SEHEMU YA
KWANZA
WATUNZI
WASTARA JUMA &@hadithizetu
WHATSAPP
0769510060
Matatizo
tumeumbiwa binadamu, mda mwingine wengi ukata tamaa kabisa kwa fikra za kwamba
wao ndio wenye manyanyaso na mateso tu, lakini chukua mda kaa hata barabarani,
kisha uliza watu kumi tu, ambao ni wapita njia matatizo yanayo wazunguka,
utaona yako madogo, unaweza kuwa mpole mwenye tabasamu lako lifichalo matatizo
yanayo kuumiza lakini binadamu wanaweza kukuumiza kwa maneno, masekenyo na hata
kutamani ufe ili iwe furaha kwao. Wasingekuwa binadamu mpaka sasa familia yangu
ingekuwa na maendeleo, amani, furaha na yenye baraka lakini nakumbuka na siwezi
kusahau kabisa, kuna siku moja nikiwa nyumbani namuandalia Frank chakula cha
jioni, maana ndio alikuwa chaguo la moyo wangu na nilimpenda mpaka akanioa
nikaanza kuishi nae pamoja, lakini siku hiyo jioni mme wangu alikuja akiwa
amenuna sana, “Frank mme wangu tatizo nini,mbona leo huna furaha”, “Wastara
nimechoka kuishi hivi, hivi unazani huko nje nachukuliwaje, yaani mda wote huo
tuko pamoja, hata kupata kichefuchefu sijawai ona, naomba uchukue vitu vyako
urudi kwenu, nimeisha choka kusemwa na ndugu” alijibu mme wangu akiwa na hasira
sana, “hapana Frank usichukue maamuzi hayo, mtoto ni majaaliwa, naamini
tutampata mtoto mme wangu, usisikilize maneno ya watu kwenye mahusiano yako,
hayajengi mme wangu, yanabomoa tu” nilimjibu frank nikiwa katika sura ya uzuni
sana.
Mme wangu
alianza kubadilika, akija nyumbani anahakikisha ameisha lewa, kutokana na zile
pombe basi akawa anaongea maneno ambayo yalikuwa yanautesa sana moyo wangu,
hata huduma ya chumbani akaanza kunibania, kila nilipo onyesha kunyenyekea ili
akae sawa lakini ni majibu mabaya tu nilikuwa nayapata, “hivi wewe mwanamke
mbona unashobo sana, kwani wanaume wapo wangapi duniani, mimi kweli nimekuchoka
Wastara naomba tu uondoke, siutafute mwanaume ambae hana uwezo wa kuwa na mtoto
kama wewe ili muishi hivyohivyo” alisema Frank bila hata huruma lakini
kwasababu nilikuwa nampenda nilipambana sana nikaendelea kuwa king’ang’anizi
kwake.
Siku moja
nikiwa nafaya usafi chumba nilicho kuwa nalala na mme wangu, kumbe Frank
alienda kuninywea pombe za asubuhi kumbe baa aliyo kuwepo kulikuwa na mdada
mmoja ambae alikuwa anauza hapohapo pombe, sasa kwasababu ya ulevi wa mme wangu
bila hata aibu akapendana na yule dada na akamwambia aje anipige kisha mimi
nichukie ili niondoke alafu frank aishi na yule Lucy pale nyumbani. Kweli
wakati nafanya usafi nilishangaa kuona yule dada alie kuwa amevaa sketi fupi
sana yenye kumshawishi mwanaume yoyote mwenye tamaa anaingia ndani, “dada
naomba upishe kwa mme wangu”,alisema Lucy, “nikupishe kwangu, nikupishe wewe
kama nani”, “kwataarifa yako umechokwa dada ehh, mtu gani uzai, mme wako yupo
hapo nje kaongee nae, kwa jina naitwa Lucy alafu waga siongeagi sana,
nimemaliza , kwa msaada zaidi labda uwe msaidizi wangu wa kazi humu ndani”
alisema Lucy akiwa anabinuabinua macho, hasira zilinipanda machozi yakinitoka,
nilimshika shingo yule dada, kisha nikamdondosha kitandani, “nakufaaa nauliwaaa
ndani, njoo unisaidie mme wangu” alisema Lucy, hapohao frank akaja, “huyo
Malaya wako ameniumiza angalia alivyo nitoboa na kucha”, Frank alichukia sana,
alinizaba kofi ambalo sitalisahau maisha yangu yote, kipindi bado nimezubaa
akanipiga mtama (ngwara) nilijigonga kichwa chini mpaka damu zikaanza kutoka
puani,na niliogopa zaidi maana hata mdomoni pia damu zilikuwa zinanitoka,
“mpuuzi sana, unampiga huyu mwanamke unamfahamu,” alisema Frank kisha akachukua
nguo zangu tu na kuzirusha nje, akasahau kabisa kipindi ananileta kwake hakuwa
hata na kitanda na hata vyombo vya ndani nilikuwa najibana hela kidogokidogo
kisha nanunua, lakini nikapewa nguo tu,hata viatu vyangu hakunipa.
