangu, sikutaki mwanamke kahaba wewe, ondoka na usirudi hapa" Mama anna aliona dunia yote chungu kwake, akampigia shangazi simu ili amsaidie ila shangazi akasema "mme wangu hata nigombeza sana hivyo tafuta sehemu nyingine shosti" Alipo enda kwa hawara yake alie muambukiza virusi vya ukimwi, akakuta amejichoma kisu shingoni, eti kwasababu baba anna alimtishia kumuua. mama anna alitamani kurudi kwao lakini aliogopa  maana wazazi wake walikuwa wakali sana, Ndipo akampigia simu hawara yake shangazi, alipo pokea simu akamwambia hivi "Shemeji naomba nije kwako nikae japo week moja maana mme wangu ameuza nyumba alafu amekimbia na mtoto"Ndipo yule hawara yake shangazi akamkalibisha kwa roho moja akijua kuwa shemeji yake amepatwa kweli na mhatatizo. Mama anna alipo fika kwa hawara yake shangazi yangu, aliingiza mizigo yake ndani na kukaa kwenye kiti, Hawara yake shangazi akamuuliza "shemeji unajua bado sijaamini kwamba mme wako ameuza nyumba na kukimbia bila kukuaga, tena kibaya zaidi amekimbia na mtoto wako."Mama anna akamjibu "nikweli shemu ameuza nyumba na kunitelekeza yaani sina mbele wala nyumba, na nimemuomba msaada mpenzi wako amekhataa anasema mme wake hatamgombeza, kwahiyo naomba usimwambie kama umeni hifadhi hapa kwako, hii iwe siri yangu mimi na wewe" Hawara yake mama alishangaa sana ila hakuwa na jinsi ikabidi avumilie tu. Kumbe mama Anna shida yake kubwa alitaka kufanya mapenzi na hawara yake shangazi, ili na shangazi aweze kuphata maambukizi ya virusi vya ukimwi, maana aliumia kuona yeye amephata virusi alafu shangazi hana, sasa akaona njia bora ya kumpatia mwezake  ukimwi ni kufanya mapenzi na hawara yake,  kisha hawara akienda kwa shangazi wakifanya mapenzi na shangazi, apate ukimwi pia. "Kweli marafiki wengine ni sumu" Sasa ilipo fika usiku kipindi mama anna yupo mule ndani kwa hawara yake shangazi, Mama anna aliandaliwa maji ya kuogoa, akaoga na kuwa tayari kwa ajili ya kulala, mama anna alipo lala kitandani, Hawara yake shangazi akalala kwenye kiti chake, maana alikuwa na chumba kimoja tu yule kaka.
Mama anna akamwambia "shemeji , mbona unalala mbali, njoo tulale wote kitandani, hakuna kitakacho haribika" Shemeji, "hapana usijali wewe lala kitandani mimi hapa pananitosha tu" Mama anna alivyo ona vile akaamka kutoka kitandani kisha akhatandika kitenge chake na kulala chini akijifanya na yeye amezila kitanda, shemeji yake akamuonea huruma akasema, "basi njoo tulale wote kitandani" Kipindi wamelala mama anna akaanza kumuangalia sana shemeji yake ili amuingize majaribuni ,, na shemeji roho yake ilikuwa ina msuta sana maana alihisi labda shangazi amemtuma rafiki yake aangalie msimamo wake kwake. Mama anna alivyo ona shem wake amekausha kitandani, akamka na kusema "shemeji zima taa maana nhataka kuvua nguo zote kuna joto" Shemu akasema "hapana shemu usivue nguo nakuomba jikaze hivyo hivyo shemu" Ila mama anna alivua nguo zote , kisha akaweka paja lake juu ya mwili wa shemeji yake.                    
 Hawara yake shangazi alivyo wekewa paja juu ya mwili wake, hisia zilimpanda sana hivyo akaanza kukhataa kishingo upande, "sitaki nhataka",maana lile paja la shemeji yake lilikuwa limemvutia sana kaka wawatu ,. Mama anna akasema "naitaji kuphata furaha anayo iphata rafiki yangu, maana hatuwezi kulala wote alafu nikaichezea bahati, wakati rafiki yangu kila siku anakusifia kwamba unaweza sana hichi kitu hivyo naomba unionjeshe pia usiku wa leo" Mama anna alikuwa na roho ya kutu ,, alifanya vile makusudi ili asife mwenyewe na lile gonjwa Kaka wawatu alivyo sifiwa, akajikuta anaanza kusema "shemeji nimekubali kufanya ila mwenzako asijue maana nimetoka nae mbali mimi"
Mama anna akasema "hapana bebi wangu, hawezi kujua chochote na hawezi kujua kama nipo hapa, ukiwa nae mpe raha za kutosha afurahi kweli kweli na mimi pia unipe kiasi changu, wewe bado kijana bebi damu yako changa" Shemeji akamwambia mama anna kwamba,"ngoja nichukue kinga kwenye droo yangu tufanye basi" mama anna akaguna kwa hasila, "etii nini, Kwahiyo uniamini sio unazani mimi ni mwasilika ama?" Shemeji akasema "haya basi nisamee shemu" Kweli mama anna alipanda juu ya mwili wa shemeji yake, kisha wakagusanisha vinywa vyao na kuanza kupapasana sehemu husika za mili yao, nguo zilitupwa pembeni kisha wakaianza shughuri ki sawa sawa! Dah siku hiyo hiyo hawara yake mama akawa amephata maambukizi ya virusi vya ukimwi pia.Walipo maliza mambo yao, Mama anna akamwambia shemeji yake kwamba "Bebi asante sana, umenifurahisha sana kwa ushirikiano wako, maana nimejisikia mulemule, na sijui kwanini sikuwai mapema"
Shemeji akasema,"sema kweli hata mimi nimefurahi sana maana unaweza sana kumzidi hata rafiki yao, yaani yule analala kama mti, hawezi kabisa sababu haonyeshi ushirikiano, lakini wewe shughuri yako sio ya kitoto upo vizuri shemu" Mama anna akacheka kisha akamwambia "mfundishe mwenzio, lakini kuwa makini mume wake akijua umeisha" Siku moja jioni nilihisi naumwa sana  kichwa, hivyo nikaenda kumuomba shangazi elfu moja tu ya dawa, dooh akaninyima, na kusema kwamba "sina hela mimi" Kipindi natoka nje nafika mlangoni tu akapokea simu ya hawara yake akiombwa elfu 60, shangazi akamwambia nakutumia mpenzi wangu.                       
Hali yangu ya kutokusikia wala kuongea nilikuwa tayari nimeisha izoea, lakini nilikuwa bado nina uwezo wa kuhisi mtu anacho kiongea na kukisema sanasana  ninapo mtazama akiwa anaongea, hivyo kitendo cha shangazi kumtumia hawara yake elfu 60 na kuninyima mimi elfumoja ya kununua dawa, kili niumiza sana roho, lakini sikuwa na jinsi hivyo nikaamua kujikaza hivyo hivyo tu. Kumbe zile pesa ambazo shangazi alikuwa anatuma ndizo hizo hizo ambazo zilikuwa zinatumika kumpendezesha mama Anna. Siku moja hawara yake shangazi alimpigia Shangazi akasema, "bebi mbona siku hizi unanipa pesa kidogo ,, wakati mme wako anakuachia pesa za kutosha za matumizi, nipe pesa pia mpenzi wangu ili nipendeze nivutie ili hata nikioneka mtaani niwe mtanashati". kumbe hayo maneno alikuwa anaambiwa na mama anna ili waendelee kumlia shangazi pesa zake. Shangazi akamjibu hawara yake wamba "mpenzi wangu , sio kwamba nakubania hela ila sahivi mme wangu anaacha pesa kidogo ndani, nashindwa nifanye vipi ili nikupe hela za kutosha, na ndiyo maana namshindisha njaa huyu mtoto wa marehemu wifi yangu ili pesa nikupe wewe" Yule hawara akamwambia shangazi kwamba aibe pesa ya mume wake kisha wanisingizie kwamba mimi ndiyo nimeiba hiyo pesa. Kweli walichukua ufunguo wa chumba cha mjomba, kisha wakaenda kuuchongesha zikawa funguo mbili, sasa ufunguo mmoja wakauweka chini ya mto wangu ninao lalia, kisha shangazi akabaki na funguo moja tu. Kweli , kutokana na shangazi kumpenda sana hawara yake, akachukua laki tatu za mme wake chumbani kisha akampatia hawara ili akanunue nguo na kwa ajili ya starehe zake zingine. Mjomba alipo rudi akakuta pesa zake hamna  akauliza "nani amechukua pesa zangu ndani".
Shangazi akasema hajachukua pesa, wakaja wote chumbani kwangu kuniuliza kama nimechukua, nika khataa kabisa kuwa sijaona hizo hela, mjomba akasema "Mke wangu sio mwizi na hajawai kuchukua pesa bila kuniambia, Sasa pesa zimeenda wapi" Ndipo mjomba akamwambia shangazi ebu mkague Nelson labda ameificha, Dooh shangazi akaenda kwenye ule mto kisha akatoa ufunguo aliyo iweka, kisha. Akamwambia mme wake kwamba "mbona huu funguo kama wa chumba chetu, au amechongesha funguo bandia ili awe anatuibia hela zetu" Mjomba alipo onyeshwa ufunguo na shangazi kwamba mimi nime uchongesha huo ufunguo ili niwe naiba pesa zao alikasilika sana ,. Akasema "mtoto wangu yaani ndiyo umefikia hatua hii ya ujambazi, yaani unatengeneza ufunguo ili uniibie, kumbe ndiyo maana nakutafutia kazi hutaki, unajifanya eti unaumwa usikii wala kuongea! kumbe nia yako ni wizi sio uniibie tu, haya sawa umeniibia pesa za ofisini unhataka nifukuzwe kazi, utakula nini ndani, utavaa vipi, nakuuliza wewe jambazi sugu nijibu?" Yale maneno ya mjomba sikuyaelewa  vizuri maana aliongea sana na mimi kwa ugonjwa wangu wa kutokusikia, sikuweza kumuelewa, maana mimi nilikuwa naelewa kwa kumtazama mtu anavyo ongea kwa utaratibu, kisha namjibu kwa ishara Mjomba akasema "nakuuliza unakaa kimya sio, unajifanya kiziwi eti bubu kumbe jambazi ulie shindikana" Shangazi akacheka nakusema kwamba, "mme wangu huyu hatatufilisi kabisa, na hatatuibia hata vitu vya ndani, na siku izi vyombo vyangu vinapotea sana! kumbe tunaishi na mwizi ndani, na hata kuwa anaiba kisha anauza vitu,  bora aondoke asituletee balaa ndani" Mjomba akasema "Nelson, tunaongea wewe unakaa kimya sio,  kwanza hatuamini kama kweli husikii maana tumeisha kujua ujanja wako hapa ndani, sasa leo utaongea tu, mke wangu niletee fimbo nzuri hapo nje" Shangazi alikimbia kufhata fimbo kwa furaha akitamani nipigwe kama punda, kibaya zaidi akaleta mwiko wa kusongea ugali ili nipigwe nao.
Mjomba kwa hasila ya kuibiwa akanipiga na ule mwiko mgongoni! Nilishikwa na hasila maana shangazi alikuwa na furaha nilijilazimisha kuongea, sauti ikagoma kutoka, nikajilazimisha zaidi damu zikaanza kunitoka machoni, niliendelea kulazimisha zaidi kumjibu, damu zikanitoka masikioni pia, nilizidiwa nguvu nikachemka mwili mzima, kipindi hicho mjomba na shangazi wameshikwa na butwaa, ndipo kwa hasila nikachukua  mwiko nikaun'ghata kwa hasila mpaka nikapoteza jino langu la mbele. Kutokana na kusingiziwa hasila hazikuisha maana nilishindwa kujitetea ndipo nikaanza kujigonga kichwa changu ukutani ili nife niachane na mateso ya dunia, mjomba akaanza kusema "mwanangu usijigonge hivyo utakufa" Baada ya kujigonga sana kichwa nikaanguka chini na kuzilai hapo hapo. Wakazani nimekufa! Nilipo zimia, shangazi alifurahi akajua tayari nimefariki,mjomba akasema ", mtoto wa dada angu amekufa" Alianza kulia maana alikuwa ananitegemea sana mimi, sababu hakubahatika kuwa na mtoto ,, Mjomba akasema, "mimi nahisi tumemuonea hajaiba yeye hela, maana asingeweza kujidunda kichwa chake vile, angalia ametoka hadi jino lake, na itakuwa kweli hawezi kuongea hivyo ameshindwa kujitetea kutokana na hasila za kupigwa bila kosa zimemfanya ajidunde, tumpeleke hospital labda mwanangu hajafa"Shangazi akajibu "mme wangu huyu kijana ameisha jiua tayari, tukimpeleka hospital tutakuwa tuna poteza pesa bure ni bora uwapigie ndugu na jamaa simu ili waje kwa ajili ya mazishi. Mjomba alikuwa tayari ameisha changanyikiwa akasema "sawa mke wangu"Ndipo akampigia simu zephania ili aje kumsaidia swala zima la mazishi, Zephania alipo fika akauliza tatizo lilitokea, mjomba akamjibu kuwa wamenikuta na ufunguo bandia wa chumba chao na nimeiba hela, hivyo walipo nipiga na mwiko nikajidundisha kichwa ukutani na kujitoa jino.
Zephania akasema "rafiki yangu we ni mpuuzi sana, kiukweli hauna akili, kwani huyu mtoto chumba chake uwa anakifunga?" Mjomba akasema hapana kinakaa wazi mda wote. Zephania akamwambia "sasa kama chumba kinakaa wazi kwani mtu hawezi kuiba hela na kumtegea huyu kijana ufunguo ili kesi imuangukie yeye, alafu rafiki yangu huyu ni mtoto wa dada yako lakini humjali kabisa miezi mingi imepita kijana haongei wala kusikia nyie mnampiga na kumnyanyasa ndani, kwanini humpige wakati unajua ni bubu kwa sasa hivi na awezi kujitetea"
Mjomba aliogopa akasema nisamee rafiki yangu ni hasila tu ,. Shangazi akasema "hivi wewe shemu unaposema kuwa anaweza kutegewa ufunguo bandia, kwahiyo unamaanisha mimi ndiyo nimefanya hivyo sio, kwahiyo mimi ni jambazi siku hizi, yaani nilete ujambazi mpaka kwenye pesa za mme wangu" Zephania hakumjibu chochote akainama pale chini nilipo dondoka akanishika mkono wangu na kushika kifua changu akasikia mapiga ya moyo bado yanagonga akasema "kweli hii familia niya kipuuzi aki ya mungu. yaani mnamuita Nelson marehemu wakati hajafa amezimia tu, hivi mnaakili nyie" Mjomba na shangazi wakashikwa na butwaa, ndipo wakanipeleka hospitali.Nilifikishwa hospitali nikiwa hoi, niliingizwa chumba cha matibabu, huku mjomba wangu pamoja na zephania wakiwa nje wana subilia kuona kama naweza kuphata nafuu. Baada ya mda daktari akatoka chumba nilicho kuwemo, na kwenda ofisini kwake, kisha akawaita zephania pamoja na mjomba ili waingie ofisini waweze kuongea. Daktari akasema, "ndugu zangu hali ya mgonjwa ni mbaya sana ,, hivi nani amembonda kichwa chake vile?"
Mjomba akajibu "huyo mtoto ni wa dada yangu mimi, sasa jana nimeibiwa pesa ndani kwangu na nilipo enda kumkagua yeye nikakuta ana ufunguo wa bandia chumbani kwake hivyo nikamchapa na mwiko! ndipo akaanza kujigonga ukutani kwa nguvu sana sababu ya hasila" Daktari akamjibu kuwa "huyu kijana tumempima vizuri kabisa, na tumekuta ana sumu kali mno kichwani mwake, na  ile sumu imeua sehemu za kumfanya mtu kuongea na kusikia, sasa kibaya zaidi sumu imetapakaa kichwani mwake,  na amefanya vibaya kubonda kichwa chake kwa nguvu maana tayari sumu imemzunguka hivyo damu zinaweza kurudi kwenye ubongo. Sasa sisi hapa niseme ukweli hatutaweza kumtibu na ili apone itabidi apelekwe INDIA ili akapate matibabu mazuri, na mkichelewa ndani ya siku tano huyo kijana wenu Nelson hatafariki na mtampoteza kijana bado mdogo sana" Mjomba alitetemeka mwili mzima akauliza "daktari gharama yake ni kama shingapi?" Daktari alimjibu,"nendeni mkaandae millioni 11, kisha mtakuja niwaandike barua ya uamisho ili kijana akatibiwe mapema kabla ya siku tano, maana damu yake inapanda kidogo kidogo kwenye ubongo, na damu ikigusa kwenye ubongo Nelson anakufa."Mjomba pamoja na zephania hawakuwa na hiyo pesa ,, walijitahidi kukopa kwa marafiki lakini hawakufanikisha, zephania akaphata wazo la kwenda kuomba msaada kupitia Radio na TV lakini waliphata millioni tatu tu, hivyo isingeweza kusaidia kabisa.
Siku ya kwanza ikaisha, nikawa nimebakiza siku nne ili nife, siku ya pili ikawa imeisha bila mafanikio yoyote ya kwenda India, hivyo nikabakiza siku tatu nipoteze maisha, siku ya tatu ilipo isha nikawa nimebaki na siku mbili tu za kuishi duniani, siku ya nne ilipo isha ndipo nikajua lazima nife, hivyo shangazi akaanza kupigia watu simu kuwa, "kesho Nelson anakufa njooni kwangu" Shangazi alipigia watu wengi simu na kweli walijazana pale nyumbani, kwamba mimi nitakufa kesho, na ile pesa millioni tatu waliyo kusanya kupitia radio na tv zilitumika kwa ajili ya chakula na maji kwenye huo msiba wangu.Ilipo fika usiku wa mwisho kwangu ambao mimi nilitakiwa kufa, nilianza kusikia maumivu makali katika mwili niliumia sana, nilijigalagaza kwa uchungu ,, nikaanguka kutoka kitandani mpaka chini, kichwa changu kilikuwa kinagonga sana zaidi ya kawaida, ndipo mapovu yakaanza kunitoka mdomoni pia, hakuna Nesi wala Daktari alie nisikia maana wote walikuwa wamepitiwa na usingizi, nilitamani kupiga kelele ili nipewe japo maji ya kunywa kwa mara ya mwisho ila sauti ilikuwa haitoki, miguu yangu ilianza kuwa migumu ikakaza pamoja na mikono, kisha jicho likawa kubwa nikakodoa sana macho, kipindi naanza kujisikia kama nakufa humo chumbani, mzimu wa marehemu mama yangu ukanitokea hapo hapo, ukaniambia "mwanangu, mwanangu haufi, hata mungu hajapenda ufe, dawa yako hii hapa tafuna mwanangu utapona"
Mzimu wa mama ulinipatia mhatawi ya mpaipai! kwamba nikitafuna tawi napona vizuri kabisa. Sasa tatizo mikono yangu na miguu ilikuwa imekaza sana siwezi kuikunja wala kuikunjua, ndipo mzimu wa marehemu mama yangu "ukhatafuna yale mhatawi na kunilisha mimi kama njiwa ananvyo lisha kinda lake! Yale majani yalikuwa machungu sana na yalipo ingia mwilini nilijihisi nimephata nguvu sana na nimekuwa na afya nzuri sana huwezi amini, yaani nilijihisi mpya katika mwili wangu, baada ya mzimu wa mama kuona nimeamka na kusimama ukapotea hapo hapo. Lakini tatizo la kusikia na kuongea nikawa bado sijapona.
Nilirudi kitandani kulala kipindi watu wa mochwali wamekuja kuuchukua mwili wangu wakakuta nacheka tu. Ndipo nikaamua kurudi nyumbani peke yangu.Nilishangaa sana kukuta watu wanalia, mjomba analia sana, watu wanakula wali na maji eti kwamba mimi nimefariki, dahh kweli duniani kuna watu wanafurahia pale unapo patwa na mhatatizo.Nilipo fika vizuri nyumbani, watu wote wakakimbia, wakiniogopa eti kwamba mimi nilikufa hivyo nimefufuka tena. Shangazi aliumia kuniona sijafa, akasema toka kwangu we mzimu umefhata nini hapa, mjomba akasema mtoto hajafa bado usimfukuze mke wangu, Shangazi aliumia sana kuona sijafa, ndipo kwa aibu akawapigia watu alio waita waje kwenye msiba, akiwambia kwamba, ", naombeni mnisamee, tuliambiwa na daktari kuwa lazima afe ndio maana nikawaita mapema msibani, tunashangaa amepona tena" Mjomba akampigia zephania ili aje kuniona kuwa mimi sijafa, zephania hakuamini hata kidogo, ndipo akamtaarifu mkewe ili waje kunitazama kama kweli sijafa, kipindi zephania na mke wake wapo njiani wanakuja kwetu ili waniangalie, bahati mbaya wakaphata ajali mbaya sana njiani! maana gari lao liligongwa na gari kubwa, hivyo yeye pamoja na mke wake wakafariki hapo hapo. sasa msiba baada ya kuwa wangu ukawa wa zephania na mkewe.

