SEHEMU YA KWANZA
Maisha ni zawadi tunayo pewa wote na mwenyezi Mungu!
maana hakuna ata mmoja anaelipa pesa mara tu pale anapo kuwa amezaliwa. Lakini
hayahaya maisha yanaweza kukufanya wewe ujutie kwa nini uliletwa hapa duniani.
Sasa mnamo mwaka 1995, kijana Alexander alionekana
kuwa kijana mchapakazi, mwelevu, alikuwa mwenye heshima, na alipendwa na kila
mtu kule kwao.
Lakini siku moja jamani, alexander aliumia sana
nakujutia kwanini alizaliwa duniani. Maana ilikuwa ni siku ya jumamosi siku
ambayo alexander na mama yake mzazi pamoja na bibi kizaa mama yake walikuwa
wote nje ya nyumba pembezoni kabisa ya
mlango wakiwa wote wanakula mahindi ya kuchemshwa na wakiwa wanafurahia kwa
pamoja.
Mama yake alexander akasema,
"Jamani mimi ngoja niwaache maana tayari
nimechelewa kwenye shughuli zangu"
Wakamjibu "sawa we wai maana leo
umechelewa"
Mama alexander akasema,
"Haya sawa, lakini alexander mwanangu mkimaliza
kula mahindi kusanya vigunzi pamoja kisha ukavitupe visizagae ovyovyo hapa
nje."
Alexander akajibu "sawa mama nitafanya
hivyo"
Baada ya mama yake kuondoka alexander akajisahau
baada ya kula muhindi wake kigunzi akaanza kukichezea kwa kukirusha juu na
kukidaka.
Sasa alipo kosea kudaka kumbe kigunzi kikawa
kimedondoka na kuangukia upande wa pili pale pale nyumbani kwao.
Sasa wakati alexander ameenda kuchukua maji ya
kunywa ndani, bibi yake masikini akawa amebanwa na haja ndogo, ndipo akaamka
polepole maana alikuwa ni mzee tayari, sasa wakati anatembea kuelekea chooni,
masikini mguu wa kushoto wa yule bibi ukawa umekanyaga kile kigunzi ndipo bibi
akawa ameteleza vibaya na kupasuka kichwa na kufariki hapohapo. Sasa alexander
wakati anachukua maji akasikia kishindo kikubwa nje! alipo toka nje akakuta
jamani bibi yake ameanguka na anatokwa damu masikioni, puani, mdomoni na akawa
amepasuka vibaya sana kisogoni! Alexander alipo enda kumtazama alishangaa sana
kuona tukio kama lile, alipo jaribu kumuita kwamba "bibi amka bado
nakupenda bibi" hakuamka masikini.
Alex alipo angalia kile kigunzi kilicho mdondosha
bibi dohh ni yeye alikitupa pale
na mama yake aliacha amemuelekeza asitupe vigunzi
ovyo. Ndipo alex akaamua..
USIKOSE SEHEMU YA PILI
SEHEMU YA PILI
No_2
Alexander masikini alipo gundua bibi yake kuwa
amefariki! ndipo akaamua kukimbia na kutoroka nyumbani kwao bila ata kumuaga
mama yake mzazi. Na wakati mama yake alex alikuwa anampenda sana mwanae na
alikuwa anamtegemea sana maana ndiye alie kuwa mtoto wake wa pekee.
Alex aliogopa sana maana alijua ni yeye amemuua bibi
yake.
Sasa wakati alexander yupo njiani akiwa anatoroka
kuelekea sehemu asiyo ijua! Alex masikini alisahau ata kumfunika marehemu bibi
yake pale nje ya nyumba akamuacha bibi akiwa na damu na akiwa ameachama mdomo
wake na kukodoa sana macho pale alipo fariki.
Kipindi alex yupo njiani anatoroka baadhi ya watu
walikuwa wanamuonea huruma! Maana alex alikuwa analia na kutokwa machozi
kipindi yupo safarini masikini dahh.
Mama yake alex alikuwa bado hajatoka kazini, na
alikuwa hana taarifa yoyote kama mama yake mzazi amefariki kule nyumbani,
Sasa ilipo fika mida ya jioni kipindi alex bado yupo
njiani akiwa analia sana mpaka macho yake kubadilika rangi na kuwa mekundu,
mvua masikini alianza kunyesha sana, na kilicho kuwa kinauma zaidi ni pale mvua
ya barafu ilipo kuwa inanyesha na kumnyeshea marehemu bibi pale nje!
Masikini wa mungu mwili wa marehemu bibi ulinyeshewa
sana pale nje bila mtu yeyote kugundua na alisikitisha sana watu! pale siafu
zilipo kuwa zikiutembelea mwili wa marehemu bibi pale nje.
Sasa siku ya kwanza ikapita bila mtu yeyote kujua
kama bibi amefariki, maana ata mama yake alex alipata dharula kazini kwake
hivyo akawa amelala kazini na ukizingatia hata simu hazikuwepo sana kipindi
kile, labda angepiga simu kwa alex ili aweze kumjulisha.
Ila sasa mama alex alipo rudi nyumbani alipitia mlango wa nyuma pale nyumbani,
alishangaa sana kuona ukimya mwingi wakati alizoea
kukuta alex akicheka na kutaniana sana na bibi yake. Alijaribu kuwaita lakini
hakuna alie itika ata mmoja.
Mama Alipatwa
na wasiwasi sana ndipo akaamua kutoka ndani kwenda kuchungulia sehemu walipo
kuwa wanakula mahindi.
Alishituka sana kukuta mama yake ameanguka chini na
akiwa ana majelaha makubwa sana isitoshe tena alikuwa amefariki. Alipo angalia
akakiona kigunzi kilivyo mwangusha yule bibi mpaka kumtoa kucha za
miguuni.USIKOSE YA_3
SEHEMU YA 3
Mama alex alisikitika sana, aliumia nakusema kwamba
"mwanangu alex kwanini umefanya hivi, kwanini umemuua mama yangu jamani?,
nitawambia nini ndugu zangu mimi jamani, nitaificha wapi sura yangu! baba yetu
aliisha fariki na tulimbakiza mama tu sasa na yeye amefariki sababu yako alex
mwanangu, nilikuzuia kutupa vigunzi ovyo hapa nyumbani"
Mama Alex aliongea haya maneno huku akiwa analia!
mpaka misuri ya kichwa akaanza kuvimba! Alilia na mvua ikimnyeshea! mpaka
mapovu yakaanza kumtoka mdomoni!
