Tuesday, March 3, 2020

NAKUFA SABABU YA PENZI



SEHEMU YA KWANZA
Mapenzi ni hali ya kupenda na kuvutiwa sana, inayo jengeka baina ya mtu mzima mmoja pamoja na mwingine. Lakini vilevile hayahaya mapenzi yanaweza kukufanya ukonde, ufe, uumie, udhalilike, na ujione hufai kabisa katika hii dunia, sababu ya msongo wa mawazo, haswa pale yule umpendae kwa dhati, akibadilika na kukusaliti wakati bado moyo wako unampenda sana. Sitasahau kabisa, maana nakumbuka ilikuwa ni siku ya jumatano mida ya saa 11 jioni, nilikuwa natoka kazini naelekea nyumbani kupumzika, sasa wakati naendesha gari, mala ghafla nikasikia kama kuna mabadiliko ya sauti ya gari langu, ndipo nikaamua kusimamisha ili niangalie tatizo ni nini, nilifungua mlango wa gari nakuanza kuchungulia kwenye uvungu wa gari, kumbe kulikuwa na njiti imenasa kwenye chuma flani hivi ndani ya gari, hivyo ikapelekea gari kubadilisha mlio wake sahihi. Wakati nafungua mlango wa gari ili niendelee na safari, nikasikia naitwa na sauti ya kike, "kaka, kaka, kaka tafadhali subili" mimi nilikuwa sina majivuno kabisaaa, na nilikuwa namsikiliza kila mtu na nilikuwa nacheka na kila mtu pia" yule dada alipo fika karibu yangu, akaanza kulia, "mhhhh! Mhhh!" Nikamuuliza, "we dada mbona sikuelewi, yani umeniita mwenyewe, nimekusubili, alafu unalia, sasa mimi nakuelewa vipi hapo?" ndipo yule dada akaniambia, "kaka yangu, naomba msaada wako, tangu jana sijaweka chochote tumboni, wazazi wangu wanashida sana kijijini, naomba msaada wako ata wa kazi tu yoyote ili nipate msaada kutoka kwako kaka, mungu atakubariki tu", yale maneno ya yule dada yalinipa huruma kubwa sana moyoni mwangu, mpaka nikawa mpoleeee, ndipo nikamuuliza, "dada lakini mbona we mchafu hivyo, angalia nywere zako, nguo hufui, yani hujijali, hivi huoni kama itakuwa ngumu sana kwako kufanya kazi kwa mtu yoyote ukiwa mchafu hivyo?" Yule dada alijibu akisema kuwa eti, yale ni maisha tu hana pesa ya sabuni ila akipata hawezi kuwa mchafu vile atapendeza sana. Kutokana na maneno yake yule dada, ikabidi tu nimchukue ili nije nae kwangu kusudi awe mfanyakazi wangu wa ndani, ili niwe naweza kupikiwa, kufuliwa na shughuri zingine za pale nyumbani. Tulipo fika kwangu alishangaa sana kupaona maana nilikuwa na nyumba nzuri na kubwa sana, sasa alipo kaa sebreni nikamuuliza dada hivi unaitwa nani, akasema "mimi naitwa Elivia, na wewe je"  nilimjibu kwamba, "mimi  naitwa Yenda" nilimuonyesha mazingira ya pale kwangu, nikamuonyesha na chumba chake cha kulala, Elivia hakuamini kabisa kama ameipata hiyo nafasi ndipo akaanza kulia akisema, "kaka Yenda mungu akubariki kaka, mungu akubariki umenisaidia kutoka kwenye njaa na dhiki, asante kaka yenda" nilimwambia usijali ila cha msingi uwe na heshima upende kazi yako ndipo tutaishi vizuri na kwa mda mrefu sana. Yule dada alikuwa mchapakazi sana masikini, na alikuwa anapika chakula kitamu mno, hivyo nikaacha kula hotelini nikawa nakula nyumbani kwangu, alijitahidi sana kufanya kazi mtoto wawatu, nguo zangu anafua mda muafaka, mpaka nikaamua kuwa nampa pesa anaenda na yeye kufanya manunuzi yake labda ya nguo mpya au kutumia wazazi wake kijijini. Siku moja nilirudi nyumbani usiku nikiwa na njaa sana, Elivia aliamka na kunipakulia chakula kisha akasema, "kaka yenda mbona leo umechelewa kurudi" nilimjibu kuwa " nikazi nyingi ofisini zilinibana" akasema "hii nyumba ni kubwa sana kaka, usiku naogopa kukaa mwenyewe" wakati ananipangia chakula, maana nilimuamsha kutoka usingizini hivyo alikuja amevaa kanga moja tu, sasa kipindi anapakua, bahati mbaya kanga ikajinasa kwenye meza, sasa wakati akaenda kwa mbele ile kanga ikadondoka, nikiwa na mtazama kwa macho yangu, Elivia aliona aibu akainama haraka haraka kisha akajifunika tena, mimi mda huo nimeshikwa na butwaa maana umbo lake lilikuwa zuri sana yule dada,  Elivia akasema "kaka yenda naomba unisamee, najua nimekukosea nidhamu nguo kuanguka alafu nimebaki na nguo ya ndani tu, lakini nakuhaidi hichi kitu hakito weza kujirudia tena." Wakati anaongea hayo maneno mimi mawazo yangu yalikuwa mbali sana, maana nilijikuta nimempenda ghafla huyo mfanyakazi wangu wa ndani, akasema, "mbona hunijibu boss, umekasilika, nisamee basi"  nilimuangalia Elivia kwa jicho la mahaba, akaniangalia pia kwa jicho zuri la mvuto tukiwa wawili humo ndani, nikataka kumkumbatia na kumsogeza karibu yangu ila nafsi ikakataa kabisa ndipo nikaamua kujikaza, kisha nikamwambia, "usijali nimekusamee maana hujafanya makusudi kudondosha nguo, lakini jitahidi kuvaa nguo ndefu unapo kuwa sebreni, kama wageni wangu wangekuwepo ungeniaibisha sana leo". Kesho yake wakati nipo kazini, akili yangu haikukaa sawa kabisa, maana nilikuwa namfikilia sana Elivia sababu mapishi yake niliyapenda sana, uchapakazi wake wote niliupenda na alikuwa mchangamfu sana, umbo lake ndiyo dahh, hivyo nikapata wazo la kumwambia tu awe mpenzi wangu ila badae awe mchumba kusudi baada ya mda nimuoe tujenge familia yetu, lakini nilikuwa nawaza tena kwamba, huyu dada nimekutana nae barabarani tu, yahani sijui kabisa historia yake ya maisha, sasa hii inaweza kuni kosti badae mimi. Kipindi nipo najifikilia alikuja Tajwid mfanyakazi mwenzangu pale ofisini akasema, " dooh kaka, we nomaa, yahani wewe sio mtu wa mchezo mchezo" nikamuuliza, "kwanini kaka" huku nikiwa natabasamu tu, alinijibu kwamba, "kaka juzi nilienda pale kwako nikakuta haupo bhana, lakini baada ya mda akaja mke wako, dah umepata mke aisee, anaongea kwa upole, anajua kukaribisha, alafu alinikaribisha chakula aisee anajua kupika weee sio mchezo, kaka yenda muangalie alivyo na shape nzuri ya kuvutia pamoja na urembo alio barikiwa, kaka hongera sana bhana umebahatisha sana" nilicheka sana, Tajwid akauliza kaka "mbona unanicheka, au nadanganya labda ni ndoto tu nimeona jini", nikasema "hahaha hapanaa bhanaa yule ni msaidizi wa kazi zangu za ndani, sio mke wangu" dooh! Akashangaa sana Tajwid, nikamuuliza, "vipi mbona unashangaa kaka" akasema yule dada alivyo mrembo vile awe mfanyakazi tu wa ndani, hapana siwezi kuamini" nilimwambia "amini hivyo", dahh baada ya tajiwid kuondoka nilikaa chini tena nikashika kichwa changu nikafikiliaaaa, nikaona ni bora tu nimu oe huyo dada maana kila mtu anamsifia, sasa ni bora ni muelezee ukweli tu awe mke wa nyumba yangu.
Nilipo fika nyumbani, nikashikwa tena na uoga nafsi inakataa kabisa nisi mtongoze, sasa wakati ananipakulia chakula nikachukua kijiko nikapakua wali kidogo kisha nikamwambia, "Elivia njoo nikulishe kidogo tu " akasema, "mhhh, unilishe kwani mi mtoto kaka" dooh nikaishiwa nguvu maana nilitaka kuanza kidogo kidogo ili nimteke akili yake, alivyo ona nimenuna yeye aliondoka akiwa amenuna, mpaka nikaona aibu sana, sasa wakati nipo chumbani kwangu nimelala mida kama ya saa tisa usiku huo, niliota nipo na Elivia kitandani, tukicheza mechi, kumbe ilikuwa ni ndoto tu, na kibaya zaidi asubui nilijikuta nimejifunga goli mwenyewe. Kesho yake ikanibidi nijipange kabisa ili nimuelezee ukweli kwa sababu  nilikuwa naona kama siku zinaenda alafu simwambia jinsi navyo muitaji awe mke wa ndoa, nakumbuka ilikuwa ni usiku wa saa saba, nakafungua mlango wangu polepole, ili nimfate mpaka kwake, ila sikutaka asikie kusudi nilale palepale kitandani kwake akishtuka tu ananikuta nipo nae, nilienda kwa kunyata, nikanya, nikanya polepole, nilipo fika nikachungulia kwenye mlango maana kwenye kitasa kulikuwa na kitobo kinaonyesha ndani vizuri, sikuamini macho yangu kwa nilicho kiona, kumbe Elivia alikuwa hapendi kulala na nguo na alikuwa hazimi taa, hivyo sehemu zake nyeti za mwili zilikuwa wazi kabisa, sasa wakati namtazama uvumilivu ulinishida hivyo nikafungua mlango wake polepole ili asisikie, yeye alikuwa uchi na mimi mda huo naingia kwa kunyata chumbani kwake, nilipo ingia ndani huku yeye akiwa ameitanua miguu yake yaani kaitupa kule amejiachia kweli kweli, dah akili zangu za kichawi zikahama kabisaa, nikaanza kutumia akili zingine kufikilia, yeye alikuwa amelala akiwa mtupu kabisa, hivyo na mimi nikapata wazo kwamba nivue nguo zangu zote nibaki mtupu kama yeye, "nikihisi labda atanionea huruma anipe" ndipo nikaanza kuvua nguo zangu zote, wakati nimevua kila kitu sasa nataka kulala,  nikamuona Elivia anajigeuza upande wa pili, dooh niliogopa nikashtuka mno, kisha nikakimbia kulala chumbani kwangu.
Sasa wakati nipo chumbani, huku mwili wangu umechemka sana natamani kucheza mechi usiku huo, nikashindwa kupata msaada, ndipo nikaingia bafuni kisha nikapaka sabuni mkononi na kuanza kijifurahisha mwenyewe. Sasa kwakuwa yule binti wangu wa kazi alikuwa analala akiwa katika hali ya utupu, hivyo basi, alipo amka asubuhi akakuta nguo zangu zipo pale karibia na kitanda chake, maana mimi nilipo vua wakati nakimbia niliziacha mulemule chumbani kwake, sasa Eliva alipo ziona zile nguo akajiuliza maswali kwamba, "hivi kaka yenda, alinibaka jana usiku au maana nguo zake zimefata nini hapa, na kama amezileta nimfulie inamaana hajagonga hodi na amenichungulia jinsi nilivyo jamani, na hajawai kunipa nguo zake za ndani nifue, inakuwaje ameleta leo" Elivia alianza kuukagua mwili wake, kama labda nilimfanya kitu kibaya bila yeye kupenda lakini hakuona chochote,  alinifata akiwa analia akasema, "kaka Yenda umenifanya nini jana usiku" nikasema kwa uoga sana "ehh nini kwani" akasema, "hizi nguo za nani?" Nikasema, "haaa!! Nimeamka nikajikuta sina nguo mwilini, wakati nililala na hizo hizo nguo, nashangaa kuona unazo wewe, umenivuaje Elivia" Elivia akasema, "kaka Yenda ata mimi nashangaa sijui kuna wachawi humu ndani?" Nikimwambia basi tu kama kuna lolote baya tutajua tu, "wakati nimekaa kwenye kiti nilisema kwamba moyoni, "kwa jinsi huyu dada alivyo dah, lazima nimpate tu, na awe mwanamke wangu wa maisha, nimempenda sana, na nitampa moyo wangu wote".....usikose sehemu ya pili. #2 mtunzi DAKTARI WA HADITHI TANZANIA, FRANK DAVID. NAPATIKANA KWA 0769510060.                                                                                                
SEHEMU YA PILI.  
Niliumiza sana kichwa, ni jinsi gani au njia hipi niitumie ili kumfanya Elivia awe mke wa maisha yangu, Siku moja nimekaa sebreni wazo likaniijia kuwa, nimuite ili nimuelezee ili ajue kwmba nampenda na nina hitaji awe mke wangu wa maisha, nikamuita, "Elivia" akaitika, "abee" alipo fika nikamwambia, "kaa chini kidogo tuongee" kweli alikuwa na heshima sana aliketi na kuanza kunisikiliza, "sasa nikapata wazo kichwani kwamba nikimwambia, nakupenda na ninaitaji kukuoa uwe mke wangu, ila nikaogopa kumwambia kwa sababu, nili hisi ata hisi kuwa, natumia u bosi wangu kumtongoza yeye, Elivia akasema, "kaka yenda, mbona umeniita, lakini nashangaa uongei chochote, umekaa tu unajifikilia" nilishtuka kidogo kwa sababu mawazo yangu yalikuwa yameama pale kabisa, nikamwambia, "samahani Elivia, nilikuwa naitaji juisi ya baridi, naomba uniletee kama hipo" akasema, "sawa kaka naleta". Ilipo fika usiku, Tajwid akanipigia simu akisema kwamba, "kaka Yenda, kuna jambo naomba unisaide, nilikuwa naomba namba za simu za huyo binti wako wa kazi," nikamuuliza, "namba za nini?" Akasema, "kaka mimi huyo binti nimemuelewa sana na nipo tayari kabisa kumuoa, wala sina nia ya kumchezea, kama unavyo jua tuna heshimiana sana hivyo siwezi kumualibia maisha huyo binti", nikamwambia, hapana kaka siwezi kukupa namba yake, huyu dada ana mpenzi wake" akasema, "dah sawa kama ndiyo hivyo". Duhh, Niliogopa kusikia maneno yale maana nilihisi Tajwid anaweza kuniwai na kumchukua Elivia kabla yangu. Baada ya masaa kwenda nikiwa najifikilia tu kichwani, "hivi ni mwambie au nisi mwambie". Nikasema potelea mbali wacha nimwambie, "akikataa sawa, akikubali sawa" nikaamka mda wa saa nane usiku, kisha nikaenda mpaka mlangoni mwa Elivia ili nimuelezee hisia zangu, nilipo fika mlangoni nika kaa sana pale mlangoni najifikilia tu, je nigonge mlango au niache" wakati nimekaa pale, kumbe Elivia alikuwa na kiu cha maji hivyo akafungua mlango ili akanywe maji sebreni, sasa akawa amenikuta pale mlangoni kwake, nimekaa nawaza tu, alipo fungua nikashtuka haraka nakuanza kukimbia kwenda chumbani kwangu, akaniita, "kaka yenda njoo, mbona unakimbia hivyo, tatizo nini?, na usiku wote huu bado hujalala umekaa mlangoni kwangu tu mbona sikuelewi kaka yangu." Dah nilishikwa na aibu sana, nikasema, "hapana Elivia, yahani kuna mdudu nimemuona chumbani kwangu,  nimeogopa kabisa kulala huko, ndiyo maana naitaji tulale wote usiku wa leo maana nimeogopa kabisa kulala peke yangu" Elivia akasema, "khaa yani kaka yangu mkubwa hivyo unaogopa wadudu wadogo tu" nikamwambia, "unajua tangia nikiwa mdogo, naogopa sana wadudu yani nikiwaona siwezi kabisa kulala naomba tu tulale wote Elivia, nisaidie kwakeli" Elivia alikubali nilale nae chumba kimoja usiku ule, sasa wakati tupo kitandani yeye alikuwa amevaa nguo siku hiyo na mimi pia nilikuwa nimevaa, baada ya masaa mawili, nikaanza kujifikilia, "sijui nimshike ata kidogo" maana yeye alikuwa amesinzia hana habari kabisa,  nikaamua kumshika kidogo kifuani, kumbe yeye pia alikuwa akilala anajiachia sana, hivyo katika kujigeuza kwake, akawa ameniwekea mguu wake juu yangu, dahh nilihisi labda anani hitaji pia, kumbe yeye ni usingizi tu, duhh sikulala kabisa siku hiyo, nikajisogeza karibu yake kabisa, ili na yeye aelewe lengo langu kwake, lakini yeye alilala fofofo, ilipo fika mida ya saa kumi bila kufanikiwa mtihani wangu ikanibidi niamke kisha niende kulala chumbani kwangu, kulipo kucha vizuri, kweli nilikuwa namuonea aibu sana maana nilihisi labda vile vitu nilivyo kuwa nikivifanya usiku uwenda alikuwa anavisikia ila kajikausha tu, ila nilishangaa yeye yupo sawa tu na ananisalimia kama kawaida,  nilijiandaa nikaenda kazini, sasa kumbe siku hiyo mama yangu mzazi alikuja nyumbani kwangu, alipo mkuta, Elivia akahisi ni mke wangu, eti nimemleta kwangu bila kwenda kumtambulisha, lakini Elivia alijitambulisha vizuri, mpaka mama akamuelewa, sasa kipindi mama yangu na yule Elivia wameshinda pale nyumbani, mama alimpenda sana Elivia, mpaka akatamani nimuoe awe mke wangu, sasa nilipo kutoka kazini, mama aliniita pembeni akaniambia, "mwanangu huyu binti anaonekana ana tabia nzuri sana na ni mrembo pia, sio mvivu kabisaaaa kama inawezekana ningependa awe mkwe wangu umuoe huyuhuyu, usiende kuangaika na wadada wengine".
Dahhh nilishangaa sana kusikia mama anaongea maneno yale, nikajiuliza sana kichwani, "hivi kwanini kila mtu anamsifia Elivia, labda huyu binti ata kuwa mke bora wa maisha yangu" nikamjibu mama kwamba, "sawa mama yangu kama na wewe umempenda huyu binti basi sina jinsi tena, itabidi niongee nae akikubali basi, atakuwa wangu wa maisha" mama alikuwa akai sana kwangu, kesho yake aliondoka  akarudi kwake, baada ya wiki moja, nikasema mwenyewe kwamba, "hivi namuogopea nini huyu dada kwani yeye ana nini, sasa mimi leo namuita, kisha namueleza, kama akikubali nakuwa nae, na akikataa nitamuomba sana msamaa ili asitengeneze chuki na mimi", ndipo nikampigia simu mda kama wa saa tano usiku. Alipo pokea simu nikawambia, "Elivia, naomba uje chumbani kwangu, kuna jambo nataka kukueleza," Elivia hakusita akaja chumbani, "nikamwambia ebu kaa hapa kitandani, akakaa lakini alikaa kwa wasiwasi sana, nikamwambia, "hapana usigope Elivia, maana nataka kukwambia jambo zuri tu, kama utakubali sawa na ukikataa sawa pia" Elivia alikuwa muoga kidogo akainama chini na kuficha uso wake, nilimshika mikono nikasema "hapana Elivia usishike uso hivyo, akaniangalia kidogo alafu akafumba macho, dah nikashindwa sasa nifanyaje, na mda huo imefika saa saba tukiwa wote chumbani kwangu, nikamuita jina, "Elivia" akasema "bee" kwa uoga nikamuuliza, "mbona kama unaogopa lakini" wakati huo yeye akiwa bado amefumba macho yake akasema, "hapana siogopi" nikajaribu kama kumlaza kwenye kitanda ili nione msimamo wake kama anataka au hataki, wakati na msukuma kidogokidogo kitandani na yeye pia alilala, sikuchelewa pia palepale nikambusu na kumwambia kwamba "nakupenda, Elivia naomba uwe mke wa ndoto zangu" akasema, "haaa, mi sitaki kaka, naogopa" nikamuuliza "unaogopa nini" akasema, kipindi umenikuta barabarani na kunileta hapa, ni kwamba nilimfumania mme wangu na rafiki yangu kipenzi, nilipo wauliza kwanini wanafanya vile, mme wangu alinipiga na kunikana kabisa na akasema nitoke kwake, hivyo siamini tena wanaume, na siwezi kuwa na mwanaume yoyote yule katika maisha yangu naomba unisamee kaka yenda kama nimekuudhi" dahh nilichoka, ila nikambembeleza sana, akasema, "sawa nipe mda nijifikilie kwanza, maana siwezi kuwa na maamuzi ya haraka haraka" sikuwa na jinsi nikamuacha na yeye pia ajifikilie anavyo weza, siku tatu ziliisha bila kunipa jibu, wiki ikakata aniambii tu chochote, ikabidi nimuite tena, alipo kuja chumbani kwangu, nikamuuliza, " Elivia mbona jibu langu hunipi," akasema, " Yenda upo tayari kunioa kabisa" nikamjibu "ndiyo nipo tayari, na ndiyo maana unaona naangaika sana uwe mke wangu" Elivia akasema, "sawa nimekubali, lakini naomba uwe na msimamo na mimi,maana  nimechoka kuumizwa na mapenzi" nilimpa ahadi za kumpenda daima na tangia hapo, mapenzi yakaanza kunoga sana.
Mimi sikutaka kuchelewa maana tayari nilikuwa nimeisha mpenda sana Elivia, ikanibidi niende nae mpaka kwetu kumtambulisha, wazazi wangu walimpokea kwa furaha sana, ndipo nikamwambia itabidi twende na kwa wazazi wako pia, ili  wanijue, nilishangaa sana kusikia Elivia anasema, "hapana bebi, kwetu bado atuwezi kwenda sahivi, lakini tutaenda tu" niliendelea kumsisitizia ili niende nae kwao lakini alikataa kabisa, akisema, "husiwe na haraka mme wangu tutaenda tu" siku moja usiku nilikasilika sana nikamwambia, "elivia unajua sikuelewi kabisa, hivi unavyo kataa tusiende kwenu unamaanisha nini, sasa kesho lazima twende kwenu niwaone wazazi wako" kweli asubui ilipo fika tukajiandaa na kwenda mpaka kwao na Elivia, dahh ama kweli niliwaonea huruma sana wazazi wake, maana walikuwa wanaishi kwenye nyumba iliyo haribika haribika na ilikuwa mbaya sana, ata mazingira yalikuwa sio mazuri kabisa, nikamuuliza Elivia, "hivi ulikiwa unaogopa kunileta kwenu kwasababu pako hivi ama" akasema "hapana mme wangu sio hivyo nisamee tu". Tulikaribishwa ndani na wazazi wa elivia, ndugu zake Elivia walimshangaa sana mwenzao kumuona amependeza vile, wakaanza kushika nywere zake na nguo aliyo vaa wakitamani avue kisha awapatie. Sasa baada ya kusalimia wazazi wa elivia, baba yake Elivia akasema, "mwanangu karibu sana nyumbani maana ni mda mrefu hujaja kabisa hapa, alafu naona umetuletea mgeni, je huyu mgeni ni nani" Elivia akasema, baba huyu ndiye mme wangu nimemleta hapa ili mumjue" baba ake alisimama kwa hasila akasema, "Elivia mwanangu umalaya umeuanza lini tena, wewe si umeisha olewa na mahari tumepewa, sasa huyu wa nini tena" elivia alipiga magoti akiwa analia akasema, "baba mme wangu nilimfumania na rafiki yangu ndani, nilipo muuliza kwanini anafanya vile akanipiga na kunifukuza, nikaokotwa na huyu kaka, na ndiye alie nisaidia mpaka leo tumependana hivi" baba yake Elivia akasema,,,, (usikose sehemu ya tatu.) Mtunzi ni mr FRANK DAVID daktari wa hadithi_Tz whtsapp 0769510060                                                                                                                        
SEHEMU YA TATU
_MTUNZI NI DAKTARI WA HADITHI/FRANK DAVID. WHTSAPP 0769510060.           
Baba Elivia akasema kwamba, "binti yangu elivia, kama kweli mme wako alikutesa na kukusaliti hivyo, basi sawa sina kipingamizi maana tayari m'meisha pendana, mimi nawatakia maisha mema kwende mahusiano yenu". Nilifurahi pale wazazi wake Elivia walipo nikubalia kuwa na binti yao, hivyo nikajihisi nipo huru kabisa, ndipo tuka hamua kupima virusi vya ukimwi mimi na mwenzagu Elivia ili kujua kama wote tupi salama, kweli tulijikuta wote tupo salama kabisaa, Sasa siku ya kwanza kushiriki na Elivia kimapenzi sikuamini nilicho kiona, maana Elivia alikuwa na tatizo la kujikojolea, yahani mkojo kama mkojo nakwabia na alijikojolea sana kila tulipo kuwa  tunafanya lile tendo, hivyo ile harufu ya mkojo ikawa inabaki chumbani na mkojo unajaa kitandani mpaka nashindwa kulala kabisa chumbani kwangu, nikamuuliza, "Elivia mke wangu, hivi kwanini unajisaidia haja ndogo tukiwa tunafanya tendo?" Aliinama chini kwa aibu, nikamwambia "usijali mke wangu, we niambie tu" akasema, "nisamee Yenda mme wangu, maana huu ugonjwa unaninyima raha kabisa, nakuwa sina amani katika mahusiano yangu, na hii ni sababu moja wapo iliyo fanya mme wangu anichoke na kuchepuka, tena kibaya zaidi akamchukua rafiki yangu ili afurahie tendo vizuri, maana aliona kama ni mateso nampatia", dah yale maneno yaliniuma sana nikamwambia, "mke wangu kwanini hukuniambia mapema, ili nikipeleke hospitali labda ungepona mapema, ukawa sawa na ukaendelea vizuri tu", Elivia alilia akisema , "sijui huu ugonjwa niliutoa wapi mimi, maana unaninyima furaha" niliamua kumpeleka mke wangu hospitali ili atibiwe, kiukweli nilitumia gharama yingi sana kumtibu lakini alichelewa sana kupona, ndipo tukamua kutumia miti shamba ili tuangalie kama angekuwa sawa, Mungu saidia Elivia alipo tumia zile dawa akawa safi kabisa na akapona lile tatizo, sasa kumbe elivia huu ugonjwa ulikuwa unamfanya anakosa raha na anakuwa na mawazo mda mwingi sasa alipo pona akawa ni mtu mwenye furaha, alibadilika sana akawa mrembo zaidi na mwenye kujiamini, mke wangu alivutia wengi walio mdharau na akawa mwenye uhuru kama wanawake wenzake, nilikuwa na muamini sana mke wangu, hivyo sikuwa na wasiwasi kabisa na yeye na wala sikufikilia ata kidogo kama angefanya tabia za ajabu nyumbani kwangu. Siku moja nimetoka kazini nikiwa nimeshikilia zawadi mkononi mwangu kwa ajili ya mke wangu ila nilishangaa sana nilipo fika sebreni, maana nilimkuta Elivia analia, nikamuuliza, "mke wangu kipenzi, chaguo zuri la moyo wangu, kwanini unalia?" Aliniangalia kwa majonzi sana maana uso wake ulijaa machozi, akiwa amejaa na mafua sana puani mwake, akasema, "mme wangu nimepigiwa simu nyumbani kuwa baba anaumwa sana, anakaribia kufa hivyo nimekosa raha kabisa moyoni" dooh nikamwambia kwa kumalipia kwa hasira sana siku hiyo, " hivi una akili kweli, yani baba anaumwa alafu unashindwa kunipigia simu tumpeleke hospitali mapema, unakaa unalia tu akifa je, emu twende tumpeleke mzee hospitali" tulipo fika kwao nikamchukua baba yake na kumpeleka hosiptali nzuri ya gharama ili atibiwe vizuri, aliangaika sana yule mzee ila baada ya miezi miwili alipona na akawa vizuri tu, yahani bila mimi baba yake angefariki maana nilitumia gharama nyingi kumtibu, nilikaa na kujifikilia nikaona baba mkwe na mama mkwe wangu wanakaa sehemu mbaya sana, hivyo nikapata wazo la kuwajengea nyumba nzuri ili wakae kwa furaha, kweli aikupita ata mwaka nyumba yao nikawa nimeikamilisha ikawa vizuri kabisaa wakaamia na kuishi pale. Elivia alifurahi sana kuona wazazi wake wanakaa sehemu nzuri, na Elivia alipendwa sana kwao kwasababu alionekana ndiye mtu alie badilisha maisha ya wazazi wake. Maisha yalikuwa mazuri sana kwenye mahusiano yetu maana tulipendana mnoo, Mungu alitusaidia mke wangu akawa amepata ujauzito, sasa niliona kama akikaa peke yake pale ndani itakuwa ni tatizo hivyo nikamletea binti wa kazi ili amsaidie kazi za pale nyumbani.
Nilikuwa sipendi kumbana sana mke wangu, kwa sababu nilikuwa namu amini sana, na nilikuwa namsikiliza kwa kila jambo, sio mimi tu bali ata wazazi wangu walimpenda sana Elivia, maana kila nilipo ongea nao walikuwa wanamsifia sana na kunishukuru mimi kuchagua mke bora, sasa ujauzito wa mke wangu ulipo fikisha miezi saba, sema kweli ulikuwa unamtesa sana, hivyo akawa anaenda hospitalini mara kwa mara kuangalia afya inaendelea vipi mwilini, siku moja mke wangu akiwa amepata nafuu alikutana na Mr Paul, kumbe huyo jamaa ndiye alie kuwa amemuoa Elivia kipindi cha nyuma kisha akamsaliti na kumfukuza. Mr paul ndiye alie kuwa wa kwanza kumuona Elivia, sasa alipo muona Elivia kwa mbali akamfata na kumshika Elivia mkono, Elivia akageuka kumuona anae mshika akashangaa kumuona Paul mme wake wa mwanzo ndiye anamshika, doooh alishtuka akasema "niache", paul akasema, "nikuache kwanini, wakati umependeza hivyo, nywere nzuri, rangi yako nzuri, ngozi yako nyororo sana sahivi, umekuwa mrembo sana mke wangu" elivia akasema, "nani mke wako" paul akasema "najua labda nilikosea mwanzo, lakini katika mahusiano kugombana kupo, na ata mwenyezi mungu mwenyewe ana twambia kwamba tumeane na tusahau, hivyo na mimi atakama nilikosa ila nipo chini ya miguu yako nisamee mke wangu" Elivia akasema, "toka hapa mwanaume usie na haya, unalala na rafiki yangu na kuni dharirisha mimi, ebu toka sitaki kukumbuka", paul akasema "ni vishawishi tu vya dunia, mimi sahivi siwezi kurudia najuta kabisa kufanya vile, nisamee sana, alafu kumbe nilikufukuza una ujauzito wangu maana naona tumbo limekuwa kabisa rudi tumlee mtoto" Elivia akasema, "nyooo, eti ujauzito wako, ujauzito gani unakaa mwaka mmoja na nusu, wewe uliniona sifai, sasa mwenzako ana gharamia na ana jali ndiyo maana na mimi nimeamua kumzalia" mr Paul alimtamani sana mke wangu maana yeye alikuwa hamjali wala ampendi kabisa hivyo Elivia akawa hovyo hovyo ndiyo maana alionekana mchafu, lakini nilipo kaa nae mimi nikamtunza vizuri kweli akaiva na akapendeza mtoto wawatu, sasa paul akaanza kulia mbele ya Elivia akasema, "mke wangu kumbuka mapenzi niliyo kuwa nakupatia kweli leo hii unaniacha, kwani umesahau tulilala njaa wote, umesahau nilivyo angaika na wewe, au umesahau ulivyo sema nakupa mapenzi motomoto na hauwezi kuniacha ata siku moja, mke wangu we mwenyewe ulisema kwamba, ata tukigombana ila penzi lako huwezi kusita kunipa, kumbe zile zilikuwa ahadi za uongo dah" Elivia alianza kushikwa na huruma moyoni mwake akasema, "paul mme wangu nakupenda ndiyo, lakini naogopa kumsaliti mme wangu Yenda, maana nina unauzito wake tayari" paul akasema, "hapana bebi sijasema umuache uyo mwanaume ki ghafla hivyo, wewe anza kutunza hela kwanza, jitahidi mali zake uzisimamie wewe maana nahisi pesa anayo, alafu baada ya mda tukimbie na tuondoke tuanze maisha yetu mapya" mke wangu aliogopa akasema "hapana paul, nakupenda lakini hizo dhambi sitoweza, maana mme wangu ameniambia baada ya miezi mi nne tunafunga ndoa" paul akasema "naomba namba zako za simu Elivia mke wangu" kweli Elivia akafanya kosa akampa namba, Paul akasema "unataka kufunga ndoa na huyo Yenda wako, wakati tayari mimi na wewe tumeisha funga ndoa, hapana siwezi kukubali, maana mimi na wewe tulisha funga ndoa tayari sasa mimi usipo kubali maneno yangu ninayo kwambia, nitakuja kanisani siku yako ya harusi yenu na nitaweka kipingamizi kuwa wewe tayari ni mke wa mtu na tumeisha funga ndoa tayari, hivyo hiyo harusi yenu ni batiri na aina baraka kwa mungu" elivia aliogopa akasema "paul usifanye hivyo" paul akasema, "kama hutaki nifanye hivyo, itabidi utupende wote" Elivia akasema, "sawa paul ngoja nijifikilie," paul akamwambia, "usijifikilie sana, anza kuchukua pesa mapema" dahaaa mke wangu akamuuliza, "sasa hizo pesa mi nitazificha wapi paul naogopa nitashikwa nazo" paul akamwambia "hizo pesa utakuwa unanipatia mimi natunza, kisha baada ya mda ukisha jifungua unamuachia Yenda mtoto wake, kisha sisi tunaondoka zetu, maana pesa itakuwepo." USIKOSE SEHEMU YA NNE                        
SEHEMU YA NNE.
MTUNZI, DAKTARI WA HADITHI tz. FRANK DAVID.   WHTSAPP 0769510060.                            