Mjomba alipo pigiwa simu kuwa rafiki yake amefariki hakuamini kabisa, ndipo akajiandaa haraka haraka kwenda kwa zephania hivyo akaniacha mimi na mke wake pale nyumbani.Shangazi alijisikia vizuri sana baada ya kusikia zephania amefariki, maana alikuwa anamchukia sana zephania eti anambana mambo yake sana.Hivyo shangazi hakutaka hata kwenda kwenye msiba. Alivyo muona mme wake ameenda kwenye msiba ndipo akampigia hawara yake simu na kumwambia kwamba "bebi wangu nimekumiss sana mimi, leo nipo mwenyewe mpenzi njoo tuwe pamoja" Yule hawara akamwambia Mama anna, "rafiki yako ameniita kwake vipi niende" mama anna alitamani sana shangazi yangu apate virusi vya ukimwi pia, hivyo akamuruhusu hawara aje nyumbani. Hawara yake shangazi alipo fika sebreni nikashangaa kuona shangazi ananiambia nitoke nje nioshe sahani zote ambazo watu walilia wali msibani, sasa kipindi nipo naosha vyombo kumbe shangazi amevua nguo zake zote anafanya mapenzi sebreni. kipindi naendelea kuosha vyomba mama ake mzazi shangazi alikuwa amekuja nyumbani, hivyo alipo fika akaenda moja moja mpaka sebreni.Mama wawatu alishangaa sana kumfumania binti yake anafanya mapenzi na yule kijana , akasema, "Haaa! mwanangu yaani nimekufhata ili twende kwa mchungaji JOSHUA ili akuombee upate mimba japo mtoto mmoja, kumbe wewe unalala na hawa vijana wahuni wa mtaani, mbona unanivua nguo binti yangu, kumbe ndiyo maana hupati hata ujauzito kumbe una laana hivi, yaani tena kwa zalau unafanya huu uchafu kwenye nyumba ya mme wako hivi una akili kweli?" Mama yake shangazi alimshangaa mtoto wake akaendelea kusema "mwanangu yaani kwa hichi kitendo nilicho kiona, nakuonea hadi aibu sijui shetani gani kakukuta" Shangazi aliinama chini kwa aibu isiyo pimika akasema "nisamee mama yangu sitarudia", mama yake akasema, "kumbe kila siku unatupigia simu kwamba huyu Nelson ni mbaya, we muongo, huyu kijana hana kosa lolote, kama kweli una heshima uwezi kumpa vyombo vingi vile aoshe mwenyewe alafu wewe unafanyia upuuzi wako hapa sebreni, huna hata aibu bora ungeenda hata bafuni ujifiche asijue, yaani mwanangu ilo pepo baya nakwambia, nikimwambia baba yako,au nikimwambia mme wako utasema nini, juzi juzi tu umetoka nyumbani amekusamee ugomvi kumbe ni kweli unamfanyia hivi mbona huu ni zaidi ya uchawi, mi mwenyewe tangia baba yako amenioa sijawai kufanya hichi kitu"
Shangazi akasema "mama mimi sipendi kufanya hivi ila kwenye ndoa kuna mhatatizo mengi mama" Mama yake akamuuliza "mhatatizo yapi sasa" Shangazi akajibu "mimi kwa mme wangu siliziki kabisa tukicheza mechi, ndiyo maana nashawishika kufanya hivi mama yangu." Mama yake shangazi akamwambia hawara yake shangazi kuwa "we kijana ebu vaa nguo, zako" yule kaka akavaa ila akasahau kufunga zipu. Nama akamuuliza, "kijana kwanini unaniharibia mtoto wangu lakini" Hawara akasema "nisamee mama sijafanya makusudi tumepitiwa tu" Yule mama alianza kulia kama mtoto akasema mwanangu umeonyesha picha mbaya sana siwezi kuamini bado, yaani we mtoto wangu ni maraya sana" Shangazi akasema "mama usilie sirudii aki ya mungu", Yule mama akakasilika sana akasema "yaani nyie hata kinga hamtumii sijui mnajiamini vipi, hivi yule mme wako akiphata maradhi utafaidi nini sasa mwanangu, yaani yeye anakuheshimu anhatafuta pesa ila wewe unafanya mambo haya."
Dooh sasa Kipindi wapo sebreni wakiwa katika majonzi mjomba akawa amewasili kutoka msibani, alipo fika akashangaa kumuona mama mkwe wake akamuuliza, "mama naona umekuja bila taarifa tatizo nini" Mama ake shangazi akaanza kulia,  mjomba akauliza, "kuna nini tena", shangazi akasema "mme wangu mama anaumwa kichwa sana" Ndipo mjomba akamuuliza ma mkwe wake kwamba "mama ni kweli unaumwa kichwa" Yule mama akasema "ndiyo mwanangu naumwa"                    
Mama yake shangazi aliona aibu sana kusema fumanizi alilo mfuma binti yake, maana alijua mkwe wake hataumia sana na anaweza kumtimua binti yake hivyo akasema anaumwa ili mjomba asigundue kinacho endelea. Sasa kibaya zaidi kwa jinsi yule kijana alivyo fanya mapenzi na shangazi, bahati mbaya shangazi yangu pia akaphata maambukizi ya virusi vya ukimwi ,, bila mjomba kugundua kama mke wake kaisha athirika tayari. Mjomba alipatwa na wasiwasi akasema "mama ni kweli unaumwa kichwa mbona siamini, na hivi kwanini kila nikija nikamkuta huyo kijana hapa lazima nikute hampo sawa, nakuta mna mawazo hamjakaa kwenye viti tatizo nini" Yule hawara akasema "hapana shemeji, nilikuwa nimemletea taarifa mke wako kuwa mama Anna anaumwa"
Mjomba akamuuliza "kwahiyo kama unaleta taarifa ndiyo usifunge zipu" Yule hawara akashtuka alipo gundua hajafunga zipu ndipo akafunga hapo hapo.Mjomba akamwambia "kwanzia leo nakuomba usikanyage kwangu nikikukuta utaniona mbaya" Mama yake shangazi aliomba aondoke maana hakuwa na hamu tena na binti yake, Na yule mama alikuwa na ugonjwa wa mshtuko, hivyo alikuwa hapendi kuona mhatatizo kama yale. Mimi nilipo maliza kuosha vyomba vyote nikaenda moja kwa moja mpaka kwenye msiba wa zephania, dah niliumia sana kumtazama zephania kwenye jeneza maana nyuso zao na mke wake zilikuwa hazitambuliki kabisa sababu ya ile ajali ya gari. Shangazi alikhataa kuja kwenye msiba eti anajifanya analia kwamba mama yake mzazi anaumwa, hivyo mjomba akasema, "pumzika mke wangu ukiphata nafuu njoo tuwazike, maana wale walikuwa watu wetu wa karibu sana" Hawara yake shangazi aliondoka kwa uoga sana ,. Kipindi mama yake shangazi amefika nyumbani kwake, wakati amekaa chini anhataka kumuelezea mme wake yaliyo mkuta kwa binti yake, mapigo ya moyo ya mama yake shangazi, yakaanza kwenda kasi na hakuweza kuongea chochote zaidi ya kusema, "binti yangu umeniua "baba yake shangazi yaani "babu" akamuuliza, "mke wangu tatizo nini"Kumbe yule bibi alikuwaameumia sana kile kitendo cha mwanae na kilimfanya mpaka yeye kuphata mshtuko mkubwa sana mwilini.Huwezi amini Mama yake shangazi alifariki usiku huo huo kwa mshtuko  , huku akisema "binti yangu umeniua”. Baada ya mama yake shangazi kufariki, mda huohuo baba yake shangazi akapiga simu kwa mjomba akamwambia kwamba, "mke wangu amefariki ghafla, baada ya kutoka kwenu, yaani alipo fika kakaa kidogo tu akafa, huku akisema binti yake ndiyo amemuua m'memfanya nini mke wangu?" Mjomba akashangaa sana akasema "binti yake hajamfanya kitu chochote mama mkwe, maana nilimkuta mama mkwe analia sana sebreni na nilipo muuliza akasema anaumwa kichwa tu, sasa sielewi kama alisema ukweli au alinidanganya tu" Ikabidi mjomba aache msiba wa rafiki yake zephania, akajiandaa na mke wake ili waende kwenye msiba wa mama mkwe wake" walipo fika kwa baba mkwe, wakati wanaingia ndani baba yake shangazi alikasilika sana kumuona binti yake kasema "sitaki kukuona kwangu ondoka kwangu, yaani wewe umemfanya mama yako kitu kibaya mpaka amekufa amekutaja kuwa wewe ndiye umemuua. naomba toka kwangu na usirudi tena hapa, kakae na mme wako huko" Shangazi aliona aibu sana , maana hakuna hata mmoja alie kuwa anamtetea, na kibaya zaidi aliandaa msiba wa wangu kumbe alikuwa anamuandalia mama yake afe, Dooh kweli usimuombee kwenzako mabaya. Maana shangazi alitamani mimi nife ila  sikufa! na kibaya zaidi shangazi akampoteza mama yake mzazi. Mjomba wangu alikonda sana , maana aliandamwa na mhatatizo mengi, na aliumia sana kuona rafiki yake zephania amefariki pamoja na mke wake. Sasa huku upande mwingine kwa Baba Anna alishindwa kuvumilia kukaa peke yake, maana Anna alikuwa mtoto wa kike hivyo alishindwa kumlea peke yake, ndipo baba Anna akaanza kumtafuta mke wake ili arudi nyumbani waishi hivyo hivyo. Kweli baada ya mama Anna kuitwa alirudi kwa mme wake na wakaanza maisha mapya. Hawara yake mama aliumia sana kuona mama anna ameondoka kwasababu alikuwa anampenda na amemzoea. Ila mama Anna akamuahidi kuwa hatarudi tena. Sasa kutokana na mhatatizo yaliyo kuwa yamemkuta mjomba wangu, ya mimi kuumwa, ile misiba miwili, wa zephania pamoja na wa mama mkwe wake, hivyo mjomba wangu akawa hajauzulia kazini kwao kwa mda mrefu sana, na kibaya zaidi mjomba akawa hajarudisha ile laki tatu iliyo ibiwa ndani, Dooh ndipo mjomba akawa amefukuzwa kazi ofisini! Shangazi aliona dunia chungu ,! Baada ya mjomba kufukuzwa kazi maisha yalianza kuwa magumu kwenye familia, maana pesa zilikhata kabisa. Shangazi akaanza kulala milalamika kila mda, maana tulianza kula mlo mmoja tu jioni, shangazi akasema, "mme wangu mimi haya maisha siyawezi sijazoea kushinda njaa, yaani tunakula mara moja kwa siku, maisha gani haya" Mjomba akamjibu, "mke wangu katika ndoa kuna shida na raha, kama jana tuliphata, leo tunaweza kukosa, sasa wewe ukishindwa kuvumilia unakuwa unaonyesha picha mbaya, sasa mimi pesa nitoe wapi wakati umeona mwenyewe barua ya offisini kwamba sina kazi tena yaani wameisha nitimua" Shangazi alilalamika sana maana aliona mme wake anakaa ndani mda mwingi anashindwa kufanya uchafu wake, na anakosa pia pesa na kumuhonga hawara yake. Mjomba aliendelea kumwambia mke wake kwamba "wewe kuwa mvumilivu mke wangu kuna kazi ya kujenga naitafuta nikifanikisha nitaenda kuchakalika na tutaphata pesa pesa ya kula, kama unavyo jua mimi sijasoma na ile kazi nili bahatika kuiphata tu, hivyo sina vyeti siwezi kuphata kazi za ofisini tena". Shangazi akasema "jitahidi upate kazi maana mimi siwezi haya maisha ya kushinda njaa kila siku bora nirudi nyumbani kwetu kuna vyakula vya kumwaga tu"
Mjomba alikasilika , akampiga kofi mke wake paahhh!! Dah lile kofi lilikuwa zito , mpaka mwenyewe niliona aibu ikanibidi niangalie chini, mjomba akasema,"yaani hapa sijaphata mke hii balaa, mimi nilizani utakuwa karibu yangu kunipa moyo na kunisii kuphata nguvu kumbe wewe mpuuzi kiasi hichi" Shangazi akasema "mme wangu tangia unioe hujawai kunipiga hivi, kwanini unanionea, au umephata maraya wako nje unao wapenda, hivi mimi napungukiwa nini mpaka unipige hivyo ehh, nakuuliza?" Mjomba akasema, "tangia nikuoe sijawai kukupiga kwa sababu nakupenda, lakini umeanza kunidhalau sahivi, huwezi kuongea maneno ya kijinga hivyo" Nilipo ona wanapigana nikashikwa na aibu ndipo nikaamua kutoka nje ili nisiendelee kumtazama shangazi akipigwa, maana nilikuwa namuogopa shangazi kwamba, mjomba akiondoka tu na mimi naanza kupigwa pia. Kwa hasira shangazi akachukua mizigo yake akhataka kwenda kwao. Mjomba alimuacha tu, shangazi alipo fika kwao baba yake alimfukuza akasema "toka hapa umeniulia mke wangu”                     Baba yake shangazi aliumia sana kumuona shangazi amerudi kwake akaendelea kusema kwamba " kila nitakapo kuona utakuwa unanikumbisha msiba wa marehemu mama yako, hivyo sipendi hata kukutazama, yaani ni bora hata nisinge sikia maneno ya mama ako, kwa kinywa chake alisema, umemuua wewe! nakuomba ondoka kwangu, tokaaa na hata nikifa usinizike, na ukija tena nakufungulia kesi ya mauaji" Shangazi akasema, "baba, mme wangu ananitesa sana, hata chakula hanipi! nisamee baba sina sehemu nyingine ya kukimbilia zaidi ya hapa nyumbani, nionee huruma baba" Baba ake shangazi alikhataa khata khata kumkalibisha mtoto wake ndani, na akasema asirudi pale kwake tena.
Kibaya zaidi hali ya uchumi ya shangazi ilikuwa ngumu sana, hivyo hakuwa na nauri ya kurudi nyumbani, ndipo akaamua kumpigia simu hawara yake ili amtumie nauri aweze kwenda kukaa kwa hawara yake, lakini bahati mbaya hawara yake alikuwa mbali na simu hivyo shangazi alipiga simu sana ila simu haikupokelewa kabisa siku hiyo. Ilipo fika usiku  kipindi bado yupo mtaani na mizigo yake, shangazi aliogopa kwamba anaweza kubakwa, hivyo akajishusha na kumuomba kijana mmoja mtaani, akamwambia kwamba, "kaka mimi ni yatima sina baba wala mama, alafu sina sehemu ya kulala wala kuhifadhi hii mizigo yangu naomba unisadie kaka yangu" Yule kaka alikubali kumu hifadhi ndipo akampeleka kwake ili aweze kupumzika siku hiyo. Sasa ilipo fika usiku sana shangazi akiwa kwenye chumba cha yule kaka, kaka wawatu uvumilivu ulimshinda hivyo akaitaji kufanya mapenzi na shangazi, shangazi alikhataa akasema "mimi ni yatima nisadie kaka usinibake," Yule kaka akasema "sio kwamba nakubaka maana nikilazimisha sitafurahia tendo, nipe japo mara moja tu mimi siku sumbui tena na mimi ni mwanaume nilie kamilika siwezi kuvumilia kulala na wewe mpaka asubui, siwezi kuphata usingizi kabisa" Alianza kulia maana alikuwa hajampenda yule kaka, hakuwa na jinsi akaamua kuvua tu na kufanya lile tendo, dah kumbe kaka wawatu alilazimisha kufanya na muathirika tendo hivyo na yeye pia akawa ameuphata, maana aliamishia nguvu zake zote kwenye tendo. Ilipo fika saa tisa za usiku yule kaka akaamka kimya kimya akaiba mizigo yote ya shangazi na akamfungia humo humo ndani shangazi kwa kufuri. Shangazi alipo amka asubui, alishangaa kukuta yule kijana hayumo ndani, alipo tazama mizigo yake akakuta hamna, dooh alitetemeka kwanza kisha akaenda kufungua mlango akakutaa mlango umefungiwa kwa nje na kufuri, shangazi alianza kulia mule ndani,
dada mmoja jirani akaenda kuuliza, "kunanini mbona vilio ," Shangazi akasema "nimeibiwa vitu vyangu vyote, na nimefungiwa kwa nje, nifungulieni" Ndipo yule dada akaita fundi aje kubomoa kufuri kusudi shangazi aweze kutoka na kuondoka mule ndani.Shangazi alipo toka mule ndani akasema nitamphata wapi huyo kaka wa hichi chumba, maana ameiba vitu vyangu, yule dada akamjibu, "shosti hata usijisumbue hauwezi kumphata, huyo kijana kila siku anaiba, na kila siku mapolice wanakuja hapa kumtafuta, na hawampati, kwahiyo ni bora to uondoke, maana anaweza hata kukudhuru" shangazi akamwambia yule dada kwamba, "dada mimi sina hata nauri naomba unisadie 5000 tu niende kwangu" Yule dada akampatia shilling 2500 tu maana ndiyo aliyo kuwa nayo. Lakini kibaya zaidi nauli ilikuwa ni 5000, hivyo shangazi akaamua kwenda hivyo hivyo, wakati konda anakusanya nauli, ilipo fika zamu ya shangazi, ndipo shangazi akaomba kwamba, "konda nisamee mimi nina nauli nusu" Yule konda akamwambia kwa sauti ndogo kwamba "mimi nakusaidia lakini tukifika mwisho wa safari ningeomba twende wote kwangu"
Shangazi akakubali, ila konda hakumuamini akamwambia nipe simu yako nishike ili niwe na uwakika kuwa tutaenda kwangu, shangazi akampa bila wasiwasi maana alijua akibisha anaweza kushushwa katikati ya safari.Walipo fika mwisho wa safari ilikuwa ni jioni pia hivyo dereva akaenda kupaki gari kabisa, sasa shangazi alikuwa yupo na yule konda ili waende nyumbani kwa konda. Shangazi alipo kuwa anaenda na konda, akakumbuka alivyo fanywa usiku na yule kijana, ndipo akaogopa na akaanza kupiga kelele kwamba, "mwizi ,, mwiziiiii amenibia simu" yule konda akasema, , situme kubaliana, watu walivyo sikia shangazi anapiga kelele kuwa mwizi wakaja na kuanza kumpiga yule konda, kaka alijaribu kijielezea hawakumuelewa, wengine walimpiga na mawe usoni mpaka meno kutoka, wengine walimchoma na fimbo machoni, yaani yule kaka alifariki kifo kibaya sana ,, Baada ya mauaji ya yule konda, mapolisi walikuja na kuchukua mwili wake kisha wakaenda nao, ndipo shangazi akaenda sehemu alipo kuwa akikaa hawara yake, hawara yake alipo muona shangazi akashtuka! Akamuuliza, "mpenzi wangu mbona umekuja bila taarifa" shangazi akamjibu, "nilikupigia simu sana hukupokea, mpaka ikazima ndiyo maana unaona nimefika bila taarifa" hawara yake akamuuliza, "vipi sasa naona leo umekuja bila wasiwasi mme wako je umemuaga vipi maana mjanja sana yule bwana" shangazi kwa furaha akajibu "nimeachana nae yule bwege, nimekuja tukae pamoja tuendelee na mapenzi yetu kwa uhuru zaidi" yule hawara akabadilika sura akawa kama amenuna, shangazi akamuuliza "mbona kama huja furahia mimi kuwepo hapa kwako leo, tatizo nini mme wangu?" Hawara akamwambia "hapana sija nuna ila najiuliza maswali mengi sana na sina jibu, hivi unapo kuja kukaa hapa unahisi tutakula nini wakati wewe ndiye unae nipa pesa za mme wako sasa umeachana nae tutakula nini hapa na vipi kuhusu nguo zako mbona huna?"
Shangazi akasema "bebi nguo nimeibiwa na wezi pale kwenye kituo cha boda boda hivyo sina nguo yoyote ile, na mme wangu hana hela sahivi maana amefukuzwa kazi" Yule hawara aliona maisha yake yhatakuwa magumu sana maana shangazi alikuwa anampa pesa mara nyingi. Shangazi alikuwa anavaa nguo za hawara yake maana hakuwa na pesa ya kuanza kununua nguo mpya. Mjomba aliendelea kuwa na maisha magumu na tulilizika kwa kidogo tulicho kiphata. Baada ya week moja, mjomba  akapigiwa simu kwamba marehemu zephania alikufa na madeni ya watu hivyo nyumba aliyo iacha ikistaili kuuzwa ili watu walipwe pesa zao, na kibaya zaidi kwenye ile nyumba mama yake mzazi zephania ndiyo alikuwa anaishi, hivyo mjomba akaambiwa akae na yule mama yake zephania amtunze maana mjomba ndie alie kuwa rafiki wa zephania sana. Dooh mjomba aliwaza sana kabla ya kukubali, akajiuliza "sasa hapa nyumbani tunakula mara moja tu kwa siku, huyu bibi si tutamtesa bure, maana mke wangu kaniacha sababu ya pesa, sasa nikikaa na bibi sindio naongeza mzigo ndani ya familia yangu" mjomba alikhataa lakini aliwaza, "huyu bibi nikimkhataa hataenda wapi ,,maana marehemu zephania alisha niambia jinsi ambavyo ndugu zake hawampendi mama yake. Mjomba aliamua kukubali kukaa na mama yake zephania, tuliishi vizuri sana, maana yule bibi alikuwa mvumilivu , yaani kama kipo tunatumia na kama hamna anavumilia pia, hivyo maisha yakaenda, lakini mama yake zephania akamuuliza mjomba, "tangia nije hapa sijawai kumuona yule mke wako, yuko wapi?" Mjomba alimwambia kuwa, "mke wangu alisema haya maisha ni magumu sana hivyo yeye hawezi kuishi ndipo akachukua mizigo yake na kuondoka" bibi akamwambia "usijali mwanangu maisha yhatamshinda tu ipo siku hatarudi." Siku moja tupo sebreni mimi, mjomba pamoja na bibi, mjomba akapigiwa simu kuwa anhatakiwa kurudi ofisini kwake, eti amesamehewa na ofisi imefatilia ikajua kweli mhatatizo ya kifamilia na misiba ndiyo ilimfanya awe mzembe kazini, mjomba hakuamini kama kweli kaitwa alijiandaa hapohapo na kwenda ofisini, akakuta kweli amerudishwa kazini na aendelee na kazi. Dooh bibi alimwambia "mungu hataendelea kukusaidia na ipo siku mke wako hatakuja kukupigia magoti."