Mungu saidia baada ya mvua kupungua ndipo majirani
wakaanza kuzisikia nduru na kilio kutoka kwa mama alex!
Dooh walipo fika walisikitika sana kumkuta yule bibi amefariki maana alikuwa
anapendwa sana na majirani zake.
Ila mama Alexa alishangaza sana watu masikini! yani
Kipindi watu wote wanajadili jinsi gani wataushughulikia mwili wa marehemu.
Walishanga jamani, kumuona mama alex amevua nguo
zake zote na kubaki uchi wa mnyama bila kuogopa ata watoto! Akisema kwamba,
"nakuraani mwanangu alex kwa kumuua bibi yako, popote ulipo usifanikiwe
ata kwenye ndoa yako"
Dooh wakina mama walivua vitenge vyao na kumfunika mama alex ili asibaki uchi uku
wakimfariji na kumtia nguvu.
Sasa wakati alex yupo njiani akiwa anaondoka sehemu
asiyo ifahamu, alisafiri sana yani mpaka pesa yake ikawa imekaribia kuisha.
alex alikuwa anawaza sana maisha yake yatakuwaje
kule aendapo, ndipo yule dada alie kuwa amekaa na Alex siti moja kwenye basi
akamuuliza "kaka samahani mbona kama unamawazo sana"
Alex akajibu, " hapana dada yangu ni mambo ya
dunia tu wala sina tatizo"
Yule binti akamuuliza " mimi naitwa Fadhira,
wewe unaitwa nani?
Ndipo akamwambia "mimi naitwa Alex"
Ila wakati Alex na Fadhira wanazungumza walitokea
kupendana sana! lakini hakuna ata mmoja alie mwambia mwenzake!
Sasa Walipo
fika mkoa wa Shinyanga! Ilikuwa imeisha fika usiku, ndipo waliamua kutafuta
sehemu ya kulala wageni, yani "GUEST HOUSE"
lakini bahati mbaya walipata chumba kimoja tu!
Dah ikabidi wakubaliane kulala wote hicho chumba!
lakini bahati mbaya masikini Fadhira alikuwa na
majini mabaya sana na yalikuwa hayamruhusu yeye kulala na mwanaume yeyote
yule..
USIKOSE YA 4
Mtunzi @hadithizetu #0769510060
SEHEMU No_4
Alex na Fadhira walipo kubaliana kulala chumba kimoja, alex hakuwa na wasiwasi wowote
lakini Fadhira masikini alikuwa muoga kiasi na wasiwasi pia maana alikuwa
analijua tatizo lake mwenyewe, kwamba akilala tu na mwanaume yeyote yule
mashetani yake lazima yaamke.
Alitamani kumwambia Alex kwamba wasilale wote,
lakini Fadhira alikuwa muoga akahisi kwamba akimwambia alex wasilale wote, alex
atamuhisi yeye ni mchoyo.
Hivyo basi akaamua kukaa kimya moyoni mwake, mapigo
yake ya moyo yalikuwa yanaenda kasi, maana alijua lazima cha moto atakipata
chumbani.
Walipo pewa ufunguo wa chumba chao, Fadhira
aliupokea ufunguo, na walipo fungua chumba na kuingia ndani Fadhira alifunga
chumba kwa ndani nakuuficha ufunguo chini ya kapeti! Ili mashetani ya kimpanda,
Alex asije kumkimbia, maana yale mashetani yalikuwa yanamtesa sana.
Baada ya kila mmoja kuoga walilala, na wote walikuwa
wamechoka sana, hakuna ata mmoja alietaka kumsumbua mwenzake siku iyo.
Lakini Alex anasema kwamba, hatasahau ilipo fika saa
sita na dakika sita na sekunde sita yaani 666. Upepo mkali ulitanda mule
chumbani! Alex alishangaa na alishtuka sana akaangalia saa yake ni saa sita.
Dooh upepo ulizidi chumbani masikini, na kibaya
zaidi Fadhira alikuwa hasikii chochote kile.
Alex akamuamsha akisema kwamba "rafiki yangu
amka, kuna upepo mkali Fadhila"
lakini alishangaa kuona haamki! Na mwili wa fadhira ulikuwa mzito
maana alikuwa hajigeuzi, yaani kama mtu aliye kufa.
Dooh Alex aliogopa akihisi labda mzimu wa marehemu
bibi yake imemfata.
Alianza kulia
kwa uoga akisema "nisamee bibi yangu nihurumie naogopa bibi"
Kumbe haukuwa mzimu wa bibi yake bali yalikuwa ni
yale majini na mashetani ya fadhira! Na mashetani siku zote yalikuwa yanakuja
kwa njia ya upepo.
Kipindi alex anawaza akisema "nyumbani nimeacha
bibi yangu amekufa, sasa jamani na hapa tena huyu dada amekufa, dooh mikosi gani
huu"
alishangaa kusikia Fadhira anaamka na kupiga kelele,
na sauti kubadilika ikawa ya kiume ikisema "kwanini mke wangu unalala na
wanaume wakati nimeisha kutolea maali na mizimu inakutambua" Alex aliogopa
masikini, maana Fadhira alianza kujipiga kichwa chake chini mpaka damu nyingi
kumtoka.
Usikose ya 5
SEHEMU YA: NO_5
Kipindi mizimu inaendelea kumtesa Fadhira masikini, alikuwa anapiga kelele
sana, akisema "nakufa mimi, naumia jamani msinisukume"
Alex alikuwa anashangaa maana alikuwa hamuoni anae
msukuma!
Alex akaongea kwa uoga kwamba "Fadhira jamani
ndiyo umeamua kuniogopesha hivi, siungesema kama hutaki tulale wote"
Alex masikini alizania labda ni masiara.
Lakini alikuwa anashangaa Fadhira anajipiga kichwa
chake chini tena sana na damu zikimtoka pia.