Mr paul alimdanganya sana mke wangu, mpaka kweli mke wangu akajikuta anakubaliana na mawazo ya mme wake wa mwanzoni mr paul. Siku moja usiku saa tisa na nusu, simu ya mke wangu iliita, nilishtuka nikajiuliza mwenyewe akilini, "hee jamani, mke wangu anapigiwa simu mda huu, nani tena huyo, au kuna tatizo lolote kwao" nilijifikilia hivyo nikiwa kitandani, lakini nilijifanya kama sijasikia simu, ili nisikilize mke wangu atakacho ongea mda huo, sasa kabla Elivia hajapokea simu aliniangalia kama nimelala au namsikia anacho taka kuongea, ila mimi nilikuwa nimejifanya kama nimelala sisikii chochote kabisa, Elivia alikuwa mjanja akaamka kitandani polepole kisha akafungua mlango akatoka na kuanza kuongea na ile simu, sasa mimi nilimka polepole nikanyata ili nikamsikilize anacho ongea, kumbe alie kuwa amepiga simu ni yule paul anaitaji kusikia tu sauti ya Elivia afurahi, mimi sikuweza kugundua siku hiyo mke wangu anaongea nini, ila alipo rudi kitandani akashangaa kunikuta mimi nimekaa kitandani wakati yeye aliniacha nimelala, nikamuuliza, "mke wangu hizi tabia za kuongea na simu umejificha umezianza lini na ulikuwa unaongea nanani" Elivia akasema, "nisamee mme wangu", nikamwambia, hapana bado ujanijibu swali langu kabisaaa, sasa unapo sema nikusamee wakati sijajua maongezi yako yanahusu nini, nitakuwa nakusamee nini sasa" Elivia alinidanganya kwamba, "mme wangu ni huyu mama Gift jirani yetu, kila siku ananisumbua eti anataka nimkopeshe laki tano ila mimi sina hiyo hela sasa kila mda ananipigia pigia simu tu mpaka naona aibu usijue." nilimwambia "usijali mke wangu, hao ni majirani hivyo inabidi tusaidiane, kesho nitakuachia hiyo pesa ili umkopeshe na akikurudishia hiyo hela, utatumia kwa matumizi yako mwenyewe" mke wangu alifurahi sana, kweli kesho yake asubui nilimpatia hiyo pesa, ila mke wangu alivyo na akili mbovu, akampigia mr Paul, kisha akamwambia, "bebi tayari nimeisha anza kupata pesa, nakutumia laki tano leo lakini uitunze vizuri" mr paul akamwambia, "kazi nzuri sana mke wangu, jitahid sana kutafuta zaidi na zaidi hii bado ndogo, ili tukifikisha kiwango kizuri cha pesa tuondoke maana nimemisi sana penzi lako", mke wangu akamjibu kwamba, "sawa usijali mme wangu, napambana sana huku" sasa mimi nilipo rudi kutoka kazini, nikamuuliza mke wangu kwamba, "Elivia vipi yule  mama Gift ulimpatia ule mzigo nilio kuachia" mke wangu akanidanganya kwamba, "ndiyo mme wangu nimemsaidia amefurahi sana na amesema atatulipa mda sio mrefu" nilijiandaa nikalala maana nilikuwa nimechoka sana na miangaiko ya kazini, sasa ilipo fika mida  ya saa tisa usiku, nilisikia simu inaita tena ya mke wangu, nikajifanya kama siisikii nikajikausha kweli kweli, alafu nikajiuliza, "hivi hizi simu za usiku za nini wakati mke wangu ana mimba na tumbo kubwa sana hivyo," sasa mke wangu alikuwa mjanja akakata simu siku hiyo alafu akaizima, nikamuliza, "mke wangu kwanini umekata simu, na mbona umezima kabisa, unamatatizo gani hayo kipenzi changu" mke wangu akasema, "mama yangu amenunua simu leo, sasa baba yupo anamfundisha jinsi ya kutuma meseji na kupiga,  nashangaa wananitumia meseji mimi na kunipigiapigia mimi mpaka nimechoka, yani toka jioni wanafanya hivyo" nikamjibu kwa kucheka, "hahahah usijali mke wangu, mama nae ni mgumu wa kuelewa ehh? Yani toka jioni wanamfundisha tu" tulilala na wala sikuwa na wasiwasi kabisa siku hiyo, maana nilikuwa na mpenda sana mke wangu. Sasa yule Mr Paul akaona, Elivia anakuwa mzembe wa kuniibia pesa za kutosha, hivyo akampigia elivia simu na kumwambia kwamba, "bebi nataka tutumie mchezo mzuri wa kumfanya mme wako atoe pesa zingine zaidi" mke wangu akamuliza, "njia zipi, maana ata mimi nashindwa kabisa kumuingia ili anipe pesa nyingi kwa wakati mmoja," mr paul akasema, "kuna dada hapa kama mama mama tu, nimeongea nae, aje hapo kwenu mme wako akiwepo, aanze kukutakana akisema kwamba alikopesha pesa zamani ukakimbia bila kumlipa, najua mme wako akisikia hivyo atakuonea huruma sababu ya huo ujauzito wako hivyo atampa hiyo millioni mbili dada atakuja tumlipe laki mbili yake aondoke, ila wewe ukubali kweli alikukopesha zamani". Kweli hazikupita ata siku mbili, maana siku moja wikendi nimekaa na mme wangu yenda kwenye ubaraza, alikuja mama mmoja muongeaji sana akaanza kusema kwamba, "wewe Elivia mjinga sana wewe, ulikopa milioni mbili zangu ukajificha huku sio, kumbe nilifanya kosa kukusaidia wewe na mme wako paul sio, sasa umeolewa huku tena unajifanya umenisahau sio" mke wangu alianza kulia akisema "najisikia tumbo linauma mme wangu," dah nilimuonea sana huruma mke wangu,  nikasema, "we mama acha kuongea hivyo atakama ulimsaidia, ndiyo umtukane hivyo, hivi huoni hari yake ya ujauzito, kwanini usimuombe polepole" yule mama akasema, "kakimbia na hela yangu mda mrefu huyo" nikamuuliza mke wangu, "Elivia ni kweli unadaiwa" akanijibu "ndiyo mme wangu, alinikopesha zamani sana maana tuliishiwa kila kitu ndani, hivyo nikakopa ili nifanye biashara ila mme wangu alikuwa anaiba hela aka ua mtaji, nikashindwa kulipa hadi leo" mke wangu alikuwa ananidanganya ili nitoe pesa waweze kufurahi na paul wake, kweli niliingia ndani nikachukua millioni 2 kisha nikampa yule mama na kumwambia "nenda ila ukirudi hapa, uje na heshima" yule mama akamfata paul, ndipo paul alimlipa laki mbili zake kisha paul akatunza pesa iliyo baki kwa ajili ya mipango yake na Elivia ili wakimbie, mimi nibaki peke yake na mtoto. Maisha yaliendelea hivyo hivyo pale nyumbani bila mimi kujua kama mke wangu anamalengo mabaya kabisa na mimi, sasa siku moja nipo kazini, mr paul akampigia mke wangu simu akimdanganya kuwa anaumwa ili mke wangu aende kwake afanye nae mapenzi, kweli mke wangu alipo ambiwa na paul kuwa anaumwa, hakuwa na jinsi akaamua kwenda kumjulia hali ili kujua anaendeleaje ki afya, Elivia alipo fika, paul akamwambia, "bebi mi siumwi, ila nilitaka uje ili tongelee njia moja nzuri sana ya kumfanya mme wako akupe pesa nyingi sana kwa wepesi" mke wangu akamuuliza, "njia gani hiyo paul" ndipo paul akamwambia, "kuna mganga mmoja hivi wa kienyeji, yule akikupa dawa inaitwa SHUNTAMA ukimuwekea mme wako basi atafanya chochote utakacho mwambia na atakuwa kama taira kwako" mke wangu akasema, "sawa hamna shida lakini isimu ue kaka wawatu maana alinisaidia sana" paul akamjibu kuwa, "Shuntama sio sumu" sasa kipindi mke wangu anataka kuondoka, paul akamshika mkono na kumvuta karibu yake, akaweka macho ya tabasamu lenye hisia ili kumteka akili Elivia mke wangu, kweli dahh, walionganisha vinywa vyao na kupapasana pale ndani, mpaka paul hisia za kucheza mechi zikawa zimemuijia, akamwambia Elivia, "bebi naomba tucheze mechi, maana najihisi nipo vibaya sana naomba msaada wako bebi"
 ,elivia alikataa akasema, "paul siwezi kufanya hivyo, ebu angalia hii mimba ilivyo kubwa hivi, alafu sio mimba yako nitakuruhusu vipi ucheze mechi, hivi uoni namuaribu mtoto umo tumboni" paul alikuwa mbishi sana alimbembeleza kwa ujanja ujanja wake akimpapasa ili kumuweka sawa, akajaribu kutoa machozi akionyesha kweli anaitaji mechi, iliniuma sana hii nilipo ijua kuwa mke wangu alivua na kukubali kufanya ule mchezo huku akiwa na ujauzito wa mwanangu, paul alionyesha ufundi mkali sana kwenye hiyo mechi, mpaka Elivia akasema, "dah paul nimekaa na wewe masaa machace tu lakini nimefurahia sana mechi, lakini yule mme wangu nalala nae usiku mzima kabisa, nashinda nae, lakini hawezi mechi kabisaaa. paul akamwambia, "nitaendelea kukufurahisha zaidi",  Sasa walipo maliza ujinga wao, Elivia alipo rudi nyumbani na hapo ndipo dharau zilipo anza ndani za kila aina, kila siku ananifanyia mimi. USIKOSE SEHEMU YA TANO. Mtunzi FRANK DAVID. WHTSAPP. 0769510060                       
SEHEMU YA TANO,
 MTUNZI FRANK DAVID, DAKTARI WA HADITHI TZ..                                                        
Mke wangu alipo onja penzi la paul, hapo ndipo akaanza dharau ndani, maana aliona utofauti mkubwa kati yangu na paul, sasa siku moja tukiwa ndani, nikamuita mke wangu kwamba, "elivia" hakuitika akabaki kimya, nikamuuliza, "mke wangu mbona nakuita unakaa kimya" hakujibu chochote akatoka nje kwenda kutema mate, maana ujauzito wake ulikuwa unamfanya ateme mate kila mda, alipo rudi ndani akalala kitandani na kujifunika shuka kabisa, dooh nikashangaa, hichi nini tena, ikabidi nimuulize, "mke wangu tatizo nini? mbona naona kama umekasilika, umenuna hutaki ata kunijibu chochote mme wako" akasema, "yani Yenda mimi unanifanya kama mfanyakazi wako wa ndani kabisaa" duuh nikamuuliza kwamba, "unamanisha nini" akasema "namanisha nini ehh, kama ujui acha" dooh sikuelewa kabisa anacho taka ninini siku hiyo, "nikamwambia, "mbona umeanza matatizo wakati hatuja timiza ata miaka miwili kwenye upendo wetu, kumbuka bado hatujafunga ndoa mke wangu na umeisha anza hizi tabia sikuelewi" dahh alinijibu vibaya eti, "utaelewa tu" yale majibu yalinichukiza ikabidi na mimi nijifunike shuka tu nilale. asubui mke wangu alikuwa amezoea kunivalisha na kunichagulia nguo za kuvaa, lakini aliacha kabisa, hivyo nilikuwa na vaa navyo weza mwenyewe kisha nambusu shavu ndipo naenda kazini, yani alikuwa ananuna nilipo kuwa na mbusu mpaka mwenyewe nikawa najishtukia, sasa kutokana na mapenzi ya mke wangu kupungua, nilikuwa nakosa raha kwakweli, maana ata pale kazini nilikuwa "nashika tama" mda wote, wafanyakazi wenzangu wakaniuliza, "vipi Yenda nakuona unakosa raha sana siku izi wakati wewe ni mchangamfu sana MAN YENDA THE BOSS" niliamua kuwambia ukweli kuwa, "dah jamani shemeji yenu ananitesa sana akili siku izi, namuuliza maswali hajibu na akijibu, ujue amenijibu ovyo ovyo, yahani ananijibu vibaya sana, mpaka nakosa raha kabisa, na kumuacha siwezi maana nimemtoa mbali sana mke wangu" wale wafanyakazi wenzangu wakaniambia, "kaka  Yenda usijali, hizo ni changamoto za familia, alafu kingine mke wako ni mjamzito, hivyo lazima afanye hivyo, tena wewe shukuru mungu wengine wanakuwa wakorofi zaidi ata ya Elivia wako" maneno yale yalinipa nguvu sana, hivyo nikajua zile dharau ni za mke wangu ni sababu ya mimba, kumbe la asha! sio hivyo bali ni sababu ya Mr paul kijana mbaya sana katika maisha yangu. Siku hiyo nikawai kutoka kazini jioni nikapitia sokoni kisha nikanunua zawadi kama za elfu hamsini kwa ajili ya mke wangu nyumbani, nilipo fika nikamuita, "Elivia" ila mke wangu hakuitika kabisa, ikabidi nimwambie, "bebi nimekuletea zawadi mpenzi wangu,"  nilishangaa zaidi maana aliamka na kwenda chumbani, dah mpaka yule mfanyakazi akatikisa kichwa ishara ya kunionea huruma, nikamuuliza yule binti wa kazi za ndani kwamba, "hivi nikiwa sipo mnaongea kweli humu ndani, maana sahivi ata kurudi nyumbani naona shida, yahani natamani kulala hukohuko kazini," yule binti akasema, "ukiwa haupo tunacheka na kufurahi sana ila ukija tu, anabadilika hivyo,  nikamfata huko huko chumbani mke wangu, nikamuuliza maswali nikiwa nimepiga magoti, "mke wangu najua katika maisha kuna kukosea, najua labda nimekuudhi sehemu flani, naomba uniambie mke wangu nipo chini ya miguu yako, sijawai ata kumpigia mama yangu mzazi magoti chini, lakini leo hii nakupigia wewe kunusuru mapenzi yetu, ebu niambie nimekuudhi nini mama" mke wangu alichukia, akanuna yani mpaka jasho likamtoka, nikaamua kutoa reso yangu ili nimfute lile jasho, dahh alichukia akasema, "niache usinifute uko, yani mimi unaniona kama mfanyakazi wako wa ndani," nikamuuliza "kwanini" akasema, "pesa zako unajiwekea mwenyewe kwenye akaunti, mimi hujanifungulia akaunt sina pesa yoyote kabisa, alafu unajifanya unapiga magoti eti unanipenda, kupenda gani uko" dahh nikasema, "mke wangu lakini akaunt zote  mbili za nini, mimi na wewe ni mwili mmoja hivyo akaunt yangu ni sawa na yako tu, tamaa zingine za nini sasa"  dahh Elivia alinuna sana siku hiyo akasema "yahani wewe mwanaume hunipendi" akaanza kulia. Sasa kumbe mke wangu mpango wake mzima ni kwamba mimi niweke pesa zangu kwake kisha wao waweze kutoroka na paul wake waniache mimi masikini wa kutupwa. Kesho yake nilipo enda kazini mke wangu akazichukua zile zawadi nilizo zileta, mpaka yule binti wa kazi akamcheka, akamwambia, "dada jana si ulizikataa hizo zawadi lakini" elivia akajifikilia kwamba, "mme wangu yenda ananipenda sana, sijui kwanini namfanyia hivi, lakini utamu wa penzi ninalo lipata kwa Paul siupati kwa yenda ndiyo maana nakosa msimamo wa mapenzi kabisa dahh sijui nifanye nini" baada ya wiki kupita paul akampigia simu mke wangu akamwambia, "bebi ule mchongo wetu wa kwenda kwa mganga ili tuchukue SHUNTAMA, umekaribia hivyo kesho jipange twende tuchukue hiyo dawa, yani ukimuwekea kidogo tu kwenye maji ya kuoga, wakati anajimwagia yale maji kwanzia kichwani, ile dawa itakuwa inafanya kazi sana na atajikuta anakupenda na kukukabidhi mali zake zote, na hapo ndipo tutakapo mfirisi huyo kaka, kisha tuondoke zetu tukafurahie hii dunia."  sasa kwakua mke wangu alikuwa ameisha mpenda sana paul, hivyo akawa mdhaifu sana kwake, maana kila upuuzi paul atakao mwambia ilikuwa ni lazima aufanye. Kweli walienda kwa huyo mganga wa kienyeji ili wapewe dawa waje kuniwekea mimi, walipo fika kwa mganga, ndipo yule mganga  akamwambia elivia kwamba, "mme wako ana nyota kari na analindwa sana mizimu yao, hivyo ukikosea tu masharti utaharibu kila kitu" Eliva akasema kwamba "siwezi kukosea mganga" mganga akawambia, "nakupa hii dawa ya shuntama, nidawa iliyo changanywa na nyongo ya kuku, ngozi ya chura alie sagwa kwa mawe, damu ya kinyonga, pamoja kinyesi cha mtoto mchanga, hivyo hii dawa utamuwekea kwenye ndoo yake ya kuogoea akioga tu tayari mmefanikiwa, yahani huyo mwanaume atakusikiliza kwa chochote usemacho, lakini nakuomba sana hayo maji yasiwe ya moto yahani yasichemshwe kabisaa, maana yakiwa ya moto, mme wako atapata ugonjwa usio tibika hapa duniani popote pale."
Mke wangu akasema, "siwezi kuchemsha maji mganga yule anapenda sana kuoga maji ya baridi" kweli siku hiyo nilipo rudi nyumbani nikashangaa kuona mke wangu ananichangamkia sana, akanikumbatia na kunibusu mpaka nikashangaa aisee, akasema, "nakupenda sana Yenda wangu, nisamee kwa matatizo madogo yaliyo jitokeza hapo hawali nisamee nakuomba, lakini ningeomba ukaoge kwanza, maji nimeisha kuandalia bafuni kwenye ndoo ukimaliza kuoga tu urudi sebreni tule chakula bebi wangi" nilifurahi sana kusikia maneno kama yale kutoka kwa mtu nimpendae, hivyo nikakimbia haraka bafuni kuoga ili nije sebreni nile pamoja na mke wangu, sasa kipindi nipo chumbani, mke wangu akatoka nje kumpigia simu paul kuwa, "paul mme wangu, huyu mpuuzi ameenda kuyaoga yale maji, na tayari nimeisha changanyamo ile Shuntama,". Sasa wakati mke wangu anafanya yale mazumgumzo siku hiyo kulikuwa kuna baridi sana hivyo nisinge weza kabisa kuoga maji ya baridi, ndipo nikamuita yule msaidizi wangu wa kazi ili aniletee maji ya moto haraka ili nichanganye kwenye yale ya baridi nioge ili nije kula na mke wangu kama alivyo sema, alileta maji ya moto nikayapokea mlangoni kisha nikaenda kuyachanganya bafuni, sasa wakati mke wangu anamalizia kuongea na simu, mimi kipindi hicho nipo bize naoga yale maji yaliyo tegwa dawa ya shuntama, nakumbe mganga alisema, maji hayatakiwi kuchemshwa yanapaswa kuwa ya baridi tu, dooh. Sasa mke wangu pamoja na yule binti wakazi wakiwa wananisubilia ili nije tule, walishangaa kuona sitoki bafuni, mke wangu akauliza, "mhh huyu mwanaume mbona haji" yule binti akasema ata mimi nashangaa, maana aliniita nimpelekee maji ya moto ili achanganye kwenye maji uliyo muwekea ya kuoga maana kasema kuna baridi ila nashangaa hatoki kabisa kuoga, hamalizi", Elivia akasema "haaaa we mpuuuzi sana, kwanini umempa maji ya moto sasa" kumbe alikumbuka lile sharti la kuwa "nikioga maji ya moto nitaugua ugonjwa usio tibika hapa duniani" ndipo mke wangu akaja haraka haraka mpaka chumbani, wakati anaingia ndani akasikia kelele ya kuku anawika, kisha akasikia kelele za vyura, dah mke wangu akaziba masikio maana alihisi ni vitu vya hajabu, ndipo mke wangu akaamua kuja bafuni ili anione nilivyo kuwa, mungu wanguu alinikuta nipo chini, damu zinanitoka sana kwenye kucha za mwishoni za miguu na mikononi, alafu nimebadila mwili mzima maana nilipatwa na ugonjwa wa ngozi yani rangi ilikuwa kama ya chura, ngozi ikawa mbaya sana masikini,  nilikuwa sitamaniki kabisa maana ngozi yote inafanana kama ngozi ya chura, yahani mabaka mabaka yamenijaa, mke wangu aliogopa akamuita binti wa kazi aje kumsaidia, kale ka binti kalivyo niona kakasema, "mfunike kwanza nguo maana sehemu zake nyeti zipo wazi" dah mimi nilikuwa sina hamu kabisa, nawashwa mwili mzima  ajikuna mpama nashindwa kusimama ngozi inawasha sana yahani sina nguvu ata kidogo, ndipo nikapelekwa hospitali, lakini daktari alisema "huu ugonjwa hauwezi kupata dawa, ata ishi hivi hivi siku zote, labda tutampa dawa za kupunguza maumivu" kweli dahh dawa hazikupatikana ata kidogo, kutokana ngozi yangu kuwa mbaya na kuwashwa kila mda, ndipo nikaamua kuacha kazi maana ule ugonjwa ulikosesha amani na uhuru katika maisha yangu, wazazi wangu walishindwa kabisa kujua nini kilicho nipata, mke wangu alikuwa anajifanya kama anaumia lakini kwenye nafsi ilikuwa ni furaha kubwa sana kwake, lakini watu walikuwa wanakuja kunitazama nilivyo haribika ngozi, kusema ukweli walilia kwa huruma, ikafika hatua ata watoto wadogo wakaanza kunikimbia eti kuwa mimi nawaogopesha, dahhh maisha yalikuwa magumu sana upande wangu mpaka dunia nikaiona chungu kabisa. Siku moja mke wangu akaenda kwa paul, sasa kipindi yupo huko paul akamwambia, "tumia hii nafasi, maana mme wako ni mgonjwa sana, miliki hizo mali tumuache hapo mwenyewe bhana sisi tuondoke" mke wangu akasema, "hapana paul subiri kwanza apate nafuu alafu tujue tunaondokaje maana jamii itanishangaa sana nikimkimbia sahivi, alafu yule kaka amenisadia mambo mengi sana, nilikuwa najikojolea akanitibu, amejenga nyumba kwetu, aliniokota kipindi umenifukuza, ata kama sijampenda kutoka moyoni, lakini ningeomba twende kwa mganga alie tupa zile dawa, ili tumlipe hela tumwambie tumekosea masharti tuchukue dawa ya kumtibu mme wangu Yenda arudishe ngozi yake, " kweli mke wangu pamoja na paul wakarudi kwa mganga ili awape dawa ya kunitibu mimi nipate ngozi yangu isiyo na mabaka mabaya mfano wa chura, ila walipo fika kwa mganga wakakuta watu wengi sana pale, paul akauliza, "ndugu zangu kunanini hapa mbona watu wengi" wakamjibu kuwa, "jana usiku kuna radi imepiga maeneo ya hapa, radi kari sana, sasa tunashangaa kwamba hii radi imemuua huyu mganga wa hapa tu wengine wote hawajafa " mke wangu akasema, "ohhhh mganga amekufa, sasa mme wangu ataponaje masikini", dah ikabidi warudi nyumbani. USIKOSE SEHEMU YA 6. MTUNZI FRANK DAVID, NIITE DAKTARI WA HADITHI tz. NAPATIKANA WHTSAPP 0769510060.                                                                        
 SEHEMU YA 6. MTUNZI FRANK DAVID| DAKTARI WA HADITHItz.  Whtsapp 0769510060.                
 Mke wangu alipo gundua mganga amefariki akajua moja kwa moja mimi siwezi kupona, alipatwa na huzuni sana siku hiyo, akashindwa kukaa nalo moyoni ndipo akasema, "paul naumia sana kumfanyia Yenda ili jambo, nafsi yangu inanisuta kwakeli, yahani naumia sana, maana huyu kaka amenisaidia sana, na sio mimi tu bali ata wazazi wangu amewafanya wawe katika mazingira bora, sasa sahivi anaumwa, usiku halali huyo mwanaume, anajikuna tu mwili wake mpaka mda mwingine, anajichubua ngozi anatoka damu kabisa," paul akamwambia Eliva kwamba, "mke wangu, lakini wewe ndiyo umefanya kosa, mganga alisema kabisa, usichanganye maji ya moto kabisa, sasa wewe umefanya uzembe, sisi tulitaka shuntama itusaidie ili akupende sana wewe, awe zezeta kwako, yahani kila unacho taka anakupa bila wasiwasi, sasa wewe umefanya ndivyo sivyo, hatuna jinsi, itabidi tukubaliane na matatizo" Paul alienda kwake, Elivia akarudi nyumbani, dahh alinikuta nipo sebreni nimevaa nguo ya ndani tu kuficha sehemu zangu nyeti, ili nijikune vizuri maana nisinge weza kuvaa nguo mwilini maana ningewashwa zaidi na zaidi, Elivia alishangaa kuniona mgongoni maana nilikuwa na mabaka ya ajabu ajabu mpaka mda mwingine yanatia ata kinyaa unaweza ata usile chakula, nilinunua mafuta ya kila aina ili nirudishe tu ngozi yangu ya zamani lakini wapi, walitushauri wakina dada kwamba, "jamani tumieni mafuta ya nivea, ata pata nafuu yale mafuta ni mazuri" tukatumia lakini wapi, dooh siku moja baba yake na Elivia alikuja nyumbani na rafiki yake, siku hiyo ilikuwa ni furaha kubwa kwangu, maana yule rafiki yake baba mkwe wangu alinielekeza dawa nzuri ya kujipaka, kweli nilitumia hiyo dawa na ilinisaidia maana sikuwashwa tena tangu siku hiyo, lakini ngozi haikupona nikabaki vilevile, nilianza kuchangamka na kupata nguvu ingawa nilikuwa naona aibu sana kuonana na watu sababu nilikuwa na sura mbaya sana, hivyo sikuweza kuangalia na mtu uso kwa uso ata siku moja, nilikuwa nainama chini kila nilipo kuwa naitaji kuongea na mtu. Mke wangu alikuwa anaogopa kulala na mimi akihisi labda tukikutana kimwili naweza kumuambukiza huo ugonjwa na yeye akawa mbaya kama mimi, hivyo ata furaha ya mahusiano sikuipata kabisa. Wazazi wangu na ndugu pia, walisikitika sana kuniona vile, mama yangu kipenzi alikuwa ananipenda sana hivyo alikuwa hana raha kabisa kuniona vile, ilifika hatua alikonda sana sababu ya mawazo maana ata chakula alikuwa hali kabisa sababu yangu. Kipindi hicho mimba ya mke wangu ni kubwa sana yahani anakaribia kujifungua kabisa, mimi sikumchoka mke wangu na wala siku muhisi chochote kibaya mke wangu, ingawa watu walikuwa wanaongea yao kwamba, "mke wake anataka kumu ua ili amiliki mali zake" lakini mimi siku amini hayo maneno kabisa na sikutaka mtu amseme vibaya mke wangu, sasa mimi kwa akili yangu nilizani labda wafanyakazi wenzangu wanataka kunifanyia ubaya ili wao wachukue cheo changu ofisini, sikuwaza kabisaa kama mke wangu anaweza kunifanyia unyama namna ile. Wazazi wa Elivia walikuwa ni wazee sana, sasa kutokana na uzee wao walikuwa wana ugua mara kwa mara, siku moja mama yake Elivia aliugua mno, sasa ikabidi mimi nimpeleke hospitali ili atibiwe na apone, haya yote niliyafanya ili mke wangu aone kuwa mimi napenda pia familia yake na siku upande mmoja wa kwetu tu. Nilijitahidi sana kumsaidia mama mkwe wangu apone lakini mungu alimpenda zaidi, maana mara ya mwisho kipindi mama mkwe anakata roho nilikuwepo, na aliacha ameniambia kwamba, "mwanangu nashukuru sana kwa msaada wako kwetu, umetusaidia sana sisi, ila nakuomba kitu kimoja mwanangu, huo ugonjwa wa ngozi ulio upata, hakuna yoyote wa kukuponesha zaidi ya mwenyezi mungu, nakuomba mwanangu anza kwenda kumuomba mungu, muombe sana mungu ili akusaidie wewe uweze kupona, fata viongozi wa dini watakuombea na kama hayo ni mapepo yataisha tu, hakuna kishindikanacho kwa mwenyezi mungu" yule mama baada ya kuongea vile alifariki hapo hapo, dooh nililia sana, maana yule mama alikuwa mtani wangu sana na tulipendana sana" sasa kipindi tupo kwenye msiba, mke wangu na yeye akajifungua mtoto mrembo sana wa kike, hivyo ilikuwa ni furaha ya kupata mtoto vilevile huzuni ya kufiwa na mkwe wangu. Baada ya mwezi mmoja mimi nilikuwa nawaza sana yale maneno ya marehemu aliyo niambia, ya kumrudia mungu ili niweze kupona ugonjwa wangu wa ngozi, kweli sikuwa na jinsi nikaamua kufanya hivyo, kuna pasta mmoja niliongea nae na ndiye alie niombea mpaka nikapona ule ugonjwa na nikarudi kuwa sawa kama nilivyo kuwa zamani, mke wangu alishangaa, ndugu na jamaa walishangaa sana, mimi pia nilifurahi mno kisha nikaanza kupambana ili mtoto wangu apate malezi bora. USIKOSE SEHEMU YA 7.                                               
SEHEMU YA SABA
MTUNZI FRANK DAVID, WHTSAPP 0769510060.
Baada ya kupona ule ugonjwa nilimuamini sana mungu, ndugu zangu na watu wengine walifurai sana kusikia nimepona maana hawakuamini kabisa kama ningekuwa sawa. Lakini nilikuwa nakosa raha sana maana mke wangu Elivia alikuwa hapendi kabisa kwenda kanisani  yahani nilipo kuwa nikimgusia maswala ya mungu yalikuwa hayamuiingii kabisa akilini, siku moja nili mbembeleza sana akamuone baba mchungaji alie niombea mpaka nikapona. Sasa wakati yupo ofisini kwa baba mchungaji mimi sikuwepo mule ofisini, kumbe baba mchungaji alimwambia kabisa mke wangu kuwa, “wewe ndiye ulie msababisha mme wako apate yale matatizo ila usirudie maana mwenyezi mungu hapendi kabisa tabia za kishirikina kama hizo” mke wangu hakuamini kabisa kama ange gundurika alitetemeka akasema, “mchungaji kwani mme wangu amejua kuwa ni mimi” baba mchungaji akamwambia, “mme wako anakupenda sana na ana kuthamini zaidi ya wewe unavyo fikiria hivyo tunge mwambia kuwa ni wewe umefanya vile, tungeiweka ndoa yenu matatani ndiyo maana tukakaa kimya tu, yeye hajui kabisa kama ni wewe umefanya vile, sasa unacho takiwa kufanya ni kutubu dhambi zako kwa mungu ili usamehewe na uache kabisa  tabia za kishirikina” mke wangu alikubali na akatubu kabisa dhambi zake ili aache mambo aliyo shawishiwa kuyafanya.
Mungu alisaidia kabisa, tukaendelea kukalea kachanga ketu, baada ya miaka kama miwili, Mr paul alivyo ona mke wangu ameisha kakuza katoto akatamani kutembea tena na mke wangu, alimuita kwake akimdanganya kwamba, “elivia naomba uje leo kwangu, ata mimi nataka unipeleke kanisani ili nikatubu dhambi zangu maana tulimkosea sana mungu kabisa,” mke wangu aliona ni jambo jema hivyo hakuwa na wasiwasi kabisa akajiandaa na kumfata paul nyumbani kwake ili waambatane wote kwenda kanisani, sasa alipo fika kwa paul, akamkuta paul amelala kitandani, akijifanya kama anaumwa, mke wangu akamuuliza “paul mbona umelala hivyo, twende kanisani sasa ujue nimechelewa kwa ajili yako” paul akasema, “elivia mke wangu najisikia vibaya sana yani tangu jana mgongo wangu ulikuwa unaniwasha sana, alafu najihisi kama kuna vipele mgongoni nilikuwa naomba unikune ili nipate unafuu” mke wangu akamwambia “acha masihara paul, nimekufata twende kusali sasa nashangaa tena unaleta habari hizo, habari za kuanza kukunana humu ndani” paul akasema, “ kumbe hunipendi kabisaaa, yahani mimi nakueleza jambo la msingi unachukulia utani, basi kama hutaki we nenda niache niangaike”, mke  wangu akamwambia” haya sawa geuka sasa nikukune unawashwa wapi” paul akamuonyesha sehemu anayo washwa kumbe ni uongo tu, sasa kwakuwa paul alikuwa amejilaza kitandani akiwa amelala kifudifudi ikabidi mke wangu aweke mkoba pembeni ili alale juu ya paul, kusudi amkune kwa wepesi zaidi, kipindi anamkuna, paul akamwambia, “mke wangu sema kweli nimeamini moyo wangu unakupenda sana, yani ulipo panda juu yangu kunikuna najihisi raha sana, endelea kunikuna bebi, mke wangu alihisi kama anamsaidia kumbe zilikuwa ni mbinu za paul ili afanye mapenzi na mke wangu.
Kipindi  mke wangu anaendelea kumsaidia paul, mara ghafla paul akageuka na kumlaza mke wangu kitandani kisha akapanda juu yake na kumwambia, “mke wangu, nakupenda sana nimekumiss pia ningeomba penzi lako siku ya leo ebu tazama sindano yangu ilivyo simama na hakuna mtu yoyote wa kuitibu zaidi yako wewe, nisaidie bebi” mke wangu alichukia sana kusikia upuuzi ule akasema, “ paul ebu toka  juu yangu, utanikera nakwambia, hivi wewe uoni nina mtoto mdogo, au unataka katoto kangu ka dhohofike sio, alafu unajua mungu hapendi kuzini, maana mimi sasa hivi ni mama nilie okoka,” kipindi mke wangu anaongea maneno yale ya kishujaa na ndiyo kipindi hicho hicho, paul alikuwa alikuwa anazishika zile sehemu dhaifu za mke wangu maana alikuwa ameisha mzoea sana eliva, sasa wakati elivia analia akisema, tusifanye mwanangu bado mdogo, sijui tusifanye mimi nimeokoka, kumbe alikuwa tayari ameisha ingia majaribuni akajikuta anasogeza mdomo wake kwenye mdomo wa paul, ndipo wakaanza kubadilisha mate yao na wakazini hukohuko.