mjomba wangu alifanya kazi kwa bidii sana, ndipo siku moja alikuja nyumbani kwa furaha sana akasema "ehh mungu wangu tangia nimekubali kukaa na mama zephania, maisha yangu yanaenda vizuri sana, leo nimeongezwa cheo ofisini na mshahala wangu umeongezeka pia mungu yu mwema "
Baada ya mjomba kuphata kazi na kuongezewa mshahara, akaamua kununua gari aina ya "Brevis". Kumbe upande wa shangazi na hawara yake yake maisha yalikuwa magumu sana, maana ilikuwa inapita hata siku awaja weka kitu chochote mdomoni, hawara yake shangazi akaanza kuchoka kukaa na shangazi ndani, ila akawa anashindwa kumfukuza ,. Siku moja mama Anna akiwa katika pitapita zake akawa ame muona mjomba anaendesha gari lake zuri jipya kabisa, umbea ukamjaa, hapo hapo akatoa simu yake kisha akampigia shangazi akasema, "halo shosti za siku nyingi, maana tangu hatujaonana ni mda mrefu sana, naona umeanza kunenepa sahivi"
Shangazi akamuuliza "kwanini" Mama Anna akasema "kwanini, kwani ujui mumeo mambo yake mazuri sahivi amenunua gari, anatembea akiwa amekaa tu hongereni shosti"
Shangazi hakuamini kabisa, maana alikuwa anajua mme wake ni , wa kutupwa kabisa, maana alisikia tetesi kuwa mumewe ana beba zege na kufanya vibarua vidogo vidogo vya kumpatia pesa ya kula. Sasa shangazi alipo sikia mume wake ana maisha mazuri, akamwambia hawara yake kama alivyo ambiwa na mama Anna, dooh hawara akasema, bebi tafadhali huu ndiyo mda wa kuanza kuphata hela, rudi kwa mme wako ili upate pesa", shangazi akasema, "kurudi sio shida, ninacho ogopa mimi je, hatakubali kunisamee, maana nilitoka kwake mwenyewe bila kufukuzwa kisa tu hakuwa na hela je nikienda leo hatanisamee kweli yule mwanaume", hawara yale akasema "haaa wee nini, mbona unaniangusha kwani wewe mtoto, we nenda pale anza kulia, mlembulie macho kidogo muombe msamaa, hata magoti chini piga, hata kusamee, wewe kuwa kama wanawake wenzako wanavyo lia uongo uongo hatakusamee". Dah kweli shangazi alirudi nyumbani akatukuta wote mimi, mjomba pamoja na bibi, shangazi alianza kulia anaomba msamaa ,.mjomba akamwambia, "kama unhataka nikusamee, niambie kwanini uliondoka kwangu na kwanini umeamua kurudi kwangu?"Shangazi akasema "nisamee mme wangu ni tamaa za dunia tu, sina sababu nyingine mme wangu", mjomba akwambia "bado hujanijibu swali langu, na usipo nijibu nakuomba utoke kwangu" Shangazi akaanza kujin'ghata ng'hata pale kisha akasema, "kweli mme wangu niliondoka kwako sababu uliishiwa pesa" Bibi akasema "ehhh kwanini sasa?, bibi alipo muuliza shangazi hakujibu, maana kwanza alishangaa iweje mama yake zephania akae pale nyumbani, shangazi hakupenda, maana shangazi alikuwa hapendi kukaa na watu. Mjomba akamuuliza shangazi kwamba, "sasa kama uliondoka sababu nimeishiwa pesa, nimefukuzwa kazini, na hauli milo yote, basi wewe ni mnafiki hauna mapenzi ya kweli, kwenu hukufundwa, sasa mimi kuishi na wewe siwezi maana nimekuvumilia mengi sana, umesababisha kidogo ni muue mtoto wa dada yangu, umesababisha wazazi wako wanahisi tumeshirikiana kumuua mama yako mzazi, nimeisha kukamhata na barua za ajabu ajabu, hivyo nakuogopa bora urudi kwa baba yako mzazi ndiyo mnawezana" shangazi alitoa machozi sana huku akiwa anampapasa mme wake mikononi akisema, "mme wangu nisamee, tumetoka mbali sana sisi, leo nimefanya kosa, nihurumie, akilizi zilikuwa zimelala ndiyo maana nilifanya makosa kama yale nisamee nakuomba", mjomba alianza kupatwa na huruma akasema, "vipi baba yako hajambo" shangazi akasema, "baba alikhataa kukaa na mimi kabisa, alinifukuza kama mbwa akisema mimi ndiye nimemuua mama kwahiyo sina kimbilio lolote zaidi kuishi na wewe"
Mjomba akamuuliza "kwahiyo ulikuwa unaishi wapi kipindi chote hicho" shangazi akasema nilikuwa nakaa kwa mama Anna. Mjomba akasema, "we mwanamke una roho mbaya sana, nashindwa hata kukusamee, maana ulinikimbia kabisa ,, wakati siku ya ndoa ulisema tutaishi kwenye shida na raha, kwanini unamkosea mungu wako lakini, mbona wazazi wako ni watu wazuri kwanini wewe unakuwa hivyo, sasa ngoja nikwambie, tangia umeendoka humu ndani wizi sijasikia, ugomvi sijasikia lakini wewe ukirudi tu lawama zitaanza"Shangazi akasema, hapana mme wangu nakupa ahadi kwamba tutaishi kwa amani na furaha". Tulimuonea huruma sana shangazi maana alikuja amevaa nguo alizo ondokea alafu zilikuwa zimepaukaaa! Na zilikuwa na viraka kila kona, " mjomba akamuuliza tena "nguo zako ziko wapi maana ulibeba mabegi yako yote". shangazi akajibu "niliibiwa nguo zote na wezi, sina nguo yoyote zaidi ya izi nilizo vaa, zikichafuka nafua kisha navaa kanga, zikikauka nazivaa hivyo hivyo, hata nguo za ndani pia zimechanika zote", Dahh mjomba akamuuliza Bibi kwamba, "mama tumsamee au tumuache" Bibi akaguna kisha akasema "yaani sisi wanawake tuna mhatatizo, iweje umkimbie mume wako kisa ameishiwa pesa, alafu umesikia ameongezwa cheo na amephata mshahara, ndiyo unajirudi unalia", shangazi akasema, "mama niombee msamaa nampenda mme wangu, nilichaganyikiwa tu maana mama yangu alifariki" bibi akamjibu "mbona mimi mwanangu alifariki tena pamoja na mkwe wangu, lakini sijachanganyikiwa acha upumbavu we mwanamke, ukiolewa tulia sio unakaa kisichana  wakati we ni mama tayari, umeolewa, kaa chini tulia na mumeo na muombeni mungu ili awapatie mtoto sio kuruka ruka tu kama kuku"
Mjomba akaanza kulia, kisha akasema "toka kwangu we mjinga sana sikutaki tena wacha nikae bila mke". Bibi akasema, "hapana mwanangu usiwe hivyo, punguza hasila najua ni vigumu kumsamee, lakini sisi wanawake tunajifunza kutokana na makosa, msamee mke wako naamini hawezi kurudia ujinga wake, mtapendana na mtaishi vizuri kama zamani", mjomba alikuwa ana muheshimu sana mama zephania, hivyo akaamua kumsamee mke wake bila kinyongo. Shangazi hakuamini kabisaaa! Alimkumbatia mume wake kwa furaha, kisha akamkumbatia bibi pia, na akanikumbatia na mimi pia. Lakini tatizo kubwa lilikuwa ni kwamba shangazi alikuwa ana virusi vya ukimwi hivyo ange muambukiza mjomba, na sisi wote tulikuwa hatujui afya yake maana, "huwezi kumpima mtu kwa kumtazama" Ndipo bibi akasema, "najua  mmesamehana, nimefurahi pia lakini dunia ya sasa imejawa na magonjwa mengi,  hivyo mkapime afya zenu kwanza, ndipo muanze kuweka ukaribu wenu wa ndoa" Shangazi alivyo sikia vile, moyo wake ulimsuta, maana alijua yeye tayari kaisha chepuka, lakini alijiamini kuwa hana ukimwi sababu alikuwa bado hajapima na hata alipo pima na Mama Anna alijikuta ni mzima, hivyo shangazi alijiamini kweli kweli. Mjomba akasema "sawa, lazima tutapima, maana kweli sijui atokapo kama ni salama".
Sasa Siku moja usiku tukiwa tumelala, shangazi alibanwa na haja ndogo, hivyo akaamka kwenda kujisaidia, yaani wakati yupo chooni mjomba akashangaa kusikia mke wake analia, "kumbe yule kijana alie fanya nae mapenzi usiku na akamuibia shangazi, alikuwa ame muambukiza kisonono pia, maana  alikuwa ana washwa sana sehemu zake nyeti na kutoa uchafu wa njano njano, Mjomba alipo sikia mke wake analia kwa maumivu makari akamuuliza, "mke wangu mbona unalia kuna nini chooni" shangazi akasema ukweli kuwa ana maumivu makari sana sehemu zake nyeti.
mjomba hakuhisi kitu chochote, ila ilipo fika asubui akamuachia mke wake laki mbili ili aende hospitali kwa ajili ya matibabu na kupima pia, shangazi alienda kupima ndipo daktari akampa majibu kuwa ana kisonono! Shangazi akashangaa kisha akamuuliza, "kisonono kipi tena, mbona mimi sijawai kuugua magonjwa ya zinaa hata siku moja" daktari akasema "inawezekana ulitembea na mtu mwenye ili gonjwa, hivyo yale maji maji yake yalipo kuingia na wewe ukaugua, ila shukuru mungu sana ume uwai ugonjwa! maana ungechelewa ungephata madhala makubwa zaidi katika mwili wako, na dalili za huu ugonjwa sio izo tu ulizo ziona kwako, bali kuna kuphata maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa, homa, Kutokwa uchafu ukeni wenye rangi ya njano au kijani, Kuvimba eneo la uke, Kutokwa damu katikati ya siku za mwezi, Kutokwa damu baada ya kufanya tendo la ndoa, Kutapika, maumivu ya tumbo na maumivu ya nyonga, Maumivu wakati wa haja ndogo na kuphata haja ndogo mara nyingi, Kutoa uchafu kwa nyuma, kuwashwa, maumivu au kutoa damu wakati wa haja kubwa, Kukauka koo, kuwashwa, kumeza kwa shida au uvimbe kooni, Maumivu kwenye macho, kutopenda mwanga mkali, kutoa uchafu kwenye macho unaofanana na usaha na vile vile Kuvimba na joto kwenye maungio ya mifupa. Daktari aliendelea kusema kwamba, "dawa zake zipo wewe nenda pale (reception) mapokezi, kalipe pesa kisha waonyeshe hii karhatasi whatakupa dawa na uzitumie ipasavyo utapona.
Shangazi alipo toka hospital akampigia simu hawara yake kisha akamwambia, "bebi kama ulikuwa unajua una kisonono kwanini uniambukize na mimi mpaka nateseka kiasi hichi" hawara yake akamwambia, "mimi mwenyewe nateseka sana sahivi maana ulipo toka kwa mme wako ukaishi na mimi hapa ndiyo nimeuphata huo ugonjwa" shangazi akagundua kuwa alipo lazimishwa kufanya tendo na yule mwizi ndipo alipo phata ugonjwa pia, shangazi akamjibu hawara yake kwamba "mimi tayari nimepewa dawa, hivyo nakutumia na wewe hela ukapewe dawa kusudi tupone wote tusije kuambukizana tena". Ndipo hawara yake akawa amepona pia.                       
Tuliendelea kuishi kwa amani pale nyumbani bila shangazi kuonyesha mhatatizo yoyote kama ya zamani hivyo hata mimi nikafurahi nikahisi mambo sio mabaya tena, kumbe shangazi , alikuwa anajifanya tu na alikuwa ana mawazo yake mabaya sana kichwani, kilicho kuwa kina msababisha afanye ujinga na upumbavu ni yule hawara yake alie mpenda sana kuliko hata mume wake. Siku moja hawara akampigia shangazi simu, akimuomba shangazi amsaidie laki moja tu, sasa shangazi hakuwa nayo, hivyo shangazi akamfhata mme wake na  kumwambia kwamba "mme wangu sema kweli tunaishi vizuri humu ndani, lakini naumia sana kuona Nelson asikii wala aongei, naomba uniachie pesa kidogo leo ili nimpeleke hospital kubwa ile ya kule juu mwembeni, akaangaliwe tatizo lake vizuri labda hataphata nafuu aweze kuongea", mjomba alifurahi sana kusikia mke wake akiongea maneno mazuri kama yake, akasema, "hama kweli mke wangu umekuwa mke mzuri sana sahivi, nakupenda sana mke wangu, chukua hii laki moja na elfu sitini, umepeleke akapime, kisha ujiandae week ijayo tukapime afya zetu pia ili tuwe na ukaribu wa ndoa", shangazi akamjibu, "sawa mme wangu kazi njema nakupenda" Baada ya mjomba kuondoka, shangazi akampigia simu hawara yake kisha akamwambia, "huyu mjinga tayari amenipa pesa nakutumia sahivi bebi wangu, lakini usi ihonge kwa wasichana wengine hela yangu, nikijua tutagombana," hawara yake alifurahi sana kupewa ile pesa akajibu "bebi mi siwezi kuhonga pesa yako nakupenda wewe tu" Mjomba alipo toka kazini kitu cha kwanza aliuliza, "vipi Nelson umempeleka hospital," shangazi akajibu ndiyo mme wangu, "wamempima ila hawajafanikiwa kuphata ugonjwa, na wametumia vipimo vya bei sana mpaka pesa imetuishia" mjomba alisikitika sana akasema, "sijui anaumwa nini mtoto wangu , ila nguvu za mungu hatapona tu". Baada ya mwezi mmoja shangazi alikuwa ameisha kuwa mchangamfu wa pesa za mme wake, maana mme wake alikuwa kaisha muamini na ana muonyesha kila siri zake, ndipo shangazi akaanza roho mbaya kwangu mimi pamoja na bibi. Siku moja akiwa anaongea na hawara yake bibi alimsikia shangazi akisema, "yaani bebi nhatamani uje tufurahie raha zetu kama zamani, lakini huyu bibi hapa ndiyo anatubana sijui nimkomesheje" Kipindi bibi akiwa bado anamsikiliza shangazi, aliendelea kumwambia hawara yake kwamba, "bebi wangu, mimi sijui kwanini nakupenda hivi, najaribu kujizuia lakini nashindwa kuphata jibu, umenifanya nichizi juu yako, maana masaa yote nakuwaza wewe tu, hata ninapo kuwa kitandani na mme wangu nakuwaza wewe tu mpenzi". Hawara yake akamjibu "naamini kuwa unanipenda maana pesa za mme wako unanipatia, kama ungekuwa hunipendi basi usingenipa pesa yoyote ile" Shangazi akamuuliza, "sasa huyu bibi tunamtoaje humu ndani mi simpendi kabisa yaani nikimuona nahisi kama nimekanyaga kinyesi," Hawara akasema, "tutafute kisa kizuri" Shangazi akamuuliza, "kisa gani sasa tutumie ili aondoke" Yule hawara akasema, "unajua mme wako sahivi anakuamini sana hivyo kila utakacho mwambia lazima aamini tu, sasa leo jioni akija mwambie kuwa, ulimkuta Nelson na bibi wanafanya ngono" Shangazi alifurahi.
Bibi alipo sikia iyo njama akanifhata nje kisha akanielekeza  kwa mikono kwamba "kuna kitu nimekisikia mjukuu wangu, leo saa nne usiku njoo tuongee nikwambie maana sahivi shangazi yako hatatusikia"Kumbe bibi alitaka kunijurisha kuhusu hiyo njama ya shangazi na hawara yake walivyo panga ili yeye afukuzwe pale". Mjomba alipo toka kazini shangazi akampokea, kisha ilipo fika saa tatu na nusu usiku wakiwa chumbani shangazi akwambia "mme wangu, hivi unajua huyu bibi anhatabia mbaya sana" Mjomba akamuuliza, "tabia gani tena wakatu bibi yuko vizuri tu" Shangazi akasema wee usimtazame kwa sura huwezi amini nimemkuta Nelson pamoja na huyo bibi wanafanya mapenzi kwenye stoo ya mkaa kule nyuma, yaani bibi kavua nguo kabisa kisha khatandika kile kitenge chini anafurahi tu" Mjomba akasema "weeh yule mtu mzima awezi kufanya hayo mambo" Shangazi akasema "mi mwenyewe sikuamini, na walipo gundua nimewaona, yaani kaomba msamaa sana, nisimseme kwako, yaani amekuwa mpole kafanya kazi zote leo, sasa wakati wanaongea kwenye mida kama ya saa nne hivi, kumbe mjomba alikuwa amesahau simu yake sebreni, wakati anaifhata na mimi ndiyo nilikuwa naingia chumbani kwa bibi maana aliniita tuongee kuhusu shangazi alivyo panga ili bibi afukuzwe,  mjomba alipo niona naingia chumbani kwa bibi usiku ule, ndipo akaamini maneno ya mke wake ,, Mjomba alipo niona naingia kwenye chumba cha bibi usiku ule yeye alirudi nyuma, ili mimi nisigundue kama amenioa, akamfhata mke wake akasema, "mke wangu hivi unajua nilikuwa siamini kama hawa watu ni wapenzi, yaani huwezi amini nimemuona Nelson anaingia chumbani kwa bibi yake usiku huu", Shangazi akasema, "ehee unaona hee nilikwambia, kumbe wameanza zamani hii tabia sisi hatujui tu, hivi kweli mama zephania ana akili kweli, yaani anambaka Nelson kijana mdogo hivyo, kama anawashwa si hatafute mzee mwenzake" Mjomba akasema, "ebu twende tusikilize kama kweli wanafanya ilo tendo"
Shangazi akasema, "hamna aja ya kusikiliza waache wameisha pendana mi sina mda wa kuwafatilia, tayari nimeisha kwambia na wewe umejionea" Mjomba akasema "sasa sijui nifanye nini mimi , yaani haya ni maajabu, huyu mama zephania namuheshimu sana yaani naona aibu hata kumwambia hichi kitu, nitaanza vipi sasa ," Shangazi akasema "mfukuze huyo bibi, anatia mikosi nyumba yetu mme wangu" "Dooh maisha haya, Yaani shangazi alisahau kama bibi ndiye alie muombea msamaa, leo hii anhatamani bibi afukuzwe ili yeye afanye ngono na hawara yake kwa uhuru. "Ilipo fika asubui mjomba akumsalimia bibi kabisa akaenda kazini, maana alikuwa ajaamini ujinga alio ambiwa kabisa, Bibi alishangaa kuona mjomba ajaenda kumsalimia asubui hivyo akamuuliza shangazi kwamba, "mme wako hajaenda kazini leo au maana hatujaonana, nimezoea kila siku ananisalimia asubui kabla ya kwenda kazini," Shangazi akamjibu,"weh!  kaa mbali na mme wangu, tumeisha kuogopa wewe mama, baki na Nelson wako niachie mme wangu, maana na yeye ukimchukua nitalala nanani sasa, baki na Nelson wako," bibi akamwambia kwamba "sijakuelewa unamaanisha nini"
Shangazi akasema, "ehh na mwaka huu utaelewa tu, lazima kwangu utoke, sina mama mimi alisha kufa, hata baba sina maana alisha nifukuza, kwahiyo kukaa na mama wawatu siwezi, nimeisha kuchoka we mama, kila saa unakaa na mme wangu unaomba hela za matumizi yako unanitia hasila, kwani huna ndugu zako"Bibi alianza kulia akasema, "mwanangu ndugu zangu walinikhataa, naomba nisaidie nisitoke hapa, maana nyie ndiyo tegemezi nililo bakiza" shangazi akasema "hapa utatoka tu unanibana sana we mama, yaani nakosa raha"                         Mjomba alikosa raha alipo jua kuwa mimi na bibi yangu tunafanya mapenzi, alimzalau sana bibi, akaniona na mimi sina akili kabisa, wafanyakazi wenzake walimuona hana raha ofisini wakamuuliza, "boss, mbona leo huna raha  tatizo nini" Mjomba akawaeleza kuhusu mimi na bibi, wale wafanyakazi wakasema "mfukuze huyo bibi, hana akili kabisa anaweka laana katika nyumba, kwanza sio mama yako mzazi ndiyo maana anafanya hivyo, mtoe hapo hatajua mwenyewe pa kwenda, na huyo sijui Nelson, muonye asirudie hicho kitendo maana akizoea anaweza kulala hata na shangazi yake wakati wewe ukiwa hapa kazini" Mjomba akajibu, "sawa ngoja tu nimfukuze huyo bibi, hata hivyo msaada nilio mpa unamtosha sana"
Mjomba alipo rudi nyumbani akakuta bibi yupo sebreni analia, mimi nipo nawaza tu, mjomba akamuuliza bibi, "mama kwanini unalia umekuwaje" bibi akamjibu "kwa sasa naona sina jipya tena kwako, mke wako ameisha kudanganya mengi kuhusu mimi, kumbe huo wote ni uongo mtupu, tuliishi wote vizuri kipindi cha nyuma bila ugomvi, lakini mkeo amekuja hata sasa hivi hunijulii hali asubui"Mjomba moyo wake ulimuuma kusikia hayo maneno ila hakujibu chochote, akaenda chumbani kumuona mke wake, akamuuliza, "mke wangu mbona siku hizi mapenzi ya wewe na hawa wengine yameisha kabisa tatizo nini" mke wake akasema mimi siongei na wazazi wasio na akili maana hawawezi kunishauri lolote, sasa mama anatembea na Nelson, anakazi gani zaidi ya kutupa sisi laana kwenye nyumba we mme wangu punguza huruma kamfukuze huyo mama" Mjomba "akasema sawa mke wangu ngoja nikamwambia ajiandae nimpe nauli na hela kidogo ya kutumia aondoke"
Pale pale shangazi akafurahi kusikia bibi anafukuzwa akaruka na kumkumbatia mjomba kisha akasema, mme wangu familia yetu inabidi iwe ya baraka sio upumbavu wa huyo mama mwishowe tuta laaniwa na sisi akiendelea kukaa hapa. Mjomba akatoka chumbani kisha akaenda mpaka sebreni ili akamfukuze yule bibi andoke , mjomba alipo fika sebreni akamwambia bibi kwamba, "mama tumeishi wote kwa mda mrefu hapa nyumbani na tulipendana sana, lakini mama yangu kwa tabia ambayo umeianzisha yako wewe na Nelson sijaipenda bora uondoke kwangu tu" Bibi akapiga magoti akasema, "nisamee baba yangu, nakutegemea sana baba"
Bibi aliumia sana , alipo ambiwa aondoke, mimi nilikuwa pembeni nikitazama, machozi yalinitoka pia maana nilikuwa nampenda sana bibi na mara nyingi nilikuwa nikikaa nae nafarijika sana. Ila bibi aliwaza sana akitoka pale hataenda wapi, ndipo akamshika mjomba mikono akisema, "baba nisaidie mama yako, tayari mtoto wangu zephania ambae ni rafiki yako ameisha kufa, nitatunzwa na nani kwa umri huu, nitaishi wapi na nyumba yetu imeisha chukuliwa," bibi akamshika mikono mjomba ili amuhurumie, mjomba akakaa kimya, shangazi alipo toka chumbani doh! akakuta bibi amemshika mikono mjomba akilia ili asemehewe, shangazi alimfhata bibi kisha akamsukuma pembeni nakusema kwamba,"we usinitafute, yaani nakuomba usinitafute maneno kabisa, kwanini unampapasa mme wangu, inamaana unamtaka sio, niachie mme wangu nampenda, mshikeshike Nelson mlie zoea kufanya ngono, mkome mme wangu" mjomba akamwambia, "kwanini una msukuma mama hivyo, hata kama amekosa, ndiyo umsukume kiasi hicho". Shangazi akasema kwamba, "ehh nini, yaani kumbe unafurahi unavyo papaswa sio, na wewe unhataka kutembea nae au?" bibi akasema, , mimi ni mama na nimezeeka, siwezi kufanya hii dhambi mnanionea mimi mnanisingizia" bibi aliongea yale maneno huku akiwa analia, mimi nilishindwa kuvumilia kumuona bibi amesukumwa chini kama mwizi, ikanibidi nilie tu, maana nilitamani hata kum'meza shangazi. Mjomba alimuonea sana huruma bibi na yeye pia akaanza kulia tu ndani, sasa mimi, mjomba na bibi, tukawa wote tunalia, lakini shangazi anacheka huku akitusonya, mjomba akasema, "mama yangu itabidi tu uondoke maana kila mtu amenishauri hivyo, isitoshe huyu mtoto ni mdogo unapo fanya nae mapenzi unamuharibu mapema, wewe tayari ni mzee, unhatakiwa kumshauri yeye asifanye mambo ya ajabu" shangazi akasema, "ndiyo mme wangu hapo upo sawa kabisa, atoke, aende kuaribu familia zingine sio hapa."