Alex alijaribu kutafuta funguo ili atoroke lakini
hakuzipata maana Fadhira alikuwa amezificha
Hivyo kutokana na kelele Fadhira alizo kuwa anapiga
masikini, wateja wote kwenye ile "GUEST" wakaamka na kuanza
kushangaa! ndipo mlinzi wa guest akaja kugonga mlango ili Alex afungue lakini
Alex hakuwa na ufunguo,
mlinzi akasema, "Jamani mbona mnasumbua wateja
wetu kwa kelele zenu hizo"
Alex yeye hakuweza kujibu maana alikuwa anaogopa
sana masikini na alikuwa anamkimbia fadhira mule ndani kwa kujibana kwenye kona
za chumbani
Fadhira alikuwa anamuinulia mkono Alex ili Alex
amshike kichwa chake, asiendelee kukipiga chini, Lakini alex alikuwa anaogopa
anahisi labda majini yata mdhuru na yeye
Basi masikini kwa sababu fadhira alikosa msaada na
alikuwa kajipasua sana kichwa chake, dooh Fadhira alikufa mbele ya macho ya
Alex jamani!
Alex alilia kama mtoto akisema kwamba. Jamani
"kwanini nimelala na mtu nisiye mjua"
Dooh mlinzi na wateja wa guest walipo ona alex
hafungui ndipo wakaanza kubomoa mlango ili waangalie kinacho endelea ni nini?
Walikuta yule binti amekufa wakasema "wewe
kijana ndiyo umemuua huyu dada" Alex alilia akisema "sio mimi ni
mizimu"
Wakamjibu "usizani sisi ni wapumbavu amekunyima
mapenzi umemuua"
ALEX ANASEMA KWAMBA,
walimpiga sana masikini, mpaka mikono na miguu yake
ikalegea. Sasa walipo mlegeza mikono na miguu. Ndipo wakamwambia achimbe kabuli
mwenyewe kisha amzike Fadhira peke yake, Alex alichimba kaburi mwenyewe.
Ikafika hatua akachoka ata shimo halikuwa refu! ndipo akamzika dada wa watu hivyohivyo! maana ata ndugu zake
Fadhira walikataa kumfata ndugu yao sababu ya majini yake! Fadhira alizikwa
bila ata jeneza jamani alifunikwa shuka tu la mule Guest.
USIKOSE YA 6
MwandIshi FRANK DAVID @hadithizetu
SEHEMU NO_6
Alex alipomaliza tu kuzika,akamfata muhudumu wa ile
gest akamwambia nashukuru sana,umenisaidia nimenusurika na polisi asante ila
nataka kuendelea na safari yangu.
muhudumu akamwambia "nani kakwambia
nimekunusuru na polisi, mauji yako pale pale na wewe ni muuaji hapa hauruhusiwi
kuondoka mpaka boss aje na nimeshampigia simu aje na polisi"
Alex akatoa macho tu.
akamwambia "kaka naomba unisamehe tafadhari,
yani hapa nilipo sina hata mwenyeji katika huu mji tafadhari sijamuua mimi ni
mizimu yake imemuua"
yule mhudumu akamwangalia Alex juu mpaka chini alafu
akamuuliza "utanipa shingapi nimpigie boss asije" Alex akachoka
kabisa akijiangalia mfukoni ana elfu 8 tu, akamwambia mhudumu aliyejulikana kwa
jina la kisukuma Maganga,
"Maganga
hapa mfukoni nina elfu 8 tu! sidhani kama elfu 8 inaweza kununua kesi nzito
kama hii? sina pesa na wala sina neno tena la kuongea"
Maganga akamwambia "shida yangu ni laki 1 tu
sawa? nipatie hiyo pesa nikuruhusu"
Alex akasema "sina" kwa unyonge akawa
anaiona jela inamkaribia masikini.
Maganga akamwangalia Alex kwa jicho la dharau afu
akamwambia
"hapa gest niko peke yangu kuna kijana uha
anakuja na kunisafishia hapa na ninamlipa kila siku elfu 1, siku nyingine
anapenda niziweke ziwe nyingi nimpe, sasa unatakiwa kuanzia leo uwe unasafisha
hii gest na kufua mashuka yote mpaka
laki 1 ninayoitaka itimie yaani hapa unakaa miezi3 na siku10"
Alex kusikia vile alifurahi sana jamani, huku akimshukuru maganga na kusema bora
mateso ya uraini kuliko jela, basi kuanzia siku hiyo alex akawa anafanya usafi
hapo gest akimaliza anatoka kwenda kuzurula na kula mitaani jioni anarudi gest
kuvizia sehemu ya kulala kama mwezi mmoja, mpaka akawa ameishazoeleka na boss
akamjua! alikuwa mkarimu mpole ila alikuwa na sifa ya kusahau na kupuuzia jambo.
Siku moja usiku sana giza tele, mzimu wa Fadhira
ulimtokea Alex, na kibaya zaidi mzimu wa fadhira ulikuja ukiwa uchi! yani mtupu
kabisa jamani dah na mzimu ulikuwa umechafuka sehemu zake za siri, matiti yakiwa waziwazi mzimu ukasema,
"alex rafiki yangu naomba unifufue jamani! sijafurahi umenizika na pedi
naitaji kuzikwa nikiwa msafi,naitaji kusafishwa"
USIKOSE 7,
@hadithizetu
Sehemu 7
Alex aliogopa sana masikini pale mzimu wa Fadhira
ulipo mtokea usiku wa manane.
Alex akauliza ule mzimu kwa uoga sana kwamba
"Fadhira kwa nini umekuja ukiwa uchi?" Mzimu wa Fadhira ukajibu huku
ukiwa unalia eti kwamba "Alex rafiki yangu nimekuja nikiwa uchi sababu
nilikuwa nakupenda sana Alex, na wala usiniogope siwezi kukudhuru ila nimeumia
sana yani umenizika mimi nikiwa nimevaa pedi chafu naitaji kuwa msafi kama wafu
wengine jamani nakosa furaha kabisa nikiwa na wafu wengine! nifufue Alex, maana
usipo nifufua mimi na kunivua ile pedi, sitochoka kukufata popote uendapo"
Palepale baada ya mzimu wa Fadhira kutamka yale
maneno ukapotea ghafla.