Mke wangu alipo maliza kufanya kile kitu aliumia sana, akasema” ehhh mungu nisamee najua nimetenda dhambi,” paul akacheka kisha akasema “haufanyi  dhambi yoyote mke wangu ni uoga wako tu, kumbuka mimi ndiye mme wako halali wa ndoa, sasa ukisema unatenda dhambi unakuwa unakosea anae tenda dhambi ni mme wako Yenda ambae hamjafunga ndoa bado” mke wangu akasema, “tungekuwa tumeisha funga tayari sema tatizo ni SHUNTAMA zako zilimletea matatizo,” paul akasema, “siwezi kukubali mfunge ndoa naitaji kuishi na wewe, jitahidi upate hizo mali za mme wako tuondoke ili tukaanze maisha yetu mapya, au sikupi mahaba matamu zaidi ya huyo yenda?” mke wangu akasema, “Mapenzi matamu unanipatia ndiyo, lakini paul kwanini tusiendelee kufanya hivihivi kwa siri kwani kinacho haribika ni nini, kama pesa nakupatia tazama unaishi sehemu nzuri na safi, vyombo vyote nakununulia, unachumba chenye kila kitu tamaa zingine za nini mpenzi wangu, nakupenda ndiyo lakini kumbuka tukitoroka nikamuacha mtoto wangu inaniuma sana maana nilimzaa kwa uchungu” paul akamwambia, “ hapana elivia kama hutaki mimi ndoa yenu haifungiki nitakuharibia kanisani na tutamtia yenda aibu sana mbele ya wazazi wake na marafiki zake wote”
Dah mke wangu alikuwa na msongo wa mawazo sana, hakuwa na jinsi akaamua tu kukubali wafanye huo mpango wao wa kunifilisi mimi kisha wao wakimbie na pesa zangu, kweli ali ingia bafuni kwa paul akaoga, sababu baada ya kucheza mechi alijihisi mchafu, kisha akaja nyumbani, alinikuta nipo na wazee wa kanisa tunafanya maombi ,na yeye akajiunga akijifanya anaomba mpaka analia,huku wakati huo mimi nafurahi sana nikisema mungu ni mwema amemfanya mke wangu  awe mpenda dini sana.
Baada ya kufanya maombi nikawambia wale wazee wa kanisa kuwa baada ya miezi miwili nitafunga ndoa na mke wangu, hivyo wawe wanatangazie kanisani ili watu wajue na wenye vipingamizi walete mapema kabla ya ndoa, mke wangu alishtuka kusikia vile akasema, “mme wangu tungesubili kwanza mtoto wetu akue maana bado mapema” nikamwambia “hapana mke wangu ili jambo jema sana la kufunga ndoa hamna haja ya kusubilia mtoto akuwe, tufunge ndoa mapema mungu abariki familia yetu”
Mke wangu alivyo kumbuka kuwa paul ata haribu ndoa yake kwa kuweka kipingamizi chake kuwa yeye Alisha wai kumuoa mapema, ndipo mke wangu  akaona ni bora afanye mpango mapema wa kuchukua pesa zangu ili wakimbie na kuniacha peke yangu naangaika.
Sasa nakumbuka ilikuwa ni jumatatu nilipo muita mke wangu na kumwambia kwamba, “mke wangu kama unavyo jua kuwa niliacha kazi yangu sababu ya yale magonjwa ya ajabu yaliyo nikuta, hivyo nataka kwenda benki nichukue pesa zangu zote ili nije tukae chini tubuni biashara kubwa kisha tuanze kujishughulisha” mke wangu alifurahi sana kusikia mawazo kama yale ya pesa akajua hapo lazima ataniibia pesa nyingi kwa wepesi zaidi.
Sasa nilipo fata ile pesa benki, Tsh million mia nne, nikamjulisha mke wangu kuwa tayari mzigo nimeisha ufata benki hupo chumbani mke wangu akauliza, “uko wapi sahivi” nikamjibu nipo kanisani naomba  maombi mke wangu,” mke wangu akasema sawa “nakusubili mme wangu,” Elivia mda huo alikuwa yupo sehemu za starehe na paul wanakula raha za maisha, kumbe alitoka pale haraka haraka akaja nyumbani akakuta pesa zote zipo kitandani million mia nne pesa za kitanzania, doooh tamaa ilimshika akampigia simu paul, kisha akamwambia kuwa kuna million mia nne ndani aje getini azichukue haraka kisha waanze mipango ya kutoroka na kuniacha mimi na umasikini wangu, kweli paul aliwai kama mashine akaja na akapewa lile begi lenye pesa zangu, mke wangu akarudi ndani akamwambia binti wa kazi aondoke arudi kwao, haraka. Binti wa kazi alilia kama mtoto ili asifukuzwe kazi, ila elivia alimfukuza masikini, Yule binti hakuwa na jinsi akamkabidhi mke wangu mtoto kisha akabeba mizigo yake, ndipo mke wangu akamlipa mshahara wake mtoto wawatu akarudi kwao,
Nilipo rudi kutoka kazini, nikamkuta mke wangu analia, doooooh. Nikamuliza, “ mke wangu unalia nini mbona huna raha” akasema “mme wangu nilikuwa nipo bafuni naoga Yule binti wetu wa kazi akaingia chumbani, akachukua lile begi la pesa kisha akamuacha mtoto analia sebreni alafu yeye akatoroka sijui kakimbilia wapi na ndiyo maana nalia”  sikuchukua ata dakika tano, nilipoteza fahamu na kuanguka chini hapo hapo.
USIKOSE SEHEMU YA NANE
SEHEMU YA 8.
MTUNZI FRANK DAVID/DAKTARI WA HADITHItz.  Whtsapp 0769510060.                        
Mke wangu alishangaa jinsi nilivyo anguka chini kama mti nakuanza kutoka damu kichwani, mwanzoni alihisi nimefariki, maana aliona nimekaa kimya mda mrefu bila kuamka, ndipo akavua kitenge chake na kuanza kunipepea upepo, huku akinipaka maji ya baridi ili nipate fahamu. Nilipo amka nilikuwa naongea ongea  tu mwenyewe kama chizi kwamba, "mke wangu pesa ziko wapi, nitaishi vipi mimi bila pesa, nitaficha wapi umasikini wangu na nimeisha zoea pesa mimi" mke wangu akasema, "mme wangu, hatuna jinsi tena, itabidi tumuachie mungu ndiyo anajua na kila kitu ni mipango ya mungu" dahhhh! Nilimkaba mke wangu shingoni kisha nikamdondosha chini, nikamniga sana shingo, maana nilihisi kama akili zangu zime hama, mke wangu aliumia maana nilikuwa sijamuachia, alianza kutoka mapuvu mdomoni, nikasema, "mpuuzi mkubwa sana wewe, yani milioni mia nne unasema muachie mungu ndiyo anajua" kipindi mke wangu anakaribia kufa maana nilimkaba vibaya sana masikini, palepale mtoto akaanza kulia, ikabidi nimuachilie mama yake kwanza, mke wangu aliishiwa nguvu kabisa akashindwa ata kunyanyua mikono yake, maana nilikuwa nimemkaba sana kidogo ata afe, sasa wakati nimekaa nawaza nafanya vipi, simu ya mke wangu ikaita, kumbe alikuwa amepiga paul, nilipokea mimi kisha nikasema, "hallow" paul alipo sikia sauti ya kiume, akasema" samahani jamani nimekosea namba", nikamwambia "hujakosea namba maana namba yako ime seviwa kuwa wewe ni paul, sasa sema shida yako", dahh paul alikata simu hapo hapo. Mke wangu alipo pata nguvu akaamka akasema, "we mwanaume mbaya sana, yani unataka kuniua kisa pesa alizo ziiba mfanyakazi kumbe unipendi mimi naondoka kwetu" nikamwambia mke wangu tafadhali najua nimekosea lakini we mwenyewe nazani umeona tatizo lililo tokea pesa zote zimechukuliwa hatuna ata mia ndani, hivi wewe unachukulia kawaida ili swala, hivi hujui tumeisha kuwa masikini wa kutupwa, pesa hamna kazi sina tutaishi vipi sasa, mtoto wetu bado mdogo sana, anaitaji maziwa, nguo, kutibiwa sasa hivi vyote atavipata vipi mtoto, kama hakuna pesa, na ndoa yetu pia tutafunga vipi kama hakuna pesa, hivi hii aibu naificha vipi mimi" baada ya kuongea vile nilianza kulia kwa sauti sana kama mtoto mdogo jamani, mke wangu alikuwa ananitazama tu ninavyo lia lakini hakuwa na huruma ata kidogo na wakati pesa alikuwa anajua zilipo. Nilitoka ndani ili niende kumtafuta yule binti wakazi popote alipo niweze kumkamata, wakati nipo njiani namtafuta nikakuta watu wengi tu wapo kwenye njia panda wamemzingira mfanyakazi wangu wa ndani maana alikuwa amegongwa na pikipiki vibaya sana kichwani hivyo ikimpelekea mpaka yule binti kufariki. Nilishindwa kumchukua yule binti kwa sababu niliona naenda kuongeza matatizo kwenye familia, sababu sikuwa ata na pesa ya kusimamia mazishi. Siku ziliendelea kwenda mbele tukiwa hatuna pesa kabisa ndani, majirani zetu walikuwa hawajui kabisa kama tunashida maana walikuwa wametuzoea kuwa sisi ni watu wenye pesa. Siku moja usiku tulilala njaa, maana sikuwa na pesa kabisa, mke wangu na yeye pia akalala njaa hivyo hivyo, sasa maziwa ya mtoto yakawa yameisha kabisa, na pesa ya kununua sikuwa nayo, mke wangu alivyo mjinga na yeye akakaa hivyo hivyo anamuona mtoto wangu analia njaa badala ya kutoa pesa kidogo kwenye ile million mia nne anunue maziwa akakaa kimya, maana alijua akitoa pesa tu nitagundua kuwa yete ndiyo ameiba zipe pesa, dahh ilibidi nimwambie mke wangu kwamba, "bebi mi nazani ile laki tano niliyo kupa ukamkopesha yule jirani sasa leo uende akupe ata nusu ili mtoto asiangaike na sisi pia tuweze kula, maana tunapo elekea tutaanza kuomba msaada kwa wazazi alafu nitaaibika sana, maana wanajua mimi nina hela, sasa nikiomba elfu kumi watanishangaa mno" mke wangu akasema ile pesa alisha nipa, na nili itumia kama ulivyo niambia kwamba niitumie kwenye matumizi yangu" dooh nilichoka kabisaaa ikabidi nikae, tulipiga sana miayo ya njaa, kumbe paul yupo anakula chips mayai, anakunywa bia na vinywaji vya bei sana zile pesa zangu masikini, mke wangu alikuwa ni mjinga sana jamani maana mwenzake paul anakula maisha yeye analala njaq pamoja na mtoto wake na mimi pia. Nakumbuka kipindi tukiwa na shida ya pesa, baba yake Elivia aliugua sana, sasa kwakuwa nilikuwa nimewazoesha kuwatibu mimi, hivyo akawa amekuja nyumbani kwangu ili mimi nimpeleke hospital, sasa kibaya zaidi sikuwa na pesa hivyo sikuwa na jinsi ikabidi nimwambie mzee augulie palepale nyumbani, baba mkwe wangu aliugulia ndani mpaka anafariki bila matibabu yoyote, huku mke wangu akiwa anamtazama tu baba yake anakufa, wakati anapesa nyingi sana, kaniibia akashindwa kumtibu ata baba yake mzazi, maana alikuwa  anaogopa kumsaidia baba yake kisa anajua akitoa pesa mimi nitagundua kuwa yeye ndiye alie iba, mazishi ya baba mkwe wangu yalifanyika na tukamzika vibaya vibaya maana hatukua na pesa kabisa, mpaka watu walio kuwa wananijua walishangaa sana wakasema, "dahh huu msiba mbona wa kimasikini hivi, yani mzee anazikwa kama vile hana ndugu, wakati huyu Yenda anapesa nyingi sana, dahh maisha haya" walisema hivyo maana walihisi nina pesa kumbe mimi najijua mwenyewe. Mke wangu aliumia sana baba yake alivyo fariki, na alijifanya hana pesa, mpaka baba yake akafa sababu baba alikosa huduma za kiafya, kumbe paul yeye hawazi kabisa anaendelea kuota shavu na anakula starehe za kila aina, mke wangu alikuwa mjanja sana kwenye hela aliniaga kuwa anaenda kutafuta kazi kumbe anaenda kwao, alipo fika kwao akaingia kwenye chumba cha baba yake, akatafuta hati ya ile nyumba niliyo mjengea baba ake kisha akaiuza kwa pesa ndogo sana alafu zile pesa za nyumba akampa paul ili aunganishe na zile millioni 400 kusudi wakitoroka wasiweze kuteseka ata kidogo. Sasa alipo rudi nikamwambia, mke wangu kwamba "kwakuwa ile nyumba ya baba yako nilijenga mimi, naomba tui uze maana wazazi wote hawapo kisha izo pesa za nyumba ndiyo tufanye mtaji ili tuanze kupata pesa upya maana hapa hamna namna nyingine"  nikashanga sana kusikia mke wangu anasema kwamba, "hapana bebi usiuze maana mzimu utatutesa wa baba, sababu ile nyumba baba alimpa urithi ndugu yetu mwingine na kesho wanaweza kuamia" kumbe mke wangu alikuwa anasema vile kwa sababu alikuwa ameiuza nyumba tayari.
Dah sikuwa na jinsi ikabidi nikubali matokeo, kumbe paul kwakuwa alikuwa na pesa zangu nyingi hivyo akapanga wazo la kununua gari. Mke wangu siku moja akaniambia, "mme wangu haya maisha yameisha anza kunichosa" nikamuuliza "kwanini?" Akasema "tunateseka sana hatuli vizuri, nguo hatubadilishi tumekaa tu kama wanyama humu ndani, katoto kangu kamekaa kama kamebemendwa, nimechokaaa" nikamwambia kwamba, "mke wangu kama unavyo jua sahivi sina kazi, na marafiki zangu wote sahivi wamenikopesha hela zao nimeshindwa kuwalipa kwa sababu sina pesa, wewe vumilia tu mke wangu" Elivia akasema, "Yenda mimi naanza kuchoka kabisaaa" nikamwambia, "usisahau ulipo toka Elivia, nilikuokota balabalani ukiwa mchafu sana, umepauka kweli kweli, nikakuleta hapa ukapendezaa, sasa sahivi unajifanya shida uzijui, nakuwa sikuelewi, maana mimi nilikupenda kwa sababu ya heshima na upole wako, kumbe nilikosea njia sio. kuwa mvumilivu na mungu atatusaidia Elivia" mke wangu akachachamaa kweli kweli, akasema, "Yenda vitu vilivyo pita sitaki kuvisikia hapa, ebu angalia mtoto anaumwa dawa hatumpi, mtoto hali akashiba pesa hutoi, hivi unataka nikajiuze nilete pesa ndani" nikasema "dooh sawa mke wangu ngoja nitafute pesa" kabla sijatoka nje nikapigiwa simu na mama yangu mzazi akasema "mwanangu huku nyumbani tumeishiwa pesa kabisa, tunaomba ututumie pesa ya matumizi," dooh nilichoka sana mpaka nikapata kiu cha maji, nikamwambia mke wangu, "bebi naomba uniletee maji ya kunywa" mke wangu akasema "bebi maji yameisha yote ndani, nasubilia unipe hela nikanunue yale maji ya kunywa" na wakati hup mfukoni sina ata pesa, ikabidi niuze gari langu ndipo akalinunua mr Paul kipindi hicho mimi bado ata sijamjua, hivyo ile pesa yangu iliyo iba mke wangu akampatia, paul alichukua milioni 25 nikamuuzia lile gari langu. Dah nilipo uza gari nikapata nafuu kidogo, sikukaa ata siku nyingi mke wangu akaanza kupendeza mtoto akaanza kupendeza pia, maana nilikuwa nawapenda sana mke na mtoto wangu. Ile pesa yote nikaamua kufungua duka zuri tu lenye vitu vya matumizi ya nyumbani, kama sabuni, ndoo za mafuta na vingine vingi tu, sasa nilipo fungua lile duka pesa yote nilikuwa nimewekeza humo, mke wangu akanishauri tuuze nyumba alafu tupange ili duka lijae zaidi tutengeneze hela ya kutosha alafu tujenge nyumba nzuri mpya badae. sikumpinga mke wangu, maana niliona ni wazo zuri kabisaa,  nikauza nyumba yangu kisha zile pesa zote nikaziweka dukani, mpaka duka langu likajaa na kupendeza zaidi, heshima yangu ikarudi kama ya zamani, Sasa siku moja usiku nikiwa nakaribia kufunga duka, walikuja majambazi pale na gari lao kubwa tu, mimi nilihisi kuwa wanataka kununua vitu kumbe nia yao wanipole kila kitu dukani watoeke navyo, aliingia kaka dukani akasema, "habari mangi, hivi hizo freestyle box zima shingapi" nikamjibu kwa usitaharabu sana kuwa ni elfu 23000, akasema ebu tuone wakati namtolea aone nikageuka nyuma, kipindi namuangalia sasa nimpe box, akatoa bastora kisha akasema toa pesa zako zote, dooh nilikuwa naogopa kufa nikazitoa zote, kisha akawambia vijana washuke kwenye gari wasombe mizigo yote dukani waweke kwenye gari, mimi nilikuwa nimetekwa hakuna raia alie jua kuwa ni majambazi walihisi kuwa ni wateja tu wa usiku wamenunua vitu, dooh vitu vyote vilisombwa duka likabaki wazi na pesa zikabebwa kisha wakanifunga mikono na miguu alafu wakanijaza mifuko mdomoni ili jisiongee wala kupiga kelele, kisha wao wakaondoka, dooh kuna mteja wangu aliingia ili anunue vocha akanikuta nimefungwa mikono na miguu kisha mdomo wangu umejaa mifuko tu, alitoa na kunifungia dahhh hakuamini nilivyo msimulia jinsi wale majambazi walivyo niteka, nikaamua tu kuacha duka wazi kisha nikaenda nyumbani kumwambia mke wangu matatizo yaliyo nikuta,
nilipo mwambia Mke wangu, alichukia sana akasema, "weh hivi hizo mali zako niza kishirikina kwamba zinapotea umeshindwa kufata mashariti au, sasa mbona zinaondoka kama vile upepo, kumbuka hii nyumba tumepanga na kesho inabidi tulipe kodi alafu unasema kwamba umeibiwa kila kitu dukani sikuelewi, sikuelewi kabisaa yahani." Dah sikuwa na jinsi sasa, ndipo nikaanza kuchoka na maisha mwili ukafubaa sana yahani naona aibu sana kuonekana mtaani, mke wangu pia akaanza kunichoka ndugu zangu wakaanza kusema huyu ndugu yetu hatupendi kabisa, anatunyima pesa wakati sisi ni ndugu zake. Nilihisi maisha machungu sana kwangu ndipo nikaanza kazi ya kuosha magari, siku moja wakati naosha magari nikaosha lile gari langu nililo liuza na nilie kuwa namuoshea alikuwa ni paul alie iba pesa zangu na yule mke wangu. Dah "kweli haya maisha hayaeleweki kabisaa" sasa siku moja nimerudi nyumbani nikiwa nimechoka sana, nikamkuta bana mwenye nyumba anatufukuza  kwake, kwamba tuondoke kwake eti mke wangu anagombana sana na wapangaji wengine, nikajaribu kumuomba msamaa ili angalau atupe mwezi mmoja, mwenye nyumba akasema, "nyie hamfai kuishi na watu, yani kodi hamlipi nawatunza tu, alafu bado mnagombana na wapangaji wangu tokenii" ndipo mtoto wetu alianza kulia pale dahh, ndipo mwenye  nyumba akapata huruma maana alikuwa anapenda sana watoto, ila akasema tuishi kwa ustaharabu, Sasa kumbe paul siku moja akamwambia Elivia kwamba, "bebi wakati sasa umefika wa kuondoka na kumuacha huyo yenda mme wako, itabidi hii wiki tuondoke maana pesa tayari inatosha, alafu huyo mtoto wako muachie mme wako sisi tuondoke zetu" mke wangu akasema "sawa paul ngoja nijiandae maana haya maisha yameisha nishinda, liwalo na liwe" kipindi hicho mimi nipo napambana sana kutafuta japo elfu moja ili mke wangu na mtoto wangu wapate kula, na wala nilikuwa sijui kama mke wangu anampango wa kutoroka na kuniachia mtoto mdogo ndani. USIKOSE SEHEMU YA TISA. Mtunzi ni FRANK DAVID/ DAKTARI WA HADITHItz. Whtsapp 0769510060                       
 SEHEMU YA 9.
MTUNZI FRANK DAVID, DAKTARI WA HADITHI_tz. Whtsapp 0769510060.                                  Kweli bhana, siku moja mke wangu alijiandaa ili atoroke na paul wake, ili waende wanapo jua wao, na Elivia alikuwa mjanja sana maana alijiandaa siku ambayo alijua mi nipo bize mtaani nikitafuta pesa, kweli aliandaa nguo zake kwenye begi kisha akaoga, sasa wakati anatoka nje, mtoto akaanza kulia, dahh mke wangu huruma ikamshika masikini, maana katoto ketu kalikuwa kadogo bado, alitamani kubaki lakini upendo wake mwingi wa moyoni ulikuwa kwa paul, ndipo mke wangu akachukua karatasi na karamu kisha akaandika ujumbe ili mimi nikija niukute, ujumbe ulikuwa unasema kwamba, "Yenda mme wangu, najua tulipendana sana kipindi chote hicho, mpaka nikakuamini na nikaamua kukuzalia mtoto, ila maisha yamenishinda nimeamua kuondoka na kukuachia mtoto wako, sehemu ninayo kwenda siijui, lakini nakutakia maisha mema na yenye mafanikio" mke wangu alipo maliza kuandika ile barua, akaikunja na kumlaza mtoto kitandani, kisha akaweka ile barua juu ya tumbo la mtoto ili nikifika niipate kwa urahisi, mke wangu alipo maliza akafunga mlango na kufuri kisha akaenda kwa paul na wakasafiri sehemu ambayo nilikuwa siifahamu. Mtoto alibaki mule ndani akiwa ajala kitu chochote tangu asubui, alilia sana mtoto wangu mule ndani, mpaka majirani wakatamani kubomoa mlango ili wampe mtoto chakula, sasa mimi nilipo rudi kutoka kazini, nikakuta watu wengi karibia na mlango wangu wananisema vibaya sana kwamba, "hii familia ya kipuuzi mno, yani wanatoka wote na kumuacha mtoto mdogo ndani akiwa na njaa na analia sana hivi dahh" nikawauliza, "jamani mbona mmenuna alafu wote mpo mlangoni mwangu", wakasema, "Yenda wewe na mke wako mmefanya kosa sana, yani tangia asubui mmefunga mlango mtoto akiwemo ndani, mtoto ajala chakula analia tu, hivi mnataka afe?" Nikasema, "niniiiii" kwani mke wangu yuko wapi, wakajibu "mke wako tangu asubui hayupo wewe pia hukuwepo ila mtoto mmemfungia ndani" dooh tulibomoa kufuri na kuingia ndani haraka, nikakuta mtoto wangu amelia mpaka macho yakawa mekundu, amejikojolea na kusidia bila kubadilishwa nguo, dahh nilitoa machozi sana, wakati naangalia kitandani ndipo nikakuta ule ujumbe kuwa mke wangu ameondoka na kuniachia mtoto, na ameondoka sehemu asiyo ijua, dooh nilihisi kuchanganyikiwa, majirani wakasema, "Man Yenda tatizo nini"niliongea huku nalia kwamba, "ndugu zangu someni hii barua", waliisoma barua ika waumiza sana mpaka wakanionea huruma, kila mtu akaanza kusema yake, "huyu mwanamke ni chizi kweli, yani kamuacha mtoto alie mzaa mwenyewe, si bora angetoroka na mtoto" wengine wakasema, "dooh wanawake wengine ni mikosi kabisa, ukiwa nao mambo yako yote lazima yakwame" dahh waliongea sana pale mambo mengi, ila mimi nilikuwa nimehisi kuchanganyikiwa tu maana kila siku matatizo kwangu yanazidi, mara ghafla mtoto akaanza tena kulia, ndipo nikachukua maziwa yake ya kopo kisha nikachanganya na maji ya baridi nikihisi ni sahihi kumbe sio, yahani mpaka maji yachemshwe na ya pozwe kidogo ndiyo mtoto anywe, sasa nilivyo mnywesha mtoto maziwa ya baridiii alikuwa anakataa huku akiendelea kulia masikini mpaka nikahisi chumba chote kichungu, maana nampa maziwa hataki alafu analia tu, dahh nilipo ona mtoto analia na mimi nikaanza kulia ndani yahani tukaanza kulia wote, dada mmoja hivi msitaharabu kweli akaja na kusema kwamba, Yenda leta mtoto nikusaidie kumbembeleza, kweli yule dada alimbeba na kumtengenezea maziwa mtoto akanywa na  akaacha kulia, akamuogesha kila kitu na mimi pia nikajifunza jinsi ya kulea mtoto kipindi hicho, sasa nikaanza kuangaika ikifika asubuhi maana nilishindwa kwenda kazini kutafuta pesa, maana sikuwa na mtu wa kumuachia mtoto, ikafika kipindi nikaanza kwenda na mtoto kazini, nikifika namtandikia chini kisha mimi naanza kuosha magari ya watu mda ukifika nampa maziwa, mpaka mtoto akazoea,  sasa kutokana na kuangaika kote kule ikabidi nimchukue mtoto ili nimpeleke kwa bibi yake  amtunze maana hali ilikuwa ngumu upande wangu, kweli mama yangu alimkubali mtoto na akakubali kumtunza maana niliamua kuwa mkweli na kumuelezea maisha yangu na matatizo yaliyo nikuta, ila mama alicho niambia ile millioni mia nne na wale majambazi walio nivamia dukani yote hiyo ni mipango ya mke wangu, na kwakuwa ameisha pata pesa basi ametoroka na kukuacha wewe kwenye shida, nikamuuliza mama, "sasa kama elivia ana pesa kwanini amemuacha mtoto wake", mama akasema, sisi wanawake tunarubuniwa sana, mi nazani amepata kijana wamependana sasa huyo kijana labda kamzuia asiende na mtoto" dahh niliumia sana nikasema, "yani msaada wangu wote kwa Elivia leo hii anaiba mali zangu zote duuh"
Siku moja nikiwa katika miangaiko yangu nikakutana na jamaa mmoja anaitwa Juma, huyu Juma alikuwa mmoja wawatu nilio kuwa nafanya nao kazi ofisini kipindi cha nyuma, akasema, "kaka hapa nilipo natokea Mtwara, huwezi kuamini nimemkuta mke wako huko na bwana mmoja hivi anapesa sana, na huyo bwana ana gari linafanana sana na lile gari lako, alafu huyo bwana amekuwa maarufu sana huko sababu anapesa sana huko Mtwara, anaitwa bwana paul," dooh sikuamini kabisa nikasema, "we juma unasema kweli au unanitania" akasema ndiyo, yani wewe kama unamjua paul basi huyo ndiyo anajivinjari na mke wako uko Mtwara" nikafikilia sana "paul ni nani, paul ni nani, paul ninaniiiiii" dahhh nilifikiria sana mpaka kichwa kikauma, ndipo nikakumbuka siku nilipo ibiwa pesa na kumpiga mke wangu, simu iliita ya mke wangu jina limeandikwa paul, kisha huyo paul alipo sikia sauti yangu akakata simu, na nikakumbuka pia alie nunua gari langu kwenye mkataba jina liliandikwa paul, alafu juma anamtaja kuwa paul ndiyo anakula maisha na mke wangu na ana gari kama langu, doooh moja kwa moja nikapata jibu kuwa mke wangu ndiye alie fanya mpango wa pesa zangu kuibiwa na kufanya mpaka mimi nifirisike, nikasema, "sikubali lazima niwafate mtwara, na lazima nilipize kisasi" nilijiandaa kisha nikasafiri bila kumuaga mtu yoyote mpaka nikafika Mtwara, sasa ubaya nilifika nikiwa sina ata pesa mfukoni, hivyo nikaanza kujiusisha na maswala ya kuosha magari kwenye ofisi za watu, kisha nikipata pesa nakula na kulipa nyumba za wageni nilipo kuwa nakaa, sasa jamani siku moja wakati naosha magari, nikaona lile gari kama langu nililo muuzia paul linakuja, dooh nikajificha chini ya gari ili nione kama mke wangu yupo mule ndani ya gari, sasa gari lilipo fika paul akasimamisha, maana walikuwa wanataka kuacha gari lioshwe alafu wao waende kula lanchi, sasa paul alivyo shuka, akaenda upande wa pili kumfungulia Elivia huku mimi nipo chini ya gari nawa chungulia tu, paul alipo mfungulia Elivia,  wakati anambusu sasa ili waende kula hotelini, nikatoka chini ya gari kisha nikasema kwa nguvu nikiwa nalia, "Elivia mke wangu, kumbe upo huku, kwanini umetukimbia mimi na mwanao, kwanini una roho mbaya sana wewe mwanamke"... USIKOSE SEHEMU YA 10.                       
SEHEMU YA 10
MTUNZI FRANK DAVID, DAKTARI WA HADITHI_tz. WHATSAPP 0769510060.                                Mke wangu alipo sikia sauti yangu nikimwambia vile kuhusi yeye kutukimbia mimi na mtoto, aliishiwa nguvu kwakweli, akatamani kunifata, paul akamvuta akasema "anaenda wapi sasa" Elivia akasema, "Yenda mtoto wangu yuko wapi, na anaendeleaje" nikamwambia, mtoto yupo nyumbani na anaishi maisha ya tabu sana, wewe upo huku mnakula maisha na paul, kwanini ulinifirisi mke wangu, mmeniibia pesa zangu zote mkakimbilia huku mtwara kwanini" paul akasema, "we elivia ebu ingia kwenye gari tuondoke" elivia alikuwa mgumu sana ata kuingia kwenye gari maana alinitazama nilivyo kuwa nikilia huku nimechafuka, nguo zimetoboka, wakati mimi nilikuwa mtu mwenye pesa zangu kipindi cha nyuma na mimi ndiye nilie muokota na kumsaidia yeye kwakweli ata yeye alijisikia vibaya sana, Elivia na paul waliingia kwenye gari kisha wakaondoka, dooh niliishiwa pozi kabisaa mpaka nikashidwa ata kuendelea kuosha lile gari, ikanibidi nirudi kule ninapo kaa, ili nipumzishe kichwa changu mawazo, hivyo basi kutoka na kuacha kufanya kazi siku hiyo nikawa sijaingiza pesa kabisa mfukoni, wakati nafikiria nifanye nini ili nimrudishe mke wangu ili niishi nae tumlee pamoja mtoto, mama akanipigia simu akasema kwamba mtoto anaumwa nitume pesa za hospital, dooh nilichoka aisee, maana sikuwa na chochote mfukoni, ikabidi nirudi kazini tu, kweli nilijitahidi nikapata elfu 30, nikatuma kwa mama kwa ajili ya matibabu ya mtoto. Paul alipo fika kwake akaanza kumgombeza elivia akimwambia, "wewe ni mjinga sana, yahani kumbe hunipendi, sasa kwanini ulikuwa unataka kumfata Yenda, kumbe bado unampenda sio" elivia akamwambia, "hapana sio kwamba nampenda lakini kumbuka nimezaa nae, mda mwingine nafsi inanisuta, alafu hizi mali tunazo zitumia hapa zote tumemuibia yeye na ameisha tugundua, hivi unaweza kuwa huru kiakili kweli, au na wewe hujifikilii" paul akasema "dahh lakini kweli elivia lazima ituchanganye kidogo" sasa mimi huku nilikuwa nawaza jinsi gani naweza kwenda mpaka kwa paul anapo ishi kusudi nimchukue mke wangu na niwaombe pesa zangu Tsh millioni 400 niondoke kurudi nyumbani. Sasa baada  kama ya wiki moja mbele, nilianza kuwatafuta nakuulizia sehemu anapo ishi huyo paul mpaka nikapajua, nikaanza kupanga mikakati ya kutaka kwenda na kufanya vurugu pale kwake mpaka waelewe. Nilipo fika getini kwao nikakuta mlinzi, nikamuomba, "kaka habari za kazi, naomba niingie ndani nataka kuonana na paul maana alisema nije kuna kazi anataka kunipa" yule mlinzi hakubisha akaniruhusu, nilipo ingia tu paul na yeye pia akawa anatoka hivyo tukagongana uso kwa uso, akasema, "we yenda kwa nini unafatilia maisha yangu, umefata nini nyumbani kwangu" nikamwambia, "paul, nimemfata mke wangu pamoja na mali zangu zote, hizi mali sio zako mmeniibia wewe na Elivia, nimefata haki zangu" paul akasema, "mjinga sana wewe, mali zako zipi hapa, nasema ondoka hauna chako hapa na ukiendelea kunifatilia nitaondoa maisha yako" baada ya kuongea vile, paul akaanza kumtukana mlinzi, "kwanini unaingiza watu kama hawa nyumbani kwangu, kazi imekushinda ama" mlinzi akasema "hapana bosi, yeye alisema umemuita kuna kazi unataka kumpatia" paul akasema, "huyu ni kibaka tu ni muongo sijamuita mimi hapa, ni mwizi mtoe haraka sana" kweli bhana mlinzi alinisukuma nikatoka nje kama mwizi, na paul akasema ukirudi hapa naku ua kwa mikono yangu miwili. Nilirudi sehemu nilipo kuwa naishi, lakini ilipo fika mida ya saa tano usiku nilikosa usingizi kabisa nikasema, "siwezi kuona watu wanafurahia maisha kwa pesa zangu na mke wangu wakati mimi naangaika ni bora nife sababu ya penzi, yahani mpaka nimpate mke wangu na mali zangu zote  zirudi", nili rudi mpaka kwa paul mida ya usiku nikaanza kuchungulia nje ya fensi ili niruke na kuingia ndani niweze kufanya vurugu tena, sasa wakati nipo kwa nje nikachungulia kwenye fenzi pale nikamuona mke wangu pamoja na paul wake wanapeana busu na kufurahia maisha huku wakinywa "wine"! dah moyo ulikuwa unaniuma nashindwa ata nifanye nini, sasa kipindi nipo nachungulia nikaona paul ameingia ndani na kumuacha Elivia peke yake, dahh sasa kwakuwa nilikuwa nampenda sana Elivia, nikaamua kuruka fensi na kuingia mule ndani, ili niongee nae, sasa nilipo ingia nikanyata polepole mpaka sehemu alipo kuwepo elivia nikamshika begani na kumwambia polepole kuwa, "nimekufata wewe mke wangu bado nakupenda naomba amka tuondoke ukamuone ata mtoto wako amekumisi mama yake" elivia akasema, "we yenda umeingiaje humu ndani, mme wangu amefata simu yake atakukuta ondoka" nikamwambia nashindwa kuishi bila wewe, bora aje aniue tu nife sababu ya upendo wako tu, maana nakosa furaha ya maisha bora nife, alafu naumia sana maana mmeniibia pesa zangu nyingi sana mimi nimebaki naangaika tu" wakati tunaongea vile akaja paul nakunikuta nipo naongea na Elivia, dooh alikasilika sana akasema, "we mpuuzi kwanini unaongea na mke wangu usiku huu tena kwangu bila ruhusa yangu" nikamjibu nakusema kwamba, "huyu ni mke wangu amenizalia mtoto, umeniibia mke pamoja na mali zangu" paul akasema "ondoka muache mke wangu nitaku ua" nikamwambia, nipo tayari kufa sababu ya upendo nilio nao kwa Elivia, sasa kama mali baki nazo ila namuomba mke wangu niondoke nae nampenda" dooh paul alichukia akasema "nisubili nakuja" Kisha akaingia ndani, Elivia akasema, "paul mme wangu ondoka, mungu akipenda nitakuja tu kumuona mtoto wetu, kimbia huyu bwana anaweza kukumaliza kweli atakuja na bunduki" dooh wakati nipo nasubilia aje aniue duhh alikuja na panga anataka kunikata, nilikwepa kisha nikakimbia nikaruka fensi haraka sana, paul alichukia sana siku hiyo, akamfata mlinzi getini kumuuliza kwanini kaniruhusu niingie ndani,  akakuta mlinzi amelala, dahh alimpiga yule mlinzi na kumuachisha kazi siku hiyo hiyo. Alimgombeza sana Elivia akimwambia, "hivi we mwanamke kwanini unaongea na huyo bwana mnataka kunizunguka sio" elivia akasema, "hapana paul, mi nimeshangaa amefika ghafla hapa nikashindwa cha kufanya". sasa mimi siku hiyo sikupata usingizi kabisa maana nilipo ongea na Elivia nilitamani sana arudi niendelee kuishi nae, siku moja nikaenda mpaka kwa paul mchana, nikakuta hakuna mlinzi maana alikuwa tayari amefukuzwa kazi, nilipo ingia ndani nikakuta paul hayupo ameenda kwenye kazi zake, ila pale nyumbani alikuwepo Elivia tu, mimi niliingia mpaka ndani sebreni, nikamkuta elivia amevaa kanga moja bila kitu chochote ndani akiwa anaangalia Tv, alishtuka kuniona akasema, "yenda toka nje,  paul, akikukuta atanipiga" nikasema hapana usijali, kwani ameisha nikuta mala ngapi niko na wewe na  hajakupiga" nikamwambia elivia kwamba, "najua unampenda paul, lakini kumbuka ata mimi nakupenda wewe elivia, ebu fikiria pesa zote mmeiba, sawa nimewaachia lakini moyo wangu upo kwako elivia naomba ukajiandae tuondoke"  elivia akasema, "yenda, naumia sana kukuacha wewe na mwanangu kwa sababu moyo wangu unajua thamani yenu, lakini huyu paul, ndiye alie kuwa mume wangu wa mwanzo na ndiye nilikuwa nampenda sana, maana aliutoa usichana wangu na ananichanganya sana akili kwa mapenzi yake, yahani najikuta nakosa msimamo wa mapenzi mpaka najishangaa,, ata wewe nakupenda yenda lakini nashindwa kuweka chaguo sahihi" nilimfata karibu Elivia nikiwa nambembeleza ili niondoke nae, sasa wakati nimemshika mala ghafla hisia za mapenzi zikanishika nikajikuta namsukumia kwenye kochi la paul nikiitaji kufanya lile tendo, nikampandia juu kwa nguvu akiwa anaogopa na kukataa, sasa wakati amelala na yeye kwenye kochi huku akinizuia nisifanye lile tendo, ghafla tu malango ukafunguliwa paul akaingia na kutukuta tumelala kama tunafanya mapenzi,, duhhh alitoka nje na kutufungia ndani, kisha akaja na vijana sita wameshiba kwelikweli, yahani wananguvu sana, walinipiga sana, tena mbele ya elivia mpaka nikaishiwa nguvu kabisaa. kipindi nimeanguka chini sina nguvu  wakanibeba na kunipeleka msituni kwenye vichaka huko mtwara, ambapo ata sipajui wakanirusha kwenye shimo lefu sana katikati ule msitu, kisha wakasema, ngoja ufe humo ndani sababu ya mapenzi. USIKOSE YA 11.                       