Bibi hakuwa na jinsi , alimka pale chini akajifunga kanga yake, akaenda ndani kwake kisha akafungasha mizigo yake yote na akaileta pale sebreni,
Mjomba akasema "mama chukua hii laki tatu utafanya nauli na matumizi madogo madogo tu," Bibi akajibu "asante mwanangu, msaada ulio nipa unatosha, pesa yako baki nayo tu, acha niondoke"  alishangaa sana kuona bibi amezira zile pesa alizo mpatia, shangazi akasema "hivi mme wangu kwanini una haribu pesa hivyo, yaani unhataka kumpa laki tatu, mpe elfu thelathini tu aondoke inamtosha" bibi hakuitaji chochote akabeba mabegi yake mawili, kisha akafungua mlango na kuondoka. Mjomba aliishiwa nguvu kabisa ila akajikaza, mimi nilishikwa na huruma sana, hivyo nikafungua mlango kwa hasira, kisha nikamfhata bibi tuondoke wote, maana nilijua nikibaki na shangazi nitateseka zaidi na zaidi. Shangazi akasema, "unaona sasa yaani mtoto wetu ameisha haribika na yeye, tazama anamfhata uyo bibi wakati ni mzee, ameisha mzoesha ngono, mtoto naye amempenda, yaani huyu mama ametuharibia mtoto kabisa kabisa"
Mjomba akasema "we Nelson rudi hapa" lakini mimi nilikuwa simsikii, dah mjomba alichoka ,, maana alibaki na mke wake yaani wawili tu ndani. Mjomba alijaribu kula chakula kika mshida, akajaribu kulala usingizi hakuphata kabisa. Mimi na bibi tuliondoka bila kujua wapi tunaelekea maana hatukuwa na pesa yoyote mfukoni, njaa ilitupiga sana tukiwa njiani, tulichoka sana, ikafika hatua tukaamua kuacha mizigo njiani na kutembea hivyo hivyo maana ilikuwa mizito sana. Kipindi tupo njiani mvua ikaanza kunyesha sana, hivyo bibi akaanza kusikia baridi na alitetemeka sana ,, kwa sababu ya uzee, ikanibidi mimi nirudi mpaka tulipo tupa ila mizigo, ili nifungue begi japo nitoe masweta na mashuka ya kujifunika popote pale tutakapo lala. Kumbe mjomba pia usingizi alikosa kabisa, mke wake alijaribu kumpapasa sana na kumpa maneno mhatamu isiturudishe pale nyumbani kusudi abaki mwenyewe kwenye nyumba yake.Mjomba alianza kulia akisema, "sijui hawa watu wapo katika usalama gani usiku huu ," Shangazi akasema "waache waondoke mme wangu wamependana, unajua nivigumu kuvunja uhusiano wa watu wanao pendana kutoka moyoni, au unhataka waendelee kufanya ngono nyumbani kwangu, mimi sitaki hiyo tabia ndani kwangu kweli nakwambia" Mjomba akaamua kulala, wakati amelala mjomba aliota kama sauti ya Zephania inamuijia ndotoni ikisema "rafiki yangu nilikuzuia kuwa na maamuzi ya haraka, mke wako alimsingizia sana Nelson mambo mengi ya uongo, usimuamini mke wako ni muongo, ana roho mbaya" Kipindi mjomba anaendelea kuota mwili wake ulikuwa unatoka sana jasho mpaka mashuka yaka lowana. Palepale akashituka ghafla kisha akakaa kitandani, shangazi akamuuliza, "mme wangu tatizo nini, mbona jasho hivi, ni ndoto gani hizo zinakushtua namna hii", mjomba akasema, "hapana siwezi kumuacha Nelson na mama wapotee hivi hivi nitachekwa mimi" shangazi akasema, "hapo tu ndiyo unapo nikera, usiku wote huu, saa tisa ndiyo unawakumbuka, ebu lala mme wangu fikiria mambo ya ofisi sio hao" mjomba akasema, "kipindi umeniacha mwenyewe, nilikaa kwa furaha sana na Nelson pamoja na mama, sasa wameondoka nimebaki na wewe, ila hata usingizi sipati wala chakula hakipiti, niache niwafate nitawhatafuta popote walipo", shangazi akanuna mpaka sura ikajikunja. Mjomba aliamka kisha akatoka nje akawasha gari ili aje kututafuta popote tulipo.Mvua ilikuwa kubwa sana siku hiyo na kulikuwa na baridi kari pia, hivyo bibi alikuwa amenyeshewa sana mvua mpaka akaanguka chini na kuishiwa nguvu kabisa, wakati narudi kumfunika mashuka nikakuta amezidiwa awezi hata kuongea maana alikuwa amezeeka mama wawatu hata nguvu hana kabisa, nikamkuta chini ya mti kisha nikamvalisha nguo mbichi na kumfunika shuka lililo lowa maana mvua ilikuwa imeninyeshea sana mpaka nilipo kuwa nikipumua hewa natoa moshi mdomoni mwangu" Sasa wakati mjomba anatutafuta, alitukosa ,, hivyo akhataka kurudi nyumbani ila moyo wake ulikuwa unamwambia asikate tamaa atutafute mpaka atupate. Bibi alizidiwa kabisa nikaamua kumbeba ili asife maana alikuwa analia na kutetemeka zaidi yangu na akawa wa baridi mno, njaa ilikuwa imetupiga na tulitembea mwendo mrefu usiku ule. Hali ya bibi iliendelea kuwa mbaya sana ule usiku, alitetemeka sana mpaka akaanza kufumbua macho yake kwa nguvu sana, doh nikaogopa, bibi alianza kun'ghata meno yake kwa nguvu sana huku akilia kwa nguvu kama mtoto , na mvua nayo hai ishi inaendelea tu kunyesha. Nilishangaa kuona bibi ananivuta shingo kwanguvu, akajikaza sana kwangu ili apate nafuu maana alikuwa anaangaika sana, lakini mvua nayo ilinyesha tukiwa chini ya mti wa mpera.Wakati huo mjomba nayeye anatutafuta    kwa hali na uvumbi, huku shangazi anampigia hawara yake simu wanacheka kwa sana tu. 53                        Wakati mjomba anaendelea kututafuta, mimi na bibi tulikuwa tunaangaika sana, mpaka nikhatamani kumbeba bibi mgongoni ili turudi kwa mjomba maana nilihisi tunateseka sana pale. Sasa kipindi nimekaa kwa mbali nikaona gari limewaka taa, nikafurahi nikiwaza kwamba wakifika karibu yetu whatasimamisha gari na kutusaidia ili tusinyeshewe na mvua zaidi ili na bibi aweze kupona, maana ile mvua ilinyesha sana siku iyo, bila hata kupungua.
Sasa kipindi gari inakuja nikashangaa kuona tena gari limesimama. Mhh nikajiuliza, "ilo gari limesimama pale usiku wote huu", ila nikajipa moyo kwamba litafika tu, kipindi hicho hali ya bibi ni mbaya sana nashindwa hata kuielezea, dooh kumbe lile gari lililo simama lilikuwa la mjomba na alikuwa ametekwa na majambazi wanhataka kumnyan'ganya na kumpora kila kitu alicho kuwa nacho, mjomba alivyo tekwa alitoka nje ya gari hakujua kama ni majambazi yeye alitaka kuwauliza wale watu kama wameniona mimi na bibi tunapita pale njiani ili atuchukue turudi nyumbani. Walimkamhata Mjomba wangu, wakamvua nguo zake zote, kisha waka mfunga na kamba miguuni pamoja na mikononi na wakaanza kumpiga ,, mpaka damu zikaanza kumtoka, lakini cha kushanganza kule nyumbani shangazi hakujua kinacho endelea, maana alikuwa amephata uhuru wa kuongea na yule hawara yake ampendae kwa dhati, mjomba kipindi anapigwa alilia sana japo wasamalia wema waje kumsaidia, ila kulikuwa na mvua sana siku hiyo hivyo hata sauti yake ilikuwa haisikiki, wale majambazi lengo lao walitaka kuakikisha mjomba anakhata roho yaani anakufa kabisa ili waibe gari bila ushahidi wowote ule waondoke.
Mimi na bibi tulisubiri sana lile gari lakini halikuja maana mda huo mjomba alikuwa anapigwa mno, Bibi alianza kama kuishiwa nguvu zaidi maana hata mdomo hakuweza kuachama tena, nikaona nikimchelewesha hatanifia mikononi, hivyo nikaamua kumbeba mgongoni ili nimpeleke mpaka kwenye ule mwanga wa gari, bila kujua kuwa nafhata majambazi ili watuue vizuri familia nzima. Niliangaika sana kumbeba bibi mgongoni maana, mimi mwenyewe nilikuwa nimechoka sana, maana ile mvua  ilifanya viungo vyangu vya mwili kuwa vinyonge sana, vilevile bibi pia alikuwa awezi kusimama pia, ila nikajikaza na mpaka nikambeba mgongoni, Nilifanikiwa kumbeba bibi mgongoni kwa shida sana, ila nikajikaza kisha nikatembea kwa mwendo wa taratibu ili niwafikie wenye lile gari tuweze kusaidiwa, kumbe mda huo mjomba nae, alikuwa anapigwa sana, mpaka akazidiwa na kuanguka chini maana walimpiga sana kwenye magoti na  mipini ya majembe, nilimuomba sana mungu niweze kuwafikia wale watu sababu bibi alikuwa mzito sana mgongoni na ile taa ya gari nilikuwa naionea kwa mbaliii!, hivyo nikaona kama si ifikii, lakini nilipiga moyo konde nikajikaza ilimladi tu niwafikie wale watu kwenye gari.
Mjomba alipigwa sana, mpaka akasema, ", nisameeni, naitaji bado kuishi, chukueni gari mniache huru," Kumbe wale watu shida yao walitaka kuondoa uhai wa mjomba kabisa, hivyo mmoja akachomoa bisibisi na kumchoma mjomba tumboni, hivyo mjomba wangu alizidiwa kabisa na kulala chini kama mtu mfu, kipindi wale watu wanasema, "mkagueni kama amekufa kweli au bado" mimi nae nilikuwa nawakaribia karibu hivyo nilikuwa na furahi kwamba wanaweza kunusuru uhai wa bibi yangu usiku ule, mjomba alipo kaguliwa kama amekufa wakasema, "bado hajafa huyu, anaweza kutusumbua badae, bora tumuue tu", jamaa mmoja akachukua panga lenye makali sana ili amkate mjomba shingo, maana walishangaa kuona kipigo chote kile lakini mtu hafi, hivyo wakaona kumchinja ndiyo suruhisho, mjomba alikuwa hawezi kujisaidia mwenyewe, maana walikuwa wamemfunga kamba na wamemkaza sana.
Na mimi mda huo, napambana niweze kuwafikia karibu.Sema kweli, nili wakaribia, lakini nilikua sioni kama kuna mtu anapigwa, kwasababu ilikuwa ni usiku na mjomba alikuwa anapigiwa pembeni ya gari, hivyo zile taa zilikuwa azimliki lile tukio. Wakati nimekaribia kufika kwenye gari, na bibi akiwa mgongoni, nilikanyaga sehemu mbaya ,, kulikiwa na utelezi mkali sana, kutokana na ile mvua,  nili angukia mgongo huku bibi akiwa mgongoni, hivyo nikambonda kichwa vibaya pale chini, kumbe kulikuwa na jiwe, hivyo bibi wawatu akawa amegonga kichwa chake kwenye jiwe vibaya sana, mpaka akapasuka kidonda kikubwa, sasa wakati namnyayua kumbe bibi alikuwa amefariki tayari ,, doohh nililia sana, nililia mno. Wale majambazi walipo niona nalia, wakahisi wamejulikana, hivyo wakakimbia wote!.                    
Kipindi nimegundua kwamba bibi ameisha kufa, nikashangaa tena kuona watu nilio kuwa nawategemea wanakimbia, dooh niliumia zaidi kwa sababu niliwaza kwamba wale watu wangenipa msaada mda ule. Ndipo nikaamua kumpeleka bibi mpaka pale kwenye mwanga ili nitoke pale kwenye utelezi. Bibi alikuwa amekufa vibaya sana, maana alikuwa ameachama mdomo wake wazi, nilipo fika kwenye gari, wakati naangalia chini pale pembeni nikashangaa kumuona mjomba amefungwa kwamba na anatoka sana damu, nikajiuliza maswali sana, "mbona ili gari kama la kwetu na imekuwaje mpaka mjomba awe vile, ndipo nikagundua kuwa alipigwa sana na wale watu."Nilimuweka bibi pembeni na kumfungua mjomba zile kamba, nilipo jaribu kumsimamisha mjomba nikashangaa kuona anaanguka chini kama mti, maana alikuwa amepigwa sana kwenye magoti hivyo asinge weza kusimama kabisa. Nilimchukua bibi kisha nikamuingiza kwenye gari, na mjomba vilevile. Sasa nikashindwa jinsi ya kuwasha lile gari na kuliondoa maana nilikuwa sijui kuendesha gari, ndipo nikaamua kufunga milango na madirisha, kisha tukalala humo humo, ingawa nilikuwa namuogopa bibi kwasababu alikuwa ni marehemu tayari. Kibaya zaidi wale majambazi walikuwa hawajaenda mbali walijificha sehemu wananiangalia tu, mmoja wao akawambia, " wahuni ehh twendeni tena tuchukue gari, unaona kuna mtoto humo twende tuwamalize wote", mmoja wao akakhataa akasema, "hapana tusiende uwezi jua labda wametuona hivyo wametuwekea mitego ya kutukamhata". Sasa kipindi naangalia angalia mule ndani, nikaona simu ya mjomba, ndipo nikhatafuta namba ya shangazi ili nimpigie aje kutusaidia, nilipo piga simu alipokea ila tukawa hatuelewani kabisa maana shangazi alikuwa anaongea, lakini nilikuwa nashindwa kumsikia na kuongea pia hivyo yeye akashidwa kabisa kuelewa inakuwaje mme wake anapiga simu alafu aongei. Niliamua kulala mule mule mpaka asubui, ndipo tukaphata msaada wa kupelekwa hospital. Shangazi alipo pewa taarifa kuwa bibi amefariki ilikuwa na furaha kubwa sana kwake, na alipo ambiwa mme wako anaumwa sana na anhatakiwa kutibiwa miguu na kufanyiwa oparesheni maana alichomwa na bisibisi tumboni shangazi akaona huo ndo uhuru wa kuonana na hawara yake kwa raha zaidi,
 Kipindi tupo hospitali, mjomba aliteseka sana, maana damu zilikuwa zinamtoka nyingi sana pale kwenye kidonda alipo chomwa bisibisi, alishindwa kabisa kukohoa maana kila alipo kohoa tu, damu zilikuwa zinamtoka nyingi kwenye kile kidonda, mjomba wangu aliangaika sana hata wakati wa kujisaidia, maana miguu yake ilipigwa sana, hivyo asinge weza kuchuchumaa wala kusimama kwa ajili ya kujisaidia. Mjomba aliwambia manesi, huku akiwa analia kwa sauti kwamba, " naombeni msimzike bibi bila mimi kuwepo, naitaji kumuomba msamaa kabla mwili wake haujaingia kabulini." Shangazi alikuwa hajaja bado hospitali maana alimuita hawara yake akimwambia kwamba, "bebi, mungu katusikia kilio chetu, yaani huwezi amini kile ki mama kimeisha kufa, sasa hivi tutakuwa huru bebi, tuta furahi zaidi"
Hawara yake akamwambia, "dooh , amekufa?" Shangazi akasema, "ndiyo bebi, hatunae tena, kwahiyo usiwe muoga nikikuita we njoo na uwe huru ufurahie maisha"Hawara yake shangazi akamuuliza, "mume wako je yuko wapi?", shangazi akacheka,"Hahahaah""Unacheka nini?" Akauliza hawara. Shangazi akajibu, "bebi mme wangu anaumwa sana, yupo hospitali nikiphata mda nitaenda kumuangalia, yaani sasa hivi tupo huru sana, nhatamani na yeye afe ili tuzimiliki hizi mali zote mimi na wewe, maana wewe ndiyo mwanaume ninae kupenda, sababu unajua kunipa kile ninacho kipenda pia" Sasa kipindi hawara yake shangazi yupo nyumbani wanakula raha, akapigiwa simu na nesi, akaambiwa, "hallo we ndiye mke wa huyu kaka hapa, mbona humjali mme wako lakini, tangia asubui yupo hapa, hajala, hajaoga, yaani umetuachia kijana hapa amuangalie wakati ni bubu na ni kiziwi tutamuagiza vipi sisi na anaonyesha mifuko yake iko tupu hana hata shilingi mia, ebu njoo umuuguze mme wako"
Shangazi akauliza, ", dada sikia kidogo, hapo nje si kuna vibanda vya chips, kwanini usimtume huyo kijana achukue haraka mwanaume wangu ale" nesi alichukia lile jibu, akakhata simu, hivyo mimi na mjomba tukashinda njaa mda mwingi. Mjomba akasema, "kweli mke mwema anatoka kwa mungu, yaani mke wangu hajafika kuniona mimi" Sasa kipindi shangazi anafanya mapenzi na hawara yake, kumbe mda huo huo baba yake shangazi alikuwa anakuja nyumbani maana alisikia mjomba anaumwa,
Shangazi alijiamini sana pale nyumbani, maana aliona bibi hayupo na mimi sipo wala mjomba pia hayupo, hivyo akawa huru sana pale sebreni kufanya lile tendo na yule hawara yake. Sasa kumbe hajui kama baba yake mzazi anakuja kumuangalia mjomba maana alisikia kuwa mjomba amepigwa vibaya sana na majambazi usiku. Sasa kipindi shangazi yupo katika hari ya raha, kajisahau kabisa, yaani katupa miguu yote kule na kuitanua wazi wazi, huku hawara take akiwa anashughulika ipasavyo, dooh baba yake mzazi, aliingia sebreni kama alivyo zoea kuingia kipindi cha nyuma,  huwezi amini alimfumania uchi wa mnyama shangazi, yaani kama mama yake alivyo mfumania hapo awali. Baba alipo muona palepale akanyanyua mikono yake yote miwili na kujifunika macho yake asione uchi wa mwanae, maana hakutegemea kumuona na mwanaume mwingine kama yule, tena kibaya zaidi anafanya vile ndani ya nyumba ya mme wake, shangazi alikuwa bado hajamuona baba yake kabisa, maana alikuwa anacheza mechi akiwa amefunga macho yake, huku akitoa sauti nzuri za mahaba kwa furaha, sasa alie muona baba wa kwanza alikuwa ni hawara yake shangazi, palepale akaishiwa ngumvu kabisaaa! Kisha akachukua kitambaa cha sofa ili ajifiche uchi wake, maana nguo walikuwa wamezirusha karibia na marangoni alipo simama baba yake shangazi, sasa kipindi shangazi anainuka akishangaa kwanini hawara amemuachia njiani, shangazi alishangaa sana kumuona baba yake mzazi, alie mzaa yupo mlangoni. Dooh Shangazi aliinaama chini akisema, "nisamee baba yangu, ni shetani tu sirudii" baba kasema nimefumba macho vaa nguo we mtoto" shangazi akakimbia uchi mpaka chumbani huku makalio yake yako waziwazi, akavaa nguo haraka kisha akarudi akiwa ameinama chini anaona aibu tupu. Baba akamuuliza, "mme wako ninae mtambua yuko wapi?", shangazi akasema "nisamee baba" Baba yake akasema, "binti yangu, sahivi wewe ni mtu mzima, na nina amini unaelewa maswali, ukiulizwa, mme wako yuko wapi? Shangazi akasema, huku akiwa anatetemeka na ameweka macho ya huruma, "mme wangu anaumwa, anaendelea vizuri tu, ila yupo hospitali" Baba alilia ,, akasema, "mwanangu tabia yako hii uliyo ifanya nazani ndiyo ilimuua mama yako, mimi naondoka lakini wewe mtoto utateseka sana, utajuta". Kipindi baba yake shangazi anageuka kuondoka akamwambia shangazi tena kwamba, "nilikuwa nimekuja kuwasamee niwaache huru kwenye ndoa yenu, ila kwa ukahaba huu siwezi kukusamee na kwangu usije kabisa, sijakuzaa mimi wewe mtoto" Baba akarudi kwake akiwa na majonzi sana, aliona haibu kabisa akakaa kimya bila kumwambia mtu.
Shangazi na hawara yake wakabaki ndani wakiwa na aibu sana kwenye nyuso zao, hakuna wa kumuangalia mwenzake, shangazi akamkumbatia hawara yake kisha akamwambia, "usijali bebi, baba mwenyewe alisha nifukuza kwake kwanza, nashangaa amefhata nini hapa, wewe sahivi ndiyo mme wangu, ndiyo baba angu, maana mama yangu alikufumania hapa, na leo tena baba amekufumania hapa, wewe unajulikana sana kwetu kuliko mwanaume yoyote yule, nakupenda sana bebi wangu" Shangazi alishituka akasema "dooh nimesahau kabisa kupika chakula cha mme wangu, wewe nenda, ngoja niandae chakula nimpelekee hospitali tutawasiliana" Shangazi alipo leta chakula akakuta mjomba ameisha pewa chakula na mgonjwa mwenzake alie kuwa amekaa nae chumba kimoja. Mjomba akamuuliza akiwa analia kwamba, "mke wangu sasa hivi ndiyo unakuja, hivi unanipenda kweli au unanidanganya tu" Shangazi alianza kulia chozi la kinafiki akisema kwamba. "mme wangu nimeamka asubui mwili wote unaumwa, nilipo anza kupika nikadondoka mule jikoni, sasa hivi ndiyo nimephata nafuu, nikapika haraka na kuleta hichi chakula" Yule mgonjwa pembeni akasema, ", sahivi magonjwa yamekuwa mengi sana, pole dada" shangazi akasema "asante" kwa unyonge, mjomba akaamini kabisa kisha akamsamee mke wake. Baada siku chake mjomba akaachiwa kutoka hospitali, ndipo tukaanza mipango ya mazishi ya yule bibi, tulishagaa sana maaana ndugu zake yule bibi walinunua maji mengi sana ya ghalama, wakanunua vyakula vya kila aina kwenye msiba, watu walikula na kunywa mpaka wakaacha, sasa mjomba akajiuliza "hivi hawa ndugu, hizi hela wanazo nunulia vitu vya msiba, kwanini wasinge jichanga na kumsaidia bibi kipindi zephania amekufa" hakuphata jibu ila akaishia kusema kwamba kweli sisi binadamu tunaroho za ajabu sana.
Baada ya msiba kuisha mjomba alipona vizuri, ndipo tukaanza maisha mapya kabisa mimi mjomba pamoja na shangazi yangu. Mjomba alibahatika sana, maana kipindi chote hicho hakuwai kufanya tendo la ndoa na mke wake, kwasababu ya mhatatizo yaliyo mkuta, vile vile aliitaji kupima kwanza ukimwi ndiyo awe huru kabisa na mke wake. Siku moja nimeamka tumbo linaniuma sana, nikamwambia mjomba kwa ishara ili nipelekwe hospitali, sasa mjomba yeye alikuwa tayari ameisha anza kazi, hivyo akampa mke wake hela ili yeye anipeleke nikapime afya, mjomba alipo ondoka shangazi alinisonya kisha akaongea mambo ya ajabu kweli, "yaani nimekubakiza wewe, lazima utatoka tu humu ndani, mnamumalizia mme wangu pesa kwani yeye ndiyo amewazaa " uwezi amini, shangazi alijiandaa kisha akatoka na kuniacha mimi nikiwa naumwa tumbo najigalagaza chini, yeye akaenda kutengeneza nywere zake, akaja amevaa wigi jipya kichwani.