Alex alishituka sana! Ndipo akaamka mida ya saa tisa
usiku akachukua koleo pamoja na jembe alilo mzikia Fadhira kisha akaenda
kumfufua kwenye kaburi lake.
Alex masikini alienda akiwa analia akisema
"bibi yangu asinge teleza na kigunzi nisinge pata haya mateso yote"
Alex alipo fika makabulini alitazama mbele na nyuma
hakuna mtu, kushoto na kulia pia hakuna mtu, ndipo Kijana Alex akaanza kuchimba
kaburi ili amfufue Fadhira kisha amtoe ile pedi na amzike upya. Kweli alianza
kuchimba kwa roho moja tu ila Alipo fika katikati ya kaburi dooh harufu mbaya
sana ya kuoza ikaanza kunuka! Maana mwili wa marehemu Fadhira ulikuwa umekaa
mda mrefu pia
Alex alijaribu sana kujikaza na ile harufu ili
angalau aweze kumfufua Fadhira lakini kadri alivyo kuwa anachimba harufu
ilianza kumzidi na kumfanya ajihisi kuumwa.
Alex alivua t_shirt lake kisha akajifunika puani
mwake ili harufu ipungue ili aendelee kuchimba lile kaburi lakini harufu
masikini ilimfanya alex azidiwe.
Wakati alex amechimba akauona mkono wa marehemu,
kipindi anaushika mkono kuuvuta juu akatoka na nyama za mkono zilizo kuwa
zimeoza zimekuwa laini.
Kijana Alex Anasimulia na kusema kwamba. Alikaa
kwanza chini akalia jamani, alilia akisema kweli maisha ni zawadi kutoka
mbinguni lakini maisha pia ni adhabu. Alex alichimba shimo kweli kisha akamtoa
binti Fadhira mpaka juu, dah Fadhira alikuwa amejaa wadudu aina ya Funza kwenye
mwili wake yani atamaniki kabisa, na wakati ameisha mvua nguo zake sasa ili
kumtoa ile pedi.....
USIKOSE_8
SEHEMU : NO_8
Alex alipo mvua nguo zote marehemu Fadhira, kipindi
sasa anataka kuitoa ile Pedi, dah masikini! akawa amekamatwa na mlinzi wa yale
makaburi, Mlinzi akamwambia "wewe mchawi unafanya nini usiku huu
makaburini, kwa nini unafufua miili ya wafu gizani?"
Alex aliogopa sana! ndipo mlinzi akaanza kupiga
kelele, wana kijiji wote wakaja pale wakiwa na panga pamoja na marungu na
kuanza kumpiga sana Alex!
Dooh yule boss mwenye guest akasema, "msimuuwe
huyu ni kijana wangu tumuulize kwa nini anafanya hivi ili tujue
tunamsaidiaje"
Wanakijiji
wakasema,
"hatumtaki hapa Alex ni mchawi na amzike
marehemu aliye mfufua kisha aondoke kutoka hapa aende kwao"
Dah masikini Alex aliinama na kuanza kumzika upya
binti Fadhira huku akiwa anachapwa viboko na mwenyekiti wa mtaa, bila ata
kufanikisha kuitoa ile pedi.
Alex alifukuzwa kama mnyama masikini na kuacha sifa
mbaya ya uchawi.
Kipindi alex yupo kwenye basi linaloenda jijini Dar,
mzimu wa fadhira ulimtokea kwenye basi umo umo dooh Alex alianza kutetemeka
sana.
Mzimu ukasema "Alex kwa nini umenizika mchafu,
kwa nini bado hujanitoa pedi "
Alex akajibu, "nilijaribu nikashindwa nimepigwa
sana kwa ajili yako"
Mzimu wa fadhira ukasema "Alex najua unatambua
nimekufa, lakini nimekufa nyama sijafa roho, nateseka sana huku nilipo,
natengwa na kila kiumbe sababu ya hiyo pedi naonekana mchafu jamani! Na mimi
nimeisha kufa hivyo siwezi kutoa mwenyewe naomba nitoe pedi wewe Alex shuka
kwenye basi rudi shinyanga kaburini kwangu kanitoe ile pedi tafadhari"
Dooh watu kwenye basi walimshangaa sana kijana Alex
wakawa wanamuangalia yeye tu yani basi zima! wakijadiriana kwamba "huyu
kaka ni kichaa au? mbona analia na kuongea mwenyewe"
Maana walikuwa hawauoni mzimu wa Fadhira wala sauti
ya mzimu.
Alex peke yake ndiye alie kuwa akiuona ule mzimu.
Kwenye lile basi kulikuwa na wachungaji wa kilokole
.na mapadri wote imani zao hazikuwaonyesha ule mzimu.
Hata hivyo mule kwenye basi pia kulikuwemo na IMAMU kiongozi wa msikiti
Imamu aliamka kutoka kwenye siti yake akamfata Alex
kisha akamwambia kijana unateswa sana na mizimu, Imamu akatoa TASUBII kisha
akaanza kuufukuza ule mzimu..
USIKOSE YA 9
.
SEHEMU No_9
Baada ya IMAMU kuomba. Alimsaidia sana Alex,
maana mzimu uliacha kumtokea safarini.
Walipo fika jijini Dar, Alex alikuwa hajui wapi pa
kuelekea! maana hakuwa na ndugu wala mtu yeyote yule alie kuwa anamfahamu.
Sasa wakati Alex yupo mjini aki shangaa shangaa!
Alibanwa na haja ndogo masikini! Ndipo akaenda
kukojoa pembeni kwenye ukuta wa kanisa!
Sasa wakati anakojoa,mchungaji wa kanisa akamuona!
Kisha akamuita, "kijana njoo hapa" Alex hakuwa muoga akaitika kisha akaenda,
Mchungaji akasema "kwanini unakojoa kwenye eneo
la kanisa, tena kwenye ukuta wa mungu" Alex alishangaa kisha akasema "nisamee, nilikuwa sijui kama ni
vibaya, maana kule kijijini kwetu tunakojoa sehemu yoyote tu mkojo unapo kuwa
umekubana " mchungaji alikasilika kisha akasema "naona unanijibu kwa
dharau sio, ngoja nikupe adhabu"
Alex alipewa kazi ya kufyeka eneo la kanisa, dooh
kusema kweli Alex alipewa eneo kubwa jamani afyeke"
kijana Alex kwakuwa alikuwa mpole na ndiyo ilikuwa
mala yake ya kwanza kuja Dar na hakuwa na pakufikia hivyo akafanya adhabu yake
tena kwa roho moja!
