SEHEMU YA NNE
WATUNZI wastara juma, @hadithizetu
Whatsapp 0769510060
Mke wa millaji alikataa katakata mimi kukaa pale kwake,
hakuwa na huruma hata kidogo, “weee siwezi kukubali kuharibu ndoa yangu, mimi
sitaki lawama Wastara, wewe ondoka Mungu atakusaidia maisha yako mbele kwa
mbele” alisema yule mke wa millaji bila hata huruma.
Niliamua kuondoka nikiwa nachechemea maana kile kidonda
kilikuwa bado kinauma sana, niliondoka bila kujua naenda wapi, ikabidi niende
palepale nyumbani palipo ungua ili nitulize akili, kibaya zaidi kipindi nipo
pale maeneo ya nyumbani mvua ikaanza kunyesha nikiwa na mtoto na nikiwa naumwa,
sikuwa na pesa japo ya kununua hata poda, sabuni na mahitaji mengine ya mtoto.
Niliamua kwenda mpaka kwa mdogo wangu ili japo wanisaidie,
kumbe na yeye pia alikuwa anakaa na mme wake chumba kimoja hivyo mambo yalikuwa
bado magumu kwangu, shemeji alinionea huruma ingawa bado alikuwa bado anaumwa
akanipa pesa ya kukaa chumba cha wageni (guest house), nilitafuta sehemu na
kweli nikapata, sasa wakati nipo pale gesti, kumbe kwa nje walikuwa wanauza
pombe na yule mwenye gesti alikuwa amelewa pia, kipindi namuita ili niweze
kumlipa hela akawa hasikii kabisa, nilipo mfata anipe chumba akasema vimeisha
lakini atanisaidia sehemu ya kulala, sikuweza kukataa maana nilikuwa nimechoka
sana kumbeba mtoto mpaka mikono ikawa inauma hapo sijala chochote, sijaoga,
sijanywa dawa nilizo kuwa nazo.
Yule baba alinipa chumba ila alicho nishangaza eti na yeye
akaja kulala humohumo chumbani, niliogopa nikajua hapa lazima nibakwe tena,
yule baba alilala akiwa amelewa huku mimi nimekumbatia mwanangu, sikupata
usingizi kabisa kwa woga kwamba nitabakwa, yule baba kuna mda alianza
kunipapasa nikashtuka, “naomba tufanye mapenzi nitakulipa” alisema yule baba akiwa
amelewa sana, niliogopa kumbemenda mtoto, ndipo nikaamka ili nitoroke, kumbe
alikuwa amefunga mlango alafu funguo kazificha, ilibidi nimlaze mtoto kwa chini
maana nilitandika nguo zilizo kuwepo pale ili mtoto asiumie, ndipo nikarudi
kitandani ili nimuelezee yule baba hali kiafya asinifanyie lile tendo, yule
baba akanibembeleza sana kwamba yupo tayari hata kunioa nikubali kufanya nae
mapenzi.
Nilikataa katakata lakini kutokana na pombe za yule baba,
bila kujua akanivuta kwa nguvu ili nivue nguo tuweze kufanya tendo, lakini kumbe
akawa ameshika na kukitonesha kidonda nilicho fanyiwa upasuaji wakati wa
kujifungua, maumivu yalikuwa makubwa sana, damu zikaanza kunitoka, ndipo yule
baba akaanza kupagawa akajua kwamba tayari ameua maana nilidondoka chini kutokana
na yale maumivu ya tumbo, ndipo yule baba akaamua kunibeba mzima mzima kisha
akaenda kunilaza nje kwa mbali kabisa na pale gesti kwake, baada ya mda huku
nikiwa nasikia uchungu tumboni ambao nisingeweza hata kuongea chochote nikaona
amemleta mtoto wangu akiwa analia usiku wa manane.
Nilishindwa kabisa kumbembeleza mtoto asilie, maana maumivu
niliyo kuwa nasikia yalikuwa makali sana, sasa basi kutokana na sauti ya mtoto
kuna watu walikuwa wanapita hao watu walikuwa wa ajabu na hata nguo walizo kuwa
wamevaa zilikuwa kama za kichawi yaani washirikina, hivyo basi walipo muona
mtoto wangu ambae alikuwa bado ni mchanga, wakataka kumchukua ili wakamtumie
kama dawa ya mambo yao ya kishrikina, wakati huo sina nguvu wala chochote cha
kuweza kujitetea ili nikomboe uhai wa mwanangu nilie mzaa kwa shida.
USIKOSE SEHEMU YA 5
WATUNZI WASTARA JUMA, @hadithizetu
Whatsapp 0769510060
Post a Comment