Mjomba alipo toka kazini akakuta mimi nimeisha ingia chumbani, maana nilikuwa sitaki hata kumuona shangazi, mjomba akamwambia mke wake, "naona leo umependeza sana mke wangu, vipi Nelson anaendeleaje", shangazi akasema, "amepewa dawa, sasa hivi anaendelea vizuri sana" Kulipo kucha asubui, niliona nafanya ujinga sana kumdekeza shangazi yangu, maana namfichia siri zake kunusuru ndoa yake, lakini hata kunisaidia nipone hhataki, hivyo nikawaza kwamba, lazima nimwambie mjomba kuwa shangazi analeta mwanaume wake ndani, wakati akiwa kazini. Nilifikilia sana nitamuelezeaje mjomba mpaka aelewe kuwa mke wake anafanya hicho kitu, maana nilikuwa siwezi kuongea kabisa, ndipo wazo likaniijia kwamba, niandike barua kisha nimpatie ili yeye afatilie mwenyewe kama kweli mke wake anachepuka kwenye ndoa. Nilichukua kalamu na karhatasi kisha nikaandika kwamba. "Mjomba wangu najua kwamba siwezi kuongea wala kusikia, lakini kuna jambo humu ndani nimeshindwa kuvumilia kukaa nalo moyoni, maana shangazi kila siku za jumhatano, anamleta mwanaume mwingine na wanafanya mapenzi ndani ya chumba chako, hivyo naomba jumhatano umuage mke wako kwamba unaenda kazini lakini ujifiche uvunguni mwa kitanda bila yeye kufahamu, ukifanya hivyo utajionea mwenyewe jinsi shangazi yangu alivyo na tabia mbaya, nisamee mjomba wangu, maana sikukwambia mapema".
Nilipo andika hii barua, nikaitunza vizuri, kisha nikampatia mjomba asubui                         Mjomba alipo soma ile barua aliumia sana ,, ila alijikaza tu, ilipo fika jumhatano mjomba akawa amesahau kabisa, kama anhatakiwa kufanya nilivyo mwambia, na kweli siku hiyo hhawara yake shangaza alikuja na wakafanya kama kawaida yao. Ikanibidi niandike tena kumkumbusha, maana alikuwa bize sana na kazi, dooh alipo kumbuka akashangaa sana kwanini alisahau. Ndipo akajipanga kwa ajili ya kuangalia kama ninacho mwambia ni kweli. Jumhatano ilipo fika, kama kawaida yake alioga asubui, akamuaga mke wake kwamba, "naenda kazini, lakini gari bovu leo nitapanda pikipiki," shangazi akamkumbatia mme wake, ili kumuaga aende kazini, sasa wakati shangazi anaenda bafuni kuoga kumbe mjomba alikuja kujificha chumbani kwangu, ndipo akarudi chumbani kwa kunyhata! kisha akaingia uvunguni polepole. Shangazi alijiandaa vizuri akhatandika kitanda bila kujua kama kuna mtu chini yake, hazikupita hata dakika 15, mjomba akiwa chini ya uvungu, shangazi akapiga simu kwa hhawara yake akimwambia aje haraka nyumbani mme wake hayupo, mjomba hakuamini akahisi labda ni ndoto, akhataka kutoka ampige mke wake, ila akajikaza ili amuone huyo mwanaume wake, doh uvunguni kulimchosha lakini alijikaza sana. Kweli hhawara yake shangazi alikuja, mjomba akamsikia kabisa jinsi wanavyo peana mabusu chumbani kwake, akajikaza kisabuni pia. Sasa wakati wapo ndani shangazi akasema, "nimekuamdalia maembe mazuri mme wangu, ngoja nikuletee", alipo yaleta hhawara yake akasema "mhh , bebi, tutayakhataje maembe, kalete KISU mpenzi", huku mjomba anawasikia tu.
Kipindi wanakula maembe, shangazi akamsukuma hawara yake kitandani, wakavua nguo na kuacha maembe pembeni, kisha wakaanza michezo yao ya ajabu. Mjomba hakuamini jinsi kitanda kilivyo kuwa kinalia akiwa chini, ndipo akaamka na jaziba, akasema "mke wangu hichi nini" dooh shangazi akashtuka mpaka akazimia pale pale, ndipo mjomba akaanza kupigana na hhawara, mjomba alimdondosha chini yule hhawara kisha akamniga kwa nguvu mno, kumbe yule hawara alikuwa na nguvu, akamsukuma mjomba pembeni, kisha akachukua kile #kisu walicho kuwa wanalia maembe, akamchoma mjomba shingoni, alafu akakichomoa na kumchoma tena kifuani upande wa moyoni, mjomba hakukawia alifariki hapohapo.          Kipindi mjomba anafariki, mimi nilikuwa chumbani sijui kinacho endelea kabisa, ila nilisikia vishindo kama watu wana angushana ndani na kupigana. Baada ya dakika kama sita, hhawara yake shangazi alikuja chumbani kwangu kisha akanifungia kwa ndani na akabana komeo mlangoni ili nisitoke kutazama kinacho endelea, sasa wakati anarudi chumbani akakuta shangazi kaphata fahamu na akiwa bado uchi analia akisema kwamba, "bebi kwanini umemuua mme wangu sasa, siunge muacha, hivi huu mwili wake tunaupeleka wapi sasa", hhawara yake akamwambia, "bebi huyu mtu sikutaka kumuua kabisa, ila ningezubaa angetuua yeye, maana alianzisha ugomvi mwenyewe, lakini usijali maana Nelson nimemfungia ndani, hajagundua chochote, hivyo tuchukue mwili wake tukautupe kwenye lile shimo la kule mwembeni, tukimtupa humo usiku hakuna hatakae tambua hata mmoja kisha tutakaa kimya kabisa". Shangazi alianza kulia maana mjomba alifariki akiwa ametoa ulimi nje, huku damu zime sambaa chumba kizima, mimi niliendelea kukaa chumbani huku nikiwa na wasiwasi kwamba mjomba anaweza kuwa amepigwa sana, maana jinsi hhawara yake shangazi alivyo funga ule mlango aliniogopesha kabisa ,, nilikaa mule chumbani mpaka usiku njaa ikiwa imenipiga sana, maana nilishinda bila kula, ndipo hhawara yake shangazi akachukua mwili wa mjomba na kuufunika na mashuka, akauweka kwenye mfuko mweusi mkubwa wakishirikiana na shangazi, kisha wakaita bajaji usiku usiku, wakauweka ule mwili ndipo wakaenda kuutupa kwenye shimo kubwa sana lilio kuwa linatumika kutupa uchafu wote wa pale mtaani kwetu. Kipindi wanarudi ndipo wakaamua kunifungulia mlango, dooh nilishtuka kuona damu zimetapakaa ovyo mule ndani, sasa wakati shangazi anarudi nje kumlipa mwenye bajaji nikaingia chumbani kwake haraka haraka, sikuamini kuona zile damu za mjomba zilivyo tapakaa mule ndani, doooh nilipo angalia pembeni nikakuta kile kisu walicho mchomea mjomba maana kilikuwa kina damu ndipo nikakichukua na kwenda kukificha chumbani kwangu, shangazi alipo rudi ndani akaanza kufanya usafi ndani ili zile damu ziishe, nilishindwa nitamuuliza vipi kuhusu mjomba maana hata kuongea nilikuwa siwezi, siku ya kwanza ikaisha bila kumuona mjomba, siku ziliendelea kuisha mpaka wiki ikakhata bila kumuona mjomba, siku moja tupo sebreni wafanyakazi wake mjomba wakaja kumuulizia mjomba pale nyumbani, maana  walishangaa kumuona mjomba hajaenda kazini mda wote huo, wakamuuliza shangazi kwamba, "shemeji, mme wako yuko wapi maana wiki imeisha sasa bila kumuona kazini, na kazi haziendi kabisa, kibaya zaidi hajatoa taarifa yoyote kama haji" shangazi akasema, "mme wangu aliniaga kwamba m'memsafirisha kikazi kwamba anaenda singida na hatakaa huko mwezi mzima, sasa nashangaa kuona mna muulizia tena, kwani mmejisahau kama m'memtuma kikazi?" Wale wafanyakazi wenzake mjomba wakasema, "mme wako kakudanganya sisi hatuja mtuma popote kikazi na ofisi imetupa hii barua ya kumuachisha kazi hivyo akirudi mfikishie ujumbe wake" shangazi alianza kulia, maana ukweli alikuwa nao moyoni kwamba mme wake amefariki, ila wale wafanyakazi wenzake mjomba wakampa moyo kwamba "usijali shemeji mme wako hatakuja tu, usiwe na wasiwasi labda kweli ameenda kufungua miladi yake uko maana yule jamaa ni mfanya biashara sana". Mimi nilikuwa nhatazama tu pale huku nikiwaza nitaishi vipi na shangazi kwasababu shangazi yangu alikuwa hanipendi kabisa mimi na alikuwa akiniona mda mwingine alikuwa akitema mate chini akijisikia kinyaa, Siku moja nimelala usiku, nilianza kusikia upepo mkali sana unavuma, dah nilishtuka nikaamua kuamka na kukaa kitandani, lakini akili ilikuwa inanituma kwamba nichukue kile kisu nikiangalie tu, dah nilipo kishika kisu mikono ilianza kutetemeka sana kama vile napigwa shoti ya umeme, mara ghafla mzimu wa mjomba ukanitokeza ukutani! ukinielekeza kwa ishara na kwa hisia kwamba, "mwanangu nimeuawa, nimekufa mwanangu, shangazi yako kaniua, jitahidi utoke hapa whatakuua pia, shangazi yako ni mtu mbaya sana nimeamini mwanangu niliyo kuwa nikiambiwa na zephania" mjomba aliendelea kusema kwamba, "naomba icho kisu leo leo saa tisa, kachimbe shimo mbele ya nyumba yangu kisha kifukie bila mtu yoyote kukuona" dooh niliogopa sana, nikaamka kisha nikaenda kulala sebreni maana niliogopa kabisa kulala mule ndani, ilipo fika saa tisa mjomba akanitokezea tena akasema mwanangu, "kafanye nilivyo kwambia chukua kile kisu ukakichimbie mbele ya hii nyumba maana shangazi yako amelala, sitaki akuone" niliamka polepole kisha nikachimba shimo kiasi, nikakifunikia kile kisu" kisha nikarudi chumbani kulala. Hazikupita hata dakika 10 shangazi akaanza kupiga kelele akisema, "nisameee nisameeeee mme wangu sikufanya makusudi mme wangu" nikatoka kwenda kumuangalia kwake nijue nini kinacho msumbua, dooh kumbe mzimu wa mjomba ulikuwa unamtesa mule ndani, kibaya zaidi, mzimu ulimuijia umeshika kisu kama unhataka kumchoma shangazi. Mzimu ulikuwa unamuuliza, "kwanini mmeniua nimewakosea nini" shangazi akaamua kutoka chumbani akakimbia kuja ninapo lala mimi ili tuteseke wote, alipo kuja kwangu mzimu akapotea. Dooh sasa shangazi akaanza kuwa na mimi karibu ili asiwe anateseka chumbani kwake, hivyo kile chumba chake akakiacha vilevile akawa analala na mimi usiku. Siku moja asubui wakati shangazi anapanga chumba chake vizuri akashika shati la marehemu mjomba wangu, ile barua ikawa imedondoka chini, nilio iandika nikimwambia mjomba jinsi ya kumfumania shangazi na hhawara yake, doooh shangazi alinuna sana akanifhata na kusema, kumbe wewe ndiyo chanzo cha kifo cha mme wangu, bila wewe asinge kufa sasa utakoma kukaa humu ndani, mimi sikumuelewa ila niliogopa sana maana aliongea kwa hasila sana. Shangazi aliumia sana, alipo gundua kuwa mimi ndiye nilie sababisha mjomba agundue michezo yake michafu. Lakini alishindwa hatanifukuza vipi kwake kwasababu bila mimi yeye asingeweza kulala ndani kwake, kwasababu mzimu wa mjomba ulikuwa unamtesa sana usiku. Siku moja usiku mida ya saa tisa, mzimu ulimtokea hhawara yake shangazi ukiwa umeshikilia kisu kama unhataka mchoma shingoni, ukamwambia, “kwanini umeniua bila kosa, kwanini umetembea na mke wangu, naomba unitoe shimoni haraka njoo unitoea, nimechoka kutupiwa uchafu kila siku njoo unitoeeeeeeeeeeeeeeeeee!” dooh hhawara yake shangazi aliogopa sana ,, maana alikuwa hakuwai kukutana na mizimu tangu azaliwe. Zile kelele za mzimu wa mjomba na kwa uoga wa kuchomwa kisu, hhawara yake shangazi aliamua kukimbia kutoka chumbani akiwa amevaa nguo ya ndani tu. Alipo fika nyumbani akakuta shangazi yupo ndani nayeye anaogopa hata kutoka nje usiku, hivyo hhawara yake shangazi akagonga mlango sana ili afunguliwe mlango aingine ndani, maana kipindi anakimbia mzimu nao ulikuwa unamfhata nyuma.
Hawara yake shangazi alipo ona afunguliwi mlango, akaamua kuruka fensi na kuingia ndani, alipo enda kwenye dirisha la shangazi kumwambia afungue mlango, akakuta shangazi hayupo, hhawara yake shangazi akaamua kuja dirishani kwangu ili mimi nikamfungulie, alipo chungulia dirishani akakuta nimelala na shangazi chumba kimoja. Hhawara yake shangazi aliumia sana kutuona tumelala wote, maana alijua kuwa mimi natembea na shangazi yangu. Alipiga kelele tukamfungulia mlango, sasa wakati ameingia ndani, akashangaa kuona mzimu umeacha kumsumbua. Maana mzimu wa mjomba haukutaka kunisumbua mimi kabisa. Sasa wakati hhawara yake shangazi amekaa ndani, akaanza kumgombea shangazi kwamba, “kwanini unafanya mapenzi na huyu mtoto, kumbe nikiwa sipo unafanya huu upuuzi na mtoto wako sio, hivi unapepo gani we mwanamke kwani sikutoshi?”, shangazi akasema, “hapana mme wangu, sio kwamba nafanya nae mapenzi, ila chumbani kwangu hapa laliki kabisa, mzimu wa mme wangu unaniijia na kisu kama unhataka kuniua, na unanipigia kelele sana, mpaka nakosa usingizi”, hhawara yake shangazi akaamini maana alijifikilia uko kote amefukuzwa, lakini alipo ingia chumbani kwangu, mzimu ukatulia. Shangazi na hhawara yake waliteseka sana mpaka wakaiona nyumba yao chungu mno, mda mwingine walala nyumba za wageni kufurahisha nafsi zao, maana mule ndani wasingeweza kabisa. Hhawara yake shangazi akaamua kumshauri shangazi kwamba waende kwa mganga wa kienyeji, ili awasaidie dawa kusudi mzimu uache kabisa kuwasumbua.Walipo fika kwa mganga, walikaribishwa vizuri, kabla hata hawajasema shida yao, mganga akawambia, “najua shida yenu, na shida yenu ni nzito sana, maana mme muua yule bwana bila kosa hatawatesa sana na mta ishi maisha ya tabu mno, maana hizo adhabu manazo ziphata bado kabisa zingine zinakuja” Shangazi aliogopa , akasema, “tusaidie dokta tunateseka sana” Mganga akasema, “hii kazi ni ngumu sana maana, kile kisu mlicho muulia mlisahau kabisa kukificha na hatujui kiko wapi, maana ndicho mzimu unatumia kuwatesa nyie” Mganga akasema, “chukua hii dawa kisha kaifukie mbele ya nyumba yako, ili kuuzuia mzimu usiweze kuja, na ukija tu, utaona hiyo nyumba kama bahari” Kweli shangazi na mjomba walifanya hivyo, maana niliwaona usiku wanavyo chimba pale nyumbani na kuzindika zile kinga.
Walifanikisha mipango yao maana mzimu ulipokuja haukufanikisha kabisa kuingia ndani. Shangazi na hhawara yake walianza kucheka kwa furaha wakifurahia kwamba wame mkomoa mjomba. Siku moja mida ya usiku sana, niliota kama mjomba amenitokezea akisema kwamba, “mwanangu nimezuiwa na mizindiko humu ndani, naomba ukachimbue vitu walivyo vifukia, uvichome moto, na ujitahidi shangazi yako asikuone”, nilifanya kama nilivyo ambiwa ndotoni na mjomba maana niliamka polepole bila mtu yoyote kugundua kisha nikaenda kufukua zile dawa, maana niliwaona wanavyo zifukia kisha nikazileta mpaka jikoni na kuzichoma kabisa. Shangazi na hhawara yake walianza kuteseka upya, ikabidi warudi kwa mganga kumuelezea kuwa mzimu bado unawatesa. Mganga akawambia kwamba, “nileteeni shati lake lolote lile alilo kuwa anapenda kulivaa,” kweli shangazi pamoja na hawara yake walifanya kama walivyo ambiwa.
Mganga alipo letewa lile shati, Akaliwekea dawa katikati kisha akaaifunga ile dawa kwenye shati na kulikaza kwa nguvu ili mjomba asiweze kuingia ndani tena.Kweli mzimu wa mjomba uliangaika sana kuingia, maana walikaa wiki nzima wanafurahi sana, mjomba alinifhata ndotoni tena akasema, “mwanangu nimefungiwa tena kuingia nyumbani kwangu, naomba uanze kufuga njiwa hapa nyumbani ndiyo nitaweza kuja kwa urahisi”.Kweli nilifanya kama nilivyo ambiwa na mjomba maana nili nunua njiwa whatano, nakuanza kuwafuga, shangazi alifurahi nilipo waleta wale njiwa ,maana kumbe na yeye alikuwa anapenda kuwaona njiwa wakirukaruka pale nyumbani, kumbe hakujua kuwa wale njiwa whata mualibia dawa zake.Usiku ulipo fika mzimu uliingia ndani kwa shangazi, ukaanza kulia na kusema kwamba, “ mke wangu huwezi kunizuia mimi kuja hapa, lakini kama kweli unhataka nisije tena hapa naomba unitoe mule shimoni na unizike kaburini’Shangazi na hhawara yake hawakuwa na jinsi, wakaamua kwenda kwenye lile shimo mida ya usiku, ili waweze kumtoa mjomba mule ndani bila mtu yoyote kugundua.Walipo fika karibia na shimoni, walishindwa kuvumilia ile harufu , maana mwili wa mjomba ulikuwa unanuka sana! Walipo rudi nyumbani wakakuta mi nimelala sina shida yoyote siwazi wala siangaiki, walinionea wivu sana ila hawakuwa na jinsi. Hhawara yake shangazi aliogopa kurudi kwake akawa anakaa pale pale nyumbani.Baada ya miezi mi nne, kipindi na mimi naanza kuponapona maana nilikuwa nakaribia kumaliza mwaka ili niweze kusikia na kuongea upya.Shangazi na hhawara yake walianza kukonda sana ,, maana walikuwa wameathirika hivyo kutokana na mawazo ya kusumbuliwa wakaanza kupungua mili, sasa yule hhawara yake shangazi vidonda vilianza kumtoka na vilikuwa vinachelewa kupona, na vikipona vikikauka vinaacha makovu mwilini, shangazi alianza kupungua uso sana, anakuwa mwembamba mpaka watu wengine wakasema anamuawaza sana mme wake kumbe sio hivyo bali ilikuwa ni ukimwi ukichanganya na usumbufu wa ule mzimu, kibaya Zaidi akiba ya pesa waliyo kuwa nayo ilianza kuisha na hatukua tunakula vizuri. Hhawara yake shangazi alipo ona mizimu inamtesa sana na anaumwa, akaamua kwenda hospitali kupima ili ajue nini kina msumbua, alipo fika alipwa kila kitu ugonjwa haukuonekana, hivyo daktari akamuomba amruhusu kumpima virusi vya ukimwi. Mjomba aliogopa kupima, lakini hakuwa na jinsi akaamua kupima tu maana ugonjwa ulikuwa hauonekani, baada ya kupima daktari alimuita na kumwambia kwamba, “kijana tumepima afya yako na tumegundua kuwa umeathirika na virusi vya ukimwi, hivyo punguza mawazo na ule vizuri ila usisahau kufanya mazoezi ili upate afya njema Zaidi” hhawara yake shangazi, alishituka hapo hapo na akapoteza fahamu kisha akaanguka chini kwenye ofisi ya daktari”
Baada ya hhawara yake shangazi kuzimia mule ndani, daktali aliamua kumpatia huduma ya kwanza, sasa alipo phata nafuu akaja mpaka nyumbani akiwa na jaziba sana akimlaumu shangazi kwamba, "hivi kama ulikuwa unajua una maambuki ya virusi vya ukimwi, kwanini hukuniambia mapema" shangazi akashangaa sana kisha akamuuliza, "kivipi?" Yule hhawara akaanza kulia akisema kwamba, "haya magonjwa tunayo ugua kila siku, vidonda, na kukohoa mara kwa mara, kumbe sisi ni waathirika wa ukimwi", shangazi mwili wake ulianza kutoka jasho maana alikuwa muoga sana wa hilo gonjwa, akasema, "ehh mungu wangu tutaishije sasa ,, na hali ya maisha imekuwa ngumu namna hii," hhawara yake akamwambia hivi, "wewe ndiyo umeleta huu ugonjwa, mimi nilikuwa salama kabisa" shangazi akasema, "mimi sina uhakika maana, nakumbuka nilienda kupima nikiwa na mama Anna, mimi nilitoka salama, ila mama Anna aliphata maambukizi mpaka mume wake akamfukuza na kumwambia aondoke, ila baada ya mda alimsamee na kumrudisha nyumbani ili wamlee Anna"
Palepale hhawara yake shangazi akagundua wapi alipo uzolea ugonjwa. Kutokana na maisha kuwa magumu na pesa kuisha ndani kabisa, hhawara yake shangazi akamwambia kwamba, " mke wangu sasa sisi ni waathirika na hatuna mda mrefu hapa duniani, ni bora tuuze hii nyumba na hilo gari, tutumie tu pesa"  shangazi akakhataa akasema, "we hivi tukiuza nyumba na u, huu tutaishi wapi tena", hhawara yake akamwambia, tukisha phata hela tutaishi pale kwangu maana kodi ninayo lipa ni ndogo, ni bora tule vizuri tuwe na afya njema maana sasa hivi tumeisha kabisa" shangazi hakuwa na jinsi akaamua kukubali wauze ile nyumba ili wapate pesa kwa ajili ya matumizi mengine ya maisha.
