Tuesday, March 3, 2020

LIACHE CHOZI LANGU : Sehemu ya 3



SEHEMU YA TATU
WATUNZI, wastara juma na @hadithizetu
Whatsapp 0769510060.
Niliendelea kujivuta huku nikisikia uchungu sana, Mungu alinisaidia mpaka nikafika mlangoni, lakini cha kushangaza kufungua kile kitasa cha mlango ndio ilikuwa shida kwangu, nilijaribu kujiinua lakini ilikuwa shida pia, “jamani fungua msije mkafia ndani kuna nini huko” alisema yule mkaka alie kuwa kwa nje, “nakufaaa” niliendelea kusema nakufa maana yale maumivu yalikuwa machungu sana. Wakati naendelea kuzubaa nikaanza kusikia kabisa mtoto amekaribia kutoka ikabidi nijikaze kama mwanamke ili nisukume yule mtoto atoke, nilijikaza huku nikilia nikijivutavuta huku na kule lakini kazi ilikuwa ngumu sana, nilijikaza kwa nguvu zote mpaka nikafungua kile kitasa ili nipate msaada, yule kaka alipo ingia ndani ikabidi awashe kibatari maana kilikuwa pale mezani, ndipo akasema nichukue kanga ili anikimbize hospitali, ndipo akanitoa nje haraka huku mvua ikiwa inanyesha, akanipakia kwenye baiskeli yake ndipo tukaianza safari, kipindi tupo njiani uvumilivu ulinishinda ikabidi nimwambie tu anisaidie ili niweze kujifungua pembeni ya mti maana hospitali ilikuwa mbali na nilikuwa naona mtoto amekaribia kutoka.
“sasa dada mimi nitakusaidiaje ujifungue maana sina utaaramu wa kumfungulisha mwanamke” alisema yule kaka akiwa na huruma sana lakini sikutaka kuwa na woga wa aina yoyote ile “wewe jaribu tu kaka angu Mungu atasaidia”, kweli  yule kaka alinibeba na kuniweka pembeni sehemu ambayo wapita njia wasingeweza kuniona, kisha akanipa moyo sana akisema, “jitahidi kusukuma hivyo hivyo, naomba ujikaze sana”, nilijikaza nikasukuma kwa jitihada zote lakini ikashindikana, yule kaka akajikaza na kunirudisha kwenye baiskeli kisha hakujali chochote, tulijikaza mpaka tukafika hospitali, baada ya kufika tu nikaambiwa nitoe pesa lakini sikuwa nayo, palepale nikajua lazima nife tu maana bila pesa nisingepata huduma, yule kaka akalipa hela iliyo kuwa inahitajika, lakini kipindi nipo ndani kwaajili ya kujifungua ikawa imeshindikana wakasema kwamba njia ni ndogo kwa mtoto kupita, ndipo wakaomba kuongezewa pesa ili nifanyiwe upasuaji, Mungu alinisiadia tena yule kaka akasema yupo tayari kulipa.
Upasuaji ulienda vizuri nikawa nimepata mtoto wa kike tulitoka hospital nikiwa naumwa nikiwa na yule kaka, kibaya zaidi kipindi tu nimefika nyumbani sikuamini nilicho kikuta, kumbe zile purukushani za kunibeba ili kunipeleka hospital kile kibatari ambacho yule kaka alikuwasha ndani, kilidondoka chini hivyo wakati tunaenda hatujui chochote kumbe nyumba nzima ilikuwa inaungua.
Nilijiona sina bahati maana ule ndio urithi wazazi walio tuachia na sikuwa na pesa ya kujenga nyumba nyingine, kweli nililia sana mpaka yule kaka akanionea huruma, “usilie sana, mimi nitakusaidia tu twende kwangu, utaishi pale ili uuguze kidonda, ukiisha pona tutajua unafanya nini ili mwanao aendelee kupata malezi bora” alisema yule kaka aitwae Millaji, sikuwa na namna ikabidi nimkubalie, hivyo nikaondoka huku niitazama nyumba ilivyo ungua, kweli moyo ulisononeka sana maana hakukua na kitu kilicho salia.
Tulifika salama pale kwa millaji, lakini cha kushangaza kumbe millaji pia familia yake ilikuwa inatatizo kama nilivyo kuwa na Frank yaani hata wao walikuwa hawajabarikiwa mtoto, sasa baada ya mke wake kutuona alikaa kimya kwanza kisha millaji akamtambulisha kuhusu mimi na tulivyo kutana, “hivi mme wangu unaakili kweli, yaani unaokota watu barabarani unaniletea hapa, sitaki kumuona huyo sijui wastara wako, chagua moja abaki yeye niondoke mimi, au ni mwanamke wako unamleta kijanjajanja” alisema mke wa millaji akiwa na hasira sana, “hapana mke wangu tumsaidie tu, Mungu atatulipa, huyu dada hana sehemu yoyote ya kuishi alafu anamtoto mchanga” alijibu millaji akimbembeleza  mke wake, niliendelea kulia kisha nikapiga magoti nikiwa na mtoto wangu na kusema kwamba, “shemeji naomba unisaidie, japo nikae sikumbili tatu tu, tazama mtoto wangu ni mchanga sana alafu nimejifungua kwa upasuaji hivyo ninakidonda, naomba msaada wako jamani”.
Usikose sehemu ya nne.
Watunzi-wastara juma na @hadithizetu
Whatsapp stories 0769510060.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only