Nilitoka nje
nikaanza kulia kisha nikarudi ndani nikisema “nisamehe mme wangu nipo tayari
kuwa mke wako wa pili, naomba unisaidie” lakini walivyo na roho mbaya bila hata
huruma walivuana nguo zao na kufanya tendo mbele ya macho yangu, kile kitendo
kiliniuma sana ikabidi nirudi kukaa nje ya mlango, na kwadhalau yule dada
akaanza kujitolesha sauti ili nijue bado wanaendelea kufanya lile tendo,
“endelea mume wangu, nakupenda bby ohhhshhh” hizi sauti zilijirudia kutoka kwa
Lucy, niliumia sana pale nje, nikatamani hata kuua, nikaona itakuwa dhambi,
wazo likasema bora nijiue lakini nikaogopa maana nilitamani kuishi,ndipo wazo
zuri la busara likaniijia kwamba, “kumbuka mme wako amelewa subiri amalize kufanya
uchafu wake huenda atakusamehe” nilisubilia pale nje kwa mda mrefu, mpaka mvua
ikaanza kunyesha, “Frank mme wangu naomba unifungulie nanyeshewa huku nje”,
“nani mme wako, ondoka mimi sikujui”
Niliamua
kukusanya nguo zangu zikiwa zimelowa, huku na mimi pia nimenyeshewa,kisha
nikaanza kutembea ili nirudi nyumbani, umbali ulikuwa mrefu na kibaya zaidi
Frank hakunipa hata mia,na hela yangu iliyo kuwa kwenye kibubu chini ya kitanda
sikuweza kuichukua maana nilisukumwa nje na sikuweza kuingia tena ndani,
kutokana na umbali wa mpaka kufika kwetu nilifika sehemu ikabidi nipumzike na
ubaya zaidi kulikuwa na kigiza, kumbe pembeni kulikuwa na vijana wanacheza kamali,
huku wanavuta Bangi, kuna mmoja aliniona akawaita wenzake, walikuja pale, “wewe
mdada unajiamini vipi kukaa masikani kwetu mpaka mda huu”,”naombeni mnisamehe,
nimepata matatizo mme wangu kanifukuza nipo naelekea kwetu lakini nimechoka
ndio maana nimepumzika hapa”, “basi hamna shida, naamini utakuwa umechoka njoo
hapo pembeni tukupe japo maji”, nilifurahi nikawaona wema sana, nilipo fika
pembeni nikasikia kwamba, “vua nguo haraka tukupe maji yako”, nikaanza kushika
begi langu ili wasije kuninyang’anya, “haaaaa, haaa ,haaa, unatubishia”
walisema wale vijana maana walikuwa nane, mmoja akachomoa kisu, nikaona kuliko
kufa bora niachie, kweli walinivua, kisha wakanichangia wote kimwili, nilipatwa
na maumivu, kibaya zaidi wakaweka nguo yangu ya ndani mdomoni na kitambaa
nilikuwa nacho eti nisipige kelele, maumivu niliyo yapata pale sikuwai kuyapata
tangu nazaliwa walinifanya niumie sana sehemu yangu ya siri, niliishiwa hata
nguvu mpaka nikapoteza fahamu, nilikuja kushtuka usiku nguo zangu zote
zimechukuliwa nikiwa nimebaki na kitambaa pamoja na nguo yangu ya ndani
mdomoni, niliivaa ile nguo kisha nikaanza kushindwa naendaje nyumbani, kipindi
kunaanza kukucha kuna wakaka wawili walikuwa wanapita, moyo ulikataa kabisa
kuwaita lakini niliogopa jamii itanichukuliaje mchana nikionekana uchi, hivyo
nikataka kuwaomba msaada wakunitafutia nguo,niliwaita wakaja, mmoja wao akasema,
“kaka hii ndio mikosi, huyu atakuwa mshirikina, ameanguka na ungo hapa,
anatakiwa kufa tuwaite binadamu wamuue”, mwenzake akajibu, “hapana kaka, tazama
dada wawatu analia, tungemuuliza kwanza anatatizo gani” niliwaelezea nilivyo
bakwa ndipo mmoja wao akanifatia nguo kisha wakanisaidia hela ya nauli, alie
nipa hela alikuwa anaitwa, Mussa, na mwingine Samweli, nilienda mpaka nyumbani
nikiwa na maumivu sana, wakati nakaribia na mazingira ya nyumbani nikashangaa
sana kukuta wanakijiji wengi pale, nilipo sogea kwa mbele nikakuta wengine
wanalia, ndipo nikauliza kuna nini watu wakaanza kulia sana, kumbe mama pamoja
na mama yangu wote walikuwa wamefariki na kibaya zaidi ndani ya siku moja…
USIKOSE EPISODE YA PILI
LIACHE CHOZI LANGU
IMEANDIKWA NA WASTARA JUMA PAMOJA NA
@hadithizetu
Whatsapp +255769510060
Post a Comment