SEHEMU 11
MTUNZI, FRANK DAVID/ DAKTARI WA HADITHI_tz. Whtsapp 0769510060.              
 Kipindi wananirusha shimoni nilianguka vibaya sana maana mkono uligonga jiwe mule shimoni hivyo nikateguka mkono na nikapata maumivu makali sana kwenye mwili. Nilibaki mwenyewe mule vichakani mpaka giza likaingia, sema kweli nilikuwa naogopa maana nilikuwa nasikia sauti za wanyama, na ndege kama bundi zikilia, nikajua humu shimoni lazima nife tu sina jinsi. Niliamua kulala mule shimoni mpaka asubui, ila sema kweli niliamka na maumivu makari sana maana nilipigwa alafu nikarushwa kwenye shimo hivyo mwili ulikuwa hoi, njaa ilianza kunishika sina sehemu yoyote ya kula, alafu nikilitazama shimo ni refu sana alafu pana siwezi kupanda juu, nilipiga magoti mule shimoni nikamuomba mungu anisaidie nisiweze kufa kwa sababu ya mapenzi yangu ya dhati kwa mke wangu elivia, kipindi nimepiga magoti nasari kumbe kulikuwa na siafu chini dahh hao siafu walini ng'ata sana siku hiyo nikajaribu kukimbia ila wakazunguka shimo zima hivyo niling'atwa sana mpaka mwili wangu wote ukawa unawashwa tu, nilikuwa siogi wala siri kwa raha mpaka nikaanza kutoa harufu mbaya sana mwilini mwangu na nikapauka sana ngozi sababu ya kukosa lishe, kilicho kuwa kinanisaidia ni kwamba juu kabisa ya lile shimo kulikuwa na mtiwa mapera hivyo nilikuwa namuomba sana mungu alete ili mti utingishike mapera ya dondoke chini nile nilale. Sasa kipindi mimi nipo nalia, najiona kabisa kuwa nakaribia kufa kwa sababu ya elivia, kumbe mama yangu nyumbani alikuwa anaumwa sana, na mama yangu alikuwa anaishi mwenyewe sababu baba yangu alifariki zamani sana, hivyo mimi nilikuwa kama msaada wake mkubwa, sasa kipindi anaumwa alijaribu kunipigia simu ili nitume pesa za dawa lakini mimi nilikuwa nimetupwa shimoni masikini sipatikani, mama yangu mzazi alianza kuni laani akisema, "yahani yenda nimekuzaa mimi nimekulea mimi alafu leo hii mama yako nafia ndani umenizimia simu mtoto wangu yahani we mbaya sana" hazikupita ata siku nyingi, masikini mama yangu aliteseka sana akiwa na mtoto wangu, maana katoto kangu kalikuwa kamemzoea sana bibi yake kakizani kuwa ni mama, sasa kutokana na ugonjwa na pesa ya chakula kukosekana mama yangu alipoteza maisha kizembe sana masikini, sasa wakati mama yangu anafariki, mtoto wangu alikuwa juu ya tumbo lake analia akiitaji bibi yake aamke ampe chakula, kipindi hayo yote yanafanyika mimi nilikuwa chini ya shimo nalia tu sijui kinacho endelea nyumbani. Kumbe mama yangu alifariki na majirani ndiyo walimtoa mule ndani na ndugu wakafika maana walikuwa hawakai tena na mama sababu ya maisha kuwa magumu, hivyo walivyo fika wakashughulikia swala zima la msiba. Sasa mimi kipindi nipo shimoni nilishikwa na kiu sana jamani, hivyo nikashindwa kabisa jinsi ya kufanya ili nipate maji ya kunywa, lakini hazikupita ata siku mbili mvua zikaanza kunyesha sana maji yaka jaa pale chini na nikanywa hivyo hivyo tu yakiwa machafu, maana mule shimoni palikuwa pachafu sababu panya walikuwa wamo mule na wadudu wengi tu, mvua zilinyesha sana mpaka zikaanza kunikera sasa maana maji yalikuwa yanajaa mpaka yanataka kunifunika na kunizamisha chini, sasa kutokana na mvua kuwa kubwa sana hivyo manyasi na miti ikaanza kuchanua, huwezi kuamini kuna manyasi yalikuwa yanaota kwa kudondokea shimoni mpaka yakawa marefu kabisa mpaka chini, sasa mimi nilicho fanya nikayakusanya yale manyasi  kisha nikayafanya kama kamba nikapanda nayo mpaka juu ya shimo maana yalikuwa yameota juu ya shimo, mungu saidia hayakuachia maana yalikuwa mengi, nilipanda mpaka juu ya shimo kabisaa nikatokamo shimoni. Dah nilivyo toka nikasema hapa nikirudi kwa paul nitakufa ni bora tu niende sehemu nijifiche kwanza alafu badae ndiyo nianze mapambano yangu ya kulipiza kisasi. Sasa kule nyumbani kumbe ndugu zangu waliamua kukaa na mtoto wangu, ila walikuwa wanakapiga sana yahani wanakatesa kila mda, mtoto akakaa bila amani kakawa kaoga alafu akajiamini kabisa, maana kalihisi kametengwa sana, sasa siku moja Elivia akiwa amelala alimuota mtoto wake usiku  mala ghafla tumbo lake la uzazi likaanza  kumu uma, paul akamuuliza "nini tatizo" elivia akasema, "nimemkumbuka mtoto wangu sana mpaka najihisi mabadiliko ndani ya mwili wangu, natamani kumfata tuishi nae hapa, maana yenda ameisha kufa, sababu mmeisha muua wewe na marafiki zako, hivyo bora tufate mtoto tukae nae sisi hapa nyumbani" kweli walipanga safari kisha wakaenda mpaka kwetu na walipo muomba mtoto ndugu zangu hawakukataa kabisa maana walikuwa hawakapendi katoto kangu". Dooh sasa mimi baada ya mda niliamua kurudi kwetu kwanza ili nimuone mama pamoja na mtoto wangu, dooh nilipo fika nikashangaa kukuta mama yangu amefariki alafu mtoto wangu amechukuliwa na paul wakizani kwamba mimi nimekufa hivyo wapo huru tu.
Dahhh niliamua kurudi mpaka mtwara kwa mr paul kusudi niweze kumchukua mtoto wangu. Sasa nilipo fika kule nikaogopa kwenda mchana maana nilijua paul akiniona tena nitatupwa mule shimoni kwa mala ya pili, ikabidi niende usiku maana nilijua wanapenda sana kukaa ubarazani mida ya usiku, nilipo fika nikachungulia kweli niliwaona wote, nikamuona mtoto wangu, elivia pamoja na paul, wapo wanafurahia tu maisha. Paul akasema "ngoja nikazime friji maana tangu jana imewaka tu na hamna vitu vya maana kwenye friji" wakati ameingia ndani nikaruka fensi haraka haraka, kisha nikaenda mpaka kwa Elivia akiwa na mtoto, elivia akakimbia ndani akisema, "paul mzimu wa marehemu yenda umekuja" mimi nikamchukua mtoto wangu kisha nikarudi mpaka kwenye gesti nilipo kuwa nimepanga. Dooh paul akaogopa akasema "yenda amefata nini tena au wewe unamuwaza tu" elivia akamwambia "twende mlangoni umuone" walipo kuja wakakuta mtoto hayupo tayari nimeisha ondoka nae. Dooh elivia alilia sana akasema, mwanangu amebebwa na baba yake nitampata wapi tena mimi, paul akamwambia "usijali elivia kama mtoto ni mzima tutampata tu"
 Niliamua kuanza kupambana na maisha yangu, nilipo pata pesa kidogo nikatafuta chumba  kule mtwara nikapanga kisha nikaweka vitu ndani alafu nikapata binti wa kazi ili amuangalie mtoto, niliona nisirudi nyumbani tu maana kule mtwara nilikuwa sijulikani hivyo aibu ya kutafuta riziki kwa njia yoyote ile sikuwa nayo kabisaa, siku moja paul akamuuliza mke kwamba, "mke wangu tumekaa mda wote huo pamoja lakini haupati mimba, wakati na mimi naitaji mtoto, maana kama pesa hipo mali zipo naitaji mtoto" elivia akasema mi nahisi twende kupima hospital tujue tatizo nini maana ata mimi najitahidi sana nipate ila sipati, kweli walipo fika hospitali ikaonekana kuwa Eliva hana uwezo tena wa kushika ujauzito yani kizazi chake kimekwisha" na hapo ndipo paul anatamani kuoa mwanamke mwingine ili amzalie mtoto na aachane na huyo elivia, USIKOSE YA 12.                       
SEHEMU YA 12
Nakumbuka siku moja nikiwa balabalani, natembea huku natamani sana kupata kazi nzuri niweze kuishi maisha mazuri kama ya zamani, nikakutana na Elivia akiwa na mr paul wanatoka kununua nguo na vitu vingine vya nyumbani, uzalendo ulinishida kabisaa nikaamua kuwafata, nikasema, “paul naomba uniachie mke wangu bado nampenda, nakosa furaha kabisa ya maisha” paul akasema “we yenda mjinga sana nilikutupa shimoni ila naona bado hujalizika yahani ujakoma kabisa, sasa kama unauwezo mshike ata mkono huyu mwanamke nikuonyeshe” kwa sababu na mimi sikutaka kuaibika mbele ya Elivia kweli nikamshika mkono, elivia akasema, “khaa! Usinishike niache,” paul akasema nazani umesikia mwanamke hakutaki, hivyo sitaki kukuona unaendelea kutusumbua ata kidogo, kaa mbali na sisi” dooh elivia akasema, “kwanza naomba unipe mtoto wangu, yahani mimi nazaa wewe unachukua tu bure, namtaka mwanangu” nikamwambia, “kwani huyo mtoto baba yake nani, ni mimi au huyo paul” elivia akasema “ni wewe” nikamwambia, “elivia sikia mke wangu, kama mtoto ni wetu basi njoo tumlee sisi wawili, siwezi kuona mtoto wangu analelewa na mwanaume mwenzangu wakati mimi ni mzima wa afya sijafa, na kama hutaki basi kaa na huyo paul wako akupe mimba uzae mtoto mwingine mumlee” dahh elivia akakumbuka kuwa ameambiwa hana uwezo wa kuzaa tena akaanza kulia, paul akasema hivi kwanini unamfanya mke wangu akose raha, ebu ondoka nitakuitia mwizi nakwambia, niligoma kuondoka, Elivia akasema, “yenda mimi siwezi kuishi na wewe maisha ya tabu nampenda mtoto wangu lakini kama hutaki kunipa basi baki nae tu” nikamwambia “elivia tuondoke mke wangu mtoto bado mdogo anaitaji malezi yako” ila Elivia alikataa kabisa, kumbe wakati naongea vile na Elivia, Paul alichukia sana akawasha gari na kumpakia mke wake kisha akanigonga na gari lake nikadondoka chini, kisha akaondoka, dahh nilidondoka chini nikiwa na hari mbaya sana, maana lile gari liligonga miguu nikaumia sana, dooh wakati nipo nalia sina msaada kuna gari moja likapita maeneo yale likasimama mwanadada mmoja hivi anaitwa Prisca akashuka na kusema “we kaka mbona umelala hapo chini tatizo nini” nikamwambia, “mr paul amenigonga na gari lake kisha akakimbia dada yangu yani miguu yangu inauma sana nahisi kama imevunjika,” yule dada alinibeba na kuniingiza kwenye gari kisha akanipeleka mpaka hospital, wakati nipo natibiwa nikamwambia yule dada kuwa nina mtoto wangu na binti wangu wa kazi hawana msaada wowote wa chakula Zaidi yangu ningeomba ukawaangalie, yule dada alikuwa na roho nzuri sana, maana aliamua kumfata mtoto wangu pamoja na yule binti wa kazi kisha akakaa nao yeye pale kwake. Sasa wakati mimi naendelea kutibiwa yule Prisca aliendelea kunisimamia katika swala zima la malipo na chakula pale hospitalini.
Mungu alisaidia sana nikapona mpaka daktari akaniruhusu nitokea hospital niwe huru ila nieendelee kutumia dawa ili nipone vizuri Zaidi.
Sasa kipindi Prisca amenifata pale hospitali akasema, “yenda mi naona bora tu ukakae pale kwangu maana naishi peke yangu alafu nyumba kubwa, alafu pale ulipo panga wewe sio pazuri kabisa, alafu kitu kingine una mtoto mdogo na mama yake amemkataa hivyo ni bora tuishi pamoja mpaka pale utakapo pata pesa na kujenga nyumba yako nzuri sehemu nyingine”, dahh sikuamini yale maneno nikakubali kabisa bila kipingamizi.
Sikuamini macho yangu nilipo fika kwa Prisca maana yule dada alikuwa na nyumba nzuri magari matatu mazuri na alikuwa mfanya biashara mzuri tu. Prisca Aliniambia “ehh sasa chagua utakaa hapa au utakaa kule ulipo panga”, nikasema “mimi nitakaa hapa dada yangu, mungu akuzidishie sana maana nahisi hii ni kama ndoto kukaa sehemu nzuri kama hii tena” akaniuliza” kwanini umesema tena kwani ulisha wai kuwa nyumba nzuri kama hii” nikamwambia kweli kuwa, “Prisca dada yangu mimi nilikuwa na nyumba nzuri sana gari zuri na pesa nyingi tu, lakini huyo mke wangu alinifirisi na kumpatia utajiri wangu mr paul, kisha akakimbia na kuniachia huyu mtoto hivyo tangu siku hiyo nikawa masikini wa kutupwa” Prisca akasema” usijali kama kweli ulikuwa hivyo basi tutafanya biashara, na ukiwa muaminifu utafanikiwa tena kama zamani”
Kweli baada ya mwezi mmoja tulianza kufanya kazi pamoja na Prisca, biashara ziliendelea kupendeza, mpaka prisca akasema” wewe ni mwanaume wa shoka, maana tangu nianze kufanya kazi na wewe mabadiriko mengi nayaona kwenye biashara zangu.
Baada ya mwaka mzima kuisha Prisca akaamua kuninunulia nyumba pamoja na gari moja kama zawadi ya kumfanyia biashara zake vizuri. Maisha yangu yalipendeza sana nikabadilika na kupata muonekano mzuri wa kuvutia, mwanangu akapendeza Zaidi pamoja na yule binti wangu wa kazi, siku moja nimeamka usiku nikakuta binti wa kazi Analia, nilipo muuliza unalilia nini akasema, “yenda mimi nashindwa kuvumilia kabisa tunakaa humu ndani lakini sema kweli moyo wangu unakupenda naomba unioe” duhh nilimgombeza sana yule binti nikamwambia, “yahani ukirudia kuniambia ujinga kama huo nakufukuza kwangu” niliongea vile maana nilihisi na yeye ni kama elivia alie kuwa ananifanyia kazi zangu za ndani nikamuoa alafu akanifanyia ubaya.
Sasa kumbe paul alikuwa anagombana kila siku na elivia maana miaka ilikuwa inasonga tu hawapati mtoto, paul akasema, “nimekuchoka, nimekuchoka, nimekuchokaaaa! Yahani mwanamke umekuwa kama sijui nini humu ndani, mimi nataka mtoto na kama huwezi mi naenda kutafuta mke mwingine anizalie mtoto.”
Elivia alianza kulia akisema, “paul kumbuka umesababisha niibe pesa za mme wangu ili tuishi wote vizuri, sasa unapo sema unataka kuoa mke mwingine sikuelewi kabisa, kwahiyo mimi niibe pesa alafu mwanamke mwingine aje kuzitumia, mbona umenizalau wewe baba”
Paul akasema, “wewe mi sikuelewi unacho sema, kama utaendelea kukaa bila kuzaa huu mwezi ukiisha namleta mwanamke humu ndani”
Elivia akasema, “bora ningebaki na mme wangu yenda kuliko wewe usie juwa thamani ya mtu anae kupenda.”
Paul alichukia sana akasema, “mpuuzi nini yani unasema bora yenda kwahiyo mimi ni bwege humu ndani” elivia alipigwa kofi zito sana. Elivia akanza kulia akisema “haaaaaa! Yahani unanipiga hivi, mbona Yenda ajawai kunipiga kofi namna hiyo, kwanini unanitesa we mwanaume”
Wakati wapo wanabishana pale mlango ukagongwa, “kho kho kho” elivia akaenda kufungua, sasa alipo fungua mlango akakuta mdada mrembo sana zaidi yake akiwa na tumbo kubwa yahani mjamzito, elivia akamwambia, “karibu ndani dada” yule binti alipo ingia ndani paul akashtuka, elivia akauliza kuna nini, yule dada akasema paul, nimefukuzwa nyumbani, baba amesema twende wote akujue maana tangia umenipa ujauzito wako haujawai kabisa kuja nyumbani. Elivia akasema “whaaaat yahani paul kumbe umeisha mpa mwanamke mwingine mimba, kwanini umenifanyia hivi, nilikukosea nini”
Paul akasema, “elivia nisamee mimi nilishindwa kukwambia mapema lakini ni kweli hiyo mimba yangu”
Yule dada mjamzito akasema, “elivia mke mwenzangu wala usikasilike mimi ni mstaharabu sana tutaishi vizuri tu humu ndani wala hamna shida kabisa”
Elivia alianza kulia akisema, “paul mme wangu, umeniharibia maisha jamani” alisema maneno yale akiwa Analia kama katoto kadogo.
USIKOSE SEHEMU YA 13
SEHEMU YA 13.
MTUNZI FRANK DAVID, DAKTARI WA HADITHI_tz. Whatsapp 0769510060.                                 
Elivia alichukia sana kitendo cha paul kumpa mimba mwanamke mwingine, aka kaa kama dakika mbili anawaza, yule dada mjamzito akasema, "mke mwenzangu mbona unawaza, tatizo nini" Elivia akampiga kofi yule dada masikini, paul akasema, "we, we, weweee, weweee, usirudie tena ata kidogo kumpiga mke wangu" Elivia akasema, "paul chagua moja, niondoke mimi au aondoke huyu dada" paul akasema, "mi nawapenda wote, kwahiyo wewe utabaki na mwenzako atabaki pia" elivia akasema, "we mwanamke naomba toka kwangu, toka kwanguuuu aki ya mumgu" paul akasema "hatoki mtu hapa, kama unataka toka wewe" dahh elivia alichoka sana siku hiyo, ndipo akachukua nguo zake kisha akabeba begi na kuondoka. Yule dada mjamzito akasema, "usiondoke elivia we baki tu tutaishi vizuri ndani wala usiondoke" elivia akamjibu, "mjinga nini baki mwenyewe" alafu akamwambia paul, "asante kwa usaliti wako mungu akulipe mema" paul akasema "sawa bhana kama umeamua kuondoka we nenda tu" elivia alijisahau akatoka ndani bila ata shillingi mia masikini wa mungu, sasa wakati yupo mtaani mida ya mchana alishikwa na njaa ya ajabu sana, na hakuwa ata na shilingi mfukoni, ndipo akaenda kwenye mgahawa japo apewe ata ukoko ili apunguze njaa yake, alipo fika akasema, "jamani mimi ni mke wa paul, nilikuwa na tatizo kidogo" yule mama mwenye mgahawa akasema, "ohh yule paul tajiri ni mme wako" Elivia akajibu "ndiyo", sasa mama mwenye mgahawa akasema, "e'hh niambie sasa tatizo lako, maana nilihisi nyie matajiri amuwezi kuwa na matatizo kama sisi wachumia juani" elivia akasema, "mama nilikuwa natoka benki, ila bahati mbaya nimevamiwa hivyo sina ata hela ya kula, sasa naomba unisaidie ata ukoko nile mama yangu" yule mama mwenye mgahawa akamuuliza, "mhh ata nyie mnaomba ukoko" Elivia akasema, "jamani kwani sisi sio watu" sasa elivia aliogopa kusema kuwa ameachana na paul maana alijua ataambiwa alipe hivyo akajifanya ni mke wa paul ili wampe chakula kwa wepesi, yule mama akamwambia, "sasa dada ukoko unao utaka upo, lakini mda mwingine huo ukoko uwa tunauzia watu, wanalipa hela kisha wanakula, hivyo kama unataka ukoko na umesema huna hela sahivi basi, nitakupa ukoko lakini ukimaliza kula naomba unioshee hivyo vyombo  vyote vichafu, yahani hizo ndoo hayo masufuria, sahani kila kitu kin'gae, kwasababu leo sina msaidizi wangu yupo nyumbani anaumwa" dahh elivia akasema, "we mama vyombo vyote hivyo nioshe mwenyewe bora ubaki na ukoko wako tu" elivia aliondoka akiwa na njaa sana maana alikuwa mvivu kufanya kazi maana alikuwa amezoea maisha ya raha, na starehe sana. Ilipo fika usiku Elivia hajaweka chochote mdomoni alizidiwa tumbo lilimuuma sana mpaka akaanguka chini, maana alikuwa na vidonda vya tumbo, hivyo alikuwa amezoea kula na kunywa maziwa kwahiyo ikawa ngumu kupata hizo lishe za maana alikuwa hana hela na ameisha ondoka kwa mme wake. Sasa wakati anajigalagaza chini tumbo linamuuma mpaka analia, kuna kijana alikuwa anapita maeneo yale, alipo muona Elivia analia akamfata kisha akamuuliza, "dada mbona unalia tatizo nini", dahh elivia alishindwa kudanganya akaamua kusema ukweli kuwa ana njaa alafu mme wake amemfukuza na hana ata shilingi mia mfukoni, alafu kibaya zaidi ana vidonda vya tumbo, yule kaka akasema "basi sawa, sahivi ni usiku, twende kwangu ukale unywe na maziwa ili upumzike maana vibaka wanaweza kuja wakaiba hiyo simu yako na wakabeba begi lako pia  wakaondoka nalo" sasa elivia alipo furahi kupata ule msaada akafurahi sana kwamba angalau mungu amemsaidia amepata sehemu ya kujihifadhi, walipo fika kwa yule kaka, kweli kijana alijitahidi akamnunulia elivia maziwa na dawa pamoja na chakula pia, Elivia alipo maliza kula akaingia kitandani ili aweze kupumzika, sasa baada ya dakika kama tatu elivia alishangaa kuona wanaingia vijana wengi kama tisa mule ndani, kumbe lile lilikuwa gheto la wauni, yahani wale  wanatafuta pesa mchana kisha wakipata hela usiku wanakuja kupumzika mule gheto, na kama akiingia msichana basi wale vijana wote tisa wanamtumia yule msichana kwa lazima kimapenzi. Dooh elivia alipo waona akaogopa kwanza, kisha akaamka na kumuuliza yule kaka kwamba, "kwani hichi chumba chako mnalala wangapi humu ndani, au hawa wengine wamekuja kukusalimia tu" yule kaka akacheka, "haahahaha, dada kwanini umeuliza hivyo, usiwaogope maana hawa wote tisa ni waume zako, na wapo kwa ajili yako usiku wa leo, dada Elivia usiku huu wa leo watakupa furaha ambayo huku wai kuipata katika maisha yako, yahani hawa wote watafanya mapenzi na wewe" elivia alishtuka akasema "haaa, we kaka mi sitaki, kama ni hivyo bora niondoke" kipindi anataka kutoka, jamaa mmoja akamshika shingo na kumtupa kitandani kisha akasema, "hichi chumba ni kama sumaku, ukiingia humu ndani unanasa na unakuwa mpole,  lazima utupe sisi wote penzi lako, sisi sio wezi hatuibi mali zako, ila kuwa mpole ili wote tuburudike, hivyo andaa nyama sisi tule" dooh elivia akasema, "jamani mimi ni mama nina mtoto nimezaa na Yenda, alafu mimi ni mke wa tajiri anaitwa paul, msinibake nitawapa pesa" wakasema, "hatutaki pesa zako, na ndiyo maana hatuja kunyan'ganya simu na begi lako tunacho taka toka kwako ni kukuvua nguo ya ndani" Elivia alianza kupiga kelele alipigwa kofi moja usoni, dahhh kweli aliumia maana alikaa kimyaaaaa! Wakamwambia, "ukiendelea kutuletea nyodo nyodo, tuna kuua leoleo" walitoka vijana nane nje akabaki mmoja kumshughurikia Elivia ipasavyo, alipo maliza akatoka nje kisha akaingia mwingine, na kila anae ingia anacheza mechi mala mbili, dahh  walipo fika wa tano Elivia alizidiwa nguvu masikini dada wawatu, akasema naomba tu mni ue maana maumivu nayo yapata hapa ni bora nife tu, sasa kipindi ana lialia wale vijana wakaogopa watu wanaweza kuja ikawa kesi, hivyo wakachukua nguo yake ya ndani kisha wakamjaza mdomoni ili asitoe sauti nje, akaingia jamaa wa sita kumbaka, damu zikaanza kumtoka elivia sehemu zake nyeti, wale wakaka walikuwa hawana huruma kabisa, wakasema, "huyu amekula chakula, maziwa, na maji, alafu tumsamehe hapana, tutakuwa hatujawatendea haki wasichana wengine tulio wafanya hivi, kweli masikini walimzunguka wote tisa mpaka mtoto wawatu akapoteza fahamu, kulipo kucha elivia alikuwa hawezi kutembea vizuri, maana kaka mmoja hivi mkorofi sana badala ya kuchezq mpira sehemu husika yeye alimlawiti  elivia, sasa Elivia alipo amka sehemu zake nyeti zilikuwa zina muuma sana, ikabidi alale tu mulemule ndani, kweli wale wavulana walimuogesha kisha wakampa chakula ila wakamwambia, dada kama utalala hapa tena leo usiku dozi yetu ni ileile tutafanya tena kama tulivyo fanya usiku wa jana, dahh elivia alivyo ambiwa vile akaona ni bora aende kwa paul mme wake aishi nae hivyo hivyo ila maisha kama yale asinge yaweza kabisa.
Elivia alitoka mule ndani anachechemea, anaumia sana masikini huku akiwa na begi lake, hana msaada kabisa na ndiyo maana alikuwa anarudi kwa paul, kwasababu alifikilia ataenda wapi hakuwa na jinsi, sasa wakati yupo njiani akiwa na maumivu, mda huo mimi nilikuwa kwenye gari langu nimevaa miwani nimependeza sana yahani nimebadilika, nikamuona mtu kwa mbele anachechemea, sikujua kama ni elivia maana sikuwaza kama angeweza kutembea kwa miguu, hivyo nikatamani kusimamisha gari ili nimpe lifti huyo dada asiendelee kuangaika kuchechemea, sasa elivia alipo ona gari limesimama akafurahi pia akijua amepata msaada wa lifti, alipo kuja karibu yangu nikashusha dirisha la gari, elivia alikuwa hajanitambua maana mimi nilikuwa nimevaa kofia na miwani ya bei, hivyo kwa haraka asinge weza kunijua, maana kwanza hakutegemea kama ningekuwa na gari zuri kama lile, sasa yeye nilipo mfungulia dirisha akaanza kusema, "samahani kaka mi ni mke wa tajiri paul, nimepatwa na matatizo naomba unipe lifti ya gari mpaka nyumbani" wakati anasema vile nikamuuliza "hooo, kumbe wewe mke wa paul, Na vipi mme wako Yenda mlie mfirisi mamilioni ya pesa," kisha nikavua miwani pamoja na kofia, elivia alipo niona hakuamini akaanza tu kulia, nikawasha gari kisha nikaondoka zangu, dooh elivia aliendelea kutembea kwa tabu mpaka akafika kwa mme wake, paul akamwambia, nilijua utarudi tu hapa maana hauna sehemu yoyote ya kwenda, sasa ona umeenda uko umepigwa sijui na nani miguu mpaka umechechemea masikini," elivia aliona aibu kusema ukweli kuwa alibakwa maana alihisi paul atachukia na kumfukuza pale kwake. Sasa maisha walio kuwa wanaishi ndani yalibadilika, hivyo paul akagawa vyumba viwili chumba kimoja cha mke mkubwa alafu kingine cha mke mdogo, hivyo paul leo analala na mke mkubwa alafu kesho pia analala na mke mdogo, alafu kumbe Elivia alivyo kuwa amebakwa na wale vijana tisa masikini wa mungu, akawa amepata maambukizi ya virusi vya ukimwi. USIKOSE SEHEMU YA 14 mtunzi frank david whtsapp 0769510060.                       
 SEHEMU YA 14.