Alifyeka eneo la kanisa vizuri sana kwa mda mchache
tu.
Mchungaji alivyo toka nje kukagua eneo alishangaa
sana akasema "kijana nani amekusaidia kufyeka, maana umefanya kazi nzuri!
ndani ya mda mchache! vijana wengi uwa nawalipa pesa zangu lakini wanafanya
kazi ovyo ovyo"
Alex akajibu "mchungaji mimi napenda sana
kazi"
mchungaji akamuuliza, "wewe unaitwa nani na
unaishi wapi?"
Alex akasema jina lake kisha akasema "mchungaji
mimi sina sehemu yoyote ya kuishi nimekuja dar leo alafu sina ndugu wala mzazi
uku mjini,nipo nipo tu"
Mchungaji alipenda sana uchapakazi na ukalimu wa
Alex, akamwambia "kijana sio vizuri kuzurula humu mjini utateseka sana
kijana wangu, ila nimependa uchapakazi wako naomba ubaki hapa kwangu uwe
unanisaidia kazi za hapa na pale kisha nitakuwa nakulipa kwa mwezi.
Alex alifurahi sana masikini kisha akafanya kazi kwa
roho moja.
Sasa baada ya miaka kadhaa kupita, Alex alikuwa
tayari ameokoka na alikuwa ameisha jenga nyumba yake nzuri ya kuishi!
Ndipo akaamua kumuoa binti wa yule mchungaji,
Na hapa ndipo laana za mama yake na bibi yake Alex,
zikaanza kumtokea!
Usikose 10
Mtunzi @hadithizetu
0769510060
No_10.
Alex alimuoa Rose yule mtoto wa mchungaji, lakini
Rose alikuwa ana virusi vya ukimwi masikini, na Alex alikuwa hajui!
Sasa siku moja usiku Alex na Rose, wakiwa wamelala
kitandani, wote walipata hisia ya kufanya tendo la ndoa.
kipindi Alex anampapasa Rose, Alex Alishangaa sana
kumuona marehemu Fadhira anamtokea! akisema,
"Alex usifanye hilo tendo nakuomba
tafadhari"
Alex akajibu nisifanye kwa nini na huyu ni mke
wangu?"
Mke wa Alex akasema "mme wangu jaman yani
unanivua nguo alafu unaongea mwenyewe mbona sikuelewi"
Rose alikuwa hausikii mzimu ukiongea,
Dah Alex akaishiwa hamu siku hiyo na hakufanya
chochote kile!
ila Mke wa Alex alichukia sana hiyo siku maana alikuwa na hamu.
Walikaa miaka mitano bila kufanya tendo la ndoa kwa
usumbufu wa mzimu! Na Kila walipo jaribu kufanya ilishindikana, ila walikuwa
wakijilizisha kwa njia zingine tu.
Baada ya miaka kadhaa kupita mama Alex, umri wake
ulikuwa umaenda sana na alitamani sana mwanae Alex aje nyumbani kumjulia hali
maana hakuwa na mtoto yeyote yule zaidi ya Alex!
Ikabidi mama aende kwa mganga wa jadi ili
amuangalizie Alex alipo, maana miaka ilikuwa mingi ajarudi kwao.
Mganga akamwambia mama Alex "ukitaka ujue
mwanao alipo njoo leo usiku saa tisa ukiwa uchi"
Mama Alex alifanya hivyo sababu ya mapenzi ya
mwanae!
Mama Alex alipelekwa ziwani akiwa uchi! Akapakwa
dawa, kisha mganga akamwambia "nyanyua matiti yako , kisha sema Alex
mwanangu njoo unyonye,Popote alipo atasikia tu"
Baada ya kumaliza vile wakaondoka.
Kesho yake Alex, kichwa kilimuuma sana jamani, ndipo
akaamua kurudi nyumbani mapema! Alipo fika kwake akaingia mpaka ndani,
Hakuamini macho yake, alifumania mkewe anafanya ngono zembe na kiongozi wa
kwaya ya kanisa.
Alex alisema "mke wangu unafanya nini
hichi"mke akasema "sijafanya kitu"
Alex akasema, angalia shuka langu mmelichafua,
jitazame ulivyo sweti, angalia hujavaa nguo ya ndani upo uchi! unasema
hujafanya kitu, Rose akasema mme wangu mimi nimechoka kuvumilia miaka mingi
sasa bila kufanya "TENDO LA NDOA" nimezidiwa mme wangu....
☆NINI
HATIMA YA KIJANA ALEX☆ USIKOSE YA 11 @hadithizetu
TENDO LA NDOA SEHEMU YA 11.
Kijana alex aliumia sana masikini , maana alikuwa
anampenda sana mke wake akamuuliza swali tena maana hakuamini kabisa kama
amesalitiwa.
“mke wangu kwanini umeamua kufanya hichi kitu yani unanisaliti tena
ndani ya chumba changu kwenye shuka langu mwenyewe”
Mke wa alex akasema “ mme wangu naomba unisamee
najua nimefanya kosa kutoka nje ya ndoa lakini halikuwa kusudio langu ni
shetani tu kanipitia na kibaya zaidi ni kwamba mme wangu tumeishi wote miaka
mingi mpaka sasa lakini haujawai kufanya chochote na mimi nimeshawishika nilipo
pata hamu mpaka uvumilivu umenishida”
Alex akamwambia Yule kiongozi wa kwanya ya kanisa
kwamba ,
“kaka hivi kumbe wewe ni mkristu hewa? Na kwa nini
usiache kufundisha ata hii kwaya yetu,
maana una dhambi nyingi sana kaka,
Alex akasema
mimi sina chochote kile cha kukufanya wewe ila naomba utoke ndani kwangu ukiwa
uchi uende mpaka kwa mke wako alipo”
Yule mchungaji wa kwaya bwana petron akaanza kulia akisema
“alex mwana mkristu mwenzangu, naomba unisamee,
naomba unihurumie maana naogopa kwenda nje nikiwa uchi kumbuka mke wangu ame
hokoka na anaheshimika sana sasa nikitembea uchi uko
nje uoni kama nitakuwa namuahaibisha,jamii itanitazamaje mimi jamani, nihurumie Alex”
Alex alikuwa amekasilika sana jamani akasema
“tangu nimezaliwa sijawai kusamehewa na
hapa nilipo nimepitia matatizo mengi sana! Hivyo ata wewe siwezi kukusamehe.