Baada ya miezi kadhaa, Siku moja sasa, walikuja wageni pale nyumbani wanao hitaji kununua hiyo nyumba pamoja na gari, kipindi shangazi na hhawara wanhataka kuuza nyumba, wakashangaa kusikia nasema, "shangazi msiuze nyumba ya mjomba" doh walishikwa na butwaa kwanza, maana walikuwa na mda mrefu sana bila kusikia sauti yangu hivyo iliwashangaza, wale wanunuzi walipo waona wananishangaa ikabidi waulize, ",, vipi tena mbona mnashangaa hivyo kuna nini kipya hapo, au nyumba haiuzwi" Shangazi akasema hapana tunauza tu
Walinishangaa wote nilipo toa sauti yangu na kuongea tena, shangazi  aliendelea kushangaa jinsi ninavyo kuwa naendelea vizuri huku wao wanakonda tu na kuumwa kila siku. Ndipo shangazi akaamua kunijibu kwamba, “tusiuze nyumba kwa nini” nikamwambia, “sasa mkiuza nyumba tutakaa wapi tena?”, yule hhawara akajibu kwamba, “sasa hivi hali ya maisha imekuwa ngumu sana, na tunaangaika mno, siku zingine hatuli tunashinda na kulala njaa humu ndani, sasa ni bora tuuze hizi mali ili tuishi maisha mazuri, maana tutakaa kule kwangu kule kodi sio kubwa sana”, sikuwajibu chochote maana sikupenda kabisa kuona ile nyumba inauzwa, niliwaacha sebreni nikaingia chumbani kwangu. Kweli wale wanunuzi wa nyumba, walinunua lile gari na nyumba kisha wakatupa siku mbili za kukaa pale nyumbani ili tujiandae kuondoka na kwenda kukaa sehemu nyingine.
Shangazi na hhawara yake walipewa million 60 tu, kwa ajili ya zile mali walizo uza, hivyo walifurahi sana maana walihisi kuwa wamefika. Walipanga jinsi ya kuzitumia mali zao bila mimi kuniusisha hata kidogo, hivyo nisinge weza kuphata hata shilling mia moja kwe ile hela, kumbe wale watu walio uziwa vile vitu walikuwa ni mhatapeli kumbe wakapanga mikakati ya kutuma majambazi ili waje kutuvamia pale nyumbani. Sasa kipindi wote tupo sebreni mida ya tatu usiku, tulishangaa kuona majambazi wanaingia ndani wakiitaji kupewa ile millioni sitini ambayo shangazi na hhawara yake walipewa. Hhawara yake shangazi akawadanganya kwamba, “, ndugu zangu, pesa zipo benki hatuna pesa yoyote hapa,” jambazi mmoja alimpiga hhawara yake shangazi teke, akamwambia, “usijaribu kuongea chochote hapa, na kama unhataka kufa tuletee ubishi” Shangazi akasema,”mme wangu tuwapatie pesa tu wanaweza kutuua hawa ,” jambazi mmoja akasema, “hoo kumbe pesa zipo ndani, tunaitaji pesa zote hapa,” hhawara yake shangazi akawa mbishi, haitaji kabisa pesa ichukuliwe, ndipo kwa hasila wale majambazi wakaanza kumpiga sana na kuna jamaa mmoja alimpiga sana hhawara yake shangazi mpaka akaishiwa nguvu kabisa, mimi hawakutaka kunigusa maana walijua sijui pesa iko wapi kabisa. Shangazi na hhawara yake walipo ona wanaendelea kuumia, hawakuwa na jinsi ikabidi walete ile pesa kama ilivyo, ndipo wale majambazi wakawaacha pale, wakiwa na maumivu sana, kumbe hao majambazi ndiyo hao hao walio mpiga marehemu mjomba wangu kipindi anatutafuta mimi na bibi kipindi cha nyuma.
Hali iliendelea kuwa mbaya sana pale nyumba na tulikuwa tumebakiza siku moja tuondoke, shangazi akaanza kusema, “siwezi kukubali nyumba yangu ibebwe, siondoki hapa”, hhawara yake akamwambia, “mke wangu hatuna chetu hapa itatubidi tuondoke tu maana hata hati miliki ya nyumba tumeisha wakabidhi, hatuna jinsi itabidi tujiandae kuondoka hapa”, nikawambia kwamba, “ niliwambia msiuze nyumba, ona sasa tutaishi wapi tena, au ndiyo tutaanza kutengana mmoja mmoja”.
Kweli wale watu walio nunua nyumba walipo kuja, hawakutaka maelezo ila walicho hitaji ni sisi tuondoke na kuwaachia mali yao.
Shangazi alianza kulia akiitaji kusameewa, lakini hawakumuelewa, ila msaada walio taka kumpa shangazi ni kuwa mfanyakazi wa ndani ili awe anawapikia na kuwafuria nguo zao, shangazi akaona ni aibu, ndipo tukaenda wote kukaa kwenye chumba alicho panga hhawara yake shangazi, maisha ya pale yalikuwa magumu zaidi, maana kila siku mwenye nyumba alikuwa anagomba akiitaji kodi yake na sisi pesa hatukuwa nayo kabisa.
Shangazi alichoka kabisa na maisha, ndipo akaamua kumtafuta mama Anna ili aweze kumsaidia , akamwambia kwamba, “mama Anna shosti yangu, naomba msaada wako maana sahivi nina hari ngumu ya kimaisha, mme wangu katoroka na kaniachia majukumu yote, huwezi amini hapa nilipo sina hhata mia, nisaidie besti”, mama Anna akasema, “besti mimi nilipo fukuzwa na mme wangu, nilikuomba unisaidie ukakhataa,sasa kumbe kweli malipo ni hapa hapa duniani,  leo na mimi nakukhataa, alafu usimsingizie mme wako kuwa ametoroka huo ni uongo, taarifa zimeisha zagaa mme wako amekufa, na umeshirikiana na hhawara yako kumuua, hakuna asie jua hizi taarifa, na mmesadikika kuwa mmemtupa kwenye lile shimo kubwaaaaaa, kule mwembeni na ndiyo maana kuna harufu sana pale.”
Shangazi aliziba uso wake maana hakuamini kama siri yake ingejulikana, kisha akasema, “shosti yangu sahivi nina mawazo sana, sina hela ya kula naomba msaada wako”, mama anna akasema kamuombe hhawara yako pesa na mwaka huu mtakonda muishe maana tayari mna virusi vya ukimwi,mda wowote mnaondoka duniani, bora yangu mimi nakula vizuri na ninatumia dozi yangu ipasavyo”.
Shangazi aliona kama anaendelea kuumia, maana siri zake kubwa zinajulikana ,ndipo kutokana na mawazo mengi mno kichwani mwake akaamua kujiusisha na maswala ya ulevi, tulijaribu sana kumzuia ili aachane na maswala ya pombe lakini hakutuelewa kabisa,
Sasa huku nyumbani , huyu hhawara yake shangazi alishikwa na mararia, ilimtesa sana pale nyumbani na kibaya zaidi alikuwa anakhataa kula chakula, tulipo ona anazidiwa ikabidi tumpeleke hospital, ila hatukuphata huduma maana wali hitaji pesa hospitalini na sisi hatukuwa na kitu chochote, wakati tumelala usiku hhawara yake shangazi akaanza kuongea maneno ya kuhuzunisha sana kwamba, “nisamee Nelson nilikufanyia makosa sana, tulikutesa sana Nelson, Nelson niombee msamaa kwa mjomba wako, niombee msamaa kwa bibi,maana bila sisi wasinge fariki, nilimuua mjomba wako kwa mkono wangu mwenyewe, nafsi yangu inanisuta kila mda” nikamuliza swali kwanini ulimuua mjomba wangu lakini, alifanya kosa gani ,, “hhawara yake shangazi kipindi anaachama mdomo wake kunijibu alizidiwa zaidi akanishika kwa nguvu mikono kisha akafariki hapo hapo”
Shangazi yangu aliiona dunia yote chungu, alitamani kujiua nikamshikilia na kumpa moyo, akasema “tutaishi wapi ,, tamaa zimeniponza leo nimewapoteza wote, mme wangu angekuwepo nisinge teseka hivi,  tusinge lala njaa hivi, ehhh mme wangu nisamee, nisamee Nelson nilikufanya usisikie wala kuongea kwa sababu ya tama, nimeathirika , na magonjwa sababu ya tamaa, nimemuua mama yangu sababu ya ujinga wangu , nitaenda wapi mimi ,”
Shangazi aliongea maneno hayo na siri zake zote kwa sababu alikuwa amelewa,maana alizani pombe ndizo zinaweza kumpunguzia mawazo yake kumbe zina muhaibisha, ilifika mpaka asubui tukiwa tumelala na mwili wa marehemu,  maana hakuna hata mpangaji mmoja alie kuja kutuona, maana hhawara yake shangazi alkuwa na tabia mbaya , yaani yeye hatembelei wagonjwa, haendi kwenye misiba, na hakuwa na ukaribu wowote na watu wenye mhatatizo, hivyo alipokuwa anaumwa hakuna hata mmoja alie kuja  kumjulia hali, na hakuna hata mmoja alie kuja kwenye msiba wake, dooh niliphata kazi kubwa maana hata msaada wa kuchimba kaburi hatukua nao,ikanibidi niende kuomba msaada polisi ili wanisaidie lile swala la kuzika, kweli nilisaidiwa mpaka akawa amezikwa makabulini, ila nilishangaa maana hakuna hata mtu mmoja alie kuja zaidi yangu na shangazi, na mimi ndugu zake nilikuwa siwafahamu hivyo nikaamua kuomba misaada ya serikari.
Shangazi aliendelea kunywa sana pombe,na alikuwa akifika kwenye vibanda vya pombe, wanaume wawatu wana mnunulia pombe kisha wanatembea nae kimwil,i mpaka akazoea maana hakuwa na jinsi, sababu hakuwa na pesa ya kulipia pombe zake.
Siku moja shangazi alilewa sana usiku, sasa wakati anatembea kurudi nyumbani , akawa ameanguka vibaya sana chini na akapiga kichwa chake kwenye jiwe kama bibi alivyo farik,i na yeye akafa hivyo hivyo yaani mda huohuo, nilipo letewa taarifa kuwa shangazi yako amekufa  doooooh, nilichoka sana akili.
Baada ya kugundua, shangazi amefariki, sema kweli nilichoka akili mno, maana sikuwa hata na shilingi mia ndani, ikanibidi kwanza nikae bila kufatilia mwili wake ulipo, maana sikuwa hata na hamu, ila kipindi nipo ndani nimejificha, nikashangaa kuona vijana wa ule mtaa wetu wameleta mwili wa marehemu shangazi yangu, eti nikao nao ndani nitazika siku nikijisikia, nilianza kulia nikasema, ", naogopa kulala na marehemu, alafu nimechoka kufiwa, naombeni msaada wenu ndugu zangu, nisaidieni mimi siwezi kuzika mwenyewe", jibu walilo nipa lilikuwa baya sana kwamba, "kaka sikiliza ingekuwa amekufa mtu mwingine huu mtaa wetu, tunge saidiana kuzika, lakini huyu mama, hatujawai kumuona kwenye msiba wowote ule zaidi ya kukutana kwenye sherehe na sehemu mbalimbali, hivyo na yeye kafa hatuwezi kuonyesha ushirikiano wowote ule ajizike mwenyewe", dooh nilimuangalia marehemu shangazi yangu, nikakumbuka mabaya yote aliyo nifanyia, ndipo nikapanga kukimbia na kutoroka ule mtaa usiku, ili nisiendelee kuangaika na msiba wake, maana sikuwa hata na senti ndani na sikuwa na msaada wowote ule, kweli ilipo fika usiku nikaandaa vitu vyangu ili nitoloke ili niamie sehemu nyingine kabisa na niachane na mambo ya kuzika mimi, maana niliwaza kwamba, "ndugu na jamaa wakisikia harufu ya mwili wa shangazi whatamzika tu bila kupenda". Nilichukua mashuka ya hhawara yake shangazi aliyo yaacha, nikaufunika ule mwili wa marehemu shangazi, huku machozi yakiwa yananitoka kabla sijatoroka,  nikasema, "shangazi yangu naomba unisamee kama nitakuwa nimekuudhi, juzi tu nimetoka kumzika yule bwana yako, kwa mateso na shida, leo tena wewe umekufa ,, mimi nakuzikaje na sina hata shillingi mfukoni, jamii yote imewakhataa kwamba, mlikuwa ni watu wa kujitenga, hivyo sina msaada kabisa, sina jinsi itabidi niondoke tu, kama wakikuonea huruma basi whatakuzika tu wananchi wa hapa," sasa wakati naondoka, simu ya shangazi ikaita, nilipo pokea, alie piga akakhata, ndipo nikaphata wazo kwamba nimpigie baba yake mzazi shangazi, labda angeweza kuja kusaidia katika mazishi ya mwanae, nilipo piga simu, akapokea mtu mwingine, nikamsalimia kisha nikamuuliza, "hallow, nilikuwa namuitaji baba yake na mke wa mjomba, maana shangazi amefariki hapa na nipo mwenyewe hakuna mtu yoyote wa kunisaidia", yule jamaa akasema, "dahhh kijana kwani huna taarifa huyu mzee alisha fariki mda mrefu sana kwa presha, yaani mpaka tuna msahau sahivi, na hii simu yake naitumia mimi maana alifariki mikononi mwangu, sasa watu wakipiga nawapa taarifa kuhusu kifo chake", sikuwa na jinsi nikakhata simu, kisha nikalala ndani, nikaacha kutoroka, asubui ilipo fika ikanibidi niende mpaka kwa mama Anna ili nimuelezee wenda angenisaidia, ila nilipo mwambia akasema kwamba, "we Nelson punguza huruma, huyo mwanamke alimuua mjomba wako na akamtupa lile shomo kubwaaaaaa, la kule mwembeni, hivyo na yeye ungemtupa humo humo ili hata mzimu wa marehemu mjomba wako upumzike kwa amani" yale mawazo niliyaona mabaya, ikanibidi niende kwa mwenyekiti kumuelezea hari iliyo nikuta, ili aweze kunisaidia, maana nilikuwa naogopa sana kulala na mtu alie kufa ndani,niliumia zaidi maana, nilikuta mwenyekiti anaumwa sana, hivyo asinge weza kunisaidia kabisa, dooh nilihisi dunia yote chungu, maana hata chumba nilikuwa nimeanza kukiogopa, na polisi niliogopa kwenda maana nilihisi whatanihisi mimi muuaji, kila siku naomba misaada ya kuzikiwa ndugu zangu, Siku ya pili iliisha bila mafanikio yoyote yale, kibaya zaidi mwenye nyumba alikuwa ananigombeza kila siku, akisema "hivi nyie watu mmeniona mimi kama msaada wenu ehhh, kodi ya nyumba hamlipi na mnakaa na mizimu ndani, ebu toa huo mwili ukauzike, unatia mikosi na laana ndani ya nyumba yangu, leo usipo toa mzigo wako nakufuza nao maana hakuna hatakae kubalu kupanga hicho chumba, wakijua kuna mtu amefua humo", dooh nilijaribu kuomba vijana wa pale mtaani japo wanisaidie sikufanikisha, ila kuna jamaa mmoja akasema, "kaka mimi kwa upande wangu nakuonea huruma sana ndugu yangu, lakini nikionekana nakusaidia tu, nita laumiwa sana na wananchi wenzangu, maana hao watu walikuwa na majivuno sana kipindi wana pesa, na hawakujiusisha kabisa na wenzao kipindi wana mhatatizo, hivyo jitahidi tu kaka ukaombe nafasi pale makaburini umzike, maana hawa watu wa kijijini kwetu roho zao kama za kutu wakiwa na hasila na wakiamua kitu uwa hawarudi nyuma na kusamee". Nilitoka pale nikiwa na hasila sana kisha nikarudi ili nibebe vitu vyangu nitoroke, wakati nafika tu nikamkuta mwenye nyumba mlangoni na vijana wawili, akasema, "kijana nimekuvumilia sana na huyo mtu wako humo ndani, sasa utambeba kichwani uondoke nae, na utatoka hapa kwangu, yaani nakuomba usirudi tena, hata nguo zako usichukue nitauza kila kitu humo ndani nirudishe pesa yangu ya kodi, maana naona nawadekeza bure nyie watu", huwezi amini wale vijana waliubeba ule mwili wa marehemu kisha wakanitwisha kichwani eti niupeleke mwenyewe makaburini kisha niuzike, dahh sikuwa na jinsi ikanibidi nifanye vile, nilipo fika pale makaburini nikaomba jembe kwa majirani wa pale, kweli walinisaidia, kisha nikaanza kuchimba kaburi kwenyewe ili nimzike shangazi, wale watu wa makaburini walinionyesha sehemu ya kuchimba na wakaniomba pesa ila nililia mpaka wakanionea huruma wakasema, "sawa chimba tu kijana" nilichimba mpaka mikono yote ikauma na nikiangalia shimo haliishi tu, doooh nilichoka mikono nikaamua kumfukia shangazi hivyo hivyo kabuli likiwa fupi. Kumbe mvua ilivyo nyesha, ilifukua ule mwili wake tena, ikabidi watu wa maeneo yale wachimbe zaidi, mimi  nilirudi pale kwa baba mwenye nyumba, ili nimuombe msaada wakukaa japo siku moja ila alikhataa khatakhata, sikuwa na jinsi ndipo nikaamua kuwa nalala tu pale nje ya eneo lake, kisha asubui nakusanya mchanga unao letwa na mvua, alafu namuuzia yeye mwenyewe anajengea, maana alikuwa fundi, baada ya miezi sita nikiwa napambana nikafikisha elfu 30 mfukoni, nilifurahi maana nilikuwa naiona nyingi sana, dah lakini isinge tosha mimi kuphata chumba na kuanza maisha yangu, ndipo siku moja nikaphata wazo kwamba niende kwa mama anna ili anisaidie niweze kukaa kwake kwa mda, nilipo fika pale nilicho kiona ilikuwa ni maajabu sana , wa mungu, maana nilikuta, yeye na mme wake wamezidiwa kabisa wanaumwa sana, maana ukimwi ulikuwa umewhatafuna sana mwilini, yaani hawhatamaniki kabisaaa, nilipo fika nikakuta Anna analia akisema "mama nina njaa, naomba chakula" mama anna alikuwa amekonda mno aliishiwa nguvu , hata kupika hakuweza, hivyo Anna alikuwa analia tu bila msaada wowote, na ukimuangalia baba anna nae mwili umeisha kabisa, "mimi niliwaomba kwamba, ", naombeni mnisaide nikae hapa kwenu, maana sina sehemu ya kuishi, baada ya mda nitaondoka," baba anna akasema "kijana yangu nhatamani sana ukae hapa kwangu, lakini nadaiwa sana pesa za watu na wamesema wanakuja kuchukua hii nyumba, mke wangu ameleta ugonjwa ndani, unatuteketeza vibaya sana, nina mtoto wangu mmoja hataangaika sana, maana ndugu zangu wana roho mbaya whatanitesea mtoto, naomba umchukue huyu mtoto ukaishi nae popote utakapo kwenda, akikua mwambie maneno niliyo kwambia," doooh nilitamani kumkhataa Anna maana maisha yalikuwa magumu sana upande wangu, ila sikuwa na jinsi ikabidi nimchukue kisha nikatoka pale haraka haraka maana sikutaka na wao wanifie mikononi mwangu, mama Anna na mme wake hawakukaa siku nyingi nikaphata taarifa kuwa wamefariki dunia pia, sasa mimi huku sikuwa na sehemu kabisa ya kukaa bali niliangaika na yule mtoto , maana nilijitahidi kufanya kazi kusudi anna aweze kuweka chochote mdomoni. Sasa wale watu walio kuwa wamenunua ile nyumba ya mjomba, walikuwa wanateseka sana mule ndani, maana shangazi yangu waganga walimpa  uchawi mwingi, hivyo ile nyumba ikawa na mizindiko mingi sana, hata kisu kilicho muulia mjomba nilikifukia pale, hivyo hakuna mtu yoyote alie weza kukaa hapo, maana wale walio nunua nyumba walifiwa na watoto wao, walipo uza ile nyumba kwa walio amia wakafiwa pia, hivyo ile nyumba ikabaki bila mtu yoyote ndani, siku moja nilikuwa nafanya kazi ule mtaa hivyo nikasema "ngoja niende humo ndani nikaombe maji ya kunywa maana nilikuwa nimepakumbuka nyumbani", alafu nilikuwa na kiu sana, ila nilishangaa mno, kwasababu sikukuta mtu ndani,maana  niligonga sana mlango hakuna alie fungua, ndipo nikaamua kuingia ndani kuangalia kuna nini, dah sikukuta mtu hata mmoja kila mtu ameogopa nyumba, kwamba niya kishetani.
Doohh mimi sikuchelewa maana nilikuwa nimeisha pazoea pale nyumbani ndipo nikakimbia haraka haraka kumfhata Anna ili tuishi pale, maana nilikuwa nimechoka sana kulala nje na kwenye vibanda, anna alifurahi sana tulipo kuwa pale hivyo na mimi nikaanza kupambana sana kutafuta hela ili tuweze kula na kusukuma siku mbele, siku moja usiku nimelala nikaanza kusikia upepo yaani kama vile mashetani yanakuja kutu ua, dooh niliogopa sana lakini nikapiga magoti kumuomba mungu anisaidie nisife, mara ghafla nikasikia Anna analia chumbani kwake yaani kama vile anakabwa koo, nikajua tayari hapa tumeisha, kipindi sasa natetemeka naogopa hata kumfhata anna chumbani kwake, mzimu wa marehemu mjomba wangu ukanitokea na kusema kwamba, "ninakulinda sana mwanangu hakuna wa kukutesa hii nyumba ni yetu na hakuna hatake weza kuishi hapa bila wewe kukaa hapa" pale pale nikasikia anna ameacha kupiga kelele, watu walikuwa wananishangaa sana mimi kukaa pale, maana ile nyumba ilikuwa inaogopwa mno na ilitelekezwa kwa mda mrefu hivyo watu walijua lazima na sisi tutakufa tu. Maisha yaliendelea vizuri maana nilikuwa najiusisha na mambo ya ujenzi ili tuweze kuishi vizuri na anna, siku moja nikaphata wazo la kumuanzisha anna shule ya msingi, maana Anna alikuwa mpole na muelewa sana hivyo nikakapenda sana kale katoto, sasa wakati naenda shule kuangalia nafasi ili Anna aanza shule, kumbe anna alikuwa anachezea kibiriti chumbani, anawasha moto anazima, akiwasha njiti anaweka mdomoni anazima, sasa wakati anafanya vile, kile kiberiti kikadondoka kwenye nguo kavu, moto ukaanza kutanda ndani anna akiwemo humo humo, huwezi amini nyumba iliteketea, Anna alizidiwa na moshi , alipiga kelele mno, ila watu hawakuja kusaidia maana waliogopa ile nyumba kuwa ni ya kichawi, kila kitu kikaugungua mpaka nyumba ikabomoka anna akafia humo humo ndani ,,
Maisha  yangu yalikuwa magumu sana, ikafika hatua nikaona bora na mimi nife tu, maana sikuona tena thamani ya kuishi duniani, ndipo nikaphata wazo la kwenda duka la madawa ili ni nunue sumu nife, maana nilifikilia maisha yale ya kulala nje nikaona sio kabisa.