MTUNZI FRANKDAVID;DAKTARI WA HADITHI_tz. Whtsapp 0769510060.                                 Kipindi elivia ame athirika alikuwa bado hajagundua kama ana ukimwi, sasa elivia alikuwa anaumia sana maana mapenzi yote mule ndani yaliamia kwa mwanamke mwenye ujauzito yahani Farida, sasa siku moja paul alilala chumba cha Elivia, kipindi wana cheza mechi akagundua kuna mabadiliko ndani ya elivia, maana ukubwa wa goli uliongezeka zaidi, maana alipo bakwa na wale vijana ni kama wali muharibia goli lake hivyo paul kwa jinsi alivyo kuwa amelizoea goli akakuta ndivyo sivyo, yahani goli limekuwa pana zaidi, mpaka kumfanya paul asifurahie mechi alipo taka kucheza na elivia. Sasa alipo muuliza elivia kuwa "mke wangu mbona unamabadiliko sana ndani yako na muonekano wa goli lako umebadilika kabisa sivyo ulivyo kuwa zamani umekuwaje?" elivia akasema "huo utu uzima paul" hakutaka kumwambia paul ukweli. Paul hakuwa na jinsi akakubali matokeo. Baada ya mda, yule mke wa paul yahani farida akawa amejifungua katoto kazuri sana ka kiume, alafu mungu saidia ukimwi ulikuwa hauja tapakaa mule ndani mpaka mtoto anazaliwa salama. Sasa wakati amejifungua ndugu na jamaa walikuwa wanakuja kumuona farida pamoja na mtoto kake, kisha wanatoa chochote walicho nacho kama hongera. Ila elivia alijifungia ndani analia, hataki kabisa kumuona mtoto wa farida, elivia akasema kwamba "yahani mimi nimekaa humu ndani siku zote hizo, sijawai kutembelewa na wageni alafu leo huyu dada anatembelewa na wageni wote hao, lazima nimkomeshe tu, hawezi kukaa kwenye mali zangu, iweje mimi niibe pesa za baba mtoto wangu alafu yeye akae bure bure tu, dahh hizi zalau kweli kweli nitamkomesha" ndipo Elivia akapata wazo la kufanya kila awezalo ili akanyonge kale kachanga ka mke mwezie kipindi watu hawapo ndani, Sasa siku moja elivia yupo barabarani na mimi siku hiyo nipo na gari langu pamoja na mtoto wangu tunaelekea sokoni kununua vitu vya nyumbani, sasa mimi nilishangaa tena kumuona ana tembea bila gari nikajiuliza, "hivi wamefirisika au" kumbe masikini wa mungu upendo ulikuwa umepungua kwa elivia paul hampendi kama zamani, nilimuonea huruma elivia, nikapata wazo la kumuonyesha mtoto wake anavyo endelea kupendeza na kunawili, nilisimamisha gari kisha nikampigia honi, ndipo akaja na kusema, "mme wangu vipi hari"nikamwambia nimekuita umuone mtoto wako yupo kwa nyuma, fungua mlango umsalimie, Elivia alipo ingia hakuamini kama mtoto wake ndiyo yule, mtoto amependeza, anavutia rangi nzurii, elivia akaanza kulia, nikamuuliza "unalilia nini" akasema, "yenda mme wangu bado nakupenda, naomba nije tuishi wote tumleee mtoto wetu" dahh nilichukia nikatoka nje ya gari nikaenda kwenye mlango wa siti za nyuma kisha nikafungua mlango na kumtoa nje elivia alafu nikawasha gari ili nimgonge kama walivyo nifanyia kipindi kile, ila nikamuonea huruma, Elivia akasema, "simama, simama" nilisimama nikamuuliza "nikusaidie nini zaidi", mimi nilikuita umuone mtoto tu, ujue kuwa yupo, maana ulisha nikana mbele ya paul kuwa uwezi kuishi na mimi mtu mwenye shida, alafu kwa mlivyo na roho mbaya mkanigonga na gari miguuni, sasa leo unataka nini tena toka ondoka," elivia akasema, akiwa analia "Yenda najua hunipendi, na najua nilikufanyia mengi mabaya, lakini katika maisha yangu yote wewe ndiye ulikuwa mwanaume wa pekee kwangu, lakini nimeichezea bahati, nakuonea wivu sana yenda, maana sina tena kizazi, mtoto nilie nae ni huyo tu ulie ni zalisha, na kibaya zaidi umenikataa hivyo mimi nitaishi maisha ya tabu sana yenda" nilimwambia kwamba, "nyie watu wabaya sana maana mlinitupa shimoni mkajua nimekufa, ila mungu amenilinda mpaka sasa nina maisha mazurin, na huyu mtoto ulimkimbia ukamuacha na njaa wewe ukaja mtwara, je angekufa?, sio hivyo tu bali ata mama yangu mzazi alikufa kwa sababu ya kukosa matibabu kipindi hicho mmenitupa shimoni naangaika na wadudu, mbu na mvua alafu kipindi hicho nyie mnakula pesa zangu tu, umenifirisi pesaaaa", nilipo ongea kuhusu kufirisiwa nikaanza kulia ndipo nikapanda gari na kuondoka.
Sasa kipindi elivia yupo kwa paul wivu ulimshika sana hivyo akaanza kupanga ile mikakati yake ya kumuua mtoto wa mke mwenzake, uwezi kuamini aliingia chumba cha mke mwezake kipindi hayupo maana alikuwa ameenda kununua pampers ya mtoto, Sasa Elivia alivyo kuwa na wivu, akaka nyanyua kale kachanga kisha akakafunika mdomo alafu akakaniga shingoni kwa nguvu sana masikini, yani mtoto sauti haikutoka ila miguu ndiyo ilikuwa inacheza cheza mpaka kakafariki, kisha akakalaza polepole kitandani, akakafunika na shuka vizurii ili mtu asijue na farida akija ajue kuwa mtoto amelala, baada ya kufanya vile akatoka nje ya chumba, sasa wakati anatoka akakutana uso kwa uso na farida pamoja na paul, wakamuuliza umefata nini chumba cha mke mwenzio kama sio uchawi huo umekupeleka, elivia akaanza kuongea kwa uoga "ha!ha! ha! hapana paul nilikuwa, nilikuwa" paul akasema "sema sasa ulikuwa unafanya nini?" Farida tumbo likaanza kumuuma ghafla tu, akashtuka akasema "mbona najihisi vibaya tumboni au amemfanya kitu kibaya mtoto wangu" walipo enda kumuangalia mtoto wakakuta damu zina mtoka mdomoni, puani, pamoja na masikioni, wakamuangalia vizuri mtoto kumbe ameisha fariki! Farida alianza kulia akisema "mwanangu mimi mwanangu, nimekuzaa kwa uchungu mwanangu, rudiiiii mtoto wangu usife" paul alisikitika sana maana alikuwa anampenda sana yule mtoto na alikuwa anampenda farida mke wake, ndipo paul akasema "elivia kwanini ume muua mwanangu" elivia akasema hapana sio mimi, nilimbeba tu bahati mbaya akafa, paul akasema, "kwanini umeingia hicho chumba cha mke mwenzio" elivia akasema,"nisamee paul mme wangu sitarudia tena ni shetani tu"  duuh paul alienda kufata kisu amuue eliva, ndipo palepale elivia akawa mjanja akakimbia haraka na kuondoka bila mabegi yake akasahau ata kutoka na hela wala chochote akaingia mtaani tena kuangaika
Sasa  kipindi paul anarudi kumuua elivia akakuta kaisha kimbia, hawakua na jinsi wakaamua kumzika yule mtoto, na wakaficha ile siri kuwa mke mkubwa ndiyo kaua, farida ali umia sana, akasema sasa haya maziwa nitamnyonyesha nani mtoto wangu amekufa jamani, ila paul akampa moyo mpaka akasahau, sasa kipindi elivia yupi mtaani alianza kuwa kama chizi, siku zingine unamkuta yupo barabarani anafagia, siku zingine anaosha vyombo vya mgahawani, sasa siku moja aliugua sana elivia kumbe vile virusi vya ukimwi vilikuwa vimeanza kufanya kazi, hivyo akawa mnyonge sana nguvu akawa hana, kazi hafanyi, akawa ali chakula na ni mwasilika masikini, dooh yahani kuna siku alizidiwa sana elivia akalala barabarani kama chizi, watu wanapita wanabaki tu kusema kwamba, "yahani mme wake yule huyo dada mr paul ni mjinga sana, kaoa mke mwingine alafu kamtelekeza huyo ebu muone huyo dada alivyo kuwa kama chizi" ila mungu saidia siku hiyo Prisca alie nisaidia mimi, alikuwa anapita yale maeneo akamuona elivia, sasa alicho fanya akamchukua elivia, akampeleka hospital mpaka akapona alafu akakaa nae, elivia akaanza kupendeza ndipo akamleta kwangu siku moja akimuombea msaa ili nikae nae ili tusaidiane kumlea mtoto
Prisca alivyo fika akasema, "yenda najua huyu mwanamke alikufirisi pesa zako zote akakufanyia ubaya mwingi sana, lakini nimemleta hapa naomba umsamee, mrudiane mumlee mtoto, maana kwa sehemu niliyo mkuta awezi kurudia kosa" nikamwambia prisca kwamba, "najua ulinisaidia sana prisca lakini huyu dada siwezi kumsamee kabisaa, maana alinitamukia kwa kinywa chake kuwa mimi simpi penzi kama paul analo mpa, hivyo nikirudiana nae bado atafata hilo penzi kwa paul" prisca akasema "elivia acha kulia sasa" kisha akaniambia"kwa heshima yangu naomba msameane kisha mumelee mtoto kwa pamoja" dahhh nilianza kulia ila sikuwa na jinsi nikamkumbatia elivia na kumsamee ili awe mke wangu tena, prisca alifurahi sana akasema najisikia raha sana mkiwa pamoja hivi, sasa nilishangaa sana ilipo fika usiku nikiwa ndani na elivia eti alikuwa anataka tucheze mechi siku hiyo hiyo ili aamini kama kweli nimemsamee, nilikataa na kumwambia kwanza asubili tupime afya ndiyo mambo mengine yafate, siku hiyo sikupata usingizi kabisa maana niliumia sana kumsamee na kukaa na elivia, na nilimsamee kwa heshima niliyo kuwa nayo kwa prisca, kesho yake nikamwambia elivia twende hospitalini tukapime afya zetu ili mambo mengine yaendelee akasema sawa ndipo tukapanda gari na kwenda hospitalini.. USIKOSE SEHEMU YA 15                       
SEHEMU YA 15.
MTUNZI FRANK DAVID. Daktari wa hadithi_Tz. Whtsapp 0769510060.                               
Tulipo fika hospitalini tukapima virusi vya ukimwi na magonjwa mengine, sasa tukaambiwa tutoke nje ili tusubilie vipimo kwanza ndiyo tupewe majibu yetu kisha tuondoke. Sasa nilikuwa nashangaa sana maana Elivia alikuwa anatetemeka sana akiogopa majibu yake maana alikuwa hajiamini ata kidogo, nikamuuliza, "Elivia kwanini unatetemeka hivyo, angalia jasho linavyo kutoka hauna raha kabisa" akasema "hapana mme wangu nipo sawa tu" mimi nikahisi labda anahisi baridi kumbe mtoto wawatu alikuwa anaogopa majibu ya ukimwi, na kilicho kuwa kina muogopesha zaidi ni wale vijana tisa walio mbaka kipindi cha nyuma, sasa wakati tumekaa pale tukisubilia majibu, elivia akaanza kulia, "nikamuuliza, unalilia nini" akasema, "yenda mme wangu, naumia sana kwa mambo mabaya ya kishetani niliyo kufanyia, ingawa tuko pamoja sahivi lakini nafsi yangu bado inanisuta kabisa" nikamwambia, "ni kweli we mwanamke mbaya sana, umenifanyia mambo ya ajabu mno, na una bahati sana maana bila prisca nisinge kusamee kabisa, yahani ningekufukuza kama mbwa, ila kwasababu mtu alie nisaidia mpaka nikapata maisha mazuri ndiye alie kuleta, nikashindwa kukufanyia ubaya kwa sababu namuheshimu sana yule dada katika maisha yangu, chochote asemacho lazima nikifanye" Elivia akasema, "Yenda siwezi kurudia mme wangu, alafu yule paul ni mtu mbaya sana, alinidanganya mambo mengi sana, maana alisema ata tukifunga ndoa mimi na wewe yeye ata haribu ndoa yetu kwa vipingamizi maana mkataba wa ndoa yangu mi na yeye anao kwa sababu kabla yako mimi nilifunga nae ndoa tayari, hivyo nikakosa msimamo wa maisha, na ujinga ujinga tu watamaa za ngono, lakini sahivi nakuahidi siwezi kurudia" kipindi tunaongea yale maneno, tukaitwa kwa ajili ya kuchukua majibu ya afya zetu, daktari alisema tumepima hapa ila tumekuta wote mna magonjwa, alafu sana sana wewe Yenda, maana una malaria, taifodi pamoja na U.T.I hivyo utachukua dawa baada ya hapa, pesa utaacha mapokezi, lakini pia tumempima mke wako Elivia tukakuta ana maambukizi ya virusi vya ukimwi yahani ni mwathirika, dooooohh elivia alianguka chini palepale, lakini hakupoteza fahamu, ndipo daktari akasema, sasa Yenda itabidi uwe makini ili usipate maambukizi pia unaweza kutumia kinga, au mafuta ya kulainishia njia au usifanye kabisa ili usiweze kupata maambukizi ya ukimwi kutoka kwa mke wako, alafu we Elivia  unatakiwa kufanya mazoezi kwa sana, kula chakula chenye dayati, usiache kuwa na furaha ili uweze kuishi maisha mengi zaidi duniani",  Elivia alilia sana masikini, ndipo mimi nikasema sawa dokta, nikamnyanyua elivia kisha nikampeleka mpaka kwenye gari, alafu nikachukua dawa nilizo andikiwa na dokta, sasa wakati tupo njiani nilimgombeza sana elivia, nikasema "wewe mwanamke mpuuzi mpuuzi mpuuuzi kabisaaa, kumbe umepanga na paul uje uniangamize sio, sasa kwangu umegonga mwamba, kama ulihisi utaniaribia maisha kama zamani sasa hivi umeshindwa mjinga sana wewe mwanamke" elivia akasema, "yenda mme wangu, nilibakwa na watu kama tisa nazani hapo ndipo nilipo upata huu ugonjwa nisamee yenda, naomba nikae kwako baba angu niwe ata mfanya kazii wa ndani, sina sehemu yoyote ya kuishi, maana ata nyumba uliyo wajengea wazazi wangu nili iuza kwa tamaa ya pesa nihurumie maana maisha ya mtaani ni magumu sana mme wangu" nilimwambia sawa, siwezi kukushusha kwenye gari hapa njiani, ngoja nikupe msaada, lakini msaada wangu kwako ni mmoja tu, na msaada wenyewe ni kwamba nakupeleka mpaka kwenye nyumba ya paul, uendelee kuishi nae muambukizane vizuri" maana sahivi nimeisha ogopa ata kukushika sababu nahisi unaweza kuniambukiza na mimi hivyo virusi" kweli nilimuendesha mpaka nyumbani kwa paul, nilipo mfikisha nikasema, "hapa ndiyo kwako, sasa kule kwangu nisikuone tena, na hivi vipimo vyako nampelekea prisca ili aone ujanja wako wa kuni angamiza umeshindikana" dah nilimshusha elivia kwenye gari akawa ana n'gan'gania hataki kutoka, ndipo nikamsukuma akaanguka chini analia tu, nikasema, "wewe lia tu, kama mlinitupa shimoni, sioni ajabu kukutupa hapa nyumbani kwako, alafu tena mwambie paul wako, na yeye mungu atamlipa hapahapa duniani maana hizi pesa sio halali yake yeye ni haki yangu mimi, niliyo ifanyia kazi kwa jasho langu" dahh niliondoka na kumuacha elivia pale getini kwa paul akiwa analia, ndipo nikaenda mpaka kwa prisca kumwambia yaliyo nikuta, prisca alinisifia sana akasema, "angekuwa kijana mwingine angefanya tendo haraka bila kupima alafu na yeye anapata maambukizi, ila achana nae maana nahisi huyo mwanamke ameumbwa kuwa mkosi kwako, sio mwanamke wa nyota yako, hivyo achana nae".  Kumbe elivia alivyo baki pale nje, alikuwa anaogopa sana kuingia ndani maana alijua kuwa kwakuwa ali kaua kale katoto kachanga hivyo paul akimuona ndani anaweza kumu ua na yeye" ila wakati yupo pale nje akamuona farida yupo kwa ndani anaendelea kupendeza tu, hasila zilimshika elivia, ndipo akasukuma geti maana lilikuwa wazi, alafu akaingia ndani. Sasa alipo muona mke mdogo akamfata kisha akasema, "yahani we malaya mkubwa sana ndiyo umesababisha napata hizi shida za dunia, naomba utoke kwangu," yule farida kumbe alikuwa muongeaji pia, akasema kwa uchungu sana, " elivia umemuua mtoto wangu kwa kumnyonga yahani hilo kila mtu anajua, ila nimekusamee, ila naona umezidi sasa, kama ninge kuwa malaya mme wako asinge nioa, wewe uwezi kuzaa ndiyo maana hakutaki, na akija akakukuta hapa atakuua maana uli muulia mtoto wake" elivia akasema leo lazima nikuonyeshe mafunzo ya kuchukua wame za watu, elivia alikuwa na nguvu, alimsukuma farida kwa nguvu sana ukutani yule dada aligonga kichwa chake vibaya mno, mpaka akapasuka kwenye uso, kipindi farida anajipanga na yeye kupigana akamfata elivia, dooh elivia alikuwa mtata akamsukuma farida chini, na mda huo huo paul alikuwa anawasili, na ndiye akawaachanisha ili wasiendelee kupigana, farida alikuwa amejaa damu, paul akachukia kile kitendo akasema, "elivi kwanini una mtoa damu mwenzako" elivia akasema, "nipo tayari kufa mda wowote ule kwa sababu ya haya mapenzi ya dunia" paul akasema, "una roho mbaya sana we elivia yani uogopi kumuumiza mwenzako unamtoa harama kiasi hicho" elivia akasema, "hiyo tabia mbaya ulinifundisha wewe, mbona hukuona ni vibaya kumuweke mwenzako Yenda Shuntama,  ikamfana awe na ngozi kama ya chura" Farida akasema, "mme wangu na wewe kumbe unaendaga kwa wachawi", elivia akasema, "ndiyo ulikuwa ujui, upo tu unakula mali hujui ata zimepatikana vipi" paul akasema, "elivia we ni mpuuzi mkubwa, pesa zangu nimeziangaikia mwenyewe, wacha kumdanganya mke wangu kipenzi ondoka muuaji mkubwa wewe, unaleta visingizio vya uongo uongo tu," elivia akasema,  "siondoki" USIKOSE YA 16.                       
SEHEMU YA 16.
MTUNZI, FRANK DAVID, DAKTARI WA HADITHI_tz. whtsapp 0769510060.                               
Elivia alikataa kata kata kutoka kwa paul, paul akaanza kumvuta akimsukuma ili atoke pale kwake, lakini elivia alionyesha na kuhusimamia msimamo wake hakutoka akakataa kabisa, paul hakuwa na jinsi akaamua tu kukubaliana na msimamo wa Elivia. Farida akaanza kulia akisema, "mme wangu nilikuwa nakuamini sana, kumbe na wewe unaamini mambo ya kishirikina" paul akasema, "hapana usilie mke wangu, huu ni uongo tu mke wangu anauleta ili kutugombanisha, mimi namuamini sana mungu sijawai kwenda au kujiusisha na mambo ya kishirikina, na wala sijawai kuiba cha mtu wala kula cha mtu, hizi ni mali zangu pesa zangu mwenyewe, achana na elivia anataka kutugombanisha" yale maneno yalimpa moyo farida mtoto wawatu akaamini kabisaa" sasa kwakuwa elivia alijua ame athirika hivyo basi alitaka kuwaambukiza na wenzake ili waugue pia ukimwi, maana paul pamoja na farida walikuwa ni wazima bado. Kama unavyo jua mtu anapo kuwa ameoa wake wawili lazima apangilie mda na siku za kulala na wake zake ili wote wasiwe na wivu na ili wote wapate haki sawa, lakini Elivia alikuwa anasikitika sana kwasababu paul alikuwa analala sana mke mwenzake yeye ametengwa tu anajisikilizia baridi, na mda mwingine alikuwa anaamka kwenda kusikiliza mlangoni kwa farida kama paul anacheza mechi, na kweli masikini kila alipo fanya uchunguzi alikuwa anakuta wenzake wanacheza mechi tu, alafu yeye hana wa kucheza nae, uvumilivu ukamshinda ikabidi amuite paul na kumwambia kwamba, "paul mbona unampendelea mke mdogo tu mimi unanitenga hivi, kila siku unalala kwake mimi khaa! hulali kwangu, nakuitaji pia mme wangu" elivia alitaka vile ili ajitahidi kueneza ukimwi kwa farida, paul akamwambia, "wewe unajifanya mbabe sana, sasa kula ubabe wako, sinili kufukuza ukakataa, sasa utaondoka mwenyewe bila kufukuzwa" elivia machozi yakiwa yanamtoka akasema, "paul mapenzi yako ndiyo yali nishawishi mimi kumkimbia mme wangu wa ukweli yenda, sasa kwanini leo unanifanyia hivi mimi, kumbuka na mimi ni mke nahitaji uwepo wako, naomba paul usinifanyie hivi"  paul akasema, "yani siku hizi sina hisia na wewe kabisaaa, yani sina ata kidogo, sijui kwanini, alafu kitu kingine wewe hauna uwezo wa kushika mimba kwahiyo sioni faida kabisa na wewe, nimekuchokaa elivia, kama unauwezo mtafute masikini mwenzako Yenda ndiye anae weza kukuzalisha tu, naomba unipe nafasi ya kutafuta mtoto, mimi nakuonea wewe wivu maana tayari wewe na mme wako yenda mna mtoto, hivyo na mimi nipe nafasi nitafute"  dah elivia alihisi kuchizi kabisaa akasema kimoyomoyo, "kweli mimi ni mjinga, nimejiaribia maisha mwenyewe jamani" paul akaondoka na kumuacha elivia anawaza tu. Kweli elivia alichukia sana na akasahau kufata ushauri kabisa wa daktari, akawa ni mtu wa kulia kila mda, anawaza sana, hali chakula vizuri, alafu ni muathirika wa virusi vya ukimwi hivyo akaanza kupungua mpaka paul akaogopa, akamuuliza "we mwanamke mbona unakonda hivyo tatizo nini huri chakula au?" Elivia akasema, "mawazo tu, nakosa raha nilikuzoea sana mme wangu na wewe ndiyo ulikuwa una ninenepesha sasa siku hizi sipati kabisa virutubisho vyako lazima nipungue" paul akasema, "oky sawa, leo nakuja kulala kwako, lakini ukiendelea kuleta dhalau nitakuwa siji kabisa, naomba uwe mtulivu na mwenye heshima" Elivia alifurahi sana kusikia kuwa paul atalala nae, maana alijua hiyo ndiyo itakuwa njia ya kumfanya farida na yeye apate maambukizi, yani elivia aliwaza vitu vya ajabu sana siku hiyo, kweli bhana ilipo fika usiku, paul akamuaga mke wake mdogo kuwa anaenda kulala na Elivia siku hiyo, na elivia alikuwa mjanja sana maana alisafisha chumba chake vizuri ili kumvutia paul kwa uraisi zaidi, walipo lala kweli walicheza mechi, alafu elivia alijitahid kucheza kwa mda mrefu zaidi ili angalau mchubuko utokee na virusi vienee ndani kwa ndani, kwa bahati mbaya Mr paul na yeye pia akawa amepata maambukizi ya virusi vya ukimwi siku hiyo, paul akamuuliza elivia kwamba, "leo mchezo umependeza sana zaidi ya siku zingine kwanini" Elivia akasema, "hatujacheza mda mrefu ndiyo maana" dahh sasa elivia na paul tayari wote wakawa waathirika, akawa amebaki farida tu kupata ilo janga la dunia.
Siku moja usiku paul alikuwa ndani na farida, hivyo aliitaji sana kufanya ilo tendo na farida, ila siku hiyo farida alikuwa anajisikia vibaya sana akamwambia, "paul mme wangu leo najihisi vibaya sana yahani najisikiwa kuumwa kabisa siwezi kufanya unacho taka, ila naomba unisamee mme wangu maana najua ni jukumu langu kufanya hilo jambo" paul akasema "ohh hamna shida mke wangu kama unaumwa basi tulale tu alafu kesho nikupeleke ukapime ili ujue nini kina kusumbua, labda tayari umeisha pata ujauzito unilitee katoto na mimi nifurahi" farida akacheka kisha akasema "mme wangu una hamu sana na mtoto mpaka najisikia raha, lakini tatizo nikizaa mke wako ananiulia tu" paul akasema, "sahivi hawezi maana tumeisha mfundisha tabia" kweli walilala bila kufanya chochote siku hiyo.
Kesho yake paul akapigiwa simu kuwa mdogo wake amefariki hivyo alitakiwa aende kijiji kwao kwenye msiba, dahh farida alilia sana akasema, "pole mme wangu kwa msiba wa shemeji, naomba twende wote msibani" paul akamwambia, "usijali mke wangu wewe baki ngoja niende tu tuzike nitarudi" elivia akamwambia, "mme wangu safari njema, sisi utatukuta tupo salama tunakusubilia tu mme wetu" paul akasema "sawa mbaki salama, na msigombane muishi vizuri" paul aliondoka akamuacha elivia na farida ndani wawili tu, dahh elivia alikuwa mkorofi sana masikini, maana alikuwa akiamka anakaa tu sebreni, kisha anamwambia farida afanye usafi, ampikie, afue, eti kisa yeye ni mke mkubwa ndani, elivia alikuwa hapendi dhalau kabisaa, na yeye akawa hapiki afanyi usafi maana aliona kama anateswa kila siku yeye tu, dahh sasa walikaa bila kufanya kazi bila kuongea mpaka nyumba ikaanza kutoa harufu, panya wanapishana ovyo, mende ndiyo usiseme mpaka wageni walipo kuwa wakienda pale wanabaki wanashangaa tu, baada ya msiba paul akaanza safari ya kurudi kwake ili awaone wake zake, wakati yupo njiani  anakimbiza gari bahati mbaya alipata ajali mbaya sana maana alikutana na basi la abilia wakagongana uso kwa uso, yahani lile gari walilo nizulumu lili pinduka vibaya sana gari likajikunja kabisa, ata kutengenezeka lisinge weza, labda kuuzwa tu kama vyuma chakavu, mungu saidia paul alipasuka kidogo kichwani na kuvunjika vidole vya mkono wa kushoto na akawa ameumia kidogo kifuani pia, hivyo akawaishwa hospitali ili asije kufariki. Wake zake walikuwa hawana taarifa kabisa, ila sasa humo ndani wamenuniana sana midomo wameikunja asubui mpaka jioni kila siku, mala huyu ameimba taarabu ya kumuumiza mwenzake, mwingine ana sonya tu kila mda. Sasa wakati elivia na farida wapo nyumbani, alikuja mgeni mmoja hivi akawambia, "jamani mme wenu amepata ajali ya gari, yupo hospitali hajitambui mpaka sahivi, na gari yake ime alibika sana, polisi wameibeba wako nayo kituo cha polisi" dooh elivia hakuumia ata kidogo, maana alijua kabisa hizo ni laana za dhuruma, farida akaanza kujiandaa ili aende na yule mgeni mpaka hospitali amuone mme wake, sasa elivia akaona ule ndiyo uhuru wa kufanya analo taka, kweli masikini, elivia alikuwa anaingiza wanaume ndani, analala na kila anae mtaka maana alihisi hana thamani tena duniani, kipindi hicho farida analia na mme wake ili apone na arudi nyumbani, huku nyumbani kumbe elivia analala ata na vijana anabadilisha kila anapo jisikia,   baada ya mda, paul akaruhusiwa kuja nyumbani ili kuuguza vidonda vyake, alimlaumu sana elivia akasema, "yahani we mwanamke nakuchukia kama nini sijui, mimi nimepata ajali ata kuja kuniangalia hutaki" elivia akasema, "sasa nije kukuangalia na nyumba ingebaki na nani wakati farida tayari amekuja huko." Paul aliteseka sana kupona vidonda vyake na vilichelewa kupona sababu alikuwa na ukimwi, siku moja paul alimuita elivia kisha akamwambia, "mke wangu kama unavyo jua gari lime pinduka sana na lime alibika mno, hivyo chukua hii kadi ya benki kisha katoe pesa millioni 12 ili tununue gari la kawaida niwe natumia kwenda hospitali kupima na kuchukua dawa na kazi zingine" elivia akasema "sawa mme wangu" sasa elivia alipo fika benki akaangalia pesa iliyo baki ni milliono 120, sasa alicho fanya ni kwamba alikomba pesa zote kisha akaja nazo mpaka kwangu akasema, "yenda mme wangu najua nilikufanyia ubaya sana ila mimi siwezi kuishi maisha mengi sahivi, bado nakupenda yenda mme wangu, ila siwezi kuwa mke wako  tena sababu mimi ni muathirika, ila nimekuletea pesa zako tulizo ziiba ingawa zimepungua ila nimeamua kukuletea zilizo baki, najua paul ataniua sababu nimechukua pesa bila kumwambia nikakuletea wewe ila ni bora nife sababu yako nakupenda sana yenda mme wangu baba wa mtoto wangu" Elivia alipo nipa zile pesa, sikuzikataa nilikubali tu, sasa alipo rudi kwa paul, akamwambia kuwa "paul mme wangu nimeenda bank nikakuta hamna ata shillingi mia kwenye akaunti, pesa zote umeweka wapi?" Paul akasema, "wehhh, usiniletee wizi wako hapa, pesa zipo bank , mimi nimeacha millioni 120 kwenye akaunti unasema hamna pesa, nakuua wewe mwanamke, usilete upuuzi" elivia akasema basi kesho uende wewe kwanza uangalie vizuri labda mimi nimekosea, paul alipo enda akaanzia kwanza hospital, paul akamuuliza daktari kwamba, "jamani mbona vidonda vyangu vinachelewa kupona" dokta akasema "na sisi tunashangaa, labda tukupime virusi vya ukimwi, maana navyo vinachagia, maana ukimwi ni ukosefu wa kinga mwilini sasa hizi kinga za mwili kama hazipo inakuwa ngumu sana kupona ugonjwa wowote ule kwa wepesi" ndipo paul akasema sawa daktari we pima tu kama ni ukimwi nijue moja". USIKOSE YA 17                       
SEHEMU YA 17.
 MTUNZI FRANK DAVID, daktari wa hadithi TZ. whtsapp 0769510060.                                Kweli daktari alimuandikia vipimo mr paul ili aende mahabara kwa ajili ya kupimwa virusi vya ukimwi, sasa siku hiyo kulikuwa na wateja wengi sana hospitalini, hivyo paul akachelewa sana kupata majibu ikabidi aulizie, "jamani mbona nimekaa mda mrefu hapa wala sipati majibu yangu" yule alie kuwa mahabara akampa karatasi ya majibu ili apeleke kwa daktari, maana ile hospitali ilikuwa ya ghalama sana, hivyo kila kitu kilikuwa kinaenda kwa mpangilio thabiti, kweli masikini daktari alipo soma ile karatasi akamwambia, "Mr paul naomba usikate tamaa na haya majibu maana nikawaida sana kwa majibu yako yalivyo kuja" paul roho yake ikadunda ghafla pahh!, paul akasema "daktari kwani kuna nini kibaya" daktari akamjibu, "mr paul wewe ni HIV + yahani una maambukizi ya virusi vya ukimwi, hivyo mchukue mke wako pia aje ili apime muweze kushauliwa jinsi ya kuishi pamoja maana angaza ni bure siku hizi" paul alihisi mwili wote unatetemeka, akasema, "daktari naomba mnipime tena labda huyo jamaa alie nipima nahisi sio mtaalamu, daktari wangu nakuomba, mimi paul siwezi kuathirika nipime tena" daktari akamwambia, "usiseme uwezi kathirika, wewe ni binadamu kama wenzio, na wewe sio roboti maana una damu hivyo ni kawaida kupata ili janga, cha msingi fanya mazoezi, kula safi na ujifurahishe mwenyewe, ukifata ushauri wangu utaishi maisha mengi sana" paul kumbe alikuwa anaogopa sana ukimwi masikini wa mungu, hivyo akaona maisha kama yame mshida akajiona hana thamani tena kwenye hii dunia, sasa basi, paul alipo toka pale akapanda pikipiki mpaka benki, ili akifika atoe pesa amlipe mwenye pikipiki, dahh yahani sasa hapo ndiyo alichoka sana maana alipo angalia akaunti ya benki akakuta nyeupeeee hamna kitu, duuh paul alianguka mulemule benki, wakamuuliza "wewe kama mbona hujiulumii yani una vidonda mwilini alafu unajiangusha chini uoni kama unajitonesha vidonda, haya angalia ulivyo jitonesha sasa mpaka damu zinavuja" paul akasema "uuuuwiii, uuwiiii, nimefirisika, mke wangu kanifirisii jamani" mhh wale walinzi wa pale benki wakamfukuza atoke nje maana alikuwa ana vuruga huduma za pale benki" paul alivyo toka nje bodaboda wa ile pikipiki iliyo mleta akamwambia "kaka yangu tangu asubui sijaingiza ata shillingi mia ya bosi, nimekupeleka hospitali, nikakusubilia hujanilipa, nimekuleta hapa benki pia, nimekusubilia hujanilipa,alafu nashangaa unalia tu na damu zina miminika kwenye vidonda, mimi sina mengi ya kuongea kaka, naomba elfu hamsini yangu uliyo sema ukifika benki utaitoa na kunilipa"  ehh kumbe paul alikuwa hana ata shillingi mfukoni, wazo lake lilikuwa kwamba, akifika benki atoe pesa amlipe bodaboda kisha pesa zingine apeleke nyumbani kwa ajili ya matumizi ya chakula na wake zake, paul akasema kwamba, "kaka najua umenileta mpaka hapa kwa pikipiki yako, ila benki humo hamna ata shilingi mia nimetapeliwa na mke wangu pesa zote maana yeye ndiyo anajua namba ya siri hamna mwingine, hivyo naomba unisindikize mpaka nyumbani kisha nimwambie elivia mke wangu, anipe pesa ili nikulipe" jamaa wa bodaboda akashikwa na wasiwasi maana alikuwa amechoma sana mafuta yake hivyo hakuwa na chochote cha kumpa boss, ikabidi bodaboda akubali tu kumpeleka, kweli  wakaanza safari ya kwenda kwa paul kuangalia kama elivia atatoa chochote kitu aisee. Kipindi wapo safarini bodaboda kwakuwa alikuwa hajapata kichwa kingine, yahani abilia mwingine, hivyo akawaza kukiimbiza pikipiki sana ili afike mapema kwa paul, achukue hela aanze kazi apate viichwa vingine ili apate pesa zaidi, kipindi sasa wako njiani huku dereva anakimbiza sana pikipiki, paul kwa kuwa alikuwa amevaa  bukta fupi ili vidonda visichubuke, dahh masikini kwa bahati mbaya paul alikuwa ameweka mguu wake vibaya ukawa umegusa pale kwenye ekisozi alafu kumbe ile ekisozi ya kutolea moshi kwenye pikipiki ilikuwa ya motooo ndipo ikawa imemchoma mguu paul, sasa kutokana na yale maumivu paul aliyo kuwa anayasikini akaamua kumshika bodaboda, wakati ananyanyua mguu akawa amemshika bodaboda na mkono ulio katika vidore hivyo akawa ameutonesha tena, yahani huwezi kuamini, paul alianguka katikati ya barabara na wakati huo pikipiki ikiwa kwenye spidi kari, mungu saidia magari yalikuwa hayapiti mda huo maana yange mpasua paul, kweli masikini paul kaka wawatu aliumia zaidi akajitonesha mwili zaidi na zaidi, alisikia uchungu zaidi yangu nilio kuwa nikiupata kipindi nimo shimoni, bodaboda akasimamisha pikipiki na kumrudisha paul hospitalini, sasa paul alipo rudishwa kwenye ile hospital alipo pima ukimwi, kumbe pesa yote alilipa mwanzo wakati anapima ukimwi, hivyo hakuwa na chochote mfukoni kwa ajili ya matibabu hivyo ile hospitali ikamkataa akaenda hospitali nyingine ya bei nafuu wakasema hawakopeshi, wanataka hela keshi wamfanyie matibabu, na wakati huo paul anasikia maumivi karibia kufa, wakati bodaboda anampeleka hospitali za kawaida za serikari ili apate matibabu ya bure, pikipiki ikaishiwa mafuta njiani na wakati huo paul hana chochote kitu mfukoni na bodaboda nae hana hela yoyote anategemea paul amlipe ili angalau apate hela ya bosi, alafu sasa paul anapata matatizo akiwa na bodaboda, alafu huyu huyu bodaboda wazo lake ni kwamba paul apate nafuu aweze kumlipa nauli aliyo tumia, pikipiki lilipo zima bodaboda alichoka, na ata kama wangekuwa na pesa kituo cha mafuta kilikuwa mbali  kutoka pale walipo kuwepo, paul alianza kulia akisema mali za dhuruma mbaya, mungu nisameee, Yenda nisameee, najua hizi ni laana zako, naumia mwili wangu mungu niulumie" duhh kutokana na mafuta kukata ikabidi yule bodaboda aanze kusimamisha magari na pikipiki ili asaidiwe, lakini watu hawakujali walikuwa wanapita speed na magari yao yahani hawana habari kabisaa, katika harakati za kusimamisha magari na mimi siku hiyo nilikuwa natoka kwenye shughuri zangu hivyo bodaboda akawa amenipungia  mkono ikabidi nisimamishe gari, nikashusha dirisha kisha nikamuuliza bodaboda, " kaka nini tatizo mbona mikono hivyo balabalani, ndipo yule bodaboda akanisimulia kuhusu paul" ikabidi nishuke nikamuangalie mgonjwa maana nilikuwa sijamjua, dooh sikuamini kama paul ninae mjua, paul tajiri alie nifirisi na kunitupa shimoni, nikauliza "we kaka huyu jamaa unamjua" akasema "kama nilivyo kusimulia kaka yangu mimi nimempa huduma ya usafiri ila matatizo yamekuwa mengi mpaka nachanganyikiwa, naomba tu unipunguzie mafuta kidogo nimfikishe hospitalini, maana yeye mwenyewe hana ata mia analia kwamba mke wake anaitwa elivia amekomba pesa zake zote" ndipo nikakumbuka kuwa elivia aliniletea pesa, ndipo nikapata huruma kidogo ya kutoa msaada, msaada wenyewe nilio utoa, nilimuuliza bodaboda "umetumia shingapi mpaka sahivi ya usafiri wa huyo mgonjwa" akasema " elfu hamsini tu kaka" nikachukua elfu hamsini nikampa, kisha nikamuuliza, "unataka mafuta" akasema ndiyo,nilikuwa nayo ya tahadhari nikampa pia, kisha nikamwambia, "kaka washa pikipiki uondoke niachie huyu mgonjwa wako, kaka wawatu akawasha pikipiki kisha akaondoka" paul alikuwa na aibu usoni akaficha sura akisema, "nisamee Yenda nihurumie yenda, nisamee baba, nilikukosea kaka" niliwasha gari langu na kumuacha paul akiwa peke yake bila msaada wowote wa matibabu wala chakula, paul alilia, alilia sana masikini nikaondoka zangu na kumuacha pale peke yake, mvua ilianza kunyesha kari sana, yenda alikuwa analia maana vidonda vilikuwa vina nyeshewa anawashwa mno na mkononi alipo vunjika vidore maji yalipo gusa pia aliumia sana masikini, kumbe nyumbani farida alikuwa anawaza sana na kuomba Dua ili mme wake arudi nyumbani salama.  USIKOSE SEHEMU YA 18. mtunzi whtsapp 0769510161.                                                
 SEHEMU YA 18.