Kweli alimnyanganya Yule mwalimu wa kwaya ya kanisa
ile suti yake kisha akamtoa nje kama mwizi akamwambia ondoka na akafunga mlango
.
Yule mwalimu wa kwaya masikini akafumba macho yake
kwa haibu kali sana mtaani akaenda kwa kujificha akiwa uchi masikini mpaka
kwake kila mtu alikuwa anamtazama watoto walianza kumcheka na watu wote
wakashangaa sana masikini.
Mwalimu wa kanisa alipo fika kwake mke wake akamuuliza”
mme wangu unatoka wapi na kwanini upo uchi”
Mme wake akasema” nisamee mke wangu sitarudia ni
shetani tu”
Mke wake akajibu “nikusamee nini”
Mme wake akasema “nimetembea na mke wa alex Yule mwenyekiti wa kanisa na huyohuyo
alex ndiyo amenifumania na kunifukuza kwake nikiwa uchi, nashindwa kukuficha
maana watu wote nje wameniona nikiwa
uchi na wanajua kosa nililo tenda ila nisamee sana mke wangu ni kosa tu
limetokea bahati mbaya”
Mke wa mwalimu wa kwaya ,alikuwa ni yatima na
alikuwa anamtegemea mme wake kwa kila kitu hivyo akaamua kumsamee maana hakuwa
na sehemu yeyote ile ya kuegemea zaidi ya kwa mme wake.
Lakini dah kumbe masikini Yule mwalimu wa kwaya
alikuwa ameambukizwa ukimwi na mke wa alex hivyo akauleta ugonjwa pia mpaka ndani kwa mkewe
masikini dooh.
Alex hakuwa na jinsi pia ila akamwambia mke wake
kwamba “kwani umeshindwa kuchukua mwanaume yeyote Yule mpaka umeamua kuchukua
mme wa mtu tena mkristu mwenzetu laana gani unaleta ndani ya familia”
Mke wake akasema nisamee sitarudia tena mme wangu.
Baada ya ya wiki mbili kupita, alex na mke wake
wakiwa chumbani usiku wamelala huku wakiwa wanachezacheza kitandani mzimu wa fadhira ulikuja umejaa vidonda mwili
mzima!
akasema “alex kwanini unataka kufanya mapenzi na
huyo mwanamke wakati ameathirika”
alex
akasema “mke wangu ni mtoto wa
mchungaji hawezi kuathirika na ukimwi”
mzimu ukamuuliza kwamba “kwani umempima mke wako kufahamu afya yake au
unamuamini tu kwa macho”
Mke wa alex akashituka kisha akasema “alex mme wangu
kwanini unaota ndoto za ajabu namna hii, yani unaniota kuwa mimi nina ukimwi
huoni kama unanikosea sana mme wangu”
Alex akasema sio ndoto ni fadhira amekuja masikini
Mzimu wa fadhila ukasema ”Alex naomba usimwambie mke
wako kuhusu mimi tafadhali”
Alex akanyamaza kimya!
Mke wa alex akaanza kulia sana akasema naona sahivi
huniamini yani nakusikia kwa masikio yangu ukisema kwamba mimi nina ukimwi.
Alex akamuuliza fadhira “ kwanini sasa hivi
umechafuka sana umejaa vidonda mwili mzima, kwanini usivae nguo unakuja uchi
kila siku”
Fadhira akasema ulikataa kunisafisha nateseka sana
huku nilipo, natengwa, nanuka ,nachekwa sababu ya uchafu lakini sina jinsi
nimeisha zoea kwa sasa”
Baada ya mzimu kuongea yale maneno ulipotea ghafla!
Palepale mke wa alex akaanza kugomba sana akisema
kwamba “yani wewe unasema mimi nina virusi vya ukimwi kumbe unaishi na mimi
alafu uniamini sio naomba kesho mapema twende hospital tukapime na kama sina
utanikoma mimi ni nani”
Alex hakuwa na jinsi aliamua kukubali tu sasa walipo
fika hospital masikini kweli mke wa alex alikuwa ameathirika ila alex alikuwa
hajapata bado maambukizi ya virusi vya ukimwi! dooh Alex alimuogopa sana mke wake akasema “mimi siwezi kuishi na wewe tena, sitaki
kuugua ukimwi, alafu kumbe fadhira alikuwa ananiambia ukweli”
Doctor akasema hapana alex kijana wangu usifanye
hivyo, huyu ni mke wako wa ndoa kama ulivyo sema hapo awali kipindi unataka kupima, sasa
ukimkimbia utakuwa hujafanya vizuri maana ata kama anaukimwi unaweza kuishi nae
na ukatumia njia mbadara na usiweze kupata maambukizi.
Alex alisema sawa doctor ngoja nikaongee na wazazi
wake ili niweze kulimaliza ili swala.
Kweli masikini alex aliwaita wazazi wa mke wake,
kisha akawambia mimi na mototo wenu tumepima leo ila mke wangu amekutwa na
maambukizi ya virusi vya ukimwi! hivyo siwezi kuishi nae tena, na mahari niliyo
toa nimeisamee, nyumba yangu namuachia yeye aishi mimi nataka kurudi kwa mama
yangu mzazi.
Wazazi wa mke wa alex hawakuwa na jinsi ikabidi
wakubaliane na mawazo ya alex, ila alex akaulizwa swali, kwanini hukumpima
kipindi unataka kumuoa, alex akasema mimi nilizania kuwa kwakuwa mkemwangu ni
mtoto wa mchungaji hivyo hawezi kuwa na mgonjwa
ya zinaa kama haya.