Nilipo fika dukani, nikamkuta bibi flani hivi anauza dawa nikamwambia, “bibi samahani naomba unisaide dawa ya kujiua maana sioni faida yangu kabisa hapa duniani”,yule bibi akasema, “ebu kaa kwenye hicho kiti kwanza tuongee”. Nikakaa, kipindi namsubilia aanze kuongea akasema, “kijana yangu, kwanini unhataka kuondoa maisha yako wakati wewe bado mdogo hivyo, usione kama wewe unamatitizo ukazani ni wewe tu, kila mtu duniani lazima apitie mhatatizo, na usione watu wamenyamaza barabarani wanacheka tu, wanamatizo yao mengi na wamekubaliana nayo, nakuomba kijana yangu ukitoka hapa, kaa chini tafuta maisha, usijifikie kujiua ni dhambi sana hata kwa mwenyezi Mungu, na ukipambana utasahau mhatatizo yako yote, itakuwa sio mhatatizo tena,bali zitakuwa story una simulia watu yaliyo kukuta kipindi cha nyuma, usinione hapa bibi yako, mimi nilifiwa na watoto wangu wote pamoja na mme wangu kwa siku moja, nilihisi dunia yote chungu ila sahivi nimezoea na maisha yanaenda”
Yale maneno ya yule bibi yalinipa faraja sana, nikaona hakuna haja ya kufanya dhambi niliyo taka kuifanya.
Lakini nilipambana sana kutafuta maisha, ila sikufanikiwa kabisa, maana nilianza kazi ya ulinzi kwa mama mmoja hivi, lakini alikuwa na roho mbaya sana hata zaidi ya shangazi na nilikaa nae miaka saba namfanyia kazi, ila mateso yake yalinichosha sana.
Siku moja nilikaa nikawaza na kujishauri mwenyewe nikaphata wazo kuwa nitoke ile sehemu nisafiri kabisa kwenda jijini Dar es salaam kutafuta maisha, lakini nilikuwa naumiza sana kichwa, je nikienda dar nitaishi wapi, wakati sina ndugu wala rafiki yoyote wa kunikaribisha.
Ndipo nikhatafuta nauli ili niondoke pale, wakati nhataka kuondoka nilipo muaga bosi wangu aliumia sana, akaanza kusema, “usiondoke Nelson nitakuongezea mshahara, baki kwangu maana vijana wengine ni wezi nikiwaleta hapa whataniibia sana vitu vyangu, mimi nimekuzoea wewe naomba usiondoke”.
Nilifikilia sana je nibaki, lakini akili yangu ilikhataa kabisa kubaki pale, ndipo nikaamua kwenda kituo cha mabasi ya kwenda dar, es salaam.
Wakati nipo safarini, nilikuwa nimekaa na baba mmoja hivi tajiri sana, maana kila basi lilipo kuwa lina simama yeye anatoa waleti yake imejaa kweli pesa ananunua vyakula na kunigawia mimi pia, nilimuelezea mhatatizo yangu kuwa naenda sehemu nisiyo ifahamu na sina ndugu yoyote kule ila yeye alikuwa analala sana kwenye basi anisikilizi kabisa ninacho mueleza.
Safari ya dar es salaam ilikuwa ndefu sana, na ilikuwa inachosha mno, maana nilishangaa basi linaondoka tu hata atufiki.
Hivyo tulikuwa tunalala na kuamka bado basi lipo njiani. Kipindi basi lipo katika mwendo mkali sana, dereva bahati mbaya nayeye kumbe alikuwa amechoka mno, hivyo ile stelingi yake ya gari ikaama, ndipo basi ikaacha njia, alipo shituka akawa amechelewa tayari, hivyo basi likaanza kwenda mlimani, lina angusha miti, watu walilia ,, tulijibonda sana ndani ya basi, kumbe dereva  na yeye ali ruka na kutoka nje, sasa basi lilipo fika juu kabisa ya mlima, likagonga mti mkubwa kisha likasimama,  kipindi limesimama, tukatulia wote, kumbe tulikuwa juu ya mlima, hivyo lile basi likaanza kurudi nyuma likibinuka, dooh, “sitaisahau ile safari ,”, basi lilirudi kwa kubinuka mpaka chini kule tulipo toka, damu zilijaa mule ndani, watu tulikuwa tunagongana, baba mmoja alikuwa na familia yake yote mule, walifariki na hakuna alie pona zaidi yangu mimi na dereva alie ruka, lakini niliumia sana mwili, nilijaa na vidonda karibia mwili mzima, ndipo magari ya hospital yakawa yamefika pale, na mimi nikajikuta nimefikishwa hospitali bila kujua.
Baada ya matibabu nikaendelea na safari ya kwenda Dar es saalam, sasa wakati nafika ubungo kwa mara ya kwanza, sikujua kabisa niende wapi, maana sikuwa na ndugu wala rafiki ninae mjua, ila wakati nipo barabarani niakona bango kwenye nguzo limeandikwa, “kuna nyumba zinajengwa hivyo kama wewe ni fundi au kama unahitaji kuwa kibarua piga namba 0769510060”, sikuchelewa nikapiga simu hapo hapo, maana ile simu ya marehemu shangazi yangu nilikuwa nayo mimi.
Nilipo fika kazini, watu wa dar es salaam walinishingaa sana jinsi ninavyo piga kazi kuwashinda hata wao, na nikaomba niwe nalala pale pale kwenye nyumba ili niwe mlinzi, kwa sababu nilifurahi maana nilikuwa nalipwa vizuri kila baada ya kazi.
Baada ya miezi sita, nikapanga chumba, na nikabadirisha kazi, kisha nikaanza kuuza, “housing za simu”.
Siku moja nipo barabarani nikakuta na dada mmoja hivi anaitwa vaileth, huyu dada alikuwa anhatafuta “housing ya simu” maana kava ya simu yake ilikuwa imechakaa, alinisimamisha na kusema kwamba, “samahani kaka naweza kuphata kava ya hii simu yangu?” nikamwambia, “simu gani” akanionyesha simu, ila kwa bahati nzuri au mbaya nilikuwa sina hiyo kava ila nikamwambia kwamba, “dada nisamee tafadhali nimeishiwa hizo kava lakini, kesho au leo jioni, nikifhata mzigo naweza kukuletea, labda uniachie namba yako ya simu, mimi nikiliphata nitakupigia tuonane ili ulifate”
Tulibadilishana namba kisha nikaondoka, kweli niliphata kava ya simu yake lakini siku hiyo nilikuwa najisikia vibaya sana, hivyo nikampigia simu na kumwambia kwamba, “besti kava nimeliphata lakini leo najiskia kuumwa hivyo siwezi kufanya kazi kabisa labda kesho nitakutafuta ili nikuletee”
Vaileth akasema “hapana kaka, nimelitafuta ilo kava kwa mda mrefu sana naomba unielekeze ulipo ili nilifate hapo hapo nyumbani kwako”
Niliogopa kumruhusu aje maana nilikuwa nakaa sehemu mbaya sana, na ndani kwangu nilikuwa sina vitu kabisa hivyo nikaogopa aibu. Nilishangaa kuona ananilazimisha apajue, hivyo sikuwa na jinsi nikamuelekeza, hazikupita hata dakika 30 vaileth akawa amefika ndani kwangu.
Nilimuonyesha kava akasema, “heeeeee , asante kaka umejuaje kuwa napenda hii langi ya njano ,”
Nikamwambia, “mimi ni mzoefu wa kazi yangu hivyo nikimuangalia tu mtu najua anapenda nini” alinilipa pesa yangu kisha akasema nikiphata shida nitakupigia, mimi nikacheka kisha nikamuuliza, “hivi dada mpaka upate shida ndiyo unipigie hauwezi kupiga tu tukaongea na kushauriana maisha”, alicheka pia kisha akasema, naona umejitahidi sana ndani kwako pazuri, “mhhhhh” nikaguna,  akauliza mbona unaguna sasa, nikasema, “lazima nigune maana unanisanifu, hivi unapo sema humu ndani pazuri, kuna nini kizuri”, alinijibu na kusema kwamba, “kutokana na kazi yako unayo ifanya, sikutegemea kama umejipanga hivi, inaonyesha una akili kubwa sana ya maisha”, nilimwambia kwamba, “nimepitia mambo mengi sana magumu, hivyo  lazima nipambane nifike mahara pazuri”
Niliendelea kuwasiliana na vaileth, na alikuwa akiniambia mambo yake mengi sana, na mda mwingine alikuwa anakuja kwangu tunakaa na kuongea kwa mda mrefu sana, siku zingine alikuwa ananunua vitu vya ndani analeta kama mashuka, mito, vyombo vya kupikia, mpaka nikajikuta naingia katika mahusiano ya kimapenzi na vaileth.
Tulipendana sana, mpaka tukawekeana ahadi ya kuoana, yeye alikuwa anaishi kwao, Ila wazazi wake walikuwa hawaitaji mtoto wao kujiususha na maswala ya mapenzi kabisaaa.
Siku moja naongea nae kwenye simu usiku, nikasikia mama yake anaingia chumbani na kumwambia, “hivi kumbe siku izi unachelewa kuja nyumbani kumbe umeanza tabia za wanaume, sasa hii simu naichukua na sikupi tena, na humu ndani utakuwa hutoki kabisa”
Yale maneno ya mama yake vaileth yaliniumiza sana maana nilikuwa nimeisha mzoea tayari yule dada, baada ya miezi kadhaa kuisha nikiwa sijaonana wala kuwasiliana na vaileth, kodi ya nyumba ikawa imeisha, na mama mwenye ile nyumba alikuwa anategemea sana kodi maana alikuwa hana mme wala kazi yoyote, dooh nilishangaa kuona ananigongea mlango, mwenye nyumba na akasema, “kijana yangu kesho andaa pesa yangu, ukitoka kazini nakuja kuifhata,”
Dooh hali yangu ilikuwa ngumu sana mwezi huo, hivyo nilivyo rudi kutoka kazini yule mama akaja tena mlangoni akasema, “Nelson rafiki yangu nimefhata pesa, sasa hivi nina hari mbaya,” ikabidi nimkaribishe ndani ili nimuelezee jinsi hari yangu pia ilivyo ngumu.
Sikuamini kusikia maneno ya ajabu aliyo sema, maana alisema kwamba, “kama upo tayari nilale leo chumbani kwako, nitakusogezea mwezi mzima, maana kama unavyo jua sina mme ila hata mimi napenda kufanya ilo tendo, niruhusu tulale wote hapa, unijari na mimi nikujali tusaidiane maisha”, nilikhataaa kabisa nikagoma lakini alinisukuma kitandani nakupanda juu ya mwili wangu huku akinishikashika sehemu nyeti kunipa hamu akisema, “nisaidie Nelson tufanye mara moja tu”
Kipindi yupo juu ya mwili wangu, kumbe vaileth alikuwa amephata nafasi ya kwenda kwenye harusi ya dada yake hivyo akatoroka na kuja kwangu ili anielezee kuwa ana mimba yangu, alipo fika akasukuma mlango na kumkuta mama mwenye nyumba yupo juu yangu ananipapasa, huku mimi nipo chini palepale kitandani.
Baada ya mpenzi wangu vaileth, kunikuta na mama mwenye nyumba ndani tena ubaya zaidi pale kitandani, alianza kulia ,, dooh, aliumia sana kisha akisema kwamba, "Nelson kumbe we ni maraya, kumbe wewe ni muongo Nelson, yaani mimi naphata mhatatizo mengi nyumbani kwa ajili yako, kumbe hunipendi unanidanganya, sasa kama hii ndiyo tabia yako, hata hii mimba yako natoa". Dooh nilishangaa nikamuuliza, "vaileth una mimba?" Palepale yule mama mwenye nyumba akasonya na kutoka nje kwa hasila. "Vaileth akaishiwa nguvu kabisa, akaanza kulia tena" nikamshika mkono ili nimuelezee kitu kilicho sababisha atukute katika hali ile, ila alisema, "usinishike, yaani nakuomba tena unikome na usinizoee, hivi unajua nimetoroka ndugu zangu kwenye harusi kwa ajili yako, kumbe hizi ndiyo tabia zako za kutembea na hawa watu wazima zaidi yako, sasa naondoka na hapa sirudi tena, na usije kunitafuta katika maisha yako yote". Kipindi vaileth anageuka kuondoka, nikamshika nguo yake kisha nikapiga magoti chini na kumwambia kwamba, "nisamehe mpenzi wangu, najua nimefanya kosa, lakini hili kosa ni shetani tu, nhawara sijapanga kufanya hivi ni shida tu za dunia zinapelekea kufanya haya yote mpenzi wangu, naomba tukae tupange kuhusu hiyo mimba ", vaileth alinisukuma kisha akaondoka kwa hasila na chuki kubwa sana kwangu, Alipo ondoka nikajaribu kumfhata ila alikimbia akionyesha wazi kuwa aniamini tena kama mwanzo, sasa wakati narudi chumbani kwangu, nikiwa kitandani nalia nikimuwaza Vaileth, akarudi tena yule mama, akasema, "Nelson, najua nimekuudhi lakini tatizo limeisha tokea tayari, we muache aondoke tu, mimi nipo kwa ajili yako," nikamwambia, "ondoka ndani kwangu, yaani sitaki kukuona hata kidogo", yule mama alinuna akasema, "yaani hujanilipa kodi yangu, alafu unanifukuza kwangu, kumbe wewe jeuri ehh, sasa naomba kesho uondoke" dooh nilifikilia sana nikiondoka pale naenda wapi tena, sikuwa na jibu kabisa, ikanibidi nikubaliane tu na shida zangu niwe mpole, nikasema, "nisamehe ni hasila tu lakini leo siwezi kufanya unavyo taka wewe",  huwezi amini, yule mama alikuwa king'an'ganizi sana, akaanza tena kunishikashika mwili wangu, akakaa tena kitandani kwangu, kisha akavua nguo zake zote na akalala juu yangu, akiitaji na mimi pia nibaki uchi tufanye tendo, sikuwa nampenda kabisa yule mama, na nilikuwa nachukia kumuona anavyo fanya vile vitu ila sababu ya u, wangu alinithawara sana nyumbani kwake, sasa kipindi yule mama ananilizimisha nivue nguo ili nifanye nae lile tendo, kiukweli nilikuwa nakhataa, lakini sikutaka ajue kama nakhataa, kwasababu nilikuwa namwambia kijanja kwamba, "subili kwanza, mbona bado mapema ,, yaani leo tu tumejuana na leo hii hii unhataka tufanye" yule mama alikuwa mjanja kweli, hakuniachia bali alianza kusema, "Nelson una macho mazuri ,, nakupenda sana, yaani unanivutia mnoo", kumbe Vaileth kipindi anakimbia kuondoka, alifika sehemu akasimama kisha akajifikilia jinsi alivyo na ujauzito wangu, akaona ni bora tu arudi nyumbani kwangu, ili anisamehe na hayo mhatatizo yaishe, na wakati huo mama mwenye nyumba amevua nguo zake kazidondosha chini hapo anhataka tufanye alafu kibaya zaidi mlango upo wazi! Kipindi sasa yule mama anajichekesha, huku na mimi pia nacheka kinafiki ilimladi tu nimdanganye danganye asifanye mapenzi na mimi, vaileth alikuja tena ili anisamehe akakuta tena yule mama yupo juu ya mwili wangu na amevua kabisa mavazi yake yote, dooh alichoka, akasema, "Nelson ulaaniwe we kaka, unanifanya nini hichi Nelson, yaani nimekuja kukusamehe, kumbe hujakoma tu na tabia yako, wee mama kwanini unanikosea hivi", yule mama akasema, "looh toka tu nje umekuwa kin'gan'ganizi sana we dada" mimi nikasema, "hapana usimwambie hivyo mpenzi wangu nampenda" vaileth akasema wehh nikome, unampenda nani, nakuuliza unampenda nani, yaani kujipendekeza kote huku kumbe wewe ni mjinga hivi, hivi kwa fumanizi hili unaweza kujitetea nini?" nilishindwa nijitetee vipi kabisa, niliona aibu sana, Vaileth alinuna, ndipo yule mama akasimama kwa zalau na akavaa nguo zake, vaileth akasema, "sasa hii minba yako  naipeleka wapi, nilihisi nimephata mwanaume bora kumbe una roho mbaya hivi, najuta hata kukufahamu we mkaka" yule mama akasema, "mimba itoe kama utaki kuzaa" dooh vaileth alikasilika kusikia yule mama anaongea vile, alimsuka chini na kuanza kumpiga, yule mama akamsukuma na mguu vaileth, ndipo vaileth akaangukia kwenye vyombo, kumbe kulikuwa na kisu kwenye vyombo, ndipo bahati mbaya kikamchoma mgongoni mpenzi wangu hakukaa hata dakika nyingi , alifariki palepale.
Sasa, kwa mara ya kwanza sikuamini kama amekufa maana kisu kilimchoma mgongoni kwa nyuma, hivyo sikukiona kisu mwanzoni, ila nikashangaa kuona damu zinamtoka mdomono na puani pia, sasa wakati namgeuza kumuangalia nikashangaa kukuta kisu kimemchoma mgongoni mwake, dooh nilihisi kuchanganyikiwa kabisa, sauti ilikhata mwili wote ulijaa jasho mikono ilikuwa inanitetemeka tu, nakajiuliza, "dooh mtoto wawatu amefia ndani kwangu, nitasema nini mimi, zaidi ya kwenda kuozea jela" yule mama mwenye nyumba aliogopa pia, akasema, "nisamee Nelson sikutaka iwe hivi", nilishikwa na hasila yaani nilimpiga kofi yule mama kisha nikamwambia, "haya yote umesababisha wewe kwa sababu ya tamaa zako za mapenzi, ona sasa umemu ua binti wawatu, alafu kibaya zaidi amekufa na mtoto wangu akiwa tumboni, umephata faida gani sasa" yule mama akasema, "Nelson tatizo limeisha tutokea tutafute njia zingine za kutoa huu mwili hapa, maana tukigundulika tu na serikari, tumeisha". Kumbe kule kwenye harusi, ilikuwa imemalizika na wanaitaji kuondoka kwenda nyumbani, sasa walishangaa kuona hawamuoni vaileth wakati walikuwa nae kwenye harusi, alitafutwa sana, hawakumphata, na walishindwa kumtafuta kwenye simu maana, mama yake alimnyan'ganya simu kipindi cha nyuma, dah walipatwa na wasiwasi sana, binti yao yuko wapi, mpaka ile furaha ya harusi ikawa imepotea. Huku nyumbani kwangu, tumechanganyikiwa tunashindwa tutautoaje ule mwili mule ndani ili tusijulikane, dah "unajua nilihisi kama ni ndoto" maana vaileth alikuwa anaujauzito wangu na anakufa nikiwa na mtazama, ikanibidi nikae tu chini nilie kwanza, yule mama akasema, "Nelson acha kulia, tuangalie jinsi ya kumtoa hapa huyu dada usiku huu huu, maana tutaphata mhatatizo makubwa sana" dah yule mama aliendelea kusema "sasa mimi nina mifuko mikubwa mule ndani, ngoja tumfunike kwanza na mashuka kisha tumuweke kwenye mfuko alafu mwili wake tuka utupe pale barabarani" nililia nikasema, "we mama acha roho mbaya kwanini tumtupe sasa" akasema, "sahivi ni saa nane usiku, hamna watu wengi tufanye haraka haraka, tukizubaa tutagundulika Nelson, kaa ukijua hii sio kesi ndogo ni kosa kubwa sana katika maisha".
Dah sikuwa na jinsi ikabidi nikubaliane na mawazo yake, tulimbeba vaileth usiku huohuo, kisha tukauweka mwili wake karibia na barabara, sasa wakati tunarudi ikabidi nimshike vaileth kwa mara ya mwisho ili anisamee kabisa mimi maana sikutaka iwe hivyo ilivyo tokea. Wazazi wa vaileth waliangaika sana kumtafuta binti yao, ila asubui ilipo fika walishangaa kuletewa maiti kuwa binti yao ameuliwa na watu kwa kisu. Dooh walilia sana wazazi wake na ndugu zake pia. Lakini baba yake alisema, "alie muua binti yangu, hatajuta maisha yake yote" kipindi tupo msibani, nilikuwa nalia sana, maana nafsi yangu ilikuwa inanisuta sana, watu wakasema, "kaka mbona unalia sana, kama vile huyo dada kakuuma mno", nikawambia, "hapana alikuwa mteja wangu mzuri, nilikuwa nimemzoea sana ndiyo maana naumia tu". Sasa baada ya msiba kuisha, kumbe baba yake vaileth alikuwa ameumia sana kumpoteza mtoto wake, ndipo baba yake vaileth akaenda kwa mganga wa kienyeji ili ampe adhabu na amuumbue alie muulia mtoto, mganga alimwambia, "mimi niletee mifuko walio mfunikia marehemu", kweli aliepekewa, kisha mganga akasema nhataka kumfanya alie muua huyu binti awe kichaa maisha yake yote, sitosahau huo mwaka, , siku moja tupo pale nyumbani, alianza kwanza yule mama mwenye nyumba kucheka cheka ovyo kila mda, baada ya wiki akachizi kabisa na akaanza kuvua nguo ovyo akisema kila mda, "nimeua, nimeua" baada ya wiki mbili na mimi pia nikaanza kusikia vitu vingi vinagongana kichwani mwangu, kisha naona kama mtu anhataka kuniua, ndipo watu wakashangaa kuniona naanza kukimbiakimbia mwenyewe, wakasema, "Nelson vipi leo, mbona anakimbia kama kichaa tena kama vile anakimbizwa" yaani hazikupita hata siku mbili, nikatoka pale nilipo kuwa nimepanga, nikaacha kila kitu changu, nikaamia sehemu nyingine, kisha nikaanza kuokota takhataka ovyo, na mimi pia nikawa kichaa kama yule mama mwenye nyumba
Maisha yangu kipindi nipo kichaa, nilikuwa siyakumbuki kabisaaa, ila nilisimuliwa tu, kwamba, siku moja nilikuwa sokoni, sehemu wanapo uzia chakula, nilifika kisha nikavua nguo zangu zote na kuinama watu wakiwa wananitazama, sasa jamii ya pale ilinichoka kabisa kwa zile tabia zangu za kubaki uchi kila siku huku watoto wakinitazama, mda mwingine mabinti wakinitazama nikiwa uchi pia, ndipo wakaamua kuniamsha mji na kunipeleka sehemu nyingine, kumbe mimi nilikuwa nhatabia za ajabu kabisa, maana kila nilipo kuwa nikijisaidia, kile kinyesi nilikuwa nakishika na kukipakaza chini ili watu wakasilike tu. Sasa kumbe yule mama mwenye nyumba ambae alikuwa kichaa, yeye pia aliteseka zaidi ,, maana alikuwa anaishi kwenye jalala chafu sana kule  alipo kuwepo, na aliendelea kusema neno lake kuwa "nimeua" sehemu yoyote aliyo kuwepo. Baba vaileth alifatwa na ndugu wa mama mwenyr nyumba, ili atupe msaada tupone ukichaa lakini yule baba alikhataa kabisa kisha akasema, "waache waishi hivyo hivyo maana waliona kumu ua binti yangu ni sahihi", siku moja usiku kipindi yule mama mwenye nyumba yupo jalalani amelala, walikuja vijana wa nne walevi tu hawajitambui kabisa akili, walimshika kwa nguvu mama mwenye nyumba, wakamziba mdomo na kumvua nguo zake zote, mmoja wa wale vijana akambaka yule mama akiwa na uchizi wake ule ule bila uoga kabisa. Sasa walivyo maliza ujinga wao, baada ya miezi kadhaa kumbe yule mama chizi alikuwa amephata mimba ya yule alie mbaka, dooh hii ilikuwa ina shangaza sana watu, maana walijiuliza sana kwamba, "inakuwaje huyu kichaa apate mimba, hivi wanaume hawaoni kuwa huyu ni kichaa mpaka wamfanyie unyama ," kweli yule mama aliendelea kuteseka na ujauzito wake, na alikuwa hapati matunzo mazuri kabisa, maana alikuwa anakula zile takhataka zake za jalalani, huku mtoto akiwa tumboni, wapita njia walikuwa wanamuonea sana huruma maana alikuwa anatumbo kubwa lakini anatembeatembea sana, mda mwingine anakimbia tu mwenyewe akisema "nakufaa" alafu baada ya dakika chache anacheka, dooh baada ya miezi tisa akiwa bado na ujauzito wake, ilikuwa usiku sana mvua inanyesha kwa nguvu mno, yaani kila mtu kalala sana, huku uchungu wa kijifungua ulimshika yule mama, alianza kulia sana damu zilipo mtoka sehemu zake nyeti, akiitaji mtu amsaidie, alijikaza na kusukuma katoto lakini ilikuwa ngumu, na wakati huo mvua inamnyeshea pale nje, mama wawatu hana kanga, hana hata kitu chochote cha kumbebea mtu au kutandika chini ili ajifungue, alipo ona anaangaika, akaamua kujikaza na kusukuma mtoto kwa nguvu sana, dooh wakati anafanya vile, mungu alisaidia akajifungua salama lakini yeye akawa amepoteza maisha yake ,, katoto kalitoka ka kike kakaanza kulia, sasa kutokana na ile mvua usiku, kale katoto kalizidiwa kakafariki pia, kesho yake asubui watu kipindi wanapita maeneo yale, wakamkuta yule mama kichaa amefariki pale jalalani, na walivyo angalia pembeni wakakuta alijifungua katoto pia kamefariki. Ilikuwa ni huzuni sana, yaani taarifa zilifika mpaka kwenye vyombo vya habari, habari zilipelekwa zikaenea sana mpaka magazetini.