MTUNZI FRANK DAVID,daktari wa hadithi-Tz, whtsapp 0769510060.                      
 Baada ya mvua kuisha mr paul alijikakamua polepole akirudi nyumbani kwake kwa miguu alafu kibaya zaidi nyumbani kwake palikuwa mbali sana, kipindi yupo njiani masikini wa mungu kaka wawatu alianguka anguka sana na kila alipo kuwa akianguka basi ilikuwa ni lazima yeye kujitonesha, mungu saidia alitembea polepole mpaka akafanikiwa kufika kwake akiwa hoi bini tabani. Farida alifurahi sana kumuona mme wake lakini Elivia alikuwa hajali ata kidogo, paul akasema, mke "wangu Elivia, kwanini umenifirisi mama, yahani umekomba kila kitu kwenye akaunti, kwanini umenifanyia hivyo" elivia akajibu kwamba, "hapana paul mme wangu, sijaiba, sasa mimi hizo pesa zote nizipeleke wapi, na nitazitumiaje wakati tunaishi wote humu ndani" paul akasema, "Elivia basi nigawie ata kidogo japo millioni mbili tu kwa ajili ya matibabu maana nina umwa sana elivia alafu sina hela" farida aliogopa akasema, "mme wangu umefikia hatua ya kuomba milioni mbili wewe, sasa tutaishije humu ndani jamani" paul akasema, "farida mke wangu elivia nilipo mpa ile kadi ya benki pamoja na neno la siri amekomba kila kitu kwenye akaunti, hatuna hela yoyote ndani" kipindi wanaongea vile luku ikaisha, umeme uka kata kukawa giza ndani, sasa paul alikuwa amezoea kwamba umeme ukikatika tu, anachukua simu yake kisha ananunua umeme kupitia simu, Elivia akasema "mme wangu nunua umeme kwenye simu, maana kuna giza ndani" paul akasema "pesa iliyo kuwa imebaki kwenye simu ndiyo niliitoa kwa ajili ya hospitali, hivyo sina ata mia, na simu yangu hii hapa, nimepata ajali huko balabalani nika achwa na bodaboda nilie kuwa nae, alafu mvua yote imeninyeshea, na kibaya zaidi simu yangu ilikuwa mfukoni imeingiliwa na maji hivyo sina tena simu na sina uwezo wa kumiliki simu nyingine maana sina pesa ya kununua simu tena" elivia akasema, "mme wangu haya yote umeyasabisha wewe mwenyewe, kipindi tupo wawili tuliishi vizuri tu bila shida wala tabu yoyote ile, sasa wewe umeoa mke mwingine, ametoka kwao uko na ushirilikina, ona sasa tumefirisika, aibu hii tunaiweka wapi, na ubaya zaidi hatukujiongeza zamani maana kama tunge fungua ata ka mladi kokote kale kama duka au ata shamba tungekuwa na hela nyingi, haya sasa luku imeisha nyumba yetu imekuwa na giza huko nje taa zimezima, hivi unategemea nini zaidi ya kuchekwa na majirani" paul alianza kulia tena kisha akasema, "farida mama, hivi ni kweli anayo yasema Elivia, hivi kweli wewe unaweza kusababisha sisi tufirisike, kama umefanya hivi naomba basi ununue japo mshumaa ili tutoke gizani" farida alikasilika akamfata Eliva kukiwa na giza vilevile wakaanza kupigana tena, sasa kwakuwa farida alikuwa mdogo hivyo elivia alikuwa anampiga kisawasawa, kipindi wanapigana gizani, paul akasema, "msipigane wake zangu pendaneni tu" wakati paul anaongea  alikuwa hana nguvu kabisa za kuwa achanisha, maana kama unavyo jua, paul alikuwa na vidonda, alipata ajali, mikono ya kuwaachanisha ilikuwa mibovu maana mkono wake wa kushoto ulikuwa hauna vidole tena sababu vilivunjika, duuh ni hatari pekee, hivyo akashindwa kabisa kuwa achanisha, sasa na wale kibaya zaidi walikuwa wanapigana kwa hasila yahani kila mtu anamchukia mwenzake, bahati mbaya elivia akamsukuma farida, wakati farida anadondoka, alimuangukia mme wake vibaya, maana alimtonesha kwenye mkono! Paul alilia, "haaaa, haaaa farida umeniua" kweli farida alipo geuka akashika mkono chini kusimama duuh alishika damu zilizo kuwa zina miminika kutoka kwenye mkono wa mme wake" ikabidi elivia awashe simu yake kuandaa maji kwa ajili ya kumkanda paul, ndipo wakaacha kupigana, sasa kipindi wanaandaa maji ya kumkanda paul, wakawa wamechanganya chumvi ili damu ikate isiendelee kuvuja, dah paul alipo kandwa na yale maji, alisikia uchungu sana masikini, alilia akisema "naumiaaaaaa jamani achaaaa! Nawashwa vibaya" Dahh wake zake wakaacha damu zilimtoka nyingi mpaka lile beseni la maji ya kumkanda likawa na langi ya damu nyekunduu tu walipo mlika kuangalia na simu. Ilipo fika asubui wakapika chai wakanywa hivyo hivyo bila kitafunwa maana hakukua na hela kabisa ndani, paul na elivia walianza kujutia, maana labda wangeomba msaada kwa majirani wangewasaidia, ila majirani walikuwa hawawapendi kina paul sababu walikuwa ni watu wa kujigamba na kujitenga, mchana walishinda njaa bila kula chochote kabisaa,  usiku ulipo fika kukawa giza kama kawaida ndani wakachemsha  chai tu wakanywa kisha wakalala, dahh kibaya zaidi hali ya paul ilikuwa inaendelea kuwa mbaya kila siku mkono hauponi vidonda havikauki vinatoa majimaji tu kila wiki, dahh ikabidi elivia na farida wampeleke mme wao mpaka hospitalini kwenye hizi hospitali za serikari ili mme wao atibiwe, sasa walipo fika pale kila mtu anawashangaa, "hee jamani huyu sini yule tajiri mr paul, na yeye analetwa hospitali kama hizi" hawakupata majibu maana kila mtu alikuwa anapiga umbea wake, "haaa hapana hao wana amua tu pesa wanayo bhana" mara dada mwingine akasema, "mhhh kwani hamkusikia kwamba paul anataka kugombea udiwani, hivyo hizo ndizo siasa za kisayansi, anakuja kujifanya eti na yeye anatembelea hospitali za jamii na yeye atibiwe huku huku ili tujue sio mbaguzi tumpe kura" yahani sema kweli kila mtu alikuwa na lake siku hiyo, maana kuna mmoja alisema, "dada koku, huyo kaishiwa pesa hana ndiyo maana umalidadi wote kwisha zake" duhh jamani kufirisika kubaya, sasa paul pamoja na wake zake walipo enda kwa nesi ili awape huduma, nesi akawambia, "jamani ndugu zangu hapa huduma ni bure ndiyo lakini mnatakiwa kununua daftari hapo nje shilingi mia tatu tu, ili mje niwaandike" wakasema sawa, wote wakatoka nje, walipo kuwa nje, wakaanza kuulizana, "nani ana mia tatu, tununue daftari, ehh kumbe wote walikuwa hawana lool masikini, umasikini uliwaingia vibaya hao watu, ikabidi paul amwambie elivia akaombe mtu yoyote awasaidie japo hiyo hela waweze kumaliza haraka matibabu ili paul arudi nyumbani akapumzike, huwezi kuamini kila mtu pale alie ombwa hela alisema hana na ndiyo maana amekuja hospitali za serikari kusaidiwa, farida akaona aibu sana ikabidi awapigie wazazi wake simu ili awaombe hela, wamtumie kwa ajili ya kununua daftari, alipo piga simu baba yake farida akamwambia, "mwanangu hemu acha utani bhana leo sio siku ya wajinga duniani, yahani wewe umeolewa na tajiri wa mtaa, alafu unasema huna hela tena shilingi mia tatu, punguza masihara binti yangu" dahh yule baba akakata simu, na akaendelea na shughuri zake, ilikuwa ni aibu sema kweli siku hiyo. Baada ya mda yule nesi akatoka ofisini akawakuta nje pale wana angaika, nesi akasema "nyie mbona mmekaa hapo mda mrefu, mgonjwa analia tu, kwanini hamleti daftari sasa" elivia na farida wakasema, "hatuna hela nesi" nesi akashangaa maana ata yeye kumbe alikuwa anamjua Mr paul mzee wa sifa, nesi akasema, acheni uongo bhana mungu hapendi, "huyo sini paul," wakasema "ndiyo" nesi akasema, "iweje mkose hela sasa" farida alilia akadanganya, "tulivamiwa, hatuna hela nesi" nesi alitingisha kichwa, akasema "lohh, maisha haya, sawa basi chukua hii elfu mbili, nunua daftari, atibiwe, mumpeleke nyumbani mapema maana juwa kari sana leo" na hiyo ndiyo ilikuwa pona pona yao, paul alitibiwa akapewa na dawa za kukausha vidonda, ile pesa waliyo pewa chenji iliyo baki wakanunua viazi vitamu vingi, maana huko mtwara vilikuwa na bei ndogo,
Waliendela kupambana sana japo waweze kuishi kibishi hivyo hivyo, ila mlo wao ulikuwa wa shida sana kila siku, lakini farida alikuwa mvumilivu dada wawatu alivumilia hivyo hivyo, sasa kutokana na tabu kuwa nyingi paul akawaita wake zake akasema, "jamani mimi ni mwanaume alafu mungu amesaidia sahivi naendelea vizuri, nilikuwa na wazo" elivia na farida wadakia, "wazo gani hilo?" Paul akasema, "nimepata wazo tuuze hii nyumba tukapange ili ile pesa ya nyumba tufungue biashara kusudi tuweze kula vizuri na maisha yaendelee" farida akakataa ila elivia akasema "wazo zuri mme wangu uza" paul akasema "hapana farida usikatae, wewe ngoja niuze utaona, maana nita jenga badae nyumba kubwa zaidi, hatuwezi kutumia taa za chemli tena" elivia alifurahi ila farida alichukia kabisaa, sasa kipindi wanatangaza kuuza ile nyumba wakati huo bado paul hajapona vizuri vizuri, eliva akaingia chumbani akafungua mabegi ya paul kisha akachukua hati ya nyumba, alafu akaniletea mimi kisha akasema, "Yenda mme wangu nafanya haya yote sababu wewe ndiyo baba mtoto wangu ata nikifa mwanangu hatateseka hii hati ya nyumba itunze maana paul anataka kuuza nyumba, na hile nyumba sio halali yake, zote hizo ni pesa zako wewe" nikasema "sawa" kama kawaida nikachukua hati ya nyumba kisha nikaificha, sasa siku wateja wa kununua ile nyumba walipo patikana, paul akapewa pesa yote mkononi, Tsh milioni 99, wale wanunuzi wakaomba hati ya nyumba pamoja na mwenyekiti wa mtaa ku sahini ili wachukue nyumba yao, paul akasema sawa naleta hati, "alipo enda kufata ile hati ya nyumba akakuta haipo, duhh alichanganyikiwa" ikabidi wale wanunuzi wachukue pesa yao waondoke maana walihisi paul ni mwizi, sasa kibaya zaidi ile hati ilikuwa na wamiliki wawili yahani paul pamoja na elivia na majina yao yalikuwepo katika ile mikataba, hivyo elivia alikuwa na uwezo wa kuuza ile nyumba pia, paul alichukia akasema "wake zangu wote njooni hapa" kisha akaendelea kusema, "jamani hivi kuna mizimu humu ndani au kuna michezo inachezwa, hivi hati ya nyumba iko wapi, mikataba yote ya nyumba iko wapi?" Elivia akasema "mimi sijui mme wangu" farida nae akasema, "jamani hiyo mikataba sijui hati tangu nije hapa ata sijui hiko wapi" paul akasema, "hoooosh! nimekwishaaa, nimekufa mimi, jamani naombeni tu hati kama hamnipendi nipo ladhi kuwaacha wote" elivia akasema, "mme wangu mi nahisi huyu Farida atakuwa ameificha, maana ata ulipo kuwa unataka kuuza hii nyumba alikuwa anakataa kwelikweli" paul akaamini maana akili ilikuwa imeruka, akasema "kweli nimeamini wewe mwanamke ndiye unaeleta umasikini humu ndani, nasema wewe ni mkosi sasa naomba toka kwangu tokaaaaaaa!" Farida akasema "mme wangu mimi sijui, mimi siajaiba, ananisingizia," paul na elivia walisaidia kutoa mizigo ya farida nje wakamfukuza kama mbwa masikini wa mungu, dada wawatu alienda kwao analia, akamkuta mama yake nyumbani, kumbe mama yake naye pia alikuwa na machozi ya karibu wakasaidiana kulia wote, kisha mama farida akamwambia mwanae kwamba "mwanangu achana nae huyo mwanaume ni mjinga sana, yahani mwanangu unaitwa mwizi leo, wakati wazazi wako tumekufunza vizuri tu hapa nyumbani, achana nae utapata bwana mwingine wa kuku oa mta ishi vizuri tu" mungu saidia,  farida alitoka kwa paul bila kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi, sasa kule kwa paul, Elivia akaanza kusema tuone sasa atauzaje hii nyumba kaisha ondoka tayari huyo mwizi, paul akasema, "najuta kumuoa huyo mwanamke kabisa, mjinga sana huyo dada, nisamee Elivia mke wangu sitarudia kuoa tena nakuhaidi mama" Elivia akasema, "unaona sasa ulikuwa unalia mtoto mtoto, achana nao hao wadada mme wangu" kweli wakaendelea kuishi pamoja kama zamani, USIKOSE SEHEMU INAYO FATA,, ya 19. Mtunzi wako ni FRANK DAVID, daktari wa hadithi Tz. Nichek whtsapp 0769510060.                       
SEHEMU YA 19
 MTUNZI FRANK DAVID daktari wa hadithi TZ Whtsapp 0769510060
Maisha ya paul pamoja na elivia yalikuwa bado niya tabu sana maana kula yao ilikuwa niya shida mno, siku moja paul akamwambia eliva, “mke wangu kwa sasa ni bora nitafute kazi ya baani, yani niwe muhudumu wa baa tupate pesa” elivia hakubisha akasema “sawa mme wangu, hiyo kazi naamini unaiweza sana, maana nakumbuka zamani ulisha wai kuifanya”. Kweli paul akaenda kutafuta kazi ili angalau waweze kupata pesa ya kubadilishia mboga, mungu saidia ile baa ya kwanza paul iliyo enda kuomba kazi akakuta nafasi zipo bila wasiwasi, yule bosi mwenye ile baa alishangaa sana kuona mtu tajiri kama paul anaomba ile kazi akamuuliza, “bosi hivi ni kweli unataka hii kazi au unanitania maana wewe ni mtu mkubwa” paul akasema “kaka haya maisha ni kupanda na kushuka, nilipo oa mke wa pili niliishiwa pesa kabisa, nikapata matatizo mengi sana hivyo kwa sasa sina kitu kabisa, naomba msaada wako kaka, maana hii kazi naiweza, na kipindi naanza maisha ya utafutaji nilifanya sana hii kazi” bosi mwenye hile baa akasema, “kazi hipo na kuna nafasi mbili, mtu wa kiume na wa kike hivyo kama umeiwai wewe na upo seriasi basi kesho mapema njoo uanze kazi”
 paul alishukuru sana akasema “asante kaka umenisaidia sana ila nimesikia unasema kuna nafasi ya watu wawili, naomba nafasi moja umpe mke wangu maana na yeye yupo tu nyumbani hana kazi yoyote ya kufanya” mwenye ile baa akasema, “kaka hizi kazi sio nzuri kufanya mtu na mke wake maana lazima upate wivu ni bora yeye aangalie sehemu nyingine” paul akalazimisha akisema “mke wangu hana shida, mke wangu yupo makini we mruhusu tu utaona” paul akaambiwa “basi sawa kama umeona hiyo ni sahihi mje wote kufanya kazi, ila malipo yangu ni ya siku, kila mkimaliza kazi nawalipa”
kweli paul alipo fika nyumbani wakapanga mipango na elivia kwa ajili ya kufanya kazi, sasa kipindi wanaanza kazi pale baa wateja walikuwa wanakuja wengi sana mpaka bosi akashangaa, yahani haikuwa kawaida ya pale, bosi akawaita elivia pamoja na paul kisha akawambia, “ndugu zangu nawapenda sana maana nyie niwachapa kazi sana mmefanya baa yangu kuwa maarufu hivyo nitakuwa nawalipa elfu 30 kwa siku kila mtu, nimewapandishia kutoka elfu kumi maana mko vizuri katika upigaji kazi” paul na elivia hawakugundua kabisa kwanini wateja wengi walikuwa wanakuja pale, kumbe masikini ya mungu wale wateja wote kilicho kuwa kinawaleta pale ulikuwa ni umbea tu, maana walikuwa hawa amini kama kweli paul amekuwa muuza baa, kwasababu vijana wengi waliamini paul ni mtu mwenye pesa sana na mke wake. Sasa kadri siku zilivyo kuwa zinaenda paul na elivia walikuwa wame pazoea sana pale baa, sasa siku moja kunawateja wakorofi sana walikuja pale sasa walipo gundua paul hana kitu tena, wakaanza kumchezea mke wake, maana paul alikuwa anashangaa watu wakiitaji pombe wanamuita mke wake ili awa hudumie na ubaya Zaidi mke wake akiwa ana hudumia walevi walikuwa wanamshika makalio yake, mara wampapase mikono, sasa elivia alikuwa anaogopa kukataa maana angekataa kushikwa shikwa wateja wake wasinge kuwa wanarudi hivyo hela ingepungua kwa boss, na paul alikuwa anatamani kupigana nao, ila bosi alikuwa anamwambia, “itabidi uvumilie tu mke wako ashikwe shikwe maana nilikwambia toka mwanzo kwamba hii kazi sio ya kufanya na mkeo” dah paul alikuwa anaumia masikini ila hana jinsi, siku moja alishangaa kuona baba mmoja hivi amekunywa amelewa kisha akambeba elivia na kumkalisha mapajani huku akishika shika maziwa ya elivia, huku elivia anajichekesha kama hataki ili yule baba asichukie, paul alichukia akamfata elivia kisha akamvuta, elivia akasema “paul, mme wangu unanifukuzia wateja” paul akamjibu kwamba, “hivi elivia hujui kuwa wewe ni mke wangu, hivi unashikwa shikwa tu mbele yangu unahisi mimi najisikiaje” yule mlevi akasema “we boya acha ushamba, tuache wenye pesa zetu tufurahie maisha, mke wako kama huwezi kumuhudumia tuachie sisi” paul alichukia sana akaanza kupigana, yule mlevi akachukua chupa ya bia akampiga nayo paul kichwani phaaaa!, dooh paul alipasuka vibaya masikini, damu zikaanza kumtoka, elivia akamuombea msamaa mme wake, ndipo bosi wa ile baa akaja kuwaachanisha, ikabidi paul apelekwe hospitali kushonwa pale kichwani alipo pigwa, kipindi Paul yupo nyumbani anauguza kidonda elivia aliendelea kufanya kazi mule baa ili apate pesa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani maana wote wangelala bila kufanya kazi nyumba ingebaki tupu na wangeshinda njaa maana wale watu walikuwa hawana kabisa akili ya kutunza pesa, wenyewe wakipata wanatumia.
Sasa kipindi paul yupo pale nyumbani alikuwa ana msihi sana mke wake kwamba, “elivia kuwa makini na wale watu wasiku laghai na pesa zao” elivia kwa upole akajibu “ndiyo mme wangu siwezi kurubunika” yule jamaa alie mpiga chupa elivia alipo rudi siku ya pili pale baa alimnunulia pombe elivia, na elivia alivyo kuwa mpuuzi akakubali kunywa, akizani ni upendo, kipindi elivia amelewa hajitambui yule kaka akamwambia elivia, “dear kuna elfu 60 hapa kwa ajili yako, naomba twende kwenye gari langu tukafanye mapenzi” elivia akasema, “mi naogopa mme wangu atajua” yule bwana akamwambia, “hapana dia, hawezi kugundua, wewe mkifunga kazi, nitakuwa pale nje, gari langu nazani unalijua, ukiisha funga utaingia tutamalizana kisha nitakulipa,” kweli masikini kutokana na tamaa za dunia, yule jamaa akaongea na bosi mwenye ile baa, kweli mwenye bar akawaruhusu waondoke, ila akasema hatomlipa pesa yake ya siku hiyo, elivia alikubali maana aliangalia faida, walipo ingia kwenye gari kutokana na ulevi elivia alifika na kujiachia mwili mzima akiwa tupu, miguu akaitupilia kule, yule bwana akafanya dhambi zake siku hiyo, kumbe masikini wa mungu yule kaka alikuwa na familia yake nyumbani mke pamoja na watoto na mke wake alikuwa mjamzito, sasa alipo fanya lile tendo na elivia bahati mbaya akapata ukimwi, hivyo alipo fika nyumbani akamuambukiza na mke wake wa ndoa pia.
Elivia alipo fika nyumbani kwake alioga akamdanganya mme wake kuwa anaumwa alafu akalala maana hakutaka agundulike kama amelewa, maisha yaliendelea mpaka ikafika hatua, eliva akaanza kujiuza kwa wateja wake wote wa pale baa, mwenye baa pia kumbe alikuwa anamtamani alafu anashindwa kusema, siku moja akamnunulia, nyama choma ya ngombe, kachumbali na ka bia pembeni wakaangaliana kwa macho ya kutabasamu, mwenye baa pia akajibebea mzigo akalala na eliva pia siku hiyo, mme wake alivyo pona uzalendo ulimshinda maana sasa elivia alikuwa kama changudoa sasa, kila mtu anae jisikia kumshika anashika tu, anae taka kumbusu shavu anabusu tu, alafu ile baa ilipendwa sana kwa ule upuuzi wa elivia, dahh paul akaona ni bora waache tu ile kazi, maana kila alipo mwambia elivia asikubali kushikwa, elivia ndiyo wapi hataki kusikia yeye anacho sema anataka wateja wake wasimkimbie kama bosi alivyo sema.
Siku moja mimi pamoja na Prisca tuliamua kwenda kwenye ile baa, japo tujiburudishe kidogo maana mda mwingi unakuta tupo bize sana, sasa kipindi tupo pale kabla elivia hajatuona hatukuamini macho yetu, yahani elivia alivyo kuwa ana hudumia mara acheze mziki akatike mauno, mara ashikwe na wanaume anajichekesha, huku paul yupo amenuna tu, nikamwambia Prisca “unaona mke ulie taka kunipa, mambo anayo yafanya sahivi,”
Kipindi tumekaa pale elivia akaja kutuhudumia, akauliza mnatumia vinywaji gani, alipo tuangalia vizuri akakuta anatujua dohh, alifunga kishikizo cha juu maana alikuwa na mtindo wa kuachia maziwa yake wazi, akasema “yenda nisamee, ni ugumu wa maisha tu unanifanya nifanye hivi” nikamwambia “sisi hatuna shida maana upo na mme wako hapa, we piga kazi tu kwasababu mme wako na yeye pia anaipenda”
Elivia aliona aibu sana siku hiyo akamfata mme wake akasema, mimi sitaki tena hii kazi naondoka.
USIKOSE YA 20                                               
MTUNZI FRANK DAVID, DAKTARI WA HADITHI tz. Whtsapp 0769510060.                              
 Paul na elivia walivyo tuona pale baa tuna waangalia wanavyo hudumia bia, wote waliona aibu wakamfata bosi wao kisha kwanzia siku hiyo wakaacha ile kazi, ila sababu kubwa iliyo mfanya paul aache ile kazi, ni zile aibu alizo kuwa anazipata, pale mke wake alipo kuwa anashikwashikwa na walevi. Kipindi wapo nyumbani kwa mala ya kwanza hawakuangaika, maana elivia alikuwa na hela kama laki mbili ndani, kwasababu kila alipo kuwa anajiuza kipindi mme wake anauguza kidonda cha kichwani, yeye zile pesa alizo kuwa anapewa na wanaume kumbe alikuwa anazitunza, hivyo zilezile pesa ndizo zilizo wasaidia pale nyumbani kwa siku mbili tatu. Baada ya zile pesa kuisha maisha yakabadilika sana, siku moja paul aliugua sana, maana ukimwi ulikuwa umeanza kutawala ndani, sasa baada ya siku kadhaa kipindi bado paul hajapona, elivia na yeye pia akaugua maana virusi na yeye pia vilikuwa vina msumbua, dooh paul alianza kukonda sana mwili unapotea, ubora wa ngozi yake una potea pia akaanza kujua hapo lazima afe tu, elivia nae hivyo hivyo alipungua mno masikini, sasa kibaya zaidi walikuwa hawali chakula maana hakuna ata mmoja alie kuwa na nguvu ya kutoka nje au kupika, sasa baada ya siku nne wakiwa hawajaweka chochote tumboni wote waliamza kualisha na kutapika miili yao imechoka sana jamani, sasa paul akagundua kuwa ni virusi vya ukimwi lakini akaogopa kusema kwa elivia, kumbe elivia nae anajua ni virusi vya ukimwi na yeye ndiye alie muambukiza mme wake ili amuambukize na farida pia. Dooh siku ya sita ilipo fika wapo ndani wanalia tu hawajala, kuna jamaa mmoja alikuwa amekuja kuwasalimia, na jamaa mwenyewe ni yule mlinzi paul alie mfukuza kipindi cha nyuma wakati mimi nilipo ruka ukuta na kuingia ndani, alifika akasema boss, "mbona mme lala chini hivyo tatizo nini" huwezi kuamini yule kaka aliwasaidia kupika uji, akawafatia dawa za maumivu kisha akawapeleka hospitali kwa pesa zake mpaka wakapata nafuu, na wote wakapewa vidonge vya ARV vya kupunguza makali ya virusi vya ukimwi pamoja na kunenepesha mwili, mlinzi alipo wasaidia akakaa nao kwa mda kama wa miezi miwili yeye huyo huyo anatafuta pesa na kuwapikia mpaka wakapona kabisa, paul akasema, "nisamee kaka, nilifanya vibaya kukufukuza" yule mlinzi akasema "nimeisha wasamee zamani sana, na ndiyo maana nilikuja kuwasalimia, nikashangaa kukuta mpo kwenye hii hali" paul akasema "dahh, kaka nimefirisika, nilioa mwanamke wa pili kanitia mikosi sana ndani, yahani nimefirisika sana, sina kitu kabisa ndani" yule mlinzi akasema, itabidi uanze miangaiko ya hapa na pale ili uweze kuishi vizuri maana mnapaswa kula na kukidhi maitaji yenu yote, baada kama ya wiki moja yule mlinzi alirudi mkoani kwao akawaacha kina paul na elivia wamo ndani wanalia. Paul alikuwa mvivu sana wa kufanya kazi ngumu za kiume,  na kibaya zaidi paul alikuwa kaisha poteza nguvu kazi, maana alikuwa na virusi hivyo yeye alikuwa amekaa kizembezembe tu kufanya kazi ngumu hawezi, elivia akamwambia, "mme wangu nimechoka kulala njaa na giza humu ndani, hivi unapo kuwa unalala unategemea mimi nitaishi vipi sasa, au umesahau tulivyo ambiwa kwamba hivi vidonge tulivyo pewa tunatakiwa kula vizuri mara kwa mara" paul akasema "mpuuzi nini, nani akufanyie kazi, wewe amka kajitafutie pesa zako kama una njaa" elivia alichukia akasema "haya sawa umeshinda" kweli elivia alianza tena tabia zake za wanaume, anabadilisha vijana ili apate pesa, elivia alinawili sana, paul kila siku anapungua tu, familia ilikuwa ya kipuuzi, mwanaume amemruhusu mke wake kuwa huru kufanya anacho taka, elivia nae akaanza kuufanya mwili wake kama duka yani jamii iliwashangaa sana, siku moja usiku elivia alipata bwana, walienda baa wakanywa sana pombe elivia alilewa sana siku hiyo, walipo malizana elivia akarudi kwake, huku pombe zimemjaa kichwani, akaanza kutoboa siri zote kwa paul, "mme gani wewe mzembe, mwizi, unalala tu ndani kama mbwa, sasa kwa taarifa yako, pesa zote benki ni mimi ndiyo nilizo toa nikampelekea Yenda , hati ya nyumba pia nimeiba mimi nimempelekea yenda, na ukimwi unao kusumbua nimekuambukiza mimi mwenyewe, sasa utakoma uliniaribia maisha yangu kwa yenda, sasa wewe ndiyo utakufa kama kibudu, sasa hivi siogopi kufa, wacha nife sababu ya mapenzi, niue tu niue, lakini pesa zote nimemrudishia mme wangu, tafuta zako mzembe wewe" duuuhh yale maneno paul hakuamini kuyasikia akamshika elivia ili ampige, elivia akamng'ata sikio kwa nguvu sana yani alikaza meno kweli kweli, duuh damu zikatoka akapata maumivu sana mwilini ikabidi amuache tu, akasema, "elivia yahani nimemfukuza farida kumbe wewe ndiyo mkosaji, sasa kwanini umempa yenda pesa, kwanini lakini," aliongea vile machozi yakimtoka, kesho yake paul akatoa kila kitu nje cha elivia kisha akamfukuza kama mbwa, elivia akasema, "mme wangu kwanini unanifukuza" paul akasema "kwani umesahau maneno uliyo sema, sasa nenda kaishi na huyo yenda wako" elivia alikuwa amesahau kabisa kama aliongea yale maneno, maana kumbe ni pombe zilisababisha aongee vile na alikuwa ataki paul ajue hiyo siri, dahh maisha ya elivia yakaanza kuwa magumu sasa akaamua kwenda kuomba kazi za ndani japo apate sehemu ya kujihifadhi, alipo fika kwenye familia moja hivi yenye uwezo, akapata kazi, yahani uwezi kuamini aikupita ata wiki moja elivia akafumaniwa na mme wa yule mama alie muajili kazi wapo chumbani wanafanya mapenzi, akaulizwa "elivia kwanini unatembea na mme wangu wewe siulisema unataka kazi za ndani" akasema, "mme wako alisema nikitaa kufanya nae nitafukuzwa hapa"  alifukuzwa siku hiyo hiyo, ila akawa ameeneza ukimwi kwenye ile familia, elivia akaanza kulala kwenye kituo cha mabasi, kisha anayafanyia usafi yakisimama alafu usiku analala humohumo kwenye basi, madereva wakijisikia wanampa ata elfu 3 wanalala nae mpaka akazoea, siku moja aliiba simu ya dereva wa lile basi alilo kuwa analala, sasa alipo iba simu akasahau kuizima, mwenye simu akaulizia sana simu yake elivia akakataa kabisa kuwa hajashika simu ikabidi dereva ajaribu kuipiga, huwezi kuamini simu ili itia kwenye nguo ya ndani ya elivia, dooh alipigwa mule stendi kila mtu akamkataa alitandikwa sana elivia mpaka nguo zikachanika, aliondoka pale akiwa anavuja damu, hajui wapi pa kwenda, ndipo akawaza kuja kwangu ili aombe msamaa. Sasa siku moja mimi nikiwa njiani wakati narudi nyumbani kwangu nikakuta vibaka wanamvamia mzee flani hivi, dahh ilibidi nisimamishe gari ili niwazuie, nilipo angalia vizuri nikakuta yule mzee wamempiga sana masikini ikabidi nimpeleke haraka haraka hospitali, wakati anatibiwa, mke wake pamoja na mtoto wake wakaja kumbe yule baba ndiyo alikuwa baba mzazi wa farida na hapo ndipo mimi nikajikuta naanza kufahamiana na farida, huwezi kuamini nilijikuta nampenda sana farida, ingawa siku mwambia mapema, baba farida alipona akarudi nyumbani ndipo mimi nikachukua namba zao zote za simu, nikaanza kuwatembelea kwao na kuwajulia hali
Niliwapenda sana kina farida maana familia yao ilikuwa inajiheshimu na walikuwa watu wema tu, farida alikuwa bado hajagundua kama nimempenda ila nilimuelezea kuwa namuitaji awe mke wangu na tutambulishane pia, akakubali ndipo nikaongea na wazazi wake nikalipa maali, kisha nikamchukua farida kama mke wa maisha yangu nikaanza kuishi nae pale kwangu, farida alikuwa mke mzuri, asie na tamaa, tulipima nikakuta ana afya njema, prisca akasema sahivi umepata mke sasa, alimpenda sana mtoto wangu, ila sasa mimi sikujua kama alisha wai kuwa mke wa mr paul, siku moja Elivia amezidiwa mtaani hivyo akaja kwangu japo kuomba ata elfu moja aweze kula, alipo fika kwangu akamkuta farida mke wangu, elivia alipo muona farida hakuamini kabisa, akasema, "heee farida mbona umependeza hivyo" farida akasema "asante," elivia akasema, "naona umepata kazi za ndani kwa mme wangu" farida akasema, "nini nani mme wako" elivia akasema "yenda ni mme wangu na nimezaa nae mtoto wa kike nazani unamlea" farida alichukia kusikia vile, akasema, "naomba umkome mme wangu, baki na paul huko, usinifatilie" elivia akasema, "siwezi kukubali bora tufe wote sababu ya mapenzi, lakini mme wangu siwezi kukuachia" wakati wanaongea vile na mimi pia nilikuwa nawasili nikawakuta, elivia akasema, "yenda mme wangu mtoto wangu hajambo" nikamjibu, "nisikilize elivia, wewe sio mke wangu, mke wangu ni farida, na ndiyo mama wa hii familia, sasa wewe baki na paul wako huko kwenu mkaishi salama toka kwangu, tokaaaaaaaa! Usiniaribie ndoa"  elivia alitoka pale amenuna sana akasema, "siwezi kukubali lazima farida afe"   Usikose ya 21.                       