Mke wa alex aliwekwa kwenye maombi na kanisa lao
zima ili aweze kuponywa maana tayar alex
alikuwa kaisha mkimbia, sasa mwalimu wa kwaya alipo sikia zile habari za kwamba
mke wa alex ana ukimwi moja kwa moja akajua na yeye lazima ukimwi anao maana
hakutumia kinga alipo fanya nae,
dooh mwalimu wa kwaya alipo enda kupima yeye na mkewe
wakakutwa wote wawili wameathirika masikini, dah mke wa mwalimu wa kwaya alikua
anauogopa ukimwi hivyo akawa amejiua maana alikuwa anaogopa aibu za watu kwamba
amekonda sana sababu ya virusi.
Mke wa alex alilia pia na akakimbia kutoka mkoa ule
na kwenda sehemu asiyo ifahamu maana alikuwa anakwepa haibu za watu.
Sasa alex akaamua kuanza safari kurudi nyumbani kwa
mama yake maana hakuwa na sehemu yoyote ya kukimbilia, sababu akuwa na ndugu
yeyote isitoshe kule shinyanga na penyewe aliacha jina baya sana masikini.
Sasa kipindi alex yupo njiani akakutana na bibi
mmoja amezeeka sana masikini alafu Yule bibi alikuwa mchafu sana, yani alikuwa
anatoa mpaka harufu chafu,
kibaya zaidi alikuwa amebeba mzigo mkubwa sana
kichwani, alex alishikwa na huruma jamani akamkumbuka bibi yake kipindi yupo
mzima alikuwa anamsaidia sana kazi ngumu ngumu na wala alex alikuwa hapendi
kumuona bibi yake anafanya kazi nzito ya kumchosha kama yule bibi alivyo kuwa
amebeba,
alex akamfata kisha akamwambia “bibi naomba
nikusaidie mzigo” bibi alinyamaza kimya na alex alikuwa bado hajamuona usoni,
dooh alex akarudia tena “bibi umebeba mzigo mzito sana naomba nikusaidie maana
unateseka sana”
Yule bibi akamjibu kwamba “asante kijana wangu
lakini kama kweli una huruma kwa wazee kwanini hukumsaidia bibi yako nyumbani
kwenu alipo kufa, alafu unataka kunisadia mimi” alex alishituka sana masikini
dah akasema kwani bibi yangu umemjuaje?
USIKOSE SEHEMU YA 12
SEHEMU YA 12
Kijana alex alisikitika sana kwa maneno ambayo Yule
bibi aliyaongea, aliamua kunyamaza kimya kisha akasema,
“bibi naomba kama unafahamu chochote kuhusu bibi
yangu uniambie”
Yule bibi akasema “kama kweli unataka ufanikiwe na
maisha yako rudi nyumbani ukamzike bibi
yako, rudi nyumbani ukamuone mama yako mzazi”
Alex akasema “sawa nimeelewa bibi yangu, lakini bado
sijajua wewe ni nani”
Yule bibi hakujibu chochote, na hapo hapo akapotea
kama upepo!
Alex alishtuka sana masikini, akaogopa pia maana
alijiuliza maswali mengi kwanini iwe hivyo kwanini huyo bibi amtokee kwa njia
kama ile?
Na Kule nyumbani kwa kina alex, mama yake alex
aliugua sana masikini na hakukua na mtu yoyote Yule wa kumuuguza, dooh mama
alex alikuwa analia akisema,
“hivi mwanangu amekuwaje jamani kwanini ameniacha
nateseka sina mtoto mwingine zaidi yake bora angekuwepo hapa nisinge teseka
maana pesa sio kila kitu”
Na mda huohuo alex alikuwa yupo njiani anaelekea
kwao!
Mama ake alex akarudi kwa mganga wake kisha
akamuuliza mbona mtoto wangu haji? na kama matambiko tumeisha fanya, mimi
nakosa furaha pale ninapo jiuguza mwenyewe wakati nimeisha wai kuzaa, mama alex
akaendelea kusema kwamba mganga ni bora tufanye matambiko upya labda mwanangu
anaweza kurudi.
Mganga akamjibu mama alex kwamba, mtoto wako lazima
arudi wewe usiwe na haraka,
mama alex alirudi kwake akiwa analia huku akisema
huyu mganga ni muongo ananipa tu moyo.
Sasa kipindi alex anarudi kwao mzimu wa fadhira
ukamtokea tena masikini ukamwambia alex naomba nisaidie kitu,
Alex naomba urudi mkoani shinyanga ukachukue mchanga
juu ya kabuli langu kisha ukae nao popote uendapo ili nisiweze kukutokea tena
maana nahisi nakuchosha ninapo kutokea nataka kukuacha huru na mimi nipumzike
pia, fadhira akasema sitakutokea tena lakini usirudiane na mke wako.
Alex hakuwa na jinsi alifanya kama alivyo ambiwa,
sasa kipindi alex anarudi kwao akamkuta mama yake ayupo, alex alikuwa bado
anakumbuka sehemu wanapo kuwa wana ifadhi ufunguo! ndipo akaufata ufunguo ili
aweze kufungua mlango wao aingie ndani.
Kweli alikaa ndani ili amsubilie mama yake,
kipindi alex
amekaa ndani alishangaa kuona picha ya bibi yake ukutani
Alex alifata ile picha akaikumbatia akasema bibi
yangu popote ulipo naomba unisamee, hazikupita ata dakika tano, alex alisikia
sauti isemayo
“nimekusameee, Nimekusamee mjukuu wangu,na mimi
ndiye Yule bibi nilie kutokea nikakwambia uje kwenu! Nimekusamee kwa roho moja
maana hukuniua wewe ila ilikuwa mipango ya mungu, na ninajua fika kuwa
ulikimbia kwa kuogopa kwamba raia kwenye asila kali wange kuuwa wakizani
uliniua, msubili mama yako pia umuombe msamaa maana aliku laani akiwa uchi wa
mnyama.