Baada ya mama mwenye nyumba kufariki, nilibaki mwenyewe nikiwa na uchizi wangu ule ule, lakini mimi nilikuwa na uhafadhari kidogo wa kujielewa, maana Vaileth sikumuua mimi. Hivyo nilikuwa sijitambui kiakili lakini nilikuwa najua kuomba chakula kwa watu, mda mwingine naenda sehemu yoyote kisha naanza kufanya kazi kwanzia asubui hadi jioni mpaka kazi inavutia, ndipo wale watu wa pale wakiona kazi yao imependeza, wananipa chakula kisha mimi kwa upande wangu nafurahi sana. Kutokana na uchapakazi wangu, kuna mama mmoja alitokea kunipenda sana, na alitamani sana nipone ukichaa ili aniajili niwe namsaidia kazi zake za pale kwake kwa sababu yeye mda mwingi alipenda kwenda kanisani kushinda uko maana alikuwa mcha mungu sana. Siku moja aliniita, sasa mimi nilikuwa na mtindo wa kukhataa watu nisio wajua, ila kama mtu alisha wai kunipa chakula akiniita tu naenda, huyu mama alisema, "Nelson mwanangu njoo", mimi nilikuwa sijitambui kiakili ila nikaitika "abeee nakuja" akaniambia, "mwanangu kijana wa Mungu, mtu akikuita, usiseme abee, maana abee ni ya wanawake, wewe sema naamu,  ndiyo yenu wanaume" mimi sikujibu nikacheka tu, akauliza tena, "Nelson, hivi kwanini umekuwa kichaa mwanangu" nilipo sikia vile dooh, nilikimbia niliogopa  ilo swali maana nilihisi kichwa kina gongwa na nyundo, yaani pah pah! Tena kwa nguvu sio kidogo, yule mama alishangaa mno na hakuelewa kwanini nimekimbia nikilia kwa sauti vile kama mtoto. Kumbe yule mama bado shida yake ilikuwa haijaisha alitamani sana kunisaidia na kuakikisha kuwa mimi Nelson napona na ninarudi katika hali yangu ya kawaida, ndipo yule mama akaenda kwa mama yake kijijini, maana yule mama yake alikuwa ni mzee sana na alibarikiwa na mungu, maana madawa yote ya miti shamba na kila dawa za mimea alizijua sana yule bibi, sasa yule mama alipo fika akamuuliza mama ake anae jua madawa kwamba, "mama kule mjini nimephata kijana mchapakazi sana, lakini nikichaa nhatamani sana apone ukichaa wake, ili nikae nae anisaidie kazi zangu za pale nyumbani" mama yake akamwambia, "dawa zipo za miti shamba za kumpa na kumfanya apone, lakini cha msingi tunahitaji kujua nini chanzo cha kumfanya yeye awe chizi" yule mama akamwambia kwamba, "mama, yule Nelson nimeisha muita akaja vizuri tu, lakini nilipo mdokezea kuhusu kwanini amekuwa kichaa alikimbia sana tena akilia hadi nikapatwa na huruma", mama yake alicheka sana, hahahaha! hahahaha! hahahaha! Kisha akasema, "mwanangu hakuna chizi hatakae weza kusema kwanini alikuwa chizi kiulahisi tu, kuna mbinu za kitaalamu zinazo tumika", yule mama akauliza, "mama mbinu zipi hizo" ndipo yule bibi akamwambia, "leo ukifika muite kisha kaa nae chini au hata ndani, alafu chukua kiwembe cha gillete uanze kumkhata kucha zake za miguuni ukianzia kidole kidogo kwenda kikubwa, hapo ukimuuliza jambo lolote hatasema tu," kweli yule mama alipo rudi kutoka kijijini kwao, aliniita, "Nelson njoo" nikaitika tena "abee" akasema "hivi wewe uelewi tu, sinilikuzuia usiitike hivyo" kuna mtu alikuwa anapita maeneo yale akasema "dada hapo ni kama unampigia mbuzi gitaa ili acheze, huyo ni chizi" yule mama akamwambia "hata wewe unaweza kuwa chizi" ndipo yule mama alinikalisha chini kisha akasema, "Nelson kucha zako ndefu sana, alafu chafu, naomba usogeze mguu nikukate" nikasema, "sawa dada" wakati ananikhata nilikuwa nasikia raha sana kwenye nafsi yangu, nilijihisi kufurahia mno akilini mwangu, kisha akaniuliza, "Nelson kwanini umekuwa kichaa" nilimjibu kwa raha teletele kuwa, " mama, mimi nilikuwa na mchumba anaitwa vaileth, tulipendana sana, lakini mimi nilikuwa na kipato kidogo cha pesa hivyo mama mwenye nyumba akanitaka mimi kimapenzi, ili nisimlipe kodi ya nyumba maana nilikuwa sina hela hivyo nisinge mpa penzi, basi angenitimua kwake, sasa kipindi yule mama mwenye nyumba ananilazimisha mimi kufanya nae ngono ili afurahi, ndipo mpenzi vaileth akatufumania tumelala kitandani mama mwenye nyumba akiwa juu ya mwili wangu, sasa yule mama mwenye nyumba wakati anapigana na vaileth, ndipo akamsukuma vaileth kwenye vyomba kumbe nyuma kulikuwa na kisu kikamchoma vaileth vibaya ndipo dada wawatu alifariki! Ikabidi tumtoe na kumpeleka barabarani, baada ya hapo tuka logwa wote na ndiyo maana mimi ni chizi" dooh wakati namsimulia yule mama kumbe yeye alikuwa analia, akajisahau kidogo akanikhata kwenye kidole na wembe, nilipo ona damu yangu dooh nilikimbia kutoka kwake bila hata kugeuka nyuma.
Kumbe yule mama alirudi kwa mama yake kijijini ili amuelezee maneno niliyo mwambia, alipo mwambia mama yake, akamjibu kwamba, "huyu kijana haja ua kabisaa, ameonewa tu bure, na dawa yake sio kubwa ni moja tu, anhatakiwa kupiga magoti chini kisha mzee yoyote wa kiume amshike kichwani, na huyo mzee hhatakiwi kujua au kuambiwa kwamba amshike kichwani bari itokee bahati nzuri au mbaya Nelson apige magoti chini kisha mzee mwenye m'vi amshike kichwani, hatapona hapo hapo na hatorogwa milele " dooh yule mama akaona ilo zoezi ni gumu maana "kama ingekuwa tunamwambia mzee amshike isinge kuwa ngumu, sasa mpaka itokee bahati nzuri au mbaya dooh" akamwambia mama yake, kwani hamna dawa nyingine mama?, "mama yake akasema, "huyo kijana amerogwa na waganga wa kienyeji, na mimi huo uchawi sina, nina uwezo wa ki Mungu tu wa kugundua dawa, sasa fanya kama nilivyo kwambia utafanikisha tu mwanangu" dah yule mama alikaa akafikilia, akasali na kufunga kama siku tatu bila kula, ili mungu ampe akili ya kunisaidia mimi ili tufanye kama alivyo ambiwa, ila hakuphata jibu kabisaaa, sasa siku moja yule mama aliniita ili anipe hela ya kununua chakula, sasa wakati nakimbia kumfhata maana nilikuwa nampenda sana ,, wakati nakhata kona, nimkaribie yule mama! Niligongana na babu mmoja  uso kwa uso, sema kweli niliumia ila yeye aliumia zaidi maana nilimgonga mimi, sasa kutokana na zile huruma na uoga wa ukichaa ikanibidi nipige magoti na kumuomba msamaa anisamee, nilisema, "nisamee baba yangu, nisamee naomba nisamee nimefanya kosa, ilikuwa bahati mbaya" yule babu akasema "nimekusamee", "ila mimi sikumuelewa nikaendelea kulia nikisema nisamee babu nisamee usini laani" yule babu akasema haya nakushika mpaka kichwa chako kukuonyesha kwamba nimekusamee kwa roho moja mwanangu, "sasa yule babu, alipo chukua mikono yake na kuiweka juu ya kichwa changu, huku mimi nikiwa nalia nimepiga magoti, yule mama akakumbuka mama yake alivyo mwambia kwamba mpaka nipige magoti alafu nishikwe na mzee kichwani mwenye m'vi, bila kuambiwa nitapona, huwezi kuamini baada ya kushikwa na yule mzee akaondoka akaniacha pale nimepiga magoti tu, baada ya dakika tatu, nilijishangaa sana kwanini nanuka, kwanini nimevaa nguo chafu kwanini nimechafuka? Yule mama akasema, "ehhh mungu wangu, Nelson umepona twende kwangu tuongee Nelson, maana hata mimi nimeangaika sana kukufanya upone ili usiendelee kuwa kichaa,nimefunga siku tatu kwa ajili yako mwanangu.
 Nilipo pona ule ugonjwa wa kuwa kichaa, kiukweli ilikuwa ni furaha kubwa kwangu pamoja na yule mama, sasa yule mama alipo sema niende nae kwake niliamua kukubali, ila niliondoka nikiwa na aibu sana, maana watu wengi walikuwa wananitazama wakiniongea kwamba, "huyu mama kweli dini imemshika, yaani anamsaidia sana huyo chizi hela anampa chakula anampa dahh!" Yale maneno yaliniuma sana, mpaka nikhatamani kuwambia kwamba, ", mimi sio kichaa tena, nimepona". Sasa wakati tunaenda kwa yule mama, bahati nzuri au mbaya tukamkuta mme wake akiwa ana msubilia mke wake, kipindi tunafungua geti, alishangaa sana kuona mke wake anaingia na mimi nyumbani kwake, akasema, "mke wangu, tabia gani hizi tena umeleta nyumbani kwangu wewe, yaani unaleta vichaa kwangu, hivi hujui huyo kijana ni muuaji na ndiyo maana ni chizi?" Yule mama akanitetea na kusema kwamba, "hapana mme wangu usiseme hivyo, huyu kijana sio chizi kabisaa, amepona na hajawai kuua maana amenisimulia tatizo lake hata mama kule kijijini kani hakikishia", mme wake akasema "sasa ume mleta hapa wa nini ili afanye nini labda" yule mama akamwambia, "baba Neema sikiliza mme wangu, kama unavyo jua humu ndani hatuna msaidizi wa kazi, na mara nyingine nakuwa bize nachoka sana pia, hivyo huyu kijana ni mchapakazi mno, nimemleta ili atusaidie kazi hapa nyumbani maana ugumu wa maisha anaujua hawezi kuchezea kazi kabisa" baba Neema alichukia mno akaongea kwa hasila sana kwamba "simtaki huyo chizi nyumbani kwangu, huyo ni nikichaa na ni muuaji, na kama kazi kwanini usitafute mtoto wa kike aje kusaidia hapa, au unampenda huyo chizi, maana siwezi jua" yule mama neema alibaki na msimamo wake, akasema, "mme wangu, usimtukane hivyo huyu kaka, maana hata yeye hakupenda kuwa hivyo unavyo sema wewe ila ni maisha tu utokea," baba Neema akasema hivi, "sasa naona unhataka kuni haribia siku, chagua moja, aondoke huyo chizi, au nikutolee mizigo yako yote nje muondoke wote", nilipiga magoti chini kisha nikasema, "baba yangu naomba nihurumie, ili nifanye kazi za hapa sina sehemu yoyote ya kuishi, naombeni msaada wenu tafadhali, mama niombee nafasi kwa baba, nisaidie ,", mama neema akasema, "mme wangu, tumsaidie kijana, hivi kama angekuwa chizi, angeweza kuomba kazi vizuri hivi, huwezi jua labda mungu katuijia kwa staili hii, ili kuangalia imani zetu, tumsaidie tu, maana msaada huu ni zaidi hata ya kutoa sadaka kanisani" yule baba alikuwa na hasila sijui za wapi ,, aliingia ndani akatoa mizigo ya mke wake kisha akasema, "naona siku hizi heshima huna kabisaaaaa, sasa kwanza nimekuchoka na wewe, toka nje na huyo mme wako kichaa mkaoane vizuri mnapo phataka, ila umaraya wenu amuwezi kuufanyia ndani kwangu nikiwa kazini" dooh niliamua kusema, "baba,  mimi naondoka, msamee mama abaki" akasema, "mpuuzi mkubwa sana wewe unanijibu nyumbani kwangu, unajua nimejenga hii nyumba kwa shingapi?, siwezi kuishi na chizi kama wewe, ondoka kwangu ondokaaaaaa, mpuuzi mkubwa wewe, tena mkiendelea kuniwekea hewa chafu hapa, nitawaua mimi" mama neema akasema, "mme wangu, hivi hayo maamuzi yako ya kunifukuzafukuza hujayaacha tu," yule baba akasema, "ohhh kumbe umezoea ehh, ninavyo kutimua na kukufhata umejua na leo hivyo hivyo, sasa sasahivi sikufati ng'ooo na utajua huko huko na chizi wako,"  nilimsogelea ili nimwambie amsamee mkewe, dooh sitasahau maana alinipiga teke kifuani nikaanguka chini kama gogo, ndipo akasema kwamba, "mjinga nini yaani unanuka shombo hivyo alafu unani sogelea sasa ngoja nifate kisu niwaonyeshe" mama neema akasema "tuondoke, huyu ni mjinga hatatuchoma kweli".
Tulitoka nje ya geti hatujui wapi pa kwenda kabisa, nikamuomba mama neema msamaa maana mimi ndiye nilikuwa chanzo cha yeye kufukuzwa na mme wake, nikamwambia, "mama naomba unisamee najua nimekukosea sana, maana mme wako sizani kama angekukasilikia bila mimi, naomba msamaa wako mama" alisema, "Nelson mwanangu we usijali, huyu mme wangu uwa ana maamuzi ya haraka, kila ninapo fanya jambo hata dogo ananifukuza alafu akikaa wiki moja ananitafuta mwenyewe" sasa itatubidi tupande daladala twende Nadungeti, maana hapo ndipo mtoto wangu ameolewa na wale sizani kama whatakukhataa maana mme wake ni tajili sana ana pesa sana, alafu uyo uyo mwanaume yaani mkwe wangu ndiye bosi wake mme wangu, hivyo twende tukamuombe, ili tukae kwake maana mimi siwezi kukuacha wewe uendelee kuangaika mtaani, wakati sisi tunakula mpaka tuna mwaga vyakula, ila Nelson, ninacho kuomba utunze heshima yako, uwe mchapakazi, usije kuni aibisha kabisaaa" nilimpa ahadi ya kutekeleza maneno aliyo niambia, kisha tukaondoka mpaka kwa mwanae neema alipo holewa, tulipo fika, ile nyumba ilikuwa kubwa sana, maana tulifunguliwa geti la kwanza, tukatembea tena, tukafunguliaa geti la pili, tukatembea tena dooh, ndipo tukafunguliwa geti la tatu na kuingia pale ndani, sasa wakati bado hatujaenda sebreni, Neema alikuja kwa furaha sana kisha akamkumbatia mama yake, sasa mimi nilikuwa mchafu sana, na bado nilikuwa sijabadilisha nguo zangu nilizo kuwa navaa kipindi bado nipo kichaa, Neema akasema, "mama huyu kijana mbona mchafu mno umemleta kufanya nini hapa kwangu" mama neema akasema, "huyu ni rafiki yangu, nimeenda nae nyumbani baba yako amenitukana sana na amenifukuza akasema niondoke nae turudi tulipo toka, sasa sisi tumekuja hapa mtusaidieni ," Neema akasema, "mama yangu wewe hauna shida unaweza kubaki, lakini huyu kaka hatuwezi kukaa nae hapa mi naomba aondoke tu, na mimi naona baba yupo sahihi awezi kukaa na kijana kama huyu, ebu angalia vidole vyake vya mguuni vilivyo pasuka pasuka, tazama hizi nguo zinanuka, alafu mama hizi huruma zingine sio kabisa" ndipo mimi mwenyewe nikasema, "dada, nisaidie ,,  mimi naweza kufagia, kufua, kudeki, hata kupika pia najua nitafanya kazi vizuri sana tena bureee" yule Neema akasema "nini, yaani wewe unipikie mimi, unhataka niarishe au unhataka niumwe tumbo, hivi hujioni ulivyo mchafu hivyo ebu toka hapa," ndipo akaita mlinzi ili aje kunifukuza, sasa kipindi mme wake yupo ndani akashangaa kuona wageni hawaingii ndani mda wote huo, na alikuwa amepewa taarifa na mlinzi kuwa kuna mgeni anakuja, sasa wakati nimegeuka nyuma nafukuzwa na mlinzi, huku mama neema analia, sababu hana jinsi tena ya kunisaidia, nikasikia sauti ya mme wake neema ikisema, "askari usimfukuze mtu hivyo mkaribishe ndani tumsikilize" mke wake akasema, "hapana baby aondoke" kipindi nageuka nyuma kumuangalia mme wake Neema, sikuamini macho yangu kumbe mme wake neema alikuwa ni yule pacha wangu Steven tulie zaliwa tumbo moja ila yeye alitoroka kipindi mwenyekiti amefariki, nikasema, "steven ndugu yangu ni wewe", akasema, "ni mimi kaka Nelson" mke wake akasema, "bebi, unamjua huyu" mme wake akasema, "mke wangu kila siku nakwambia mimi nina pacha wangu kijijini, ambae nilikimbia kuja mjini nikamuacha yeye anateseka sana kule ndiyo huyu" mke wake alishikwa na aibu sana, mama neema akasema, "ehhh mungu nikupe nini, Neema mwanangu unaona sasa ulikuwa unamfukuza shemeji yako kwamba ni mchafu, angalia sasa kumbe unafukuza ndugu ,, usiwe na roho mbaya kama ya baba yako mwanangu" yule dada akasahau kama mimi ni mchafu akanikumbatia hivyo hivyo na kunikaribisha ndani, tulipo ingia ndani, nikamsimulia pacha wangu mhatatizo yote yaliyo nikuta kipindi cha nyuma, dooh alisikitika sana , na akasema "ndugu yangu sahau shida zote za nyuma, kwa sasa utaishi maisha mazuri kama yangu, ila nisamee sana maana nilitoroka na ningebaki huko nazani ninge uliwa na wale watu". Nikamwambia, "nitasahau yote, lakini sitasahau KISU kilivyo nisababishia mhatatizo mengi hapa duniani, kilitumika kuua mjomba wangu kipenzi, kilimuua mpenzi wangu wa dhati vaileth mpaka nikarogwa nikawa chizi, kisu, kisu nakiogopa" mjomba akasema, "jitahidi kusahau ndugu yangu, maana hata mimi hapa tumboni nina alama kubwa sana, sababu nilivamiwa na majambazi wanhataka pesa, nilivyo goma kutoa pesa walinichoma tumboni na kisu, yaani kidogo nife, hivyo kisu nakiogopa pia" mke wake pacha wangu aliniomba msamaa akiwa amepiga magoti, ili alete heshima ya ushemeji, ni mimi sikusita nilimsamee pia, Baada ya miezi kadhaa nilipendeza sana, nilikuwa kijana mwenye mvuto, pacha wangu alikuwa na ofisi nyingi, ndipo akasema hataniachia moja niwe bosi wa hiyo ofisi, sasa kipindi anaenda kunitambulisha mimi kama bosi wa ile kampuni, kumbe baba  eema alikuwepo pale na alikuwa ameajiliwa na ndugu yangu, hivyo mimi nilikuwa naenda kuwa bosi wake na wakati alinifukuza kwake kama mbwa, nilikabidhiwa ofisi nikaphata pesa nyingi sana, yule baba Neema alinifhata mwenyewe na kuniomba msamaa, sikuwa na jinsi nilimsamee tu, maana sikuwa na roho mbaya ya kutu, ndipo akarudiana na mama neema mke wake. Kiukweli nilimpenda sana mama Neema na nilimpa zawadi nyingi na kumtunza sana, maana alikuwa mkombozi mkubwa wa maisha yangu, baada miaka mitano nikafungua kituo cha watoto yatima na kuwatunza buree kabisa, na mpaka sasa hivi  nina mke na watoto wa nne, ila pacha wangu hakubahatika kuwa na watoto kabisa, kama marehemu mjomba wangu.
HUU NDIYO MWISHO


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only