SEHEMU YA 21.
MTUNZI FRANK DAVID, daktari wa hadithi_Tz. Whtsapp 0769510060.                             
 Elivia aliumia sana masikini, akasema kwamba,  "hee! Kweli huu ni mkosi, yani farida ana bahatika kumpata mwanaume bora kama Yenda, dahh sijui nifanyeje waachane, ni bora ningeacha aendelee tu kukaa na paul wake, dooh sasa kama Yenda ameoa, basi sina nafasi kabisa kwake tena" Elivia hakuachia hapo tu bali aliwaza zaidi kwamba, "farida nilikuwa namtesa sana, sasa leo hii yeye ndiyo mama atakae mlea mwanangu, sijui atamtesa kwa kulipiza kisasi dahh ehh mungu nisadie" Sasa baada ya elivia kujifikilia mambo mengiii, bila kuyapatia majibu ndipo akaamua kwenda kwa paul ili ampe umbea kuhusu farida wake, elivia alipo fika kwa paul akamkuta amelala unabalazani anawaza sana, elivia akafungua geti kisha akasema, "habari yako paul" paul akasema, "akakakakakaa, we malaya umefata nini kwangu toka hapa, tokaaaaa, mjinga sana, yahani nakuchukia, sitaki ata kukuona mbele yangu ondokaaa nitakuua nakwambia, ondoka nakuomba wewe umenifanya nimfukuze farida wangu alafu unarudi, hivi unazani nitamrudisha vipi mke wangu wa dhati" elivia akasema, "paul mimi sijaja kukaa kwako, na sipataki ata kidogo, ila nimeleta umbea tu, yule mke wako farida ameolewa na Yenda na wanaishi pamoja sahivi, ni ilo tu la leo kwaheli" paul akasema, "heee! Subili kwanza elivia, eti nini" elivia akarudia alivyo sema kwamba "mke wako farida ameolewa na Yenda na wanaishi pamoja sahivi," dooh paul akasema, "Noo! Hapana siwezi kukubali, bora nife tu, pesa sawa amechukua ni zake, nyumba hii amechukua hati zake ni halali yake, ila kwa farida anakufa mtu sababu ya mapenzi, siwezi kukubali itakuwa vita nasema" elivia hakutaka tena kuongea akarudi mtaani kuendelea kuangaika na njaa zake. Siku moja elivia alirudi kwa wale vijana walio mbaka na kumuambukiza ukimwi kuongea nao, mmoja wawale vijana akasema, "dahh! We dada yahani hujakoma tu unataka tena turudie tulivyo kufanya" Elivia akasema, "hapana ndugu zangu mimi mmeisha nisababishia matatizo sana, maana nimeathirika kwa sababu yenu, hivyo na nyie mkapime" waliogopa wale vijana maana walikuwa hawajui afya zao, wakamuuliza "sasa umefata nini kwetu" elivia akawajibu vizuri tu kuwa, "kuna ndugu yangu anaitwa farida simpendi ata kidogo, naomba niwaelekeze kwake mkambake, na wanapesa sana hivyo mtapata pesa mkifanya hicho kitu, maana wale wanapesa mkimtishia kidogo tu anatoa pesa zote alizo nazo, maana ni muoga na hana nguvu kabisaa" wale vijana walicheka sana maana walikuwa ni wahuni, wakasema, "yahani hapo umetufikisha tunapenda sana watu kama nyie, haya eheee vipi kuhusu mme wake anakuwepo saa ngapi kwake" elivia aliwajibu kuwa "mme wake uwa anafanya kazi sana hivyo mkienda saa saba mchana mpaka saa kumi, mnamkuta ndani mwenyewe" wale vijana walielekezwa na Elivia vizuri mpaka nyumba yangu wakaijua ili kuja kumfanyia mke wangu vibaya bila mimi kugundua, sasa siku hiyo wanajipanga kuja mimi nilikuwa nipo pale nyumbani maana nilikuwa najisikia vibaya hivyo nilikuwa chumbani nimelala tu napumzika kidogo, walivyo kuja wakagonga mlango, "khokhokho" nikamwambia mke wangu, "nenda kaangalie ni nani anagonga mlango" farida alipo kuja kufungua mlango akaona watu tisa yahani vijana walio shiba vizuri pale mlangoni, akawambia, "karibuni ndani," wakaingia, farida akawauliza "ehh niwasaidie nini wageni wangu" jamaa mmoja akasimama kisha akamvuta  farida, alafu akamziba farida mdomo kwanguvu sana ili asipige kelele, mwingine akaenda kufunga mlango vizuri ili mtu asiwafumanie, jamaa mmoja akaanza kuchana nguo za mke wangu ili abaki uchi waanze kuzitumia vibaya nyeti zake, farida alibanwa sana mwili masikini, akawa anachezesha tu miguu ili asibakwe, kipindi hicho mimi nipo chumbani sisikii chochote, na kibaya zaidi nilikuwa nasikiliza miziki kwenye radio yangu ya aina ya bufa hivyo ata zile purukushani sikuweza kuzisikia, sasa wakati farida anatokwa tu machozi vijana wameisha mvua na kumshika kwa nguvu, kaka mmoja akavua nguo kwa ajili ya kuanza kazi na kibaya huyo kaka pia na wenzake wote walikuwa waathirika wa virusi vya ukimwi, hivyo na farida nae alikuwa anaelekea huko huko, yule jamaa alivyo maliza kuvua akamshika farida kiunoni maana alikuwa ameshikwa mikono na miguu huku mdomo wake umebanwa, sasa kazi ili kuwa imebaki kwake huyo kibaka kucheza mechi kwa lazima, kipindi sasa anataka sasa kucheza mpira, simu ya farida ndani iliita, nikaichukua kumpelekea sebreni ili apokee maana alikuwa ni baba yake mzazi, dooh wakati natoka nilishangaa kukuta farida yupo anajikaza ili asibakwe, anaangaika masikini wa mungu dahh nilirudi nyuma polepole maana nilijua awawezi kumbaka kirahisi maana farida alikuwa anajivuta mwili sana, nikapigia simu polisi haraka kwa maasikari ili waje kwangu kuwa kamata, mungu saidia kituo cha polisi kilikuwa karibu na nyumbani kwangu, sasa kipindi yule kaka anasema, "tulia mpila uingie, kama hutaki nakuchoma kisu" hapo hapo maasikari wakafika, na mimi nikatoka haraka na kwenda kuufungua ule mlango, walikamatwa wote na mpaka leo hii wapo jela, dahh mke wangu alikuwa amechoka sana maana walimbana sana puani hivyo akapumua hewa kwa shida, ikabidi nimpeleke hospitali, wale vijana wakasema, "tusameeni jamani tulitumwa na mdada mmoja anaitwa elivia," serikari haikutaka kuelewa ikawajibu, "yahani wanaume wote nyie mnambaka mwanamke mmoja,  si bora mngetafuta machangudoa wanao jiuza, yahani mnambaka mke wa mtu alafu ndani kwake, , wajinga sana nyie mtaozea hapa hapa jela" Elivia alipo sikia hizo taarifa alijificha sana masikini hakutaka ata kuonekana,
Alafu Kumbe masikini wa mungu mke wangu farida alikuwa ameumizwa sana mwili maana alikaa hospitalini kama wiki mbili nzima bila kupona, ila mungu saidia wale watu hawakufanikiwa kabisa kufanya lile tendo walilo kuwa wakili hitaji. Kipindi farida yupo hospitalini, aligundulika kuwa ni mjamzito, nilifurahi sana kusikia farida ana mimba maana nilitamani sana mke wangu anizalie mtoto, sasa siku moja nipo nyumbani na mke wangu, mala ghafla nikashangaa geti limefunguliwa, kumbe ni paul amekuja anamuitaji mke wake, alipo fika akasema, "sijafata chochote hapa, nimemfata mke wangu" paul akasema tena kwamba, "farida mke wangu amka tuondoke" farida akasema, "wee nikome kwani ulinitolea maali, we si ulinifukuza kama mbwa pale nyumbani kwako, sikutaki toka kwetu" nikamuuliza paul maana nilikuwa kama sielewi, "we paul hivi kwanini wewe kila ninapo oa unataka kuharibu, ulimchukua elivia nika kaa kimya sasa unamtaka na huyu sio, ebu ondoka paul sitaki kukuona kwangu" paul akasema "naondoka sawa lakini hapa, lazima mke wangu arudi siwezi kukubali farida wangu umchukue, utakufa wewe au mimi sababu ya penzi na upendo niliyo nao kwa farida" baada ya kuongea vile paul aliondoka, farida akaanza kulia akasema, "huyo mwanaume alisha wai kunioa, lakini alinifukuza kwake, simpendi ata kidogo" nikamjibu, "huyo mwanaume aliniibia mke wangu wakanifirisi na kunifanya mambo mabaya, simpendi pia" dahh nilikaa na mawazo sana, mpaka nikaamua kuweka mlinzi nyumbani kwangu ili amlinde mke wangu asifanyiwe ubaya wowote kama nikiwa kazini, na nikaenda kuchukua, RB polisi ili paul akifanya kitu chochote kibaya akamatwe, sasa elivia alipo ona maisha yamemshida akaona ni bora amrudie mungu kwa mara ya pili aokoke awe mtu mwema, kipindi ameenda kwa mchungaji kwa ajili ya kuombewa na kutubu dhambi, mchungaji alianza kumuombea kinafiki, akawa anampa pesa za matumizi, na akapewa sehemu ya kukaa palepale kanisani, kumbe yule mchungaji alikuwa muongo muongo tu maana alimlaghai elivia wakaanza kufanya mapenzi, na alipo mchoka elivia, yule mchungaji akampa elivia elfu ishirini tu ya kuanzia maisha kisha akamfukuza maeneo ya kanisa maana walikuwa wameisha anza kugundulika hivyo kuna baadhi ya waumini wakaanza kukimbia lile kanisa, dahh elivia alichoka ikabidi tu aanze kuuza nyanya sokoni, maana alikuwa na elfu ishirini aliyo pewa na mchungaji, akauza nyanya akipata pesa anakula sehemu yake ya kulala palikuwa ni palepale sokoni kwenye vibanda vidogo, hama kweli alikuwa anapigwa baridi sana usiku elivia akaona hana faida tena ya kuishi duniani, hivyo akaona ni bora kukikucha salama, akanunue sumu ameze afe tu aachane na mateso ya dunia.  usikose sehemu ya 22. Mtunzi frank david whtsapp 0769510060                       
SEHEMU YA 22
MTUNZI FRANK DAVID daktari wa hadithi_Tz, whtsapp 0769510060.                              
Kulipo kucha elivia akanunua sumu kweli ili ajiue, maana alikuwa amechoka sana na maisha, kwasababu ata mwili wake ulikuwa umefubaa sana, ngozi imenyauka, muonekano wake wa urembo wote ukapotea. Dahh sasa wakati ameshikilia ile sumu anataka ameze ili afe, roho ya kujiurumia ikamuingia akaogopa kujiua masikini, ila kutokana na mawazo akashindwa kuendelea na kazi yake, hivyo zile nyanya zikaoza, mtaji wake wote ukakata akaishiwa pesa yote, elivia akasema, "dahh hii mikosi vipi hii, kila ninacho fanya sifanikiwi jamani nifanyeje mimi, ndipo elivia akaanza tabia mbaya ya kukopa pesa za wakina mama wanao jishughulisha pale sokoni akipewa anatumia, alafu hawarudishii pesa zao, akimkopa leo huyu kesho anakopa kule, duuh wale wakina mama wakamchoka, kisha wakamwambia, "wewe elivia wewe, umezoea sasa  we mwanamke, kila siku kukopa kukopa pesa zenyewe tunakupa ila huturudishii, sasa sikia, hatutaki kukuona hapa sokoni, alafu na kwenye hivi vibanda hatutaki kukuona unalala usiku, maana tumesikia tabia yako mbaya kweli kweli, yaani we elivia unalala na walinzi juu ya hivyo vibanda mnafanya ngono usiku, hivi una akili kweli wewe, thamani yako iko wapi, sasa tumekuchoka maana hatutaki mikosi kwenye biashara zetu, yaani kwanzia leo hatutaki kukuona hapa, ondoka kabla hatuja kupiga" elivia huku machozi yakimtoka, akasema, "wakina mama wenzangu, mimi ni mwanamke kama nyie, sina mume, sina ndugu nikitoka hapa nitalala wapi" wakamjibu kwa kumfyonza, "mjinga kweli wewe, kila siku unauza nyanya faida yote unatia tumboni, umeshindwa ata kujiongeza ukapanga chumba, ondoka" dahh, elivia alijiona chizi akajiona kama katengwa na jamii nzima, alitoka pale sokoni na aibu kila mtu anamshangaa, wateja waliokuwepo wakamshangaa pia, ndipo akaanza tena maisha ya kuangaika mtaani, siku moja elivia alikuwa anaumwa sana, maana ule ugonjwa wa kisasa (ukimwi) ulikuwa ukiamka anateseka sana masikini, sasa kutokana na zile baridi za kulala chini ya miti na kulala pia nje ya maduka ya watu wakifunga usiku, siku moja elivia aliumwa sana tumbo, na kibaya zaidi elivia alikuwa ana alisha, yaani kila baada ya dakika kumi elivia ana alisha mpaka damu, aisee tumbo lilikuwa lina msokota sana mpaka akawa analia kama mtoto, wale watu wa maduka wakamfukuza elivia asilale madukani kwao, maana alikuwa aendi sehemu sahii ya kujisaidia yeye popote pale anashusha kinyesi, sasa wale wenye maduka asubui wakija, wanakuta harufu sana pale madukani kwao. Sasa kuna siku moja hivi, njaa ilimshika elivia mpaka akahisi kama anakufa, akamfata kaka mmoja hivi anaitwa Stide, akamwambia, "kaka nina njaa naomba unisaidie" stide akasema, "ehh we dada yaani mi niokote makopo, wewe uje kilaini tu nikupe hela ya kula, kama upo tayari kwanzia kesho tuwe tunaokota makopo kisha tunauza ili tupate hela yako ya kutumia" elivia hakupinga maana ugumu wa maisha tayari alikuwa anaujua, kweli bhana, elivia akaanza kazi za kuzunguka mtaani asubui mpaka jioni, mda mwingine ata usiku pia, anaokota kisha anakusanya mpaka ule mfuko mkubwa ukijaa ndipo anaenda kuuza  kwa bosi kisha anapewa hela, elivia alikuwa anafanya hiyo kazi kisha inapo fika jioni anateseka sana sehemu ya kulala, maana ule mtaa walimfanya kama jamvi la wageni, wale vijana usiku walikuwa wanamsumbua sana, elivia analia lakini wapi hawa muhurumii, wao wanambaka tu masikini, dahh ikabidi elivia  awe rafiki yake sana stide wawe wanalala wote pale pale nje kusudi asiweze kusumbuliwa na vibaka akabakwa tena. Siku moja tupo barabarani mimi na mke wangu farida tukamuona elivia kwa mbali anaokota makopo, mengine kaya ninginiza begani yuko bize kweli kweli, jasho linamtoka na amevaa mabuti makubwa sana, alafu mchafuuu, maana alikuwa aogi hivyo ile harufu ya mwili wake ilikuwa sio nzuri kabisa, Nikamwambia farida kwamba, "baby ebu muone mama wa mtoto wangu alivyo kuwa sahivi jamani," farida akasema "heeee, nini hiki, elivia kafikia huko sahivi, mbona mchafu sana, au kichaa sahivi atakuwa,  yaani amebadilika amekuwa kama bibi kabisa wakati bado ni mdogo yule, tumsaidie mme wangu" nikamuuliza farida, "tumsaidieje sasa maana ata mimi huruma imenishika" farida akasema twende nae nyumbani tu, nikamwambia, "weee! Nikome maana roho ya yule mwanamke naijua mimi, maana ata kipindi sijamuoa nilikutana nae mtaani hivihivi nikamsaidia, ila alini alibia maisha sana huyo binti, siwezi kumpeleka nyumbani" nikachukua elfu 20 kisha nikamwambia mke wangu ampeleke hiyo hela ili japo anunue chakula, farida akashuka kwenye gari kisha akamuita elivia kwa nguvu akasema "njooo ufate hii hela ukanunue chakula ule," elivia alipo sikia hela akageuka haraka bila kuangalia magari upande wa pili kumbe gari lilikuwa linakuja spidi sana, wakati anavuka masikini, gari lilimgonga vibaya mno, elivia alianguka hapo hapo na kupoteza fahamu! Duuh watu walijaa pale ikabidi walio mgonga wamkimbize hospitali, alipo fikishwa kule hospitalini,   kumbe mkono wake wake wa kushoto pamoja na miguu yake yote, ilikuwa imevunjika, hivyo alitakiwa kukatwa miguu maana ilivunjwa na ile gari, maana lile gari lilikuwa spidi sana, elivia alichanganyikiwa akasema, " dokta mimi ni muokota makopo njiani, nitatembeaje sasa bila miguu kutafuta makopo, dokta kama kuna sindano ya kuchoma mtu afe, naomba unichome tu nife, siwezi tena kuishi naomba uni ue dokta" daktari akamwambia, "dada hii sio sehemu ya kuua, hapa tuna tibu tu, hivyo kuwa mpole utibiwe na mambo mengine yatafata mbele kwa mbele" kweli masikini elivia alikatwa miguu yake yote kwanzia magotini kisha akakatwa mkono wake wa kushoto, duh!  Lilikuwa pigo kubwa sana kwenye maisha ya elivia lakini alivumilia hivyo hivyo mpaka akapona, yule jamaa alie mgonga akasema, "dada kwakuwa mimi ndiye nimekugonga, naomba ukakae kwangu mpaka siku utakayo jisikia kuondoka mwenyewe, alafu huko kwangu utakula, utakunywa, hauta teseka kabisa, ila naomba unisamee kwa ajali iliyo tokea, maana bila mimi usinge vunjika" elivia hakuwa na jinsi akakubali kuishi kwenye familia ya yule kaka alie mgonga na gari.
Siku moja paul alikuja kwangu amelewa sana, mlinzi akampiga sana maana alileta vurugu, nilipo toka nje nikamkuta anapigana na mlinzi nikamzuia mlinzi aache kumpiga, paul akasema, "yenda namuomba mke wangu, nataka kumchua mke wangu nampenda, namtaka farida, sitaki chochote paul" nikamuuliza "wewe kila nilie nae unampenda, hivi utapenda wa ngapi, elivia nimekuachia, huyu wa nini sasa, haya utamtunza wapi maana ata nyumba unayo ishi niya kwangu mimi na vibali ninavyo ndani tena mda wowote naichukua hiyo nyumba sasa mtaishi vipi na farida" paul akaanza kulia, yule mlinzi akasema, "bosi huyu amelewa usimsikilize" sasa kwa huruma niliyo kuwa nayo, nilimrudushia paul vibali vya ile nyumba kisha nikasema, "haya sasa vibali vya nyumba tayari nimekupa ila naomba kaa mbali na mke wangu, nimeisha chukua RB polisi ulifanya chochote kibaya utaozea jela nakwambia" paul aliondoka akiwa amenuna sana, kumbe alivyo mpuuzi akatafuta wateja kisha akauza ile nyumba haraka kwa milioni 80, ili atumie hizo pesa kumpata farida upya, baada ya kuuza nyumba paul alipanga chumba kimoja ili aanza mipango ya biashara, paul alikuwa tayari amenunua simu nzuri tu na akajitahidi kubadilisha muonekano wake akapendeza vizuri mtoto wawatu, sasa kipindi yupo pale alipo panga, siku moja paul mida ya saa sita usiku alikuwa anawasiliana na jamaa mmoja hivi mfanya biashara mkubwa anaitwa petron ili wafanye mipango ya biashara. Paul akamwambia petron, "kaka mimi humu ndani nina milioni 70 tu, kesho mapema nakuja hapo kwako tuangalie tunafanya biashara gani" petron akasema, "sawa mr paul tajiri mgumu kufirisika kesho njoo tuangalie hiyo mikakati ili tupige kazi" kumbe wakati paul anaongea hayo maswala ya pesa kubwa kubwa usiku, kuna vijana walimsikia dirishani, hivyo wakaenda kujipanga ili waje kumvamia na kuchukua pesa zote alizo nazo ndani, majambazi walipo fika wakagonga mlango wakisema, "jirani mwema fungua ni mimi jirani yako hapa nina shida kidogo" paul akafungua bila wasiwasi, kipindi yupo mlangoni anafungua wakati anachungulia kumuona jirani alipigwa bonge la kofi la uso, paul akazubaa maana hakutegemea kupigwa yeye alihisi ni jirani, wakati anauliza "kuna nini jirani" paul akaongezewa kofi jingine, kisha akapigwa teke la tumboni, paul alianza kutoka damu mdomoni wakamshika vizuri akapigwa tena ngumi ya sehemu zake nyeti, ndipo wale majambazi wakasema, "tunaomba hizo pesa zote kabla hatuja ondoa roho yako" paul akasema, "jamani nisameeni mimi masikini sina pesa" wakampiga ngumi nzito sana sikioni kisha wakamwambia, "ohhh oky! kumbe unataka kufa ehh, tumekusikia kwa masikio yetu dirishani unaongelea pesa kubwa kubwa mamilioni 70 na kuendelea tunazitaka" paul akasema "zipo benki" kaka mmoja akachomoa kisu akamchoma paul kwenye paja lake, kisu chote kikazama, wakamwambia "toa pesa tuta kuua", paul akaanza kulia akisema sina kitu mimi, ndipo jamaa mmoja akaanza kumchoma machoni na vidole vyake anasukuma macho kwa ndani, huku wenzake wamemshika kwa nguvu sana paul, duuuh paul akasema pesa zipo chini ya kitanda, walipo ziona wakamfunga mikono na miguu kisha wakakimbia, wakati wezi wameondoka ndiyo wapangaji wakatoka kwenye vyumba vyao wakasema, "kaka paul pole sana kwa kuvamiwa, huku mtaani kwetu kuna wezi wengi sana usiwe unaongelea pesa kubwa kubwa hivyo usiku" paul akalia akasema, "ndugu zangu hizo pesa niliuza nyumba yangu ili nifanye biashara, sina nyumba tena wala sina pesa, nimekwisha" dahh wapangaji wa pale wote walikuwa waoga wakiona visu na mapanga, ndiyo maana walishindwa kumsaidia, na wengi pale walikuwa wanawake hivyo isinge kuwa lahisi kumsaidia paul. Ndipo paul akaishiwa nguvu, asubui ilipo fika tajiri petron akampigia simu paul eti, "kaka mbona huji tufanye biashara," paul alishindwa kujibu, akakata simu,  kisha akasema, "pesa zangu zote zilibebwa, nyumba pia nimeuza pesa zimebebwa, lool, kweli vitu vya dhuluma sio vizuri kabisa" ndipo mr paul  akafunga kamba juu ya paa la nyumba ili ajinyonge afe aachane na mateso yote ya dunia. USIKOSE 23.       


SEHEMU YA 23.
MTUNZI FRANK DAVID daktari wa hadithi_tz. Whtsapp 0769510060.                                
Mr paul alipo funga kamba juu, akaweka stuli chini ili akijifunga kamba shingoni apige teke ile stuli kusudi yeye anin'ginie kwa juu afe, Kweli akafunga vizuri kisha akapanda juu ya stuli ndipo akapiga teke ile stuli kisha akanin'ginia juu masikini, sasa kumbe ile kamba ilikuwa imeoza mara ghafla ikakatika! Paul hakufa akaanguka chini, weeh kwa ule uchungu alio usikia kipindi ame nin'ginia hakutaka tena kurudia, akasema, "mhh kama kufa ndiyo hivi, sirudii tena huu mchezo aki ya mungu". Sasa kipindi Elivia bado yupo anatunzwa na yule kaka alie mgonga na gari, Elivia alikuwa ni mtu wa mawazo sana, kila anapokaa analia na kujutia mabaya yote aliyo nifanyia, kuna siku alizidiwa sana masikini maana magonjwa kila wiki yalikuwa yana muandama yeye tu sababu ya mawazo na virusi, yaani Elivia usiku na mchana wote analia, ata wakimpa hela, wakimnunulia nguo hapati furaha kabisa. Siku moja akaja kwangu, nilikuwepo mimi farida pamoja na mtoto wangu, elivia alipo fika tukamkalibisha kwa furaha tu bila kinyongo kabisa, na siku hiyo aliletwa na jamaa mmoja hivi kwasababu elivia alikuwa hajiwezi tena hivyo asinge weza kuja mwenyewe. Kipindi tupo ndani alianza sana kulia, akaliaaaaa yaani alilia sana siku hiyo, nikamwambia, "Elivia nyamaza basi usilie maana ukilia aisaidii kitu", Elivia akajaribu kuacha kulia ili aweze kuongea ila alishindwa kuongea, maana kilio kilimbana sana, yule jamaa alie mleta akasema, "ndugu zangu naombeni msitushangae kabisa, maana Elivia ametwambia nyumbani kuwa, tumlete hapa aje kuomba msamaa, sababu mda wote nyumbani yeye analia tu anakosa raha kabisa ya maisha, na kila tunapo muuliza nini tatizo anasema tatizo ni Yenda mme wake, sasa alivyo sama tumlete hapa ndipo nikaambiwa nije nae mpaka hapa kwako muongee aombe msamaa" nikamwambia, "hamna shida kabisa, kama amekuja kuomba msamaa ni vizuri pia maana alinikosea sana huyu mwanamke, nilimsadia yeye, nika wasaidia wazazi wake kwa moyo mmoja, mpaka nyumba nikawajengea, na huyu elivia alikuwa na matatizo yake binafsi sehemu zake nyeti, nikamtibu kwa ghalama sana mpaka akapona, nilimuamini sana huyu mwanamke lakini alicho nifanyia mimi sitokuja kukisahau, uwezi kuamini huyu mwanamke aliniibia millioni mia nne ndani akampa hawara yake, akanitumia majambazi waka komba duka langu lote, yote hayo nilivumilia tu maana nilijua ni mapito, ila kilicho niuma ni pale alipo muacha mtoto wake ndani kisha akatoroka na kukimbilia huku mtwara, niliteseka sana na mtoto, maana nilikuwa muosha magari, mpaka mda mwingine nilikuwa naenda kazini na mtoto, yote hayo nikaya vumilia nikajua ni mapito pia, kilicho niumiza mimi ni pale yeye na mme wake walipo nitupa shimoni kule msituni, tena shimo lefu sana, ndani ya shimo kuna sisimizi, kuna mizoga, na chakula changu kilikuwa ni mapela yaliyo kuwa yana dondoka kutoka juu upepo unapo piga na kuchezesha mti, maji ya kunywa nilikuwa nakunywa machafu sana mpaka mvua inyeshe, na mvua ikinyesha nalowa sana shimoni, nilipoteza mawasiliano ya nyumbani maana nilikuwa shimoni mpaka mama yangu mzazi akafariki kwasababu ya kukosa matibabu, sasa leo hii wameisha firisika, wana maambukizi ya virusi vya ukimwi, amepoteza viungo vya mwili, ndiyo anakuja kuomba msamaa ili nimuhurumie" sasa wakati nawa simulia machozi yalikuwa yananitoka, farida alilia sana, yule mgeni akaanza kujifuta na kitambaa machozi, elivia ndiyo usiseme, mpaka mtoto wangu pia akaanza kulia alipo tuona wazazi wake tunalia. Elivia akasema, "yenda nisamee, naomba nisamee sana, najutia tamaa zangu za kimwili, niliangalia kulizishwa kimahaba, nikasahau maisha sio ngono tu, yenda nimekuja kutubu leo nisamee dhambi zangu, maana wewe ndiyo ulikuwa mume wa pekee ila sikujua kabisa, nisamee maana nilikuendea kwa mganga akanipa dawa inaitwa shuntama ili ikufanye wewe uwe unanipa hela na kunisikiza chochote ninacho kitaka, lakini sikufanikisha kabisa, maana nilikosea masharti ile dawa ikakufanya wewe uanguke bafuni na kuwashwa sana ngozi yako na ikakubadilisha ngozi ikawa mbaya sana, nisamee maana nilimsingizia mfanyakazi kuwa ndiyo mwizi wa millioni 400 kumbe niliiba mimi na kumpa paul ili tukimbilie huku mtwara tule raha, nisamee yenda kwa kukusabibishia aibu maana ulikuwa umeandaa mipango ya harusi ila nika kuaibisha sana kwa kukuzuia mipango yako ya harusi, hii yote ilikuwa sababu ya paul, nimekuja kutubu mme wangu nisamee, naumia sana yenda maana nilimkimbia mtoto nilie mzaa mwenyewe, sio hivyo tu, nilifanya kosa sana kufanya mapenzi na paul nikiwa na mimba ya mtoto wako, mme wangu natubu kwanza kwako ukinisamee wewe, najua ata mungu ata nisamee, sio wewe tu yenda ata farida pia naomba unisamee mama ata ningekuwa na miguu ningepiga magoti chini, farida unisamee maana nilimuua mtoto wako chumbani kwa kumniga shingo lake kipindi umetoka nje, uchungu wa kuzaa naujua ila naomba unisamee farida, hizi dhambi zangu ni nyingi zimenipa sana mikosi, nimebakwa sana, nimejiuza sana, nime lawitiwa sana mimi, nimetembea na viongozi wa dini, ata wame za watu pia, nimefanya dhambi nyingi sana farida nisamee mama. Mme wangu yenda, sina pa kukimbilia maana wazazi wangu wote wameisha kufa, mimi ni muathirika, nitaishi vipi, yule paul ni shetani sana, ni mtu mbaya sana na amenialibia maisha yangu yote, sina jipya tena urembo wangu wote umepotea, yenda mme wangu, najua umeoa, na mungu alivyo wa ajabu umeoa mwanamke alie kuwa ameolewa na paul, nilijitahidi kumfukuza kwa paul kumbe nilikuwa namtengenezea mazingira mazuri ya maisha bila kujua, mimi siwezi kukubali kuona mnaishi wote kiukweli napatwa wivu sana yenda, endeleeni kuishi salama mimi ni bora tu nife  ili nisiendelee kuwaona, nakufa sababu ya penzi yenda wacha nife tu niondoke maana mimi ni mwanamke nina wivu, ila farida naomba umleee binti yangu vizuri, usimuue kama nilivyo muua wako, maana kila jambo baya unalo mfanyia mtu, kumbe mungu anaona, na malipo sio popote ila ni hapahapa duniani". Baada ya elivia kuongea yale maneno, nilimwambia, "mimi sina kinyongo na wewe nakutakia maisha mema popote uendapo, tukumbukane kwa maombi na Dua"  farida pia akamsamee elivia, baada ya hapo akaondoka, aikupita ata wiki moja tukaletewa daftari ya rambi rambi kuwa elivia amefariki na ameacha ujumbe kuwa amekufa sababu ya kukosa upendo wa mme wake yenda, dahh tulienda kwenye msiba tukaona jinsi elivia alivyo kuwa mwili wake, tuliumia sana maana mwili wake ulikuwa mweusiiiii, alafu umevimba na macho yake yakawa makubwaa, kumbe alimeza sumu mbaya sana masikini.