Alex aliendelea kulia akijutia maisha yalivyo mpiga
hakutamani kabisa kuishi tena lakini alikuwa anajikaza, sasa wakati kijana alex
yupo nyumbani anamsubilia mama yake mzazi aje ali amuombe msamaa, alishangaa
sana kuona watu wanakuja nyumbani tena baada ya masaa mawili wakiwa wamebeba
jeneza lenye mwili wa mama yake dooh!
Alex alilia kama mtoto masikini, alijigalagaza.
Akauliza nani amemuua mama yangu?
Wakamjibu alex kuwa kuna dada amemgonga mama yako
barabarani na gari, lakini aliye mgonga alitaka kukimbia tumemkamata na
tumempiga mpaka amefariki,
Alex akalia zaid mpaka akatokwa na jasho lisilo
pimika
Akasema “nionyesheni huyo mtu natamani sana nimuone.”
Kweli walimchukua alex wakampeleka mpaka eneo la
tukio kisha wakamuonyesha alie muuwa,
Dooooh masikini alex alilia zaidi maana kumbe alie
mgonga mama yake na gari mpa kumuuwa alikuwa ni Yule mke wake mtoto wa
mchungaji, hivyo vilio vikawa mala mbili.
Maisha ya alex yalikuwa machungu kwa takribani kama
miaka sita, na siku moja usiku alex alimeza sumu akitaka kujiua lakini majrani
walimsaidia kwa kumpa maziwa ili asife, kipindi alex anapiga kelele akitaka
kukata roho.
Alex aliendelea kuishi kama kichaa, na watu
walishangaa sana kuona anaongea ongea mwenyewe kila mda akisema,
“SINA BABA, SINA MAMA ,SINA BIBI, SINA MKE”
Alex alikuwa akiongea hayo maneno kila mda. kila
saa, bila ata kupumzika
Ndugu na jamaa walimuonea sana huruma, na mala
nyingi walikuwa wakimletea chakula pamoja na kumfanyia usafi wa mwili wake
maana alex alikuwa anajisahau ata kuoga kwa msongo wa mawazo
Ndipo Kijiji kilikaa chini nakusema kwamba,
MAMA ALEX ALIKUWA MAMA MMOJA MZURI SANA, NA
ALIPENDWA NA KILA MTU, WAKUBWA NA WADOGO
PIA,
HIVYO LEO HII
AMEFARIKI HATUWEZI KUITAZAMA FAMILIA YAKE INAANGAIKA SANA HIVI, NI BORA TUMTAFUTIE HUYU KIJANA ALEX MKE,
ILI AISHI NAE
NDANI LABDA ANAWEZA KUKAA VIZURI SIKU MOJA.
Wanakijiji wote walikubaliana na yale mawazo na
hakuna ata mmoja alie pinga lile swala
Kweli wanakijiji walijichangia pesa kwa ajili ya
mahari ya binti atakae olewa, maana kimila walikuwa wanatoa ngombe.
Pesa zikapatikana lakini hakuna ata binti mmoja alie
kubali kuolewa na kijana alex.
Mabinti wote walisema kwamba “kijana ni mchafu na
anaongea mwenyewe kama kichaa nani aishi nae, dooh tena kwanza ali laaniwa na
mama yake na ndiyo maana yupo vile, hatumtaki sisi hatuwezi kuishi na bwana
kama yule”
Wanankijiji walichoka kumtafutia alex mke, hivyo
wakashindwa ni jinsi gani wanaweza kumsaidia aweze kuishi vizur,i ikabidi
wamuache alex kama alivyo.
Alex aliendelea kukaa ndani kwa tabu bila kuoga wala
kula vizuri alex alianza kutoa harufu kitendo kilicho mfanya mpaka yeye
mwenyewe kutoka ndani nakuanza kutembea nje kama vichaa wengine,
Kumbe masikini wa mungu ni zile laana za mama yake
zilikuwa zinafanya kazi.
Alex aliteseka sana jamani, maana aliacha nyumba
yake bila mtu yoyote kukaamo mpaka nyumba ikaanza kuota magugu na kuchakaa kama
pango.
Siku moja usiku alex akiwa amelala mzimu wa mama
yake mzazi ukamtokea na kusema kwamba
“NIMEKUSAMEE MWANANGU, HAMKA, RUDI NYUMBANI”
Palepale jamani ukichaa ukaisha alex akaanza
kujishangaa ilikuwaje mpaka akawa chizi, alex alikuwa hatambui, alex
alijishangaa yupo kwenye mauchafu jalalani, ndipo akaamua kurudi mpaka kwao
akiwa na aibu tele
Alex alishangaa kukuta vinyesi nimepakwa ukutani
kwenye sebure yao ,kumbe ni yeye
alifanya vile kipindi anaumwa uchizi.
Wanakijij walishangaa sana kumuona alex amepona.
Watu wakamwambia alex jinsi mabinti walivyo mkataa alivyo taka kuozeshwa.
Alex alipo ingia chumbani kwa mama yake alikuta
nyoka mkubwa sana chumbani na kibaya zaidi Yule nyoka hakuwa na nia ya
kumdhuru, bari nyoka aliingia uvunguni na kisha akapotelea humohumo. Wakati
alex ameinama uvunguni akitaka kumuuwa Yule nyoka papo hapo alishangaa kukuta
begi lenye milioni 200 za mama yake mzazi alizo kuwa ameziacha.
Kumbe Yule Yule nyoka alikuwa mzimu masikini,
Alex alianza kufanya biashara mpaka akawa tajiri
mkubwa wilayani kwao na hakuna mtu yoyote alie weza kumshinda,
alex
alifungua shelli za mafuta alifungua maduka na shule na vitega uchumi vingi,
vilivyo mfanya yeye kuwa na pesa nyingi
sana
Wale wadada walio mkataa alex asiwaoe walianza
kujileta tena wakiomba msamaa lakini alex aliwakataa wote akasema mke mwema
uletwa na mungu maana niliteseka sana nilivyo owa kwa haraka na hata sikufaidi
tendo la ndoa……….
MWISHO MWISHO MWISHO WA HADITHI YETU YA TENDO LA
NDOA
MTUNZI FRANK DAVID
FACEBOOK INSTAGRAM AND GOOGLE @HADITHIZETU
WHATSAPP +255769510060
CALL ME
+255673510161
Post a Comment