Tuesday, March 3, 2020

LIACHE CHOZI LANGU : Sehemu ya 2



SEHEMU YA PILI
WATUNZI- wastara juma na @hadithizetu
Whatsapp 0769510060.
Nililia sana baada ya kuwapoteza wazazi wangu wote, nilihisi hata maumivu ya kuingiliwa kinguvu na wanaume nane yameisha kabisa, kilicho niuma nipale mme wangu alipo pata taarifa ya kuja kuwaaga wazazi wangu kwenye msiba lakini alikataa kabisa kuja sababu mke wake alimzuia, Baada ya mazishi kuisha, niliendelea kukaa na mdogo wangu ambae alikuwa anaishi palepale nyumbani na wazazi, lakini baada ya wiki chache nikaanza kujisikia utofauti mwilini mwangu, kumbe nilikuwa nimepata ujauzito kutoka kwa wale vijana walio nibaka! ujauzito ulinishangaza maana nilijihisi wa furaha vilevile nikajiona wa uzuni pia maana mme wangu alikuwa anasema sina uwezo wa kuwa na mtoto ila chakushangaza nilivyo bakwa nikapata ujauzito.
Maisha yaliendelea taratibu huku tumbo likiendelea kukuwa, baada ya miezi sita Janeth ambae ni mdogo wangu wa kike akawa amepata mchumba, na hawakukaa hata siku nyingi akawa amechukuliwa nyumbani hivyo nikaanza kuishi mwenyewe pale nyumbani. Nilicho mshukuru Mungu mdogo wangu alikuwa anakuja kunitembelea hivyo sikujihisi mpweke sana, na hata mme wake pia alimruhusu kwamba awe anakuja kunitembelea maana nilikuwa nachoka sana kutokana na ule ujauzito, kuna kipindi ambacho siwezi kusahau kabisa maana ilikuwa imebaki mwezi mmoja tu nijifungue lakini kwa bahati mbaya mme wake Janeth akaugua sana, ikabidi mdogo wangu akamuangalie mme wake kwanza maana alikuwa na hali mbaya kiafya.
Ujauzito ulinitesa sana, maana sikuwa na mtu wa kunisaidia, kibaya zaidi hata ndugu zetu baada ya msiba hakuna hata mmoja alieweza kuja kututembelea pale nyumbani, tumbo lilikuwa linanisumbua sana na sikuwa na pesa ndani hivyo ilinibidi niwe napalilia mwenyewe shambani ili niweze kupata chakula, hata nilipo umwa sana nilikuwa natumia dawa za kyenyeji maana hospitalini palikuwa mbali na hata hivyo pesa ya matibabu sikuwa nayo kabisa.
Maisha yaliendelea kuwa magumu sana mpaka nikaipoteza furaha nikawa mtu wa mawazo sana, sikuwa na mtu wa kumdekea maana kipindi mama yupo hai mda mwingine alikuwa anatufariji wanae.
Siku moja usiku mvua ikiwa inanyesha sana, nilipata uchungu wa kujifungua, sikuwa na mtu yoyote pale nyumbani wa kunisaidia na nilikuwa nasikia mtoto anatoka, nilianza kupiga kelele maana ilikuwa mida kama ya saa nane lakini hakuna hata mmoja alie sikia nje, hali ilikuwa ngumu nguvu zikaniishia kabisa nikajua moja kwa moja lazima nife na mtoto afe tu, kipindi natapatapa huku na kule mule ndani, huku mvua kubwa inanyesha, kumbe kuna mkaka mmoja alikuwa anapita usiku uleule na baiskeli akaona bora ajikinge pale nyumbani, sasa wakati yupo kwa nje akasikia mimi nalia kwa ndani, ndipo akaanza kugonga mlango ili nimfungulie, nilipo sikia mtu anagonga nikatamani kuamka ili nimfungulie anisaidie, lakini nilipo jaribu kuamka tu nilianguka hapohapo nguvu sina ila nikasema nikizubaa tu namuua mwanangu ndipo nikaanza kujivuta kama nyoka ili niufikie mlango kusudi niweze kusaidiwa ili mtoto atoke salama.
USIKOSE SEHEMU YA TATU
WATUNZI wastara juma na @hadithizetu
Kwa hadithi nyingi zaidi follow @hadithizetu
Whatsapp group 0769510060

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only