Nililia kumuona elivia mke wangu nilie mpenda sana zamani amekuwa vile, ila kilicho niumiza zaidi sikumuona paul kwenye msiba wa elivia, wakati ni watu walio kuwa wanaishi pamoja na kwa mda mrefu, sasa kumbe paul kipindi yupo kwake, siku moja mdudu alimuingia jichoni, dahh paul aliteseka sana kumtoa yule mdudu anakajaribu kuchokonoa jicho na kidole ila wapi, mdudu hatoki tu, dahh paul akashindwa kabisa kumtoa yule mdudu, akakosa wa kumtoa yule mdudu maana wapangaji wengine walikuwa ndani na wame zao kuwaita akashindwa kabisa, ndipo akaingiza kichwa chake kwenye ndoo ya maji akatikisa kichwa akiwa amefumbua lile jicho ndipo yule mdudu akatoka, paul aliwaza sana akasema, "dahh farida angekuwepo mke anae nipenda na kunijari angenipuliza jicho wenda mdudu asinge nisumbua hivi, lazima nimpate mke wangu, lazima nimrudie tu, ni bora nife sababu ya penzi, au bora yenda akose na mimi nikose nijue moja" siku zikawa zinaenda tu mi nipo bize na maisha napambana tu ili familia yangu iishi vizuri, sasa kuna siku paul aliingiza mke wa mtu ndani jirani yake wa mlango wa pili, ili afanye nae mapenzi sasa kipindi wapo ndani, yule dada akasahau maana alivulia viatu vyake nje hivyo kila alie pita pale mlangoni alijua moja kwa moja kuwa huyu mtu yupo ndani kwa paul, sasa kumbe yule dada mme wake alikuwa ni dereva wa magari makubwa, yeye akiondoka kikazi, anakaa ata wiki nzima kazini au ata wiki moja nusu, sasa siku hiyo akaja bila taarifa alafu kumbe mke wake yupo kwa paul wanacheza mpira, jamaa alipo fika akakuta mlango wake upo wazi mke wake hayupo, alipo angalia mlango wa paul, akaona viatu vya wazi vya mke wake nje ya mlango  wa paul, dahhh akajua hapa lazima mke wake anafanya tendo baya na paul, jamaa akagonga mlango wa paul, "kho kho kho" paul akamwambia yule dada, "nani tena huyo anatu alibia starehe zetu" yule dada  akamwambia, "kamfungulie mlango umsaidie shida yake hapo hapo mlangoni ila asiingie ndani, maana sijavaa" ndipo paul akavaa taulo kwenda kumsikiliza anae gonga, paul alipo fungua mlango dahhh! Akakuta ni mme wa yule dada, yule jamaa alikuwa msataharabu sana akamuuliza paul kwamba, "jirani mwema, mke wangu umemuona kweli, maana nimetoka kazini nimechoka sana, nashangaa hayupo ndani, alafu mlango kaacha wazi na kaacha mboga jikoni imeungua" dooh paul alichoka sana akaanza kutetemeka kisha akasema, "hapana sijamuona braza labda ukamuangalie haa kule nje nafikiri yupo  pale dukani" yule kaka akasema, "paul mi nahisi mke wangu yupo ndani kwako ana nisaliti mumewe" kisha yule kaka akaanza kulia, "paul akasema hayupo ndani kaka" yule kaka akasema paul angalia hapa chini, hivi ni viatu vyake kavulia hapa nje mlangoni kwako sasa kama hayupo fungua niangalie" kumbe wakati huo wanaongea yule dada kumbe asikii chochote wanacho ongea paul na mme wake, ndipo yule dada akasema kwa sauti, "mme wangu mbona huji nimekumiss mwenzio haaa" yule jamaa akasema "huyo ni nani kaka" akausukuma ule mlango kisha akakuta mke wake yupo uchi, nyeti zake zipo waziwazi, akamuuliza "mke wangu, mimi naangaika silali, natafuta pesa nakupa, unanunua nguo za ndani alafu kumbe una wavulia wanaume wengine sio" dada alizilahi aki ya mungu, maana haku amini lile tukio, majirani wote wakatoka nje paul alikuwa amevaa taulo tu aliona aibu, yule kaka akachukua mizigo yote ya mke wake kisha akaiweka kwenye chumba cha paul, kipindi yule dada amepata fahamu akawambia, "sasa kama mlikuwa mnafanya kwa siri, nimewapa uhuru kwanzia leo muishi pamoja alafu wewe mwanamke sitaki kukuona tena ndani kwangu tena, na uki thubutu kuja nakuua" majirani na watu wa pale walicheka sana paul pamoja na yule dada,  ilikuwa ni aibu sana masikini, yule mwanamke akaona awezi kuvumilia ile aibu, alibeba vitu vyake kisha paul akampa nauli, yule dada akaondoka tangu siku hiyo hakujulikana ameenda wapi na hakuonekana tena. Sasa kutokana na paul kufanya vile ikabidi mjumbe amuite ili amshauri, akamwambia, "paul hii tabia yako ya kuchukua wake za watu sio nzuri kabisa, hivyo kama unataka kukaa kwa amani na sisi tunaomba utafute mke ndani ya hii wiki alafu oa wewe ni mtu mzima oa" dahh ndipo paul akapata wazo la kuja kumchukua farida, amtoe kwangu kwa nguvu zote ili akaishi nae yeye. USIKOSE SEHEMU ya  24                                                                        
SEHEMU YA 24. MTUNZI FRANK DAVID, daktari wa hadithi_tz. Whatsapp 0769510060.                                 Paul alikaa akawaza sana kwamba, "mjumbe ameniambia nioe, na sasa hivi sina pesa kabisa ndani, na nisipo oa ina maana nitafukuzwa huu mtaa, je ni mwanamke gani atakubali kuishi na mimi katika hii hari, sina pesa sina chochote kinacho eleweka ndani, ata jiko lenyewe sina nafanyaje sasa,dahh hapana yenda atanisamee tu lazima nimpate farida wangu, maana huyo ndiye mwanamke nilie ona mvumilivu wa raha na dhiki" sasa siku moja mimi na mke wangu tupo nyumbani usiku tunaongea, nilikuwa nalalamika sana kuhusu paul, nikamwambia mke wangu kwamba, "yaani yenda akili zake hazipo sawa kabisa yule mtu, alimtoa elivia mtoto wawatu kwao, akamleta huku Mtwara, sasa bahati mbaya elivia amefariki, huyu  paul ameshindwa kumpeleka elivia akazikwa kwao, duhh elivia masikini amezikwa na watu ambao ata sio ndugu zake imeniuma kwakweli, angalau basi paul angefika ata kwenye msiba ingekuwa afadhari kidogo" farida akasema, "mme wangu paul tabia zake mbaya sana, mimi alinifukuza kwake kama mbwa, maana marehemu Elivia, alikuwa anampa maneno ya uongo na yeye anaamini tu, hajielewi yule mwanaume, ata mama yangu ataki kumuona wala kumsikia kabisaaa" kumbe wakati sisi tunamuongelea paul, na yeye kule alipo anawaza jinsi ya kuja kunivamia kwangu, ili amchukue mke wangu aondoke nae. Siku moja mchana kipindi nipo kazini sina habari yoyote ya nyumbani, kumbe mr paul alivamia kwangu masikini, alikuwa amekuja na panga pamoja na wembe kwa ajili ya kumchukua farida kwa nguvu ili akaishi nae. Kipindi paul amefika kwangu, alijua mimi mda huo sipo nyumbani nitakuwa kazini, hivyo akaja kwa mashambulizi ya kupambana na mlinzi wangu, nilie muweka kwa ajili ya kumlinda farida asichukuliwe na mr paul, sasa mlinzi wangu siku hiyo alijisahau masikini, kumbe mlinzi alikuwa katika mahusiano ya mapenzi na dada wangu wa kazi, hivyo kwasababu mimi nilikuwa mida ya mchana sipo, kumbe yeye anautumia huo mda kufanya mahaba na binti wa kazi, maana farida alikuwa mjamzito na mda mwingi yeye alikuwa analala sana, sasa wakati mlinzi yupo kwenye chumba chake karibia na getini anafanya lile tendo, paul akapata upenyo wa kuweza kuingia mpaka sebreni, paul alivyo kuwa pale sebreni akakuta farida hayupo yupo chumbani kalala, alafu ubaya zaidi mtoto wangu nilie zaa na elivia alikuwa pale sebreni anachezea vidori vyake, hivyo paul kwa sababu hakumuona farida akamchukua mtoto wangu na kuondoka nae mpaka kwake. Mke wangu alipo amka akakuta mtoto hayupo sebreni, vimebaki vidori tu, akashangaa! "Ehhh, mtoto yuko wapi" akamuita binti wa kazi, kisha akamuuliza, "mwanangu yuko wapi" binti akasema "dada mimi nilikuwa hapo nje mtoto yupo ndani sijui alipo" dooh farida akachanganyikiwa kabisaa masikini akasema, "jamani mtoto ameenda wapi sasa, sasa mimi namwambiaje mme wangu mtoto wake alipo, tutaonekana wazembe humu ndani, mimi wewe pamoja mlinzi, mtoto mdogo anapotea tupo ndani" ndipo wote wakaanza kumtafuta, wakatafuta, wakatafutaaa, ila hawakumpata, wakapita kwa majirani wote, mtoto hayupo, lool, farida alichoka akaanza kulia, binti wakazi nae akaanza kulia, mlinzi akasema, "nitamwambia nini bosi wangu mimi, nitafukuzwa kazi mimi, nitakula wapi tena jamani" dahh baada ya masaa kama mawili, farida akapiga simu analia, "mme wangu nisamee" nikamjibu "nikusameee?, nikusamee nini" farida akasema, "njoo nyumbani maana mtoto amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha" dooh sikuchelewa, hapohapo nikarudi nyumbani haraka sana, nilipo fika nikawauliza, "jamani mtoto amepoteaje, wakati watu wazima mpo ndani, mtoto wangu nimemzoesha kukaa sehemu moja mimi, sasa mnataka kusema ameisha anza kuruka ukuta wakati mtoto bado mdogo ata ajielewi, mke wangu mbona sikuelewi, we binti ebu niambie mtoto alipo, na wewe mlinzi nimekupa kazi nzuri, nakulipa vizuri, unaishi hapa kama ndugu yangu, inakuwaje mtoto anapotea na wewe upo hapa" kila mtu alikuwa kimya familia imekaa kwenye huzuni, nilichoka nikaishiwa nguvu kwenye miguu hapo hapo nikalala chini, nililia kama mtoto nikisema, "jamani mwanangu nimeangaika nae sana, mama yake alimtelekeza akiwa mdogo mno, niliishi nae kwa tabu sana, sasa iweje apotee mpo ndani, kama mwenyewe niliweza kukaa nae hakupotea, sembuse nyie watu wazima wote humu ndani, watu watatu mtoto anawapotea vipi" nikasema kama "mna nitania naomba punguzeni matani, maana hapo mtakuwa mmezidi" kila mtu akaanza kulia pale, dooh nikajua hapa kweli sio utani mtoto kweli kapotea" nikamwambia mke wangu kwamba, "najua elivia alikuulia mtoto wako, ila naomba kama ume muua ili ulipize kisasi niambie ili nisiangaile kumfukuza" mke wangu alichukia sana akasema, "yenda mme wangu umefikia huko, sasa mimi nimuue mtoto amefanya kosa gani, kumbe tunavyo kaa humu ndani huniamini sio, yenda kama huniamini ni bora niondoke tu nirudi kwetu maana siwezi kuishi kwa raha bila amani, sababu hayo maneno yako nimachungu sana mme wangu" farida akaanza kulia upya. Nikamwambia "hapana  sija maanisha hivyo, mimi niliuliza tu mke wangu, maana tatizo kama hili limetokea, nilazima nijiulize mambo mengi kichwani" niliwambia wote kuwa, "kama mtoto amekufa basi tumuachie mungu tu, ila kama hajafa naamini mungu atatusimamia na tutampata mtoto" ndipo nikaenda kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi, nikapeleka matangazo makanisani na misikitini, ili wanitangazie mtoto wangu kuwa amepotea na atakae mpata tutampa zawadi ya millioni 2, sikufanikiwa kabisa, nikaamua kupeleka taarifa kwenye radio, nikatangaza pia na zawadi juu, ila hatukumpata, ndipo nikapeleka taarifa kwenye taarifa za habari mbali mbali za (TV) ili tuonyeshe picha za mtoto nikaweka na zawadi juu ili atakae mpata mtoto amlete, sikufanikiwa kabisa yani, dahhh nilichoka, pesa nilitumia nyingi, kazi zangu zikakwamakwama, familia yangu ikakosa furaha kabisa, ilikuwa ni tabu sana. Nikasema, "si bora tu nijue kama mtoto wangu amekufa nimzike, kuliko sijui yuko wapi anafanywa nini" watu walikuja kunishauri kwangu mambo mengi sana maana nilipungua ata mwili, sina amani sina raha, wengine wakasema, "kaka huku kwetu kuna wachawi wengi, mtoto wako kachukuliwa kishirikina, nenda kwa waganga kaka" dooh sikulitendea haki ilo wazo, wengine wakasema "ndugu yangu mwanao ameisha fariki cha msingi wewe msahau fanya kazi, mke wako ni mjamzito atakuzalia mtoto mwingine" dahhh liliniuma sana hilo wazo, sikulitendea haki pia, kumbe kuna watu wengine walikuwa wanasema kwamba, "huyo yenda ni mshirikina, kamtoa mtoto wake kafara ili apate pesa nyingi alafu anajifanya tu" ila wazazi wa farida pamoja na prisca, walinipa moyo kwamba nisikate tamaa, niombe sana mungu na nimtafute mtoto nitampata tu popote alipo, kweli na mimi nikawasikiliza wao.
Sasa kumbe kipindi chote hicho mimi naangaika, kumbe paul alikuwa amemficha mtoto wangu ndani hamtoi nje wapangaji wakimuuliza mtoto wa nani anasema wake, kibaya zaidi paul alikuwa hampi mtoto chakula vizuri, mtoto akabadirika kutoka rangi yake nyeupe mpaka akaanza kuwa mweusi, maana alikuwa hamuogeshi, mwezi ukapita mtoto habadilishiwi nguo, chakula anampa mala moja tu kwa siku, mtoto wangu alikonda masikini, mtoto akaanza kutoa harufu mbaya sana maana ata nguo ambadilishi, kama akijikolea ata kama haja kubwa hamtawazi mtoto, paul anakaacha hivyo hivyo pale chini kwenye sakafu ya baridi kanalala tu, katoto kanaliaaaa, kakilia sana, paul alikuwa na radio ndani, akawa anaiwasha sauti kubwa ili wapangaji wasisikie, paul hakuwa na huruma na hakujua kama yule ni malaika hapaswi kuteswa, ila yeye mda mwingine usiku mtoto wangu akilia anampiga makofi kichwani, usoni kila kona kwa hasila eti kwamba ana muaribia usingizi, paul alifanya ujinga sana masikini hakujua kama ni dhambi, siku moja paul alishika kisu usiku kama wa saa tisa ili amtoboe mtoto shingo amuue, maana paul aliwaza kwamba, "siwezi kumuona yenda anafanikiwa na huyu mtoto, wakati ameniibia mke wangu na kibaya zaidi huyu mtoto ni wa elivia, alafu huyu huyu elivia alimuua mtoto wangu akiwa mdogo sana,  hivyo na mimi namuua leo huyu tukose wote kwa sababu mtoto analia kila mda, naangaika kumlisha chakula kama vile ni wangu," kipindi paul anataka kumchoma mtoto na kisu, mlango wake ukagongwa, akaficha kile kisu, kisha akaenda kumfungilia alie gonga, kumbe alikuwa ni jirani yake alie mfumania paul na mke wake, paul akamwambia "karibu" jamaa akasema "paul naomba unisaidie kisu maana kuna matunda humo ndani nataka kula alafu kisu changu sikioni kabisa aisee," paul akasema, "dahh kaka unakula matunda usiku wote huu, haya sawa, chukua kisu hichi hapa" kisu kilivyo toka nje, akaacha kumuua mtoto wangu, cha kushangaza na kuumiza paul akamchukua yule mtoto kisha akampandisha juu ya mwili wake eti anamgandamiza hili alizishe hisia zake za mapenzi, huku akisema, "elivia amenizalia mke" bora ata hivyo kibaya zaidi ni pale paul alipo kuwa akipanua uke wa mtoto wang mdogo jamani, huku anamtukana kwamba "kwanini unajikojolea mpuuzi kweli we mtoto" hama kweli kuna watu wana laana duniani. Mimi sikuchoka nikaanza kuzunguka nyumba na nyumba kuulizia mtoto wangu, maasikari pia walinipa msaada wao, nilianza kuzeeka nikiwa kijana, sababu ya mawazo, nikasema kuwa, "mtu yoyote atakae leta mtoto wangu nampa mali zangu zote," farida alipungua sana masikini na kipindi hicho ana mimba, sikuwa na raha kabisa mimi, chakula kilikuwa hakipiti, nikila kidogo nashindwa, nikilala usiku sipati usingizi kabisa, niki jaribu kulala nashindwa, nikipata usingizi kidogo mawazo yana niijia kwamba "je mimi nalala mtoto wangu yeye amelala?, au je mimi na cheka mtoto yeye pia anacheka" wachungaji na mashee walinifanyia dua na maombi ila sikupata jibu, niliwambia watu kwamba "msiombe mpotelewe na mtoto isikie kwa mwenzako tu" dahh maisha yangu nilianza kuyaona ni magumu sana, hivyo nikaugua vibaya sana, nilipo pelekwa hospitali nikaambiwa kuwa nina vidonda vya tumbo pamoja na kisukari, dahh sema kweli nilichoka maana ata vyakula vyangu vilibadilishwa nikawa sili vyakula kama wenzangu vyenye mafuta na sukari, ila hii yote ilikuwa ni sababu ya kumkosa mwanangu kipenzi. Sasa siku moja mchana nilikuwa nyumbani, Paul akanipigia simu kisha akasema, "Yenda, yenda, yenda, adui wa maisha yangu, pole sana kwa kumpoteza mtoto, pole sana kwa mawazo, pole na ghalama zote hizo ulizo tumia, napenda kukwambia kwamba, mtoto wako nipo nae mimi, na nipo mbali sana, huwezi kupajua, sasa kama unamtaka mtoto wako, naomba unirudishie mke wangu farida kwanza, na ukichelewa tu, mtoto wako atanifia ndani mimi,  maana anaumwa sana, maana sina pesa ya matibabu mimi,  sasa ukichelewa akafa, mimi  namtupa shimoni alafu napotea, maana kwanza nimeisha choka na maisha" nikamwambia "nitaamini vipi kama kweli upo na mwanangu kaka" paul akamfinya mtoto kwanguvu kwenye kitovu, mtoto alilia sana masikini, nilipo sikia sauti yake analia dooh nikaamini. Dooh nilipumua kidogo, pale nilipo sikia sauti ya mtoto wangu, paul akasema, "umemsikia ehh"  nikatamani kwenda polisi, ila niliogopa kwamba, nikisema popote paul anaweza kumuua mtoto, ndipo nikamwambia, "paul sasa mke wangu ana mimba nitakupaje hivyo hivyo, naomba unipe mtoto mimi nitakupa chochote unacho kitaka, naweza kukupa ata fedha, lakini usimuue mwanangu, paul alipo sikia hela na alikuwa kwenye wakati mgumu akakubali, ndipo akasema tukutane sehemu ili anipe mtoto nimpe hela, ila akasema nikienda na polisi atamuua mtoto na yupo tayari kwa lolote lile, dahh kweli nikachukua millioni 6 kisha nikaenda nazo, nilipo fika nika mkabidhi pesa, ndipo paul akanipa mwanangu. Ila nilihisi kuchanganyikiwa nilipo muona mtoto alivyo konda, alivyo badilika rangi, alivyo kuwa ananuka, nguo alizo potea nazo, ndiyo hizo hizo, karudi nazo. nikamwambia paul "wewe sio mtu paul,  wewe ni gaidi, na ukirudia kufanya hivi kwenye familia yangu nitakufanya kitu kibaya,"  paul akacheka kama mafia,"hahahahaha"  kisha akaondoka, ndipo nikamchukua mtoto haraka haraka, nikamkimbiza mpaka hospitali, maana alikuwa mnyonge sana, na amekuwa na jotooo, nilipo fika hospitalini binti wa kazi akaja, hivyo nikamuacha binti wa kazi pale amuangalie mtoto akiwa anatibiwa, huwezi kuamini mtoto hakukaa ata siku mbili masikini wa mungu, na yeye alifariki dunia, na kumfata marehemu mama yake mzazi. USIKOSE YA 25.                       
SEHEMU YA 25.
MTUNZI FRANK DAVID daktari wa hadithi_tz, whtsapp 0769510060.                              
Baada ya mwanangu kufariki nilihisi kuchanganyikiwa kabisaa, kwasababu, pesa nilimlipa paul ili mtoto asife, alafu kumbe paul ali mlea mtoto wangu vibaya mpaka akapata maladhi yaka muua, kwahiyo nilipoteza vyote, pesa pamoja na mtoto, ohhshh nilichoka, nikajutia sana usitaharabu wangu, maana ni bora kama ningeenda na ma polisi wangenisaidia kumkamata mr paul afungwe kwa kosa la kumuua mtoto wangu na kumteka pia. Msiba wa mtoto uliisha salama lakini tulimzika pembeni na kaburi la mama yake kule makaburini, maana vifo vyao vilifwatana, hivyo sikuwa na jinsi kabisa ya kufanya, nilikaa na mawazo kwa mda mrefu sana, nawaza jinsi ya kulipiza kisasi kwa mr paul, maana hivi vifo vyote alivisababisha yeye kitendo kilicho nikela sana, ila watu walinishauri kwamba, "muache tu huyo paul hajielewi kabisa, muachie mungu Yenda, maana yeye ndiyo anae jua kila kitu, na siku zote lolote litokealo ni mipango yange mwenyewe" sikuweza kuwaelewa maana uchungu wa mwanangu nilikuwa naujua mimi, hakuna mwingine. Farida alikuwa karibu sana na mimi, anajaribu kuni poza ili nikae sawa, ubaya zaidi, kisukari  kilikuwa kinapanda kila siku, na tumbo lilikuwa lina nisokota sana kwasababu ata hamu ya kula sikuwa nayo na nilikuwa na vidonda vya tumbo. Sasa kumbe mtoto alivyo fariki paul akawa kama akili imeruka, ukimuangalia unamuona kama ni mtu mwenye akili zake lakini kumbe hayupo sawa kabisa, maana siku moja aliamka asubuhi akajiandaa kisha akaenda kwenye ile nyumba yake aliyo uza, eti akawambia kwamba wampatie nyumba ni yake na yeye hajawauzia, wale watu walimtukana sana, wakamletea hati na barua za makubaliano ya kuuza nyumba, paul alipo shika yale makaratasi akaya chanachana akisema kwamba, "nyumba sijauza, na hii mikaratasi yenu ya mia mia hamuwezi kuifananisha na ghalama ya nyumba yangu" wale watu wakamuona kama paul ni chizi, maana walimkalibisha vizuri wakijua ni kama ndugu sababu walisha fanya biashara ya kuuziana nyumba alafu anataka kuwageuka, wakamfukuza kwa hasila sana paul akakataa kutoka eti anawambia wao ndiyo waondoke nyumba ni yake, wakaanza kumpiga paul, dahh paul akasema "kumbe hamnijui sasa subili" kweli masikini, paul akafata panga aje kuwakata, alipo rudi wale vijana walipo muona ana panga, wakakimbia kwenda ndani, kisha wakafunga mlango, sasa ule mlango pia ulikuwa na komeo la kubana kwa nje, paul akawafungia ndani humo humo, sasa kwa sababu nilikuwa nimempa pesa kwa ajili ya kunipa mtoto wangu, sasa yeye alipo wafungia wale ndani, akatumia ileile pesa kwenda kununua petrol ili aje kuchoma ile nyumba, ili wale watu wafie humo humo ndani, kipindi anaenda kununua petrol, wale wakaanza kuwapigia watu wao simu, ila wale vijana kila walie mpigia aje kuwasaidia alikuwa hapokei, paul alivyo rudi akamwaga petrol maeneo ya ule mjengo kisha akaweka lile dumu la petrol mlangoni, wakati anafata kiberiti dukani, kama bahati wageni wakawa wamewasili pale siku hiyo kusalimia, na kuwapa hongera ya kupata nyumba, daaah na hiyo ndiyo ikawa pona pona ya vifo vya wale vijana. Pamoja na ile nyumba kuteketea. Sasa mimi baada ya mtoto kufariki ikabidi niende kutoa taarifa kituo cha polisi ili Paul aweze kukamatwa, ndipo wale maasikari wakamtumia barua  paul kuwa anaitajika kutuo cha polisi kwa kesi ya mauaji pamoja na kumteka mtoto, paul ikabidi atoroke, alipo kuwa anakaa kisha akaamia sehemu ya mbali kidogo ili asipatikane na sijulikane kabisa, siku moja paul aliugua sana maana na virusi vilikuwa vina msumbua sana, alikuwa ana jisaidia aja kubwa ya majimaji kila sasa, chakula hali, nguo habadilishi maana hawezi na hana msaada kabisa ndani anaishi mwenyewe tu, dahh baada ya kupata nafuu kidogo akaamua kwenda hospitali ndipo akawapewa dawa zikamfanya apate nafuu,
Watu wa ule mtaa paul alio ama walifurahi sana, sababu walikuwa hawampendi, maana yeye alikuwa mkorofi na mwenye majivuno, anapigana anavyo taka, mpaka anapiga wame za watu wana aibika mbele za wake zao jamani. Sasa mtaa alio amia walikuwa hawamjui tabia zake kabisa, ila mungu saidia siku moja usiku paul amelala, alibanwa na haja ndogo hivyo akaenda chooni na choo ilikuwa nje ya chumba hivyo ilikuwa ni lazima atoke nje tu kwenda msalani,, sasa alivyo toka tu kuna kijana ule mtaa alikuwa ni mwizi sana, akaingia haraka kwenye chumba cha mr paul akachukua begi lake lote akatoroka nalo ili aibe nguo akauze, alipo fika akafungua lile begi, huwezi kuamini, akakuta millini 4 na nusu ndani ya begi ambayo paul alikuwa amebaki nayo, kwenye ile pesa niliyo mpa, paul alipo rudi ndani hakugundua kama ameibiwa yeye alilala tu, kesho yake asubui ameamka anaangalia begi ili achomoe pesa kidogo ya matumizi, akakuta halipo, dooh akahisi labda ni usingizi akalala tena kidogo, lakini alikuwa ameisha ogopa maana alikuwa hana ata mia mfukoni, wazo lake pesa zipo kwenye begi, paul alipo amka akafumbua macho tena hakuliona begi, hakutaka kuamini kama begi halipo maana ndiyo lilikuwa uhai wake, yaani bila zile pesa paul asingeweza kufanya chochote kile, ikabidi paul afumbe macho ili asione kama lile begi alipo, kisha akaanza kupapasa kwa mguu sehemu ambapo lile begi lilikuwepo ili aliguse, dooh akakuta kweli hamna, paul alipiga yowe, "uuuuuwii, uuuuwii, uuuwii" kama mala tatu hivi maana hakuamini, akatoka nje haraka, jamani alie iba begi langu anirudishie, watu wote kimya, majirani wakamuuliza kaka mbona kelele asubui yote hii, alafu umetoka nje hujavaa ata nguo, umavaa nguo ya ndani tu, wake za watu wapo hapa watoto wapo hapa, ebu kavae nguo paul, ndipo akarudi ndani kuvaa nguo, maana alijisahau kabisa kuvaa, kibaya zaidi nguo zake zote ziliibiwa ndani ya sanduku, hivyo alikuwa amebaki na nguo moja tu aliyo kuja ameivaa, paul aka anza kulia, "nimeibiwa begi langu, wameiba nguo zote pamoja na millioni nne na nusu zangu" wale wapangaji wakamshangaa sana kwamba, "yaaani wewe kaka unaweka hiyo pesa yote kwenye begi, haukuwa na uchungu wa hiyo pesa ehhh, huu mtaa wetu una vibaka wengi sana, hiyo pesa huwezi kuipata tena" paul alijihisi kufa masikini  akaingia ndani anawaza sana, ila wale watu wakamuonea huruma wakawa wanampa chakula wakihisi ni mtu mwema, baada ya wiki wakamchoka kila mtu akamnyima, wakamwambia  oa mwanamke wako aje kukupikia chakula sisi hatuwezi tena", sasa paul kila alipo ambiwa jambo kuhusu mke wa kuoa, yeye alikuwa anamkumbuka farida, hivyo paul akaanza kujipanga kwa ajili ya kumchukua mke wangu kwa nguvu zote na kumleta pale kwake ili aishi nae.
Sasa mimi baada ya matatizo yote yale kutokea, niliamua tu kuwa mpole ili nitafute pesa kwa ajili ya familia yangu, nashukuru mungu kweli biashara zangu zilikuwa zinaenda sawa na pesa ilikuwa inapatikana. Sasa kumbe paul alikuwa amejiandaa na siraa mbali mbali kwa ajili ya kuvamia pale kwangu ili amchukue mke wangu kwa nguvu ampeleke huko kwake pasipo julikana ili amu oe, na wala paul hakuwa na akili ya kujiongeza kuwa farida wangu ni mjamzito yeye alisema atakaa nae hivyo hivyo tu, sasa kipindi paul ameisha fika maeneo ya nyumbani kwangu, yupo anawaza ataingiaje ndani kupambana na mlinzi, akashangaa kumuona farida anatoka nje amebeba mfuko mweusi kuja kutupa nje takataka maana nje ya geti ndiyo kulikuwa kuna shimo la takataka, nilitamani sana kama labda binti wa kazi ndiyo angekuja kutupa taka, lakini mke wangu alikuwa ni mtu wa kusaidiana kazi hakuwa mzembe ata kidogo, sasa paul alipo muona alikimbia kisha akamziba mdomo alafu akamuwekea kisu shingoni na kumwambia kwamba ukiongea tu ata kidogo nakuua, paul akaanza kumvuruta anapeleka haraka haraka farida nyumbani kwake, farida akalazimishwa kwa nguvu masikini akiambiwa "twende kama hutaki nakuua, mm ndiye mme wako sahihi twende" mlinzi ndani akashangaa mbona farida harudi ndani, alipo toka kuangalia akakuta hayupo kuna mtoto mdogo akamwambia, "polisi polisi" maana mlinzi wangu alipenda kujiita polisi, kale katoto kakasema, "dada yenu amewekewa kisu shingoni na ametekwa wamepita hapo" dahh mlinzi ikabidi aanze kumtafuta farida, binti yangu wa kazi akashangaa wenzake hawapo na hawaja muaga na yeye akatoka nje pia, kale katoto kakamwambia hivyo hivyo, binti nae akaenda kumtafuta, mimi nilipo rudi nyumbani, nikagonga sana honi ila sikufunguliwa geti ikabidi niingie ndani nikashangaa, watu wote hawapo na simu zimeachwa ndani, moyo ulidunda nikaogopa sana maana sikutegemea kabisa, kumbe paul alikuwa anamvuluta mke wangu kwa nguvu anampeleka kwake wakati mke wangu ni mjamzito, farida alichoka kupandishwa kilima ikafila hatua akaanguka chini, na mda huo huo mlinzi wa nyumba yangu akawa amefika, paul akamwambia, "umefata nini hapa" mlinzi akasema, "kaka kumbuka nipo kazini nimepewa jukumu la kumlinda huyo mwanamke naomba niondoke nae" paul akachomoa kisu, mlinzi akashtuka maana hakuwa na siraa yoyote ile, paul akamwambia kama unaweza mchukue, mlinzi akakaa kimya tu, mda huo huo binti wangu wa kazi akawasili akasema, "dada farida umekuwaje" paul akasema "shiiiiiii kama kimya" mda huo farida amechoka sana alafu tumbo likaanza kumuuma masikini, sasa mimi nyumbani nikaona hamna mtu nikahisi wote wameisha tekwa na mr paul, hivyo nikaenda polisi kisha nikachukua mapolisi watano tukaanza msako mtaani, binti wangu wa kazi akaanza kupiga kelele "mwiziii mwiziiiii mwiziiiiii tusaidie" watu wakatoka haraka kisha paul akawaonyeshea mlinzi kwamba ndiyo mwizi, mlinzi alipigwa sana maana kulikuwa na kelele hivyo yule binti wa kazi akashindwa kabisa kutetea, kwenye wale vijana walio kuwa wana mpiga mlinzi, baadhi yao walikumemo wale ambao paul aliwauzia nyumba na alikuwa anataka kuwachomea ndani, wakasema jamani mtu mbaya sio huyu ni huyooo, mlinzi alikuwa anatokwa damu kila kona, ila hakufa lakini maumivu aliya pata, watu wakasema mbona huyo yupo na mama mjamzito, paul akasema mimi sio mwizi mimi ni baba wa familia, na huyu ni mke wangu, wakati anaongea vile mapolisi walikuwa wamepata taarifa kuwa kuna vurugu pale hivyo tukaenda pale kuangalia labda ninge mpata mke wangu, kweli tulipo fika nikashangaa kumkuta farida amelala chini hana nguvu mlinzi anatokwa damu, binti wa kazi analia, nilipo ambiwa ameitiwa mwizi sikuamini kabisaa, nikaamua kusema ukweli kwamba, "huyu kijana ni mlinzi wa nyumba yangu, alafu huyu dada hapa chini ni mke wangu, na huyu paul mnae mjua kama tajiri sahivi kafirisika sana amekuwa jambazi, ameniulia mtoto maana alimteka hivi hivi mpaka mtoto akafariki, sasa amemchukua mke wangu pia akamuue " paul akasema "ni muongo huyu  ni mke wangu nampenda sana mimi, nipo tayari kufa ata sahivi kwa sababu ya upendo kwake"  watu wakamuuliza farida, "nani mme wako hapo" farida akaniangalia mimi kisha akaninyooshea kidole, dooh kaka mmoja alikuwa na panga alienda akakata mguu wa paul ukapinda, mwingine akabeba jiwe zito akalidondoshea kichwani mwa paul, kipindi watu wanampiga mr paul, kuna mama alikuwa anapitisha kuni kubwa kubwa pale za kuuza, watu walimnyan'ganya kisha wakaanza kumpiga kichwani mr paul na zile kuni, paul alisimama akashindwa mguu tayari umelegea, akasema, "naumiaaaa, nisameee" kila mtu akawa anapiga anapo pataka, ma askari wakaanza kuzuia wanachi wakagoma, paul akasema "Farida mke wangu nakufa sababu ya penzi lako farida,  nakupendaaaaaa, nakufa sababu ya penzi farida😥😥" walimpiga sana siku hiyo, maana walimchona na miti machoni hivyo akaanza kupoteza taswila, kipigo alicho pata kilikuwa kikubwa, alianguka chini akalala kimya, tukazani amekufa, wale maasikari walishindwa kusaidia wakaondoka zao pale maana walikuwa wamemchoka sana paul kwa tabia zake, ila wakasema "msimuue adhabu imemtosha" baada ya dakika chache paul akatikisika, daah watu wakasema huyu kakaa mbona ana roho ngumu hivyo, paul alibebwa akiwa mzima mzima mpaka makabulini, wakachimba shimo vijana, kisha wakamzika paul akiwa mzima na anapumua, kipindi wanamfukia mchanga alilia sana, ila alizikwa hivyo hivyo, serikari ilivyo gundua mtu kazikwa mzima mzima, mapolisi wakaja wengi na mabomu ya machozi raia wakakimbia, paul akafufuliwa ila masikini wa mungu akakutwa amefariki tayari, ndipo akazikwa upya.
Mimi na familia yangu tukaanza maisha mapya yenye mafanikio, mke wangu alijifungua mtoto wa kike, anafanana sana na malehemu mwanangu, tulipendana sana mpaka sasa tupo vizuri na kwenye familia ya upendo na amani teletele.........
MWISHO
MTUNZI FRANK DAVID.
STORY IMEZAMINIWA NA HADITHIZETU. TUNAPATIKANA KWA +255769510060